Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
22 Nov 2025
79 views
VYOTE NDANI GONGA94
KUOA NABII YAAQUB NA KUFA MKEWE
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Nabii Ya’qub (a.s) alitoroka Palestina kwa amri ya mama yake, aliyekuwa na hofu juu yake kwa sababu ya chuki na hasira ya ndugu yake Esau, ambaye alimchukia kutokana na urithi wa unabii kutoka kwa baba yao.
Alipofika nchini Iraq, kwa mjomba wake Labani, alimwona binti mdogo wa mjomba wake aitwaye Rahel, ambaye alikuwa mrembo sana na mwenye tabia njema. Akamwomba mjomba wake amuozeshwe Rahel, lakini mjomba wake Labani akamwekea sharti:
“Utachunga kondoo wangu kwa miaka saba.”
Ya’qub akakubali.
Miaka saba ikapita, na Nabii Ya’qub akatimiza ahadi yake. Lakini mbele ya watu, mjomba wake Labani alimletea yaaqub binti yake mkubwa Lea ili amuoe badala ya Rahel. Lea alikuwa kinyume kabisa cha dada yake hakuwa mrembo na alikuwa dhaifu wa macho.
Ya’qub alihuzunika sana, akamuuliza mjomba wake kwa nini amemlaghai. Mjomba Labani akajibu kuwa katika desturi zao binti mdogo hawezi kuolewa kabla ya mkubwa. Kisha akamwambia Ya’qub achunge kondoo wake miaka mingine saba ili apate kumuoa Rahel. Nabii Ya’qub akakubali kwa ajili ya mpenzi wake Rahel.
Baada ya muda kuisha, akamuoa Rahel. Na wakati huo haikuwa bado imeharamishwa kuoa dada wawili; hilo lilikuja kuharamishwa baadaye katika Taurati na Qur’an. Hivyo Nabii Ya’qub aoa binti wawili wa mjomba wake baada ya kuingia katika dini ya Nabii Ibrahim (a.s).
Watoto wa Nabii Ya’qub:
Kutoka kwa Lea, alizaa:
Sham’uni, Lawi, Isakhar, Yahudha, Zabulun na Rubeni.
Rahel, kwa upande mwingine, alichelewa kupata mtoto. Akamwomba Allah amruzuku mtoto mwema, na Allah akamjibu. Akajifungua mtoto mzuri anayefanana na bibi yake Sara, mke wa Nabii Ibrahim, na akamuita Yusuf ambaye alikuwa mtoto aliyempenda zaidi Nabii Ya’qub.
Rahel aliishi na Nabii Ya’qub kwa miaka 12 nchini Iraq. Hakuwa mwabudu masanamu, tofauti na watu wengi waliokuwa wakiishi huko wakati huo.
Baadaye Allah akamletea wahyi Nabii Ya’qub aondoke na kurudi katika ardhi takatifu. Akachukua familia na mali yake, na kusafiri hadi kijiji kinachoitwa Hairun, katika mji wa Khalil (Hebron), ambako pia aliishi Nabii Ibrahim (a.s).
Huko ndiko Rahel alipojifungua mtoto wake wa pili, Binyamin. Naye alikuwa mpendwa kwa baba yake kama ndugu yake Yusuf.
Upendo wa Nabii Ya’qub kwa Yusuf uliwasha chuki na wivu mkali katika mioyo ya nduguze. Ya’qub akaliona hilo, hivyo akamwambia Yusuf asiwapelekee nduguze ile ndoto yake ya kuona nyota kumi na moja, jua na mwezi wakimsujudia.
Lakini ndugu zake wakamfanyia njama, wakamtupa Yusuf ndani ya kisima ili atoweke kwenye macho ya baba yao kwa miaka arobaini. Muda huo wote Ya’qub alihuzunika sana kiasi cha kupoteza uoni wake kutokana na kulia kwa uchungu juu ya mwanawe mpendwa.
Mama yake Yusuf, Rahel, alikuwa tayari ameshafariki wakati wa kumzaa Binyamin, baada ya maumivu makali ya uzazi. Alizikwa Bethlehemu Palestina.
Nabii Ya’qub (a.s) naye alifariki akiwa na umri wa miaka 180, na alizikwa karibu na baba yake, kama alivyoagiza kwa mwanawe Nabii Yusuf (a.s).
Ukimaliza kusoma andika moja miongoni mwa majina matukufu ya Allah(s.wt)☝️♥️
#SufianMzimbiri
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
This pic from Ishq is pure 90s madness and I love it ! You’ve got Ajay Devgn with his serious, intense vibe… Kajol looking all fiery and expressive… Juhi Chawla
with that cute bubbly energy… and Aamir Khan being his mischievous, romantic self. What a combo yaar! Ishq was not just...
Mother India (1957) is not just a film, it’s an emotion for Indian cinema lovers. Directed by Mehboob Khan, the movie starred Nargis in one of the most powerful performances ever seen on screen, along with Sunil Dutt, Rajendra Kumar and Raaj Kumar
. It was actually a remake of Khan’s earlier film Aurat (1940), but Mother India became much bigger in scale and impact....
Shahnaz Lalarukh Khan, born in 1960, is Shah Rukh Khan’s elder sister and one of the most important people in his life. She’s about six years older than him and lives with SRK and his family at their beautiful Mumbai home, Mannat
. After their father passed away in 1981 and later their mother in 1991, Shahnaz was deeply affected. Their father’s sud...
Rohan Kapoor and Farah Naaz made their Bollywood debut with Faasle, directed by Yash Chopra. They were introduced as the lead pair — Rohan played Vijay, and Farah played Chandni
. The film told a simple, emotional love story. Vijay and Chandni fall in love, but their relationship faces strong oppo...
Nabii Ya’qub (a.s) alitoroka Palestina kwa amri ya mama yake, aliyekuwa na hofu juu yake kwa sababu ya chuki na hasira ya ndugu yake Esau, ambaye alimchukia kutokana na urithi wa unabii kutoka kwa baba yao.
Alipofika nchini Iraq, kwa mjomba wake Labani, alimwona binti mdogo wa mjomba wake aitwaye Rahel, ambaye alikuwa mrembo sana na mwenye tabia njema. Akamwomba mjomba wake amuozeshwe Rahel, lakini mjomba wake Labani akamwekea sharti:
“Utachunga kondoo wangu kwa miaka saba.”
Ya’qub akakubali.
Miaka saba ikapita, na Nabii Ya’qub akatimiza ahadi yake. Lakini mbele ya watu, mjomba wake Labani alimletea yaaqub binti yake mkubwa Lea ili amuoe badala ya...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/kuoa-nabii-yaaqub-na-kufa-mkewe
Maoni