Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

TAMU YA SAKINA 01

23rd Jun, 2025 Views 18

TAMU YA SAKINA 01.
FOLLOW Hadithi Za Mkatili
Kwa majina naitwa SAKINA ni binti nilielelewa kwa malezi ya mzazi mmoja ambaye ni mama tuu...wengi hupenda kusema
(single mother)

Katika maisha yangu yote hayo sikuwahi kumuona Wala kumjua baba yangu hata kwa picha...nilipomuuliza mama kuhusu ilo,aliniambia tu kuwa baba yako alikukataa toka mimba..nilipoomba kuelezwa kwa undani zaidi mama alisema utakapokua mkubwa nitakuelezea...

Siku zilipita nilihuzunila Sana hasa pale nilipoona watoto wenzangu wakisimulia habari za baba zao Hali ya kuwa Mimi sikuwahi kupata Wala kuonja mapenzi ya baba.Ila nilivuta tu subra kwa kusema huenda ipo sababu na mama amekwisha kuniahidi ipo siku atanieleza kwanini baba yangu aliamua kunikataa Mimi na kukaa mbali kabisa na maisha yetu.

Siku zilisonga,mama alikua akiuza bar ama grocery ili tuweze kujikimu kimaisha...nilifanikiwa kumaliza elimu yangu ya msingi na kuanza masomo rasmi secondary,hapo ndipo akili yangu iliendelea kutanuka zaidi Kwan niliweza kujua hili zuri hili baya.
Nikiwa kidato Cha tatu,mama aliniita na kuniambia,sakina usiku wa leo Nina mazungumzo na wewe.nikamwambia sawa mama,akasema natoka kazini saa tano usiku Kama nitakukuta umelala Basi tutazungumza kesho asubuhi kwakua ni weekend najua hutaenda shule.

Nakumbuka iyo siku hatukufanikiwa kuongea Jambo lolote,kwani Hadi muda aliorudi alinikuta tayari nimelala,asubuhi na mapema sote tuliamka kabla ata atujatoka kitandani mama akasema sakina Jana nimerudi nimekuta tayari umeshalala,nikamwambia nilikusubiri lakin usingizi ulinizidi nguvu...akasema sawa tunaweza kuanza kuongea Sasa...

Mama alianza kwa kusema,SAKINA binti yangu ushakua mkubwa,najua Kuna mambo mengi Sana unataman kuyajua ila Hadi Leo hii unabaki na maswali mengi Sana kichwani mwako,na siku zote za ukuaji wako nilikuahidi kuwa ipo siku nitakueleza kuhusu baba yako Basi Leo nitakupa historia kwa ufupi...nilitega masikio yangu na kusikiliza kwa umakini zaidi mama akaanza kuongea....

Hapo zamani miaka kama 18 au 19 iliyopita nilikua nikifanya kazi za ndani muda huo nilikua bado msichana hata wewe sakina nilikua bado sijakupata mwanangu.

Kama ujuavyo mwanangu sakina elimu ya mama yako hapa ni darasa la Saba tuu,kwaio sikuweza kuendelea zaidi ya kuangaika kwenye majumba ya watu wanaojiweza ili kujitafutia riziki.nilifanya kazi za ndani kwa malengo kwani kila Senti nilioipata Kama mshahara niliifadhi Hadi ilipofika pesa ya kuweza kununua godoro na kulipa Kodi ya miezi mitatu.

Hapo ndipo nilimuaga boss wangu na kumwambia kuwa naacha kazi Sasa nahitaji kujitegemea Mimi kama mimi.boss hakuwa na neno niliondoka na kwenda huko uswahilini kuanza kujitegemea,mwanangu sakina,hapo nilikua nimetokea maisha ya kijijini,kwaio jijini nilikuja tu kufanya izo kazi za ndani.

Basi nilifanikiwa kupata chumba Cha Giza na bei rahisi zaidi,nilinunua godoro kwa mtu ambalo limeshatumika ilikua ni Bei nzuri kuliko ningenunua dukani.

Niliwaza maisha yangu yatakuaje Kama nitabweteka tuu bila kufanya kitu chochote?nilinunua beseni na mtaji kidogo nikaingia sokoni na kununua mboga mboga za majani tofauti tofauti,Kama vile tembele,mchicha,bamia,nyanya chungu na zinginezo.

Haikua rahisi lakini niliingia mtaani na kuanza kuuza nyumba Hadi nyumba...mtaani waliponizoea Sana wakaanza kuniita mama mboga...baada ya kuuza mboga kwa muda mrefu nikapata wazo la kuuza uji lishe Kila jioni.kwaio nilichokua nakifanya ni kwamba,asubuhi naenda sokon nanunua mboga napita kuuza mtaani,ikifika mchana napumzika,jioni naanza kuandaa uji najaza kwenye chupa natembea kwenye vijiwe watu wanapocheza bao,gereji,na madukani kuuza uji Hadi ikifika saa tatu nakua nimeshamaliza.

Kwakweli iyo ilinisaidia sana mwanangu,nilikua naweza kupata hata pesa ya kumtumia Bibi yako huko kijijini.basi maisha yalisonga,Hadi pale nilipokutana rasmi na baba yako.

Nakumbuka iyo siku nikiwa nauza uji nilipita mahali nikakuta vijana wawili wamekaa kwenye gogo,mmojawapo ambaye ni baba yako aliniita na kuniuliza;vipi dada unauza kahawa?nikasema hapana nauza uji,basi yule kaka Akaniambia tuwekee vikombe viwili hapa utapitia vikombe vyako.nilimimina Kisha nikaondoka...
Nilipomaliza kuzungukia wateja wangu wote nikawapitia hapo kwenye gogo walipokua wamekaa...walinipatia pesa na vikombe,ila walinisihi niwaletee kila siku,sikusita ila nilifurahi kwani nilikua nimeongeza mteja mpya kwenye biashara yangu.

Ikawa ni kawaida kila nikipita lazima anisimamishe nimpatie uji,tukazoeana Sana,ila kwa kipindi hichi nilikua nikimuona yeye peke yake hakua na yule rafiki ake...

Alinizoea Sana,tukajuana aliniuliza naitwa Nani nikamwambia Mariam,nayeyey akasema anaitwa saidi,alipajua kwangu japo kwake sikupajua,nilipomuuliza akasema kwamba yeye sio mkazi wa DAR ila yupo tu kikazi ni anaishi Arusha,na dar amefikia nyumba za wageni tuu.

Urafiki wetu ulipamba kasi Sana,akawa ananipatia pesa nyingi ili niweze kupika nyumbani kwangu tule wote...nilijiona Kama nimepata ndugu tuu maana sikua na ndugu hapo dar.

Alinishauri vitu vingi vya maisha,alininunulia kitanda ili nisilale chini kwenye godoro,licha ya kunifanyia yote hayo hakuwahi kunitongoza hata siku moja.

Alikuja akaondoka na kwenda kwake Arusha ila aliniahid atarud wiki moja mbele kwani ile kazi iliomleta dar bado aijaisha.kipindi hicho sikuwa na simu niliishi kwa tabu Sana kwa muda huo wa wiki moja kwani nilikua nimemzoea Sana,hadi siku aliporudi Tena,

Alikua akija kula kwangu anaenda kulala gesti alipofikia,siku moja baba yako saidi alivunja ukimya na kuamua kuniambia kuwa ananipenda na anataka anioe.nilifurahi Sana na kujiona mwenye bahati Sana.kwani hata Mimi nilikua tayari nimeanza kumpenda...

Basi tulianza kuishi pamoja,haikuchukua muda nikawa nimeshika ujauzito,maisha yetu yalikua ya furaha,ila baada tu yakumuambia kuwa ni mjamzito,alibadirika na kuniambia yeye hataki mtoto kwaio ni kiranga changu tuu kubeba mimba,alikua namimi kwaajili ya starehe na sio kuzaa,hapo ndipo akaniambia kuwa wiki ijayo anaondoka na kwenda Arusha kwani mradi wake uliomleta unaelekea kuisha,akaniambia sitokaa nione sura yake,na mimba sio yake🥹nililia Sana,sikuamini nikasema saidi mbona sijawahi kukutegemea Kama unaweza kunifanyia hivi?

Akasema nakupeleka wapi Mariam?Mimi nnafamilia yangu mke na watoto na saidi sio jina langu harisi kwaio pole kwa yote na nakuachia ela hapa tafuta namna yakuweza kualibu hiyo mimba kabla haijawa kubwa,hiyo mimba sio yangu watoto nilionao wananitosha Sana.

Aliniachia pesa hapo kitandani Kisha akaondoka,niliona Kama naota,ila ndo ilikua kweli aliondoka moja kwa Moja kwenye maisha yangu baba yako....
ITAENDELEA......
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

TAMU YA SAKINA 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/tamu-ya-sakina-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 34

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA 33

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA_32

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA_31

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA _26 & 27

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA_25

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA_24

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA_23

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA_22

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA _20 & 21

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA_18 & 19

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA _16 & 17

majario rewards 100 Comments 0
 

SAKINA 14 & 15

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 13

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 12

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 11

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 10

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 9

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 8

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 07.

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 06.

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 05.

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 04.

majario rewards 100 Comments 0
 

TAMU YA SAKINA 03.

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈19

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 38

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈18

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈18

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈15

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 34

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TUWASHUKURU KINA BABA

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu ya 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MARIA Sehemu ya 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA sehemu ya 37

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA sehemu ya 36

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest