๐จ_|| ๐ฌ๐๐ก๐๐ ๐ช๐๐๐๐ช๐๐๐ ๐๐จ๐๐ข๐ ๐๐ ๐ ๐๐๐๐ญ๐ข ๐ช๐ ๐๐๐ฅ๐๐ฌ 1965 ๐ฐ๐ฐ
๐น๐ญ๐ฎ๐ธ๐ฎ๐๐ฎ๐ธ๐ฎ๐๐ถ : ๐๐ฒ๐ผ ๐๐ฎ๐๐ถ๐ธ๐ฎ ๐๐ถ๐๐๐ผ๐ฟ๐ถ๐ฎ๐น
โก๏ธ Tarehe kama ya ๐ท๐ฎ๐ป๐ฎ, mwaka 1965, watani wa jadi wa soka la Tanzania, Yanga na Sunderland, walicheza mechi yao ya kwanza kwenye ligi ya taifa.
โก๏ธ Kabla ya hapo hakukuwa na ligi ya taifa, badala ya yake kila mkoa ulikuwa na ligi inayojitegema.
โก๏ธ Ligi moja ya taifa ikaanza 1965 na watani wa jadi wakapangwa kukutana siku kama ya ๐ท๐ฎ๐ป๐ฎ, Juni 7, 1965, kwenye uwanja wa Ilala, sasa Karume.
โก๏ธ Timu zote zikaja uwanjani, lakini Yanga wakagoma kucheza kupinga kuwemo kwa mchezaji fulani wa Sunderland.
โก๏ธ Sunderland wakagoma kumuondoa mchezaji wao kwenye kikosi.
โก๏ธ Yanga wakaja na hoja nyingine, hawamtaki mwamuzi.
โก๏ธ Rais wa chama cha soka, FAT, Balozi J Maggid, akamteua kocha wa timu ya taifa, Milan Celebic, achezeshe.
โก๏ธ Yanga wakakubali kuingia uwanjani, Sunderland nao wakagoma, wakitaka wachezaji wawili wa Yanga waondolewe kwa sababu walifungiwa.
โก๏ธ Mwenyekiti wa Ligi (sasa Bodi ya Ligi), bwana Abdul Hussein, akasema wao kama waendeshaji wa ligi hawajawafungia hao wachezaji.
โก๏ธ Kutokana na malumbano haya, mchezo ukachelewa kuanza...matokeo yake giza lilitinga kabla mchezo haujaisha, huku Yanga wakiongoza 1-0 kwa bao la dakika ya 15 la Mawazo Shomvi.
โก๏ธ Kutokana na giza, mwamuzi Milan Celebic, akavunja mchezo kwa sababu uwanja haukuwa na taa.
โก๏ธ FAT ikaamua mchezo urudiwe, Yanga wakakataa wakasema wao walishashinda.
โก๏ธ Mwenyekiti wa FAT, Balozi J Maggid akasisitiza kwamba mchezo lazima uridiwe, atakayekataa kucheza atakatwa alama.
โก๏ธ Yanga wakasema wakikatwa alama watavuruga uchaguzi mkuu wa serikali ambao ulipangwa kufanyika Oktoba mwaka huo.
โก๏ธ Huo ndio ulikuwa uchaguzi wa kwanza baada ya uhuru.
โก๏ธ Mwenyekit wa FAT, Balozi J Maggid akasema mpira na uchaguzi havina uhusiano...waje wacheze au tuwakate alama.
โก๏ธ Akaongeza Yanga walikuwa sehemu ya tatizo lililosababisha mchezo kuchelewa kuanza kwa hiyo hawana haki ya kupata alama kwa mchezo ambao haukuisha.
โก๏ธ Yanga wakakataa kucheza mechi ya marudio, wakajitoa kwenye ligi.
โก๏ธ Sunderland wakapewa point za mezani na mwisho wa siku wakaibuka Mabingwa
(Follow ๐๐๐น๐ ๐๐ถ๐น๐ถ๐ฎ๐ป๐ฒ๐ฒ
#Dibahvansports.