Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
01 Dec 2025
69 views
VYOTE NDANI GONGA94
Abbas Kumar Ganguly akaja kutambulika kama Kishore Kumar. Mdogo wa gwiji wa maigizo Ashok Kumar
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
ukiweka orodha ya waimbaji bora wa nyimbo katika filamu za kihindi, ukaja kumwacha huyu utakuwa umefanya kosa la jinai. Anaitwa Abbas Kumar Ganguly akaja kutambulika kama Kishore Kumar. Mdogo wa gwiji wa maigizo Ashok Kumar anayetajwa ni moja ya waigizaji bora kuwahi kutokea India.
Kishore Kumar alizaliwa mwaka 1929 akiwa ni wa mwisho katika familia yao. Wakubwa wake wakiwa ni Ashok Kumar, Sati Devi ambaye ni mke wa Sashadhar Mukherjee (huyu ni bibi yao mzaa baba kina Kajol na ndugu zake), pia kuna Anoop Kumar ambaye ni mwigizaji.
Kishore alifuata nyayo za kaka zake Ashok na Anoop ila uigizaji haukuwa uliyompa jina na heshima. alikuja kupata kwenye uimbaji. Huyu ndiye mwimbaji wa nyimbo maarufu kama Rhote Rhote, Andhaa Kaanoon, Khatoon ki khidimati mein. Alishinda tuzo nane za Filmfare. Katika maisha yake ya muziki aliimba jumla ya nyimbo 2905 kwa makadirio.
Kishore alifariki dunia mwaka 1987 kwa mshtuko wa moyo, ugonjwa ambao umeondoa maisha ya waimbaji wengi wa filamu za kihindi akiwemo Mukesh, Mohammed Rafi na wengineo. Alifariki katika siku ya kuzaliwa kaka yake Ashok, ikafanya ndugu yake asiisherekee tena hadi kufa kwake.
Katika maisha yake alioa mara nne, alimuoa Ruma Ghosh mwaka 1950 akamtaliki 1958, akamuoa Madhubala kuanzia 1960 hadi alipofariki mwaka 1969, akaja kumuoa Yogeeta Bali (mke wa Mithun Chakraborty wa sasa) mwaka 1976 na kuachana 1978, mwishowe akamuoa Leena Chandavarkar mwaka 1980 hadi anafariki alikuwa mkewe. Aliacha watoto wawili wa kiume ambao wote waliingia kwenye uimbaji, mkubwa akiwa ni Amit Kumar na mdogo ni Sumeet Kumar.
#Mambosreview
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
This pic from Ishq is pure 90s madness and I love it ! You’ve got Ajay Devgn with his serious, intense vibe… Kajol looking all fiery and expressive… Juhi Chawla
with that cute bubbly energy… and Aamir Khan being his mischievous, romantic self. What a combo yaar! Ishq was not just...
Abbas Kumar Ganguly akaja kutambulika kama Kishore Kumar. Mdogo wa gwiji wa maigizo Ashok Kumar
ukiweka orodha ya waimbaji bora wa nyimbo katika filamu za kihindi, ukaja kumwacha huyu utakuwa umefanya kosa la jinai. Anaitwa Abbas Kumar Ganguly akaja kutambulika kama Kishore Kumar. Mdogo wa gwiji wa maigizo Ashok Kumar anayetajwa ni moja ya waigizaji bora kuwahi kutokea India.
Kishore Kumar alizaliwa mwaka 1929 akiwa ni wa mwisho katika familia yao. Wakubwa wake wakiwa ni Ashok Kumar, Sati Devi ambaye ni mke wa Sashadhar Mukherjee (huyu ni bibi yao mzaa baba kina Kajol na ndugu zake), pia kuna Anoop Kumar ambaye ni mwigizaji.
Kishore alifuata nyayo za kaka zake Ashok na Anoop ila...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/abbas-kumar-ganguly-akaja-kutambulika-kama-kishore-kumar-mdogo-wa-gwiji-wa-maigizo-ashok-kumar
Maoni