*MKAKA KAUZU HUYU JAMANI* *SEHEMU YA NANE* Kwanza ka moyo kangu kakafanya paaaaah
"Frank Ebu acha mambo yako Sawa? Narudia Tena, chochote kile ambacho kilitokea kati yetu ilikuwa ni mistake na ujinga wangu wa kushindwa kujiheshimu mbele yako"
"Aaaah Anaya usinifanyie hivyo Basi mwenzio, na usiseme hivyo wewe sio mjinga, mjinga ni Mimi ambaye niliweka Hasira zangu mbele pasi na kufikilia kuhusu wewe, Anaya kWa generation hii ni kazi sana kumkuta mwanamke akiwa na usichana wake Karna wewe, ninachoongea Namaanisha nakupenda sana"
Nyieeeeh kWa Mara nyingine huyu kaka ameniambia Kuwa ananipenda jamani eti nikubali au nikatae, lakini naanzaje kumuamini Tena haraka haraka ikiwa ni mtu ambaye aaminiki kabisa, Mimi na yeye hatukuwai ata Kuwa na mazungumzo ya amani zaidi ya vita Mpya kila siku.
"Nitolee ujinga wako hapa frank Sawa 7 Na Leo
iwe mwanzo na mwisho kukuona hapa Nyumbani kwetu Sawa? Halafu Kama utaki pia kuniona ofisini kwenu ni Sawa nitatuma barua ya kuachana kazi ili Nikuache uwe na amani
"Jamani, Mbona Unafika mbali sana kiasi hiko ? Mimi naitaji kuendelea kukuona naitaji uendelee Kuwa partner wangu please usiwe na hasira
kiasi hiko
"Frank unaondoka au nimwambie baba yangu kila kitu ?"
Hapo kidogo frank alishtuka sana kisha kWa
sauti ya utulivu akaniambia.
"Basi wacha Mimi niende, lakini natalajia kukuona tena ofisini Sawa"
"Ondoka Bwana"
Nilizungumza kisha kwa mwendo wa haraka na nikiwa na jazba nikaingia Ndani na kumuacha frank akinishangaa tu.
Frank aliniangalia kwa muda kisha akatabasamu na kuondoka zake
KWa upande wangu nilishika njia moja kwa moja na kwenda chumbani, nyleeeeh nilifika chumbani kwangu na kuanza kurukaruka kwa furaha kama zote, yaaani nilijikuta nikiwa na
raha ya kutosha kudadeki zangu, Sijui niwaambie kitu gani lakini nilikuwa Ninafuraha sana Tena sana......
"Kulikoni mwenzetu Mbona Kama umeshinda Jackpot?"
Aliniuliza dada yangu baada ya kuingia chumbani kwangu na kujikuta nikiwa na furaha isiyokifani.
"Yaaani hapa nasikia kama napaa vile, Yaani nahisi Kama namiliki dunia dada yangu
Nilimwarribia dada yangu kisha nikamkumbatia. "Kuna nini nawe sasa si uniambie"
"Ooooh God kumbe raha ndio ziko hivi, au niseme Kuwa sijawai kupata raha na Leo ndio Mara ya kwanza, eti dada yangu raha ndio ziko
kWa Namna hii au? Yaani hapa ata ukinipa misumari naweza nikatafuna ujue"
Dada yangu akaniangalia kwa muda kisha kwa hasira akaniambia
"Ebu Niache Kama utaku kuniambia furaha yako ni juu ya nini maana hapa nilipo Nina mawazo yangu ya kutosha
Haraka nikamuachia dada yangu na kumuangalia usoni maana Alizungumza akiwa serious sana ni wazi Kuwa kuna kitu kilikuwa kikimsumbua
"Kuna shida qani dada?" Nilimuuliza, swali langu lilionekana Kuwa zito
sana kwa dada yangu ambaye aliishia kuniangalia usoni kisha akanikumbatia kWa nguvu kabisa na kuangua kilic
"Kuna nini dada Mbona unanitisha
Nilimuuliza dada yangu nikiwa na wasiwasi wa hali ya juu.
"Nimeisha mimi, nimedhalilisha familia yangu mwenzio
"Unaniogopesha dada kuna nini kwani Umefukuzwa kazi au ? Kama ni kazi Mimi nitaongea na flora uje ufanye pale kazini kwetu"
"Sio hivyo, Anaya, Mimi ni mjamzito wa miezi miwili na baba Mtoto amekataa hii mimba,
amesema ili mimi na yeye tuendelee Kuwa na
mahusiano lazima nitoe unauzito, Anaya Mimi naogopa sana, lakini pia sitaki Kuwa single mama
Alizungumza dada yangu akiwa analia sana Tena kwa uchungu wa hali ya juu na hii ilionesha ni kiasi gani moyo wake una maumivu makali.
Kabla sijazungumza kitu chochote kile, gafla
mlango wa chumbani kwangu ukasukumwa na Kaka yetu mkubwa Abdull akaingia na kuuliza.
"Huyo mpuuzi mwenzio anapatikana pande gani
Yooooh kwanza Mimi na dada yangu tulishtuka sana na kubaki tukiangaliana tu, najua wengi
mtashangaa Kwanini tumekuwa waoga sana
lakini taratibu za Nyumbani kwetu ndio kitu ambacho kinatufanya sisi Kuwa na wasiwasi
"Kaka usiongee kwa sauti
Alizungumza dada akimtuliza kaka Abdull ambaye alikuwa na hasira sana kwa wakati huo.
"Weeeh chini nini, Yaani niongee kWa Sauti ya
chini kwa sababu ya nini? Hatutaki aibu kwenye familia Sawa 7 Huyo mpuuzi mwenzio atakubali hiyo mimba na atafata taratibu zote na Utakuwa
mke halali kwake"
Alizungumza kaka kisha akataka kutoka nje kwaajili ya kwenda kumwambia baba, lakini nikawai na kwenda kumzuia mlangoni.
"Kaka Mbona Kama hivyo jamani, kwanza si uzungumze na dada kwanza, si unaona Kuwa hayuko Sawa lakini
Hapo kidogo kaka alitulia na kumuangalia dada kisha kwa upole akamsogelea na kumkumbatia kWa Nguvu sana
Baada ya muda watatu sisi tukaweka kikao chetu na kuweka mambo Sawa kisha kila mtu akaenda kwenye shughuli zake.
Siku iliyofuata Kama kawaida nikaingia zangu ofisini nikiwa na shauku sana ya kuonana na frank, ila mapenzi nyleeeh Akiwa mbele yangu najifanya namlingia akiwa mbali sasa, Ka moyo kanabaki kanamuwaza tu
Niliingia ofisini na kukuta ofisi ikiwa kamya kabisa ni wazi Kuwa frank hakuwa amefika ofisini kwa wakati huo.
Basi kwa unyonge wa hali ya juu, nikasogea na kukaa kwenye meza yangu ambapo nilikutana na kadi nzuri sana ambayo moja kwa moja nilijua Kuwa imetoka kwa frank.
"Dear Anaya, samahani kwa kila kitu ambacho kimewai kutokea kati yetu, Nisamehe kWa
kujujengea mazingira ya Kuwa sikupendi ikiwa
moyo wangu ulikuwa ukitaabika kwaajili yako, nimegundua Kuwa uwezi kunisamehe hivyo nimeamua kwenda mbali na wewe, ubaki
salama nakupenda mno
Weeeeh kwanza nilinyanyuka kWa Jazba na kuanza kulalamika.
"Kwahiyo kukutania tu ndio umeamua kuondoka kabisa si ndio ? Frank nakupenda sana umeenda wapi?"
Haraka nikavuta simu yangu na kumpigia simu frank
Picha linaanza sasa simu ilisikika Ndani ya ofisi umo umo, na muda huo huo ikapokelewa.
"Hellow princess"
Ilikuwa ni sauti ya frank ambaye alinyanyuka akitokea kwenye uvungu wa meza yake ya kazi, shoga yenu nika..
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni