*NTAKUSEMA KWA BABA UNANIUMIZA* *1-5* * *SEHEMU YA KWANZA* Naitwa Angel Deus๐, mini ni daddy's daughter, binti wa baba nipo mwenyew nimelelewa na baba tu bila mama
Amenifanya niamini kwenye ule memory wa (true love never die) , mhh kama unavyojuaa binti akilelewa na baba ni anadekezwaa mnoo yaani , mimi nadeka sana yaani baba yangu sio kwamba ana maisha mazuri ya kunipa magari ya kifahari , nyumba nzuri, simu za bei kali, skin care ya 500k hapana hawezi hilo ila naweza sema ni best dady on the world hajawahi tokeaa baba kama wakwangu na hata kaaa atokee mimi ndio nasema hiloo ๐ , baba yangu yupo radhi aumiee kwa ajili yangu na nisitamani cha mtu amenipa kila kitu kwenye maisha yangu hususani upendo wa kweli ๐, hichi kinafanya nizidishe guarantee nyingi kwa baba yangu na nimpe mauwa ya kumwaga yaani ๐, amehakikisha nasoma mpaka degree na nimepata kazi na leoo ndio siku yangu nzuri sana kuachana na ile ya jana ya kwenda kwenye interview, leoo nilikuwa naingiaa kazini yote hii ni baba alikuwa na rafiki mzee Michael ambe ndio kama connection hii ya pale kazini naenda kwenye kampuni kubwa ya uzaaji ,usamabazaji, wa bidhaa mbali mbali ndani na nje ya nchi inaenda kwa jina la MIRACLES COMPANY
"Malaika" baba alikuwa ananiita huwa anapenda kuniita hivyo coz ndio tafsiri ya jina langu "baba nakuja namaliziaa hapa " nilimjibu huwa najiandaa chap chap naweza sema sipo kama wale wadada wanaojiandaaga masaa matatu hapana mimi huwa najiandaa mapema sana ni dakika tu na kitu kingine huwa sina mambo ya kujiremba remba kama wadada wengine pia mimi nakuwaga nachekesha sanaa muda mwingine nahisi ni kwasababu pia nimelelewa na mwanaume , basi nilijiandaa nikatoka nilipendeza na suti yangu ilikiwa pambe ๐, ilijuaa kunikaa jamani mhh na vile nina sura nzuri hata bila make up nakonekana mzuri plus na dimpos nazidi kuonekana mzuri hasa nikicheka na vile nina cheko zuri saaa jaman ๐
Nilifika officine na Toyo yangu iliyonileta , jamani ni bonge la jengoo yaani pazurii nyiee mhh , pazuri sana yaani nilifika mpaka reception nikajielezeaa walinipa kitambulisho changu na kunielekeza officine mwangu pia , na sehemu ya kusain kama nimefika nilisain nikaelekeaa officine kwangu mhh na kwenyew ni pazuri nilifika nikakaa nilikuta kuna laptop ๐ป mezani coz maelekezo yote nilikuwa nishapewa jana niliendeleaa kufanya kazi yangu kama nilivyotakiwa kufanya mwanzo ,
Nilikiwa nimekaa mwenyew akaingiaa mdada mmoja anatembea kwa maringoo kweli means cat walk ๐ถโโ๏ธ wadada nao hapana ๐, nilikuwa nipo naimba nyimbo yanagu ya west life sole dad naipenda sana , cha ajabu alikuja tu na kikombe cha kawaha akanimwagiaa kwenye karatasi zangu "ooh sorry " afu akaanza kujichekesha kama chzii nilikasirika sana ila cha ajabu nikaanza kutoka machozi sasa
Itaendelea .....๐ฅ
NTAKUSEMA KWA BABA UNANIUMIZA
Ep 02
"Hee baby gal mbona unaliaa shida nini ni bahati mbaya ujuee๐" alikuwa anaongea kwa kebehi mimi nilizidi kukerekwa kwakweli mimi sipendi mtu anaejishauaa mimi "okay I wanna tell you kwamba umeingia officine hujareport kwangu hivi unajua kuwa wewe ni mfanyakazi mpya hapa?" Nilimtizama tu alikuwa ananikeraa hajui tuu " okay hii ni adhabu yako hakikisha mpkaa muda wa lunch hizo karatasi ushaziandaa upyaa sawa madam?" Nilimtizama kwa hasira ni vile hajuii tuu mimi anavyonikeraa jamani "okay madam usinitizame mimi ndie executive manager hapa okay have a nice day bye bye ๐ " aliondoka jamani , mimi niandaee wakati hata sielewi zilikuwa zinahusu nini jamani ndio kwanza nimezikuta juu ya meza yangu ujuee mimi nilikuwa najuaa uonevu upo shule tu mhh hadi kwenye kazi , nilijikuta naliaa mimi kama mtoto, sio kwamba ndio mara ya kwanza mimi nimedeka sana kitu kidogo tu naweza lia mimi kama sitokuja nilie tena "mimi nikirudi nyumbani ntamsemea kwa baba huyu , baba yangu ana nguvu atampiga" ujuee ๐๐ nachekesha sometimes mara nyingi mimi huwa kama mtoto ambae hero wangu ni baba yangu nina utoto mwingi sana mimi jamani na sijui nitakuja kukua lini mimi duuh, yote hii si unajua ukilelewa na baba au kaka unavyodeka nyiee ๐ , nadeka sana mimi hadi kwenye mambo ya serious mimi nadeka
Nilijitahidi mpaka nikajuaa zilikuwa zinahusu nini tena baada ya kumuuliza mfanyakazi mwingine anaitwa Mary aliniambiaa ilikiwa inahusu nini na ni inabidi after lunch ipelekwe kwa boss , aliniambia pia yule mdada ndio ni executive manager ila anajishaua sana anaitwa Suzy nilijikuta nampenda sana huyu binti wanamuitaa Mary akawa ndio kashakuwa rafiki yangu japo sinaga tabia za kuwa na marafiki maan baba yangu huwa anasema marafiki wengi mwisho wa siku hugeuka maadui hasa ukioata mafanikio niliibeba kauli ya baba yangu maan siwezi jua mkweli ni yupi na ambae atakuwa adui yangu nikifanikiwa ni nani piaa , nilikubali tu awe rafiki yangu kishingo upande hivyo hivyo yaani maan alinisaidia
Baada ya lunch nilizikusanya karatasi mpya nilizokuwa nimeshazichapa na kuzipeleka mpKa kwa boss nilikuwa sijui nilielekezwa nikaenda mpaka pale officine kwa boss nilipiga hodi nikakaribishwa huyu boss mzuri mjuee mhh sijui kwanini ila ni mzurii sana jamani ๐, afu na yeye anamadimpoo hajaongea tu lakini yanaonekana jamani ana sura ya kitoto kuliko mimi ambae nimejidekeza mhh wakak wengine kama wameshushwa jamn
"Okay then hii ndio kazi yako ya kwanza madam , ila mbona umechelewa dakika kama saba hivi maan muda wa lunch umeisha ni kama nusu sasa inaonekana mzembe sana wewe Angel" alisema boss sikuuliza kwanini labda kajua jina ni kwamba taarifa zote huwa anazipata za wafanyakazi na mambo yanayojiri officine "haya nijibu kwanini umechelewa" ujue anaongea kitoto nyiee kunizidi
"Hamna boss ujue yule mdada alikuja officine akanimwagia chai kwenye karatasi etty ni adhabu yangu kwanini nilivyofika sikwenda kwake , hapo mwenyew nimejitahidi sana kuwahisha hyo kazi mana kanitishia hadi kunifukuza kazi ujue boss wewe muadhibu tu haina cha nini wala ni kweli unaona ni sawa kutishiwa?" Niliongea kwamadeko kweli kama vile namwambia baba yangu hapo na uongo juu nimeongeza ila mimi nahuzunisha, boss ikuwa ananitolea macho huyu ananishangaa
"Wewe hiyo ndio sauti yako! ๐ฒ" Aliuliza katoa macho balaa
Itaendelea....๐ฅ
NTAKUSEMA KWA BABA UNANIUMIZA
Ep 03
"Enhee ndio sauti yangu " nilimjibu ila bado nilikuwa nadeka kama mtoto si unajua mtoto akiwa anastasia anavyokuwa anaongea eeh "hhhh inafurahisha sana ujue so hata mbele za watu huwa unaongea hivyoo?" Nilimtizama nikatabasamu afu madimple yangu yakatoke "wow you look like mee also I have dimples ๐" alitabasamu nilitamani kucheka mimi na huyu ni kma tunafanana akili yani wote machizi "okay kwahyo unasema kuwa hujapata lunch zcoz ulikiwa unandaa kazi yangu si ndio ?" Nilimtizama nikatikisa kichwa kwa kuashiria kukubali ni ukwli "wonderful tunaweza tukaenda kuhave lunch wote at least ntapata company leo" nilimtizama tu "hapana nikila tofautu na officine baba yangu hatopenda" alinitizama tu akafungua maji akanywa kwanza afuu akaendelea kunitizama nyie huyu mjue hadi tazama yake ya kitoto, sura yake ya kitoti anavyoongea sasa ndio usiseme mtoto mtupu yaani mhhh ๐ ni kazuri kama wale watoto wakihindi ninavyokuwaga nawangaliaa kwenye movie yani "okay thanks kwani baba yako atajua hili?" Aliniuliza nilitabasmu "hapana ila nitamwambiaa kwasababu kila kitu ntamuhadithia atachukia najua na mimi sitaki akasirike zaidi" niliongea huku napandisha mabega na macho kama katoto ๐ alinitizama "mhh kwa muonekano wewe ni mkubwa ila una akili za kitoto sana yaani , unaonekana umedeka sana" mhh huyu boss alionekana mchangamfu sana nilifurahi kukutan na boss kama huyu ma'am nilikuwa najua ntakutana na boss hadi kukaa kwenye office ๐ฌ dakika tatu unaogipa yaani boss hachekeshi ila huyu kabla ya kuongeaa tu unatabasamu tu nilijisikia amni mno "ila ni sawa unaweza kwennda kama unaona hauko comfort , sana ila nimependa sana unavyoongea asante by the way naitwa Johnson "aliongea akiachiaa tabasamu Pana lenye kuonesha kufurahiaa kweli nilivyookuwa naongea na mimi kiujumla
Nilitoka officine ila nilifika njiani nikazuiliwa na yule executive manager Suzy "Hey kwa boss unaendaje moja kwa moja mimi pekee ndio naruhusiwa kwenda kwa boss sawa binti?" Nilimtizama sikuwa na jibu la kumpa mimi kubishana siwezi hata "okay last warning โ ๏ธ nisikuone tena unaenda kwa boss office nzima huwa nafika kw boss mimi peke yangu umenielewa hapo madam Angel , mhh usijikute malaika mbele za watu okay umalaika ni kwenu๐คจ " nilimtizama tu nikajuaa huyu ana hasira zake binafsi na mimi nikaachana nae nikaondoka maan baba alinambia wanawake tunaweza kumchukiaa mtu bila sababu nilijua hivyoo , nikaachana nae mimi nimekaa kitoto ila sio kila idara
Muda wa kwenda nyumbani uliwadia sasa nilienda kupanda toyo hadi nyumbani nilifika nikatuliaa zangu nilimkuta baba " enhee binti yangu vipi kuhusu kazi imeendaje endaje mwanangu?" Nilimtizama nikamkumbatia nikamuhadithia vyote "mhh binti yangu asa hivi wewe ni mkubwa kuna mengi utapitiaa sio kila siku ntakuwepo kuna muda utahitaji kuwa na maisha yako kuanzisha familia na mengine mengi sana utahitaji kuwa nayo nakuomba tu usiwe mnyonge nakupenda sana binti yangu wewe ni wa pekee kuliko kila kitu , ila tafadhari maneneo ya watu yasikuvunje imani kabisa sawa binti yangu I know you are the best ๐ unaweza kumshinda huyo haya njoo unikumbatie baba yako mwisho wa siku uachie tabasamu nimemisi madimpo yako" nilimkumbatia baba yangu huku natabasamu
Itaendelea.....๐ฅ
NTAKUSEMA KWA BABA UNANIUMIZA
Ep 04
Siku mpya ilifika sasa nilifurahi niliagana na baba yangu aliendelea kunipa maneno ya ushindi na ya kishujaa ili kunijenga na niliondoka nikaelekea kazini ila leo baada ya kusaini nilinyooka moja kwa moja mpaka kwa Suzy nako nikarepot kama nimefika officine nikaondoka zangu kuelekea kwenye office yangu
Nilikuwa nipo busy na kazi maan ni maisha yangu ila kiukweli nilikuwa siwazi kumuacha baba yangu siku moja nakwenda kuanza maisha yangu binafsi labda peke yangu ila nilikiwa sina jinsi zaidi ya kutafuta mimi nilikuwa nafanya kazi kwa kumfurahisha baba yangu ila sikuwahi kuwaza ety nafanya kwa ajili ya maisha yangu binafsi exactly hapana kwakweli nisiwe mdanganyifu nikaja kupata dhambi za buree miee wa watu , nikiwa mwemyewe alikuja boss officne mwangu "okay madam jana ulikataa offer yangu ila mimi leo nataka useme tunaenda wapi labda unapotaka wewe" nilimjibu tu "mhh siwezi kutoka na wewe labda mpaka niongee na baba" aliniangalia "hapana huhitaji ruhusa kwa baba yako naongea kama boss wako hapa na huu ni muda wa kazi fanya kuinuka ila nimekupa offer unipeleke sehemu ya kipekee ambayo wewe unajua nitafurhi kwasabau sina muda mwingi nitaondoka kufatilia mzigo huko Dubai tuliuagiza sasa umekwama naomba fanya hivyoo ni amri " nilikuwa sina jinsi zaidi ya kuinuka tu niliinuka tu "ila unapendeza wewe ni wa kitofauti na wengine haupaki make up kama wadada baadhi yao ila ni mzuri bado" nilimuangaliaa tu sikumjibu maan nilijisikia aibuu ni kama alikuwa ananisifiaa sana mimi niliona aibu kusifiwa na mkaka jamani ๐ค , tulitoka mapaka parking akachukua gari tukapanda jamani gari lake zuri huyu mkaka jamaji kama la kike linanukiaa mhh , sijui ni aina gani nisiwe muongo sijui aina za magari kwakwel
Niliamuaa kumpeleka sehemu za kuchovya na kwasababu alisema mimi ndio nichague niliona hapo kutamfurahisha jamani nimempeleka mshua uswahili duuuh , ila sasa sijui sehemu zingine "samahani kama hujapapenda ila ni pazuri kw apande wangu nahsi utafurahi" alibaki kasimama ananishangaa tu ,na kutoa macho mimi nilichukuaa bakuli langu la pili pili na lingine la kachori na pweza nikaw nakula jamani napendaa duuh hapa naongea mate yashajaa mdomoni ๐ alikuwa bado ananishangaa tu nilifata nikampa aonjee jamani si ndio akaonegewa mhh alikula kama 30 hivi na anavyokula pilipili kama muhindi vile jamani ๐, anaonekana kufurahi mnoo , tulimaliza hapo tukaamua kuondoka kwenye gari alinambia "nimefurahi sana kuliko nilivyodhani nataka nikirudi safarini tuje wote tukule tena pweza ๐" alinikonyeza nilijisikiaa haya mimi mhh nikainama chini nikatabasamu tuu tukafika officine alinambia aatondoka na Suzy cozy ndio executive manager
Ila kufika officine Suzy alisema yeye hayupo sawa na kapendekeza mmi niondoke na boss nilijua kwanini aliongeaa maan tu fika mimi ni mshamba na sijawahi panda ndege ni nitaogopa ni kama alikuwa ananikomoa vile mimi nilikuw na wasi wasi huo mndege uje ulipuke ila ndio ilikiwa tamko la officine "okay jindae kesho kutwa safari , najuaa unaogopa kuhusu kusafir na ndege upo sahihi ila ushamba lazima utoke safari njema mh mimi sipo saw " alisem mbele ya watu mimi sikupenda wala sikufurahishwa na hii hali japo ni kweli nilikuw nina wasi wasi sana na hii safari sijawahi panda ndege kabisa ila nilikubali tu na muda wa kwenda nyumbani ulipofika nilienda nyumbani
Itaendelea.... ๐ฅ
NTAKUSEMA KWA BABA UNANIUMIZA
Ep 05
Nlifika nyumbani nikamuelezea baba yangu kila kitu kinachoendeleea officine baba alifurahi nilishngaa "baba mimi nina wasi wasi sana ๐ baba sijawahi kusafiri na ndege baba kwanza nasikia kuna uwezekano wa ndege kulipuka mimi naogopa sana ujuee " baba alinishika mikono na kunambiaa "binti yangu usijali naelewa hiloo una wasi wasi sana mrembo wangu ila baba yako ni anakuombea ufike salama na uhakika utafika salama naamini hiloo kipenzi changu sawa" nilikubali tu ila kwa shingo upande, ila hizi siku mbili kabla ya safari nilikuwa mlokole ghafla wakati mimi sio pigo zangu kabisa yaani mhh baba alikuwa anaungana na mimi katika maombi ila inachekesha ukifikiria safari imenifanya nionekane kuwa mchaMungu jamani hhh , pia nilikuwa siendi kazini kwasababu nilikuwa nimepewa siku za kujianda
Siku ya safari ilifika nikaenda mpaka Airport baba alinisindikiza tu nilifika kwa usalama na nilimkuta boss na gari lake pia alikuwa ananisubiri "umechelewa kidogo ungemuona mama yangu ๐" nilimtizama tu sikuwa na amani moyoni alisalimiana na baba mwisho tukapanda ndege haoo tukaondoka ila sasa humoo kwenye ndege nilienda namshikiliaa Boss njia nzima yaani , hadi nikajikuta namuadithia kila kitu kuw mimi nimelelewa na baba tu na sitamani kumuacha coz atabaki mwenyewe alikuwa ananicheka huku ananipa moyoo tulifika mpaka Dubai sehemu moja hivi panaitwa BurjKhalifa nyie ni pazuri mhh nachoka mee jamani tulichukua hotel
Ila palivyo pazuri sikutaka kupumzika hata nilitaka kula bata tu nikapige picha ๐ธ na nini nirekodi alinambia tunaweza kwenda keshoo baada ya kutoka kufatiliaa hiloo jambo lililotuleta , nilikataa alinambia ni amri nilikubaliana na hiloo akaenda chumbani kwake na mimi nikaelekea chumbani kwangu ila kuna mtu akabisha hodii chumbani kwangu ilikuwa ni mida ya usiku tayari nikafunguaa mlango nikijua ni boss nilichukua nguoo nikaweka juu ya night dress hee cha ajabu alikuwa mtu mwanaumee akaingiaa ndani akaanza kupaaangaliaa angalia mimi sasa akili zangu zikanituma ni kibaka maan ni nchi za watu sijui sheria zaoo niliogopa nyiee nikatoka nakimbiaa akawa ananiita hapo sikujali ni nani nilinyooka moja kwa moja chumba cha boss hakikuwa kimefungwa nikajikuta naenda kumkumbatia hakuwa amelala pia
"Naogopa naogopa kuna mtu chumbani kwangu" Kama kawaida yangu huwa naongea kitoto "Miss ni mimi ndio niliyomtuma aje chumbani kwako kuangalia usalama maan cctv ya kule ni mbovu sema ni hakujielezeaa samahani ujuee kama umeogopa" nilikuwa bado nimemkumbatiaa boss kwa uogaa nilijikuta napata uoga tu nilimkumbatia bila hata kujishtukiaa
Akaniinuaa akanitizama akaanza kunisogeleaa "boss unataka kufanya nini" wee halo utoto uiondoka kabisa yaani , "nakutoa wasi wasi" aliongeaa huku pumzi zetu zikiwa zimekutana jamani niliogopa nilitetemeka kuna kitu nilihisi mimi wa watu alinisogeleaa akaanza kunipa juicee , uwii sijui nini kimenituma kuja huku , alikuwa ananipa juice vizuri ila mhhh afu analips laini huyu ๐ , hiki kulinifanya niendelee kuganda kwenye ๐ ๐ lips zake
Itaendelea..... ๐ฅ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni