Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
13 Dec 2025
134 views
VYOTE NDANI GONGA94
NATAKA KUACHA KUJIUZA ILA NASHINDWA NAOMBA MSAADA WENU
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Shikamoo madam .Naitwa Janeth ni mama wa watoto wawili samahani kwa kuja inbox kwako bila ridhaa yako ila mimi nina changamoto ni mama ambae ninajiuza ili familia yangu ile,isome ,tulipe kodi na maisha mengi kwa ujumla yaende imefika muda nimekuwa mlevi kabisa wa ngono,sitamani kabisa kuacha ila naumia sana ninapoona mabinti zangu wanakuwa wakiniona mama yao najidharirisha,maana nina binti mkubwa kwasasa wa miaka 8 ameshaanza kupata ufahamu maana kuna wakati nawatoa nje usiku ili niingize mwanaume ndani mpaka nimalizane nae ndo warudi ndani hii kitu imekuwa ikinitesa sana.
Maana imefika muda naweza nikalala hata na wanaume saba kwa siku ili tu maisha yasonge mbele maana nina binti wa pili ambae ana changamoto ya sickle cell na ana miaka miwili yani nimekuwa mpumbavu sana mama angu, changamoto za maisha na kutengwa na familia ndo kunilifanya niingie huku natamani kuacha ila sijui nianzie wapi naomba walau ushauri au mtu wa saikolojia kama ataweza nisaidie nijitoe huku maana hii ishu inaninyima amani sana mama angu haswa ninapoona watoto wangu wanakua na mama yao ndo hivyo sina muelekeo wa maisha.
Kiukweli mtoto wangu wa pili simjui baba yake maana nilipata katika harakati za kujiuza ila binti yangu wa kwanza baba yake alifariki kwenye maandamo.Nitashukuru sana kama nitapata njia maana natamani sana kuacha ila nashindwa pia imenijenga kisaikolojia kuwa siwezi maisha bila kudanga hii inanikula sana ubongo na maisha yangu yote nayaendesha kwa kuutoa utu wangu na kuna wakati binti yangu mkubwa inabidi nimlaze nje kwenye kibaraza ili niingize wanaume kuna wakati nalala hata na wanaume watatu kwa mara moja.
Natamani siku moja na mimi nisimame nifanye biashara niwatunze watoto wangu ila pesa ninayopata kama ina laana naishia kula na kuna wakati mpaka kodi kwangu inakuwaga changamoto.
Mara nyingi napenda nyumbani kwasababu ile pesa ya guest wanakuwa wananilipa mwenyewe kwahiyo nakuwa naiokoa pesa ya guest pia usalama nishawahi kupigwa sana huko guest mpaka kuunguzwa na moto mguuni na pasi na mwanamke kisa mwanaume ila kwangu nahisigi usalama unakuwaga wa kutosha kwasababu ninapoishi naishi mpangaji peke yangu na kuna usalama wa kutosha na mama mwenye nyumba wangu si mfuatiliaji hajui hata nafanya kazi gani
Nisidanganye zaidi ya kumsomesha binti yangu wa darasa la tatu na kumtibia binti mwenye sickle cell hakuna mafanikio niliyofanya zaidi ya kula,kulipia kodi na kuhudumia watoto tu
Nimewaza biashara ila kila nikipambana nashindwa nahisi nikipata walau mwanasaikolojia akanitengeneza vizuri naweza nikasimama kama mama na kuachana na hii kazi haramu.
Haya wadau tuje tumsaidie mwenzetu avuke hapa.
Kitabu cha MAZUNGUMZO YA KIKE kinapatikana kwa 25,000/= tu.
Marm'z Relationship Hub 0710474782
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
This pic from Ishq is pure 90s madness and I love it ! You’ve got Ajay Devgn with his serious, intense vibe… Kajol looking all fiery and expressive… Juhi Chawla
with that cute bubbly energy… and Aamir Khan being his mischievous, romantic self. What a combo yaar! Ishq was not just...
Tangazo - MY Wangu season one, season two, season 3, season 4 and season 5 final
MY Wangu season one, season two, season 3, season 4 and season 5 final
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA
NATAKA KUACHA KUJIUZA ILA NASHINDWA NAOMBA MSAADA WENU
Shikamoo madam .Naitwa Janeth ni mama wa watoto wawili samahani kwa kuja inbox kwako bila ridhaa yako ila mimi nina changamoto ni mama ambae ninajiuza ili familia yangu ile,isome ,tulipe kodi na maisha mengi kwa ujumla yaende imefika muda nimekuwa mlevi kabisa wa ngono,sitamani kabisa kuacha ila naumia sana ninapoona mabinti zangu wanakuwa wakiniona mama yao najidharirisha,maana nina binti mkubwa kwasasa wa miaka 8 ameshaanza kupata ufahamu maana kuna wakati nawatoa nje usiku ili niingize mwanaume ndani mpaka nimalizane nae ndo warudi ndani hii kitu imekuwa ikinitesa sana.
Maana imefika muda naweza nikalala hata na wanaume saba kwa siku...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/nataka-kuacha-kujiuza-ila-nashindwa-naomba-msaada-wenu
Maoni