Mmiliki wake akafanya jitahada za kumtoa lakini akashindwa.ikabidi aite wana kijiji wamsaidie .
Wanakijiji walipofika wakaona kule chini shimoni ni mbali sana isinge wezekana kumtoa yule punda.
Hata hivyo mmiliki wake akaona alisha kuwa mzee tayari hvyo hata ange fia mle kusinge kuwa na hasara yeyote ile
BAsi waka azimia wamwage mchanga mle shimoni wamfukie
SASA walipo kuwa wakifukia basi yule punda akawa anajitingisha kisha ule mchanga ulio kuwa mgongoni mwake unamwagikia chini.....ukimwagikia chini ukawa unampandisha juu yule punda basi wale wanakijiji wakawa wanashangaa kuona yale walio kuwa waki yaona hata hvyo hawakuacha kufukia.
BAADA ya kufukia kwa muda mwingi mchanga ukajaza shimo punda akafanikiwa kutoka nje.
👉Sikiza DUNia itajaribu kukufukia na changamoto za hapa na pale lakini hautakiwi kukata tamaa jitingishe kuondoa changamoto zako alafu endelea mbele.
bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
23 Isaya 40 :31.