Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
09 Dec 2025
143 views
VYOTE NDANI GONGA94
Sophia (Urvashi Sharma) binti anayeendesha maisha yake Goa
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Sophia (Urvashi Sharma) binti anayeendesha maisha yake Goa alifuatiliwa na kushambuliwa na mbakaji aliyeitwa Rakesh. Baadaye anaamua kuhamisha makazi yake Dubai anapanga nyumba ya tajiri aliyeitwa Karan Oberoi (Bobby Deol). Miezi sita baadaye Karan anafikisha ombi la kutaka kumuoa na binti analikubali.
Muda mfupi kabla ya ndoa Sophia anakutana na mwigizaji anayejitafuta anayeitwa Vikram 'Vicky' Malhotra (Akshay Khanna) anavutiwa naye sana ila anaamua kuendelea na mpango wake wa ndoa. ila alikuja kubadilika akiwa madhabauni alipoamua kumkataa Karan na kumdhalilisha vibaya kisha akaenda zake kwa Vicky. Jambo lile lilipelekea Karan kuumia na kuchukua uamuzi wa kujiua.
Sophia alipokuja kujua alijuta sana na alijiona wazi yeye ndiyo chanzo cha kifo chake. Baadaye inakuja kujulikana Vicky ndiyo chanzo, Alipewa nafasi na mwongoza filamu aliyeitwa Rohit Shroff, akitakiwa kuigiza filamu ya kuhusu maisha yake. Akatakiwa aingie kwenye maisha ya Sophia. Binti aliwaka sana na kumwambia ampigie huyo Rohit aje hapo muda huo, naye akatii na kumpigia kumwita. Bwana wee Rohit anawasili hapo na inajulikana kumbe yule Karan ni Rohit na hakufa.
Inakuja kujulikana kumbe Karan au Rohit alitaka kupiga pesa akaamua kutengeneza filamh kuhusu maisha ya Sophia na akamwajiri Vicky aingie kwenye maisha yake wawe wapenzi. Baadaye akaja kuunda tukio feki la kifo chake likiwa ni sehemu ya filamu na si kweli.
Kibaya zaidi Sophia kuna siku alipewa karatasi asaini akajua nu mambo yao ya ndoa, kumbe alisainishwa mkataba wa filamh hawezi kushtaki kwani kuna saini yake. Humo ndani walipoishi aliwafungia kamera, karekodi kila kitu wakibanjuka. Akawatishia watulie kama hawataki video zao zivuje mitandaoni wawe mastaa wa filamu ya ngono. Wakaishia kuwa wapole waache filamu itoke.
Miezi mitatu baadaye filamu ikazinduliwa, Karan alipanga siku hiyo ya uzinduzi kuwepo na tukio bandia la yeye kupigwa risasi kuongeza mvuto zaidi. Basi watu wawili katika kundi la utayarishaji wakaamua kuwajaza upepo Vicky na Sophia wasikubali aliwatumia. Wakachukua bastola zilizoandaliwa kwa ajili ya tukio wakamtungua Karan.
Kumbe bunduki zina risasi halisi si bandia Karan akaumizwa vibaya na baadaye alijeruhiwa vibaya akapelekwa hospitali. Janga lote likawa kwa watayarishaji tukio lile, huku Vicky akiachiwa kuonekana hana kosa lolote. Akaenda hospitali alipopelekwa Karana akamkuta Sophia ambaye alimpa habari ya kufariki Karan.
Kumbe aliyebadilisha zile bastola kusudi ni Sophia na mpango waliufanya na Karan, ushahidi ukawaangukia wale ambao walichochoea wakafungwa. Sophia akachukua mali za Karan, Vicky akawa mwigizaji maarufu kwani hiyo filamu iliweka rekodi yake sokoni..
Ni NAQAAB yaani KINYAGO, Bobby alipoamua kufanya mchezo mchafu maisha ya watu. Matokeo filamu iliuza na hakunufaika na chochote.
#Mambosreview
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
SHAMIRA sehemu ya 34&35
Mwandishi; lissa wa huru media Basi nikajiiinua taratibu tukaingia bafuni. Mwanaume akanikumbatia uku tunaoga. Aseee uy...
Sophia (Urvashi Sharma) binti anayeendesha maisha yake Goa
Sophia (Urvashi Sharma) binti anayeendesha maisha yake Goa alifuatiliwa na kushambuliwa na mbakaji aliyeitwa Rakesh. Baadaye anaamua kuhamisha makazi yake Dubai anapanga nyumba ya tajiri aliyeitwa Karan Oberoi (Bobby Deol). Miezi sita baadaye Karan anafikisha ombi la kutaka kumuoa na binti analikubali.
Muda mfupi kabla ya ndoa Sophia anakutana na mwigizaji anayejitafuta anayeitwa Vikram 'Vicky' Malhotra (Akshay Khanna) anavutiwa naye sana ila anaamua kuendelea na mpango wake wa ndoa. ila alikuja kubadilika akiwa madhabauni alipoamua kumkataa Karan na kumdhalilisha vibaya kisha akaenda zake kwa Vicky. Jambo lile lilipelekea Karan kuumia na kuchukua uamuzi wa kujiua. ...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/sophia-urvashi-sharma-binti-anayeendesha-maisha-yake-goa
Maoni