AAAAAASH BOSS ENZOO* *Chapter 9*
Nilijikuta nikipata mshtuko na wasiwasi wa hali ya juu.
"Ina Maana ma Mdogo amemlipa Enzo kuja kunirudisha hapa?"
Nilijiuliza kimoyomoyo.
Baada ya kimya cha muda mfupi kidogo, enzo akaniambia.
"Haya Shuka tumefika"
Nilimuangalia kwa macho ya huzuni sana lakini enzo hakuweza kuelewa kitu chochote kile, zaidi akafungua mkanda wa siti na kufungua mlango wa gari.
"Kwahiyo Uko serious umenileta Mimi kwenye hii Nyumba ?"
Nilimuuliza enzo kwa sauti ya kutaka kulia kabisa, uku tayali macho yangu yakiwa yameshaanza kulegwa na machozi.
"Ulitaka nikupeleke kwenye familia yangu ili ukaizuru si Ndio? Ishani nakurudisha kwa boss wako ili ajue Kuwa kazi aliyokutuma kwenye familia yangu imekushinda"
Niliganda nikimuangalia enzo, nilitamani sana anielewe na ajue Kuwa Mimi sio mtu mbaya na sina nia mbaya na familia yake lakini hali hiyo ilionekana Kuwa ngumu sana kwa Enzo.
"Haina haja ya hayo yote enzo, niko radhi Kuwa chokolaa wa MTAANI kuliko kurudi kwenye hii Nyumba, niko tayali, Kuchomwa na jua asubuhi MCHANA kuliko kuja Tena kwenye hii Nyumba, niko tayali kunyeshewa na mvua na kupigwa na baridi lakini sio kuja kujistili kwenye Nyumba ya kishetani kama hii.
Kwa haraka nikashuka kwenye gari ya enzo na kuondoka zangu Kwa mwendo wa kukuambia uku nikiwa Sijui ni wapi naenda mbwa Mimi.
Kabla sijaendelea mbele ngoja niwambie kitu watu wangu, kwenye haya maisha, kuna changamoto nyingi Sana, kuna vikwazo vya kila aina, kuna majanga na matukio, lakini kikubwa, ni kumuomba Mungu akutunzie wazazi wako, na mzazi omba Mungu akupatie maisha marefu ule watoto wako Maana hii dunia yetu Haina huruma ata kidogo.
Baada ya Mimi kukimbia enzo alibaki akinishangaa tu, mwisho akatoa begi langu la nguo na kuliweka getini kisha akaondoka zake akiamini Kuwa amefanya Jambo sahihi.
Kwa upande wangu nilikimbia umbali mrefu ambao nilihakikisha Kuwa nakuwa mbali kabisa na Nyumba ya ma Mdogo.
"Sasa nitaenda wapi Mimi? Au niende tu kwa madam Groly? Lakini itakuwaje Kama Enzo atanikuta kule ?"
Nilijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu sahihi, nikiwa nimekaa kwenye kituo cha daladala Kama abilia anayesubilia gari.
Nilikaa kwenye kituo iko kwa muda mrefu sana, nilikaa nikiwa Sijui nini cha kufanya na wapi niende.
Hatimaye Ka Giza kakaanza kushika nafasi yake, ishani wa watu nikajikomba Komba mpaka nikafika NYUMBANI Kwa shoga yangu tusajigwe ambaye anajiita Tuntu.
"Wewe si unajifanya malaika Binti Ila sisi Ndio mashetani, Mimi sina muda na wewe kwakweli, sina msaada na wewe kabisa Labda Kama utakubali kurudi kwa mama yako Mdogo, Ila Kama utaki wacha jiji la Dar likunyooshe ma mchungaji"
Alizungumza tuntu baada ya Mimi kufika NYUMBANI kwake na kumuomba Ifadhi.
Aaah cha mtu si chako kwakweli, nikakung'uta makali yangu na kuingia Tena mtaani, nyieeeeh hii situation omba isikukute kwenye kwenye maisha yako Maana unaweza kuona Kuwa dunia nzima umeibeba kichwani.
Nilizunguka sana kwenye sehemu ambazo ata Mimi sikuwa nikiizifahamu na mwisho nikapata sehemu ya kujilaza, ilikuwa ni Nyumba kubwa klasi, na ilikuwa ni Nyumba ambayo ilikuwa inaendelea na matengenezo naweza kusema Kuwa ni boma.
"Mungu nilinde mja wako"
Nilizungumza kimoyomoyo uku nikijilaza kwenye sakafu ya mchanga iliyopo kwenye boma ilo.
INAENDELEA
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni