1. Acha kutangaza mipango yako
Unaposhirikisha watu wengi, unaathiri maendeleo yako. Fanya mambo yako kimya kimya. Shirikisha wale wanaotakiwa kuongeza thamani ama kuchalenji kwa njia chanya inayojenga mipango yako.
2. Tambua wakati wa kusema HAPANA.
Watu imara hujali hali zao kwanza kabla ya kuwafurahisha wengine. Fanya mazoezi ya kusema hapana mara nyingi zaidi.
3. Fanya uamuzi, na ushikilie
Watu wengi sana hawana nidhamu na huzirudia ruwaza dhaifu. Amua kubadilika na shikilia maamuzi hayo.
4. Kuna nguvu kwenye namba
Hakuna aliyefanikiwa maishani kwa kufanya mwenyewe. Unahitaji timu itakayokuinua na kukuwezesha. Acha kuwa mbwamwitu mpweke.
5. Ondoa kabisa usumbufu, lisha fokasi yako
Fokasi kwenye malengo yako badala ya misisimko inayotokana na dopamine. Utafanikisha chochote utakacho.
6. Wakati wote wape thamani wengine.
Kuna siri moja kubwa ya mafanikio: kufanya maisha ya wengine kuwa mepesi. Katika biashara na mahusiano, kuwapa wengine thamani kutakufanya wewe kuwa kipaumbele chao.
Asante kwa kusoma na kushare
"Waliofanikiwa mara zote huwa na vitu viwili kwenye 'lipsi' zao: ukimya na tabasamu.".