MWANAMKE JIJENGE KIFIKRA
Umemmiss mumeo unampigia simu hapokei, unatuma meseji hajibu siku yako inaharibika, unaanza kuwaza anafanya nini huko?
Labda yuko na Mwanamke mwingine, labda kanichoka, labda hivi na vile.
Badala ya kuwaza mambo mengine unatumia muda wako wote kuwaza vitu vibaya ambavyo kwa akili yako unahisi anavifanya,
kwa maana hiyo, bila kujua anafanya nini huko alipo unaumia kama mtu aliyetoka kumfumania uso kwa uso.
Hapa hata akija kujielezea, akakupa jibu la kueleweka, utamuelewa lakini utakua ushaumia, tayari sumu ishaingia mwilini.
Ningumu sana kuwa na furaha ukiwa hivi.
Sasa hembu leo nikufundsihe siri moja, umemtafuta mtu hajapatikana, unajiona unaanza kumuwaza, hapana, hembu tafuta kitu kingine cha kufnaya.
Kwanza jiambie hata nikiwaza haisaidii chochote, kisha tafuta kitu kingine cha kukufanya uwe bize.
Fanya #Uamuzi, pitia darsa kwa magroup ulioko nayo, soma quran,Biblia Fanya mazoezi, , salimia marafiki, , pika au fanya kitu kingine chochote.
Unafanya unaona bado akili iko kwake, sasa chukua kalamu na karatasi, anza kuandika vitu vingine ambavyo anaweza kuwa anavifanya na si kuchepuka.
Kumbuka mara ya mwisho wewe kutokupokea simu labda umepigiwa na Mama yako ulikua unafanya nini?
Andika chini kitu kingine, mfano, andika, labda amepitiliwa na usingizi, akaisahau simu kwenye gari, yuko bize ofisini hawezi kupokea, anaoga, anamambo mengi yanamchanganya… andika kila kitu.
Baada ya hapo chagua kimoja labda “Ana mambo mengi yanamsumbua kichwani akiwa sawa atanitafuta”
Ilazimishe akili yako kuondokana na mawazo machafu, hata kama anafanya hivyo vitu, ila anza kujifundisha kutokuumia kama mtu hapatikani.
Acha kupiga simu mara kwa mara, kutuma meseji nyingi kulalamika kwakua tu hapokei simu, usifanye kitu ukiwa na hasira.
NB: Unaumizwa zaidi na mambo mabaya unayoyawaza kuliko mambo mabaya unayofanyiwa, badilika.
TUKUTANE KWENYE GROUP.
0769228130..