π‘ππ’π π¬π π ππππ π‘π π π¨π¨ππ π©ππ§π¨π ππ¨π *1 - - - - - - - 5* SEHEMU YA 1 MWANZO.......... "Basi ndo hivyo shoga angu. Yule bwana wangu mzungu amekuja yupo Zanzibar
"Wewe ujue unaongea kama vile umechanganyikiwa?"
"Na nimechanganyikiwa kweli shoga acha tu. Siamini kama naenda ulaya na mie ujue. Kimasihara masihara nasepa bongo hivyo"
"Wee Suzy si unaolewa jumamoss na mjeda khaaaa! Ulaya tena unafuata nini unaota wewe eeeeh!"
"Hivi mfano ndo wewe ndo mimi. Unaambiwa uchague moja, kuolewa au kwenda ulaya na huko unauhakika wa ndoa bia maana wazungu sio vigeugeu kama waafrika wakipenda wanapenda kweli. Wee ungechagua kipi hapo?" Suzy aliniuliza. Kabda ya kumjibu nilimtazama kwa sekunde kadhaa nilijua ni kiasi gani amedata.
"Ningechagua kuolewa" nilimjibu Suzy.
"Aiiiiih! Basi kaolewe wewe shoga badala yangu. Yaani kwanza nimefurahi umejoosha jibu haswaaa sema si unajua rafiki yangu kila mtu na machaguo yake. Nakuachia mjeda kiroho safi"
"Suzy unaongea nini mbona sikuelewi leo, kwani umekunywa pombe au. Ujue umebakisha siku mbili tu uolewe na Meck"
"Nimebadili maamuza na wala sijalewa mimi. Gonna nimebadili tu naamuzi nineona ni bola kwenda ulaya nikaolewe na mzungu kuliko kuolewa na Meck. Mwanaume mwenyewe kwanza ni pasua kichwa haswaaa! Si unajua tabia za wajeda lakini?"
"Lakini sidhani kama upo sahihi na hayo maamuzi yako, hivi unawezaje kusema umeghahiri kuolewa na bado siku mbili tu ndoa ipitr. Vipi kuhusu familia yako?"
"Mama anajua kila kitu yupo upande wangu"
"Amekubali?"
"Hawezi kunipinga chochote nikiamua umesahau kuwa mimi ndiyo naiendesha familia yangu kimaisha. Baba yangu ni mlevi kupindukia hajali chochote kuhusu familia, mie ndo nikadange watu familia ile. Sasa watanipingaje".
"Sikia Ginna!, tuongee sasa ishu serious". Nilitega vizuri masikio yangu kumsikiliza Suzy.
"Nataka wewe ndo uolewe badala yangu mimi, shoga angu na wewe upate bwana wa maana uachane na hao vinuka mkojo"
"Wee mtu leo hata sikuelewi unaongea habari gani. Yaani mimi niolewe na Meck badala yako. Wee Suzy upo timamu kweli au ndo umeanza kuchanganyikiwa mdogo mdogo kwanza inawezekana vipi bwana ako anioe mimi atakubali na anavyokupenda kama mpu.....mbavu.
"Wee niambie kama upo tayari kuolewa au upo tayari kufa masikini maana watu wengine mmezaliwa mkiwa na fungu la kukosa. Mateso mwanzo mwisho mpaka kifo"
"Umeanza kunikwaza sasa?"
"Sasa mtu unataka mwenyewe kuteseka na Hisia na bado maisha yakutese si kujitakia huko. Shoga angu katika maisha ya sasa kupata ni kuchagua ulitambue hili. Ukiwa mjinga mjinga magorofa utayaona tu kwa mbali ila hutowai kuyafikia wala kukanyaga ardhi yake"
Suzy ana maneno makali nyie acheni tu. Nikajisemea moyoni "ila ukweli unauma na mchungu haswaaa, huyu mb.....wa yupo sahihi kama nitachezea bahati basi nitakufa masikini.
"Shoga unawaza nini, eeeeh basi nakupa siku moja unipe Jibu kamili kama itashindikana nitafute mtu mwengine"
"Hivi Suzy upo serious kweli au unatania?"
"Wee unaona na hata repe la utani hapa. Ebu nitolee umasikini wako huko. Yaani niache pesa nje nje huko mambele kisa kuolewa bongo, bongo yenyewe majanga kibao, pesa ngumu kama jiwe kuu la pembeni".........nilibaki nacheka tu kwa maneno ya Suzyπππ.
Shoga angu huyu ni kweli sijui ana bahati maana kwa muonekano wake wala sio wa kuwapagawisha wanaume kabisa alafu ni mswahili mpaka mswahili tena na zaidi anamdomo yaani anaongea, anachamba, anashushua, haogopi mchawi wala polisi, wavuta bangi ndo mashaji zake balaa huko mtaani wanamuita kiboko yao.
Niliondoka nyumbani kwa kina Suzy nikiwa nimepewa masaa 24 yaani siku moja tu, nipeleke jibu kama nimekubali au laaah!
" Wee Regina, ebu toka humo ndani njoo unashangaa nini mboga yenyewe ndogo utakula ugali mkavu jirembe tu huko" mama alipaza sauti walipokuwa kibarazani wanakula kwa mtindo wa kisinia.
"Ameshiba huyo muache bhana mama unambembeleza wa nini, kwani hajaona tulivyokuwa tunatenga chakula, si ametupita hapa tunatenge akaenda chumbani" mdogo wangu Tinna alizungumza.
Na nikifanya masihara nitakula ugali mkavu kweli, ila aiiiiih bora nikubali tu kuolewa na huyo mjeda. Maisha gani haya ya kugombania mboga". Niliyasema nikatoka chumbani kuwai mboga kabda haijaishaπππ............
ITAENDELEA...........
SEHEMU YA 2
ENDELEA.......
Nijiwai mboga kabda haijaisha. Tuliendelea kula huku tunapiga story za hapa na pale.
"Hivi mfano mkisikia nimeolewa gafla tu bin vuu! Na tajiri si mtafurahi sana maana mtakuwa mnakula nyama humu ndani kila siku mpaka zitawakinai" nilijiongelesha.
"Mmmmh" Wote mama na wadogo zangu waliguna.
"Unaolewaje na tajiri na huyo sijui black boy, mvuta bangi wako unamuachia nani. Wewe kula ugali ushibe usishibe ukalale hizo ndoto zako za mchana usituletee hapa" mdogo wangu anayenifuatia aitwae magrety aliongea hayo.
"Kwaiyo mnavyonipinga inamaana mnayakubali haya maisha ya umasikini si ndiyo?"
"Wee Regina ebu bhana tuache tule kwanza au umeshiba wewe" Mama aliongea.
"Mama nilikwambia huyu ameshiba muache si unaona kaja kutukombea mboga tu hapa na story zake za kuakisi" Tinna alilalamika.
"Basi niwape taarifa tu kuwa kesho kutwa naolewa na mwanaume tayiri pesa sio shida zake. Na hizo nyama mtaendelea kuzisikia maana mshajikatia tamaa na maisha, subilini mzee masu mzee masu akiludi huko Singida awaletee uyoga maana ndo nyama yenu hiyo". Niliongea hayo wote waliangua kicheko hawakutaka hata kunisikiliza tena.
Kabda ya mboga kuisha nilinawa mikono huyo nikaingia ndani. Waliangua kicheko cha kufa mtu huku mama akiongea.
"Tulipokuwa tunakwambia usome uje ukomboe hata familia yako wewe ulituona sisi wajinga leo hii unaongelea utajiri gani. Komaaa na kupika vitumbua ujimpatie wa hazi yako. MUNGU mwenyewe anasema nakupa wa kufafana na wewe" Mama aliongea basi hao wadogo zangu mbavu hawanaπππ. Walichekaaaaaa mpaka wakapaliwa.
"Na nipo tayari kuolewa na huyo mjeda. Ngoja nitawashangaza hawa masikini jeuri na hawatoamini" niliongea hayo na muda huo huo nilinpigia Suzy.
"Eeeh niambie shoga angu?"
"Shoga nipo tayari na hiyo ndoa mie"
"Eeeeeh mambo si ndiyo haya bhana" Suzy alifurahi balaa. Basi tulipanga kesho yake tukutane kwaajili ya mipango.
"Weee! Unalala mpaka saivi unaumwa au?, wateja wako wamekufuata?" Mama alikuja kuniamsha chumbani majira ya saa moja kasoro asubuhi.
"Waambie leo vitumbua hakuna?"
"Hupiki?"
"Ndiyo, mama bhana nimechoka niache nipumzike mie. Kawaambia leo sijapika vitumbua"
"Ungebandika hata bango hapo nje ya mlango. Ndo nini kunisumbua mie, watu wanagonga mlango kama hawana akili nzuri"
"Kawafukuze na uwaambie kabisa kuanzia leo hapa hakuna vitumbua tena".
" Khaaaaa! wee Ginna wewe upo ndotoni au. Ebu amka amka ukae kwanza nisije kuwa naongea na mtu anayeota"
"Mama bhana nini lakini"
"Mji..nga wewe nimekwambia amka" Mama alifoka kwa sauti. Wadogo zangu nao waliamka maana tulikuwa tunalala wote chumba kimoja na kitanda kimoja.
"Kuna nini asubuhi asubuhi makelele tu na nyie khaaa!" Magrety alilalamika huku anajinyoosha kwa uchovu.
"Si huyu dada yenu anasema sijui hapiki tena vitumbua kuanzia leo"
"Sasa mama ndo iwe vita, makelele mpaka nyumba ya tatu huko wanasikia. Muache kama hataki kufanya kazi si maisha yake?" Tinna aliongea.
"Wee mpu....uzi nini. Unafikiria kama dada Yenu nae ataacha kufanya kazi nani atanisaidia kuwalisha. Hamjui hata kuleta unga wa ugali nyumbani nyie kazi yenu kununua mawigi ya ki shumileta tena na nguo za twende na wakati. Hamna huruma na mimi kabisa"
"Eeeeeh mama basi yaishe na wewe, hela zenyewe hatuna tutatoa nini sasa alafu mimi last born jamani" Tinna aliongea. Mama alimkata jicho.
"Mage kawaambie wateja vitumbua leo hakuna mpaka kesho ili watawanyie hapo nje"
"Si leo tu. Awaambie nimeacha kabisa kupika vitumbua. Wakatafute sehemu nyengine"
"Heeeeee!" Wadogo zangu walishangaa. Mama hakutaka kuzungumza chochote tena. Alitoka chumbani kwangu alienda kuwaambia wateja vitumbua hakuna.
Sms iliingia kwenye simu yangu kutoka kwa Susy.
"Saa nne asubuhi tukutane kwenye mgahawa wa mama papa pale tupate na supu ya mwisho mwisho shoga angu"
"Nilitabasamu tu baada ya kusoma ujumbe wa Suzy. Niliamka kitandani nikaanza kufanya kazi za home. Wadogo zangu wamelelewa kimayai hawajiwezi kwa kazi kabisa.
"Mama hawa wanao umewalea vibaya, leo hii mimi nipo hapa kesho sipo utaisoma namba nakwambia"
"Sasa mimi nifanyaje na watoto wenyewe ni wa bishi jamani, usinilahumu"
"Jiandae tu lolote linaweza kutokea" Niliyasema alafu nikaendelea kuosha vyombo...............
ITAENDELEA...........
SEHEMU YA 3
ENDELEA.........
Saa nne asubuhi tulikutana na Suzy kwenye mgahawa wa kishua wa mama papa. Tuliangizia supu ya kongoro na chapati.
"Kula jigalagaze leo shoga angu yaani kunywa supuuuuu weeee! Suuza hilo koo, tumbo,kongosho mpaka maini nataka hii siku iwe kumbukumbu nzuri sana kati yangu na wewe"
"Naona leo umeamua kujimaliza yaani wee Suzy wakunipa uhuru mimi wa kula nitakavyo na ulivyo mbahili mmmh"
"Ndo maana nakwambia hii siku itakuwa kumbukumbu nzuri kati yetu. Ujue kesho asubuhi naondoka?"
"Yaani nimekubali ila hata siamini ujue wee mb....wa"
"Hahahahaaaa! Maisha nishayapatia mwenzio"
"Kwakweli naona haya mie. Ila naogopa huyo mjeda mwenyewe umemwambia au?"
"Kumwambia kuhusu nini, huyu mjin.....ga hajui chochote na hatakiwi kujua kwa sasa mpaka pale mtakapofunga ndoa. Wee usiogope bhana, Meck hana shida na ni mpole sana sema ni silent Killer"
"Ukimaanisha ataniua au hiyo Silent Killer vipi mmmh"
"Hawezi kukuua na wewe unakubalije kufa kizembe tu mtoto wa uswahilini wewe acha kuzubaa, yaani Ginna umekaa kijinga jinga mpaka unaniboa ujue. Ndo maana unapata mabwana masikini wanazidi kuuchakaza usichana wako. Wewe ni mzuri haswaaa! Kama ungeutumia uzuri wako kama fulsa basi saivi ungekuwa mbali sana".
" heeee! Usianze kunisimanga na supu yako nitakususia. Niambie kusema huyo mjeda wako Silent Killer ndo una maana gani"
"Ususe hii supu ukafe na njaa, subutu uone kama utakuja kuipata tena kirahisi hivi. Namaanisha Meck ni ma...la....ya wa chini chini yaani anakula mademu kimya kimya so usiogope".
"Mmmmmh nipe moyo ila na mie yakinishinda nitakimbia hata kijijini kwetu huko singida"
Basi tuliendelea na mipango itakavyokuwa hiyo harusi. Suzy alinihakikishia mama yake atakuwa bega kwa bega na mimi na sio mama yake tu familia yake kwa ujumla.
Baada ya kunywa supu tulienda matembezi , hapo Suzy ananiambia ndo tunaagana mala ya mwisho mwisho hiyo kesho mie ndo bye bye.
"Nitakuachia laini zangu zote kesho kwaajili ya kuwasiliana na mjeda, mie nishasajili laini mpya".
"Ni sawa".
Tuliludi matembezi tukapitia tena kwa mama Papa majira ya saa moja usiku. Tulikula tena msosi wa maana.
" tufungie chips kuku, fanya kama kisinia cha elfu 30 tunaondoka navyo" Suzy alimwambia muhudumu. Nilibaki namshangaa tu.
"Nataka uwapelekee home kwenu"
"Heeeee!" Nilishangaa wazi wazi mpaka watu wa karibu nao walinishangaa pia.
"Wee leo umelogwa au" Nilimuuliza Suzy maana shoga angu huyo anasifika kwa ubahiri hata mchaga ana nafuuπππ.
"Ebu acha ushamba na wewe ona mpaka watu wanatushangaa". Nikatuliza komwe langu.
Nilifika nyumbani saa mbili usiku na mfuko mkononi. Hawakuamini kama nimewaletea chips za kula na kusasa pamoja na kuku mzima.
" Wee Ginna wewe hela ya kununua mazaga zaga yote haya umeitoa wai na leo haujapika vitumbua na najua huyo muhuni wako hawezi kukupa hata elfu 10 tu. Usije kuwa unataka kututoa kafara wee mtoto maana watoto wa sikuizi mmejawa na tamaa ya kutaka mambo makuwa ambayo hamna uwezo nayo"
"Bhana wee bi mkubwa tatizo unaongea sana, kama kula kama una njaa na kama umeshiba pia acha".
" kwanza kwa mazaga zaga haya tunashibaje hata kama nimeshiba nitakula mpaka nijinyee kikubwa viishe tu wee vitu vyenyewe hivi adimu humu ndani nibakishe nimuachie nani" Tinna aliongea.
"Kwanza mie hata akitaka kunitoa hiyo kafara na msosi huu anitoe tu lakini siwezi acha kula halooooo! Nikanawe mie niwai paja". Wadogo zangu hao ni chenga yaani uswahili umewaharibu sana".
Mage alienda kuchukua maji ya kunawa na akanawa huko huko ili awai paja πππ ila bahati haikuwa kwake. Alimkuta Tinna anamalizia paja la pili yaani alianza kula hata bila ya kunawaππππ.......
ITAENDELEA.............
SEHEMU YA 4
ENDELEA..........
Mage analudi na maji kwenye bakuli anamkuta Tinna anamalizia paja la pili. Ugomvi ukaibuka.
"Nyie gombaneni mkimaliza hamtakuta hata mfupa" mama aliongea. Kusikia hivyo waliacha kugombana wakaanza kula.
"Ila Regina unanishangaza ujue wee mtoto?"
"Na bado nitawashangaza sana mama wee subili utaona. Yajayo yanafurahisha. Mie nipo chumbani".
Nilienda chumbani niliwaacha wanakula kwa kufukuzana kama vile mashindano ya mbio.
"Tunakula tu na hatujui vimetola wapi?"
"Mie nashangaa mama umepagawa na hivi vitu, mbona ni vya kawaida sana hata mimi kwa kujibana vi pesa vyangu naweza kuwalisha kwa wiki mala moja" Mage aliongea.
"Mb....wa weee hununua hata mafuta ya kula ya mia tano kwa pesa yako hujawai unaongelea vitu vya elfu hamsini sijui huko utaweza. Tena nyamaza usinipandishe kisukari wee mtoto" Mama aliongea kwa hasira.
"Basi jamani yaishe eeeeeeh!. Dada Mage na wewe punguza mdomo" ukimya ulitaeala kila mmoja akawa busy kufakamia chips kuku.
Saa mbili asubuhi nilikuwa nyumbani kwa kina Suzy.
"Kesho ndoa Saa tisa mchana. Yaani bila mzungu wangu kesho ningeufunga huu mtaa nakwambia"
"Uliipania sana unanishangaza jinsi ulivyobadilika gafla.
Ebu subili kwanza. Mzungu wangu ananipigia hapa Video call. Baada ya kumaliza kuongea na mzungu wake alianza kuruka ruka.
" kulikoni?"
"Huwezi amini bwana mzungu ameninunulia iPhone 17 uwiiiii! nitakufa kwa raha mimi'
" watu na bahati zenu".
"Kwakweli watu na bahati zetu sura hata mbuzi anayo, ila shoga na wewe ndo bahati yako hapo kwa mjeda unatakiwa kucheza kama pere asikuache. Yaani akupende mpaka anisahau mimi. Japo sidhani kama anaweza kumpenda mwanamke mwengine tofauti na mimi?"
"Kwanini unasema hivyo au ulimpa limbwata?"
"Walaaaaa! uchawi na ushilikina ndo kitu siwezi kwenye mapenzi maana sio mambo ya kudumu. Hata wewe nakushauri usije ukamloga mwanaume ili akupende shoga utaula wa chuya nakwambia".
"Mjeda alinipendea shoo yangu kitandani nipo kila engo, mipinduko, misamba, beki, salalasi, komfuu πππ, niache kwanza sitaki kucheka mie"
"Aiseeee kumbe ndo unatumikaga vibaya hivyo haloooo! Bola kuolewa na maskini mwenzio mwenye utu. Ujue kuna style nyengine hata sijui tutamueleza nini sir God maana balaa tupu. Mie najua style iliyohalalishwa ni kifo cha mende tu" Niliongea hayo aiseee Suzy alicheka mpaka aliachia mashuzi π€£π€£π€£π€£.
"Ndo nini sasa. Inamaana naongea ujinga au?"
"Kuna muda huwa nahisi huna akili vizuri, yaani umekulia uswahilini ila umekaa kishamba zana Ginna" aliongea hayo alafu akaendelea kucheka.
"Basi tuachana na hayo maana tunapoelekea sio kabisa" Niliongea kwa makasiriko.
"Ndo hivyo shoga mipinduko ndo iliyompagawisha huyu bwana mjeda ndo maana nasema kwangu hachomoki muda wowote nitakaomtaka nampata bila kutumia nguvu" Suzy aliongea hayo kwa kujiamini sana.........
ITAENDELEA...........
SEHEMU YA 5
ENDELEA.........
"Watu hawaogopi zambi ya kubinuliwa binuliwa na kuchokonolewa kama samaki jamani mmmh" niliongea hayo moyoni huku namtazama Suzy.
Jioni ya siku hiyo nilimsindikiza Suzy kivukoni kwaajili ya safari yake ya Zanzibar kwa bwana mzungu. Alinisisitiza sana nisimuangushe na zaidi aliniachia pesa laki mbili.
Nililudi nyumbani baada ya kusalimiana na mama aliniuliza kuhusu biashara.
"Ndo umegoma kweli kuendelea na biashara?, maisha yameanza kuwa magumu na unajua kabisa wadogo wako hawana msaada wowote"
"Mtoto umleavyo nivyo akuavyo"Nilimjibu mama.
"Ni kweli wao sikuwalea kama wewe saivi ndo najua umuhimu wa kuwalea watoto kwa usawa. Usinilahumu mwanangu kwa hilo maana nilishakosea tayari". Siku hiyo mama aliongea kwa unyonge sana. Kitendo cha mimi kuacha kufanya biashara kilimuuliza sana.
"Sijui utajisikiaje baada ya kuyapokea majibu hayo kwa uhalisia japo nilishakwambia kabda ila na mimi nipo kwenye kujaribu bahati yangu" Niliongea hayo nilimuacha mama njia panda
"Una maana gani Regina".
" Shika hii pesa, ni laki mbili kamili. Hakikisha hii pesa unaitumia vizuri na itapendeza kama utaiongezea kwenye mtaji wako au kufikilia namna ya kufungua genge hapa nyumbani na sio kutembeza tena mtaani. Itumie vizuri hii pesa maana kwa sasa sina hela tena na sina uhakika wa kuipata pesa kilahisi"
Niliongea hayo kwa uchungu pasipo kutegemea nilianza kulia mbele ya mama.
"Shida nini binti yangu. Nisamehe mwanangu naelewa haya majukumu sio yako kabisa ila tutafanyaje sasa mwanangu bila kusaidiana na baba yako ni kama vile ametutelekeza anatupa pesa kwa kujisikia"
"Sina maana nalia kwasababu nimebeba majukumu yenu ila nalia je leo au kesho mimi sipo au nimepata shida kiafya maisha yatakuwaje hapa nyumban?. Nakupenda mama yangu na usije ukahisi kama nimewatenga au kuwatelekeza". Niliongea hayo huku nikiwa nalia πππ.
Kwa pamoja mimi na mama tulilia. Mage na Tinna walifika. Walishangaa kwanini tunalia.
" kuna msiba?" Mage aliuliza.
"Mb....wa nyie na endapo tukifa utakuwa machokora kabisa. Kutwa kuzurura tu mkiludi mnataka kula".
"Heee! Mama maneno gani haya looooh!" Tina aliongea.
"Hata sijui wamevulugwa na nini. Ebu tuwaache kama walivyo kwanza" Tinna na Mage waliingia chumbani.
Majira ya usiku tukiwa tunakula chakula huku. Siku hiyo tulikuwa kimya sana, kila mtu alikuwa anawaza lake kichwani. Nilivunja ukimya kwa kunzungumza.
"Kesho Suzy anaolewa"
"Naibariki ndoa yake wakadumu na mume wake" mama aliongea hayo.
"Hatutaenda kanisani lakini ukumbuni lazima tutinge. Tayari nishanunua wigi langu la laki mbili na kigauni changu weeeee! Mbona pambe tu" Tinna aliongea na Mage akadakia.
"Yaaani pambe haswaaaa! Kesho mambo lele leleeeee!" Nilikuwa nawatazama tu kwa zamu.
"Nasikia anaolewa na mwanajeshi tena captain kabisa?". Mama aliniuliza.
"Ndiyo mama"
"Mwenzio mjanja amepata mwanaume wa maana ila sasa wewe mwanangu ndo unaangaika na hawa vibaka wa mtaani wanakutia nuksi tu sijui hata utaolewa lini na sisi tucheze harusi tutunzwe jamani" mama aliongea hayo. Wala sikumjibu.
"Mama nae kwani hujui kama kuolewa ni majaaliwa alafu dada umri bado unamluhusu mbona ndo mwanza ana miaka 26 usimsimange bhana" Mage aliongea hayo.
"Wote nyie ndo wale wale. Nawaambia ukweli wala siwasimangi ila mtajijua wenyewe. Umri ukienda sana bila ndoa utaitwa pa....ka la bar, shauri zenu".
Wao wanaongea mie nawaza yangu. Niliona kama vile wananipigia makelele nilinawa nikainuka huyo chumbani.
"Kesho shoga ake anaolewa na simuone kuwa na heka heka yoyoye si ajabu hata nguo mpya hajanunua wala viatu. Kichwani ndo kama hivyo ana twende kilioni" Mage aliongea hayo wakaangua kicheko yeye na Tinna. Kwakuwa niliwasikia sikutaka kuwavungia nilisimama kwenye mlango wa chumbani alafu nikazungumza.
"Niangaike na nguo sijui maviatu na nywele ili iweje, wanaambia hamtoamini macho yenu kesho baada ya kuniona nipo ndani ya shela safi kabisa nikiwa nimependeza kama malaika". Niliyasema hayo nikiwa serious aiseee wote mpaka mama waliangua kicheko............
ITAENDELEA............
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni