*MENEJA KAJICHANGANYA* Sehemu 1 Mimi naitwa Conrad maarufu kama Cony
Kwa muda wa miaka mitatu sasa naishi Bagamoyo baada ya kuhamia kutoka mkoani..
Ni mfanyakazi wa kiwanda kimoja huku bagamoyo nikiwa kama fundi wa mitambo na mashine za kiwanda...
Mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya hali ngumu sokoni na mzigo mkubwa wa madeni ya kodi na tozo mbalimbali alizokutana nazo boss wangu basi alijikuta akifunga kiwanda chetu alichokuwa amefungua huku bagamoyo tangu 2021..
kiwanda kilikuwa ni cha kuzalisha vifungashio vya bidhaa tofauti tofauti kama chupa, makopo na mifuko ya plastiki...
Kwa elimu yangu ya ufundi mitambo niliyoipata veta basi nilibahatika kupata ajira kama fundi mitambo pale kiwandani tangu kiwanda kinaanza pale..
Nilikuwa napata mshahara mzuri na posho za hapa na pale zilizonipa ujasiri mjini na kuamua kupanga nyumba eneo zuri kidogo ambako walipanga pia wafanyakazi wa taasisi kubwa kubwa kama walimu, benki na halmashauri...
Hili wazo nililipata kwa boss wangu siku moja kwenye story nae alinishauri nisipende kuishi uswazi sana ili nisibaki na mtazamo kuwa maisha ni marahisi sana au magumu sana..
Basi katika kuishi pale nilijikuta nikipata marafiki wa hadhi ya juu na Mimi nikapata morali ya kujituma kazini kwangu ili kipato kiongezeke niweze kuendana na rafiki zangu..
Mdogo mdogo niliongeza bidii ofisini na nilianza kuaminika nikiwa nabeba majukumu makubwa ya kiwanda na kupada cheo hadi kuwa fundi mkuu wa kiwanda..
Boss aliniamini na kunipenda sana, basi nikatoka kwenye kuvaa ovaroli hadi kwenda ofisini na tai shingoni..
Kipato kilipanda na nikabadili chumba kutoka chumba kimoja nikahamia chumba na sebule nikaacha kwenda na bus la kiwanda nikanunua pikipiki kali ya kutembelea..
Basi mashine zote za kiwanda nikawa nazijua nje ndani kinagaubaga na kufanya kuwa mfanyakazi mwenye umuhimu sana ofisini.. boss wangu akawa ananitumia kila anapotaka kuagiza mashine zake tofauti tofauti kwa ajili ya kiwanda kile na viwanda vyake vingine alivyonavyo maeneo mengine..
Nikaanza kuwa bize sana na kweli nikawa sionekani mtaani kwangu..
Natoka mapema narudi jioni sana niko hoi au nimeshawaka basi naingia kulala tu moja kwa moja..
Mazoea na majirani ikawa sina tena kiviile..
Basi kwa kipindi cha kama miezi nane nikiwa kama fundi mkuu na kiwanda kinafanya vizuri sana basi pakatokea changamoto kadhaa kwa boss wangu.. nadhani alipishana na baadhi ya wanasiasa waliokuwa na ushawishi serikalini na hapo ndio changamoto zikaanza kwa kiwanda chetu cha bagamoyo...
Sokoni pakawa pagumu, Kodi kila mara zinaongezeka mara tozo za mazingira na mambo mengine mengi...
Hiyo hali iliendelea kama miezi kadhaa mbele hivi hadi pale boss alipokuja na uamuzi wa kufunga kiwanda kwanza..
Daah ilikuwa ni uamuzi mgumu sana kwa kila mmoja wetu kwenye kiwanda kuanzia kwa boss mpaka kwa mfagiaji wa ofisi..
Hali ilikuwa ngumu sana kwani tulikuwa kama wafanyakazi waajiriwa kama 130 hivi kwa ujumla..
Basi boss aliitisha mkutano wa pamoja akatangaza na kutuambia kila mmoja apitie kwa meneja mkuu achukuwe barua na malipo yetu yataingizwa kwenye account zetu ndani ya siku Saba..
Basi mmoja baada ya mwingine tukafuata utaratibu kwenda kwa meneja aliyekuwa mdada mmoja wa rika la kati kama miaka 32 hivi............
Sehemu 2
Basi tulikuwa tunaitwa kwa vitengo vyetu yaani.. watu wa utawala, masoko, manunuzi na usafirishaji, ufundi, usalama na chakula..
Basi kila kitengo kilienda kwa wakati wake huku wakiongozwa na Mkuu wa kitengo husika..
Mimi na timu yangu ya mafundi tulikuwa tumetulia tu kwani kwa aina ya kitengo chetu basi tulikuwa tuna siku tatu za kuendelea kufanya kazi pale kwani tulipaswa kufungua mashine zote na kuhakikisha zinapelekwa kwenye karakana za boss zilizoko maeneo ya gongolamboto huko...
Kwa kuwa ile siku ilikuwa tayari ina msongamano wa watu pale ofisini hatukuweza kufanya kazi yoyote zaidi ya kupiga story na kucheza draft tu na washkaji..
kimsingi sisi tulionekana hatujaumizwa sana na maamuzi ya boss kwani wengi wetu tulikuwa tuna uhakika wa kupata kazi maeneo mengine lakini pia baadhi yetu walikuwa na vijiwe vya kazi za karakana na ufundi..
Basi tulikaa pale hadi mchana wa saa tisa hivi wadau wakaanza kuhoji kuhusu msosi wa siku hiyo maana hadi wapishi walishafunga kazi kwa maelekezo ya boss..
Basi nikiwa kama fundi mkuu niliwajibika kwenda kwa meneja kuuliza kuhusu hilo....
Kwa muda mrefu kama dakika 20 nilijikuta nagonga mlango wa meneja bila majibu na wakati nina uhakika yumo ndani...
Kwa ghadhabu ambayo sikuitarajia nilishangaa kumuona akitoka ndani na kipochi chake mkononi na kusema MUDA WANGU WA KAZI UMEKWISHA NAONDOKA, TUTAENDELEA KESHO...
Nilijaribu kutaka kumueleza shida yangu ni ishu ya chakula na wala sio barua alijibu tena bila kuniangalia FUNDI NIMESEMA TUONANE KESHO....
Nikabaki natoa macho bila majibu ila akili ilicheza haraka nimpigie boss moja kwa moja........
Kweli boss akadaka waya chap ...
Boss: Niambie Cony mmeanza kufungua za upande gani....
Daah.. nikaishiwa pozi kidogo kwanza... nikamwambia... Ndio watu wanaishia saa hizi hapa ila Kuna mkwamo hapa kidogo boss...
Boss: nini Cony tena? iyo kazi sitailipia siku za zaidi ukumbuke...
Mimi: Ndiyo boss.. ishu ni msosi tu hapa watu waanze kupiga mzigo angalau mpk 12 jioni hivi...
Boss: Ahaaa.. basi hilo msijali nimemwita Jane hapo aje hapa Zinga pub Kuna chakula niliweka order... Vipi ameshatoka hapo??
Nikajibu: ndio ametoka hapa amesema muda wake umeisha wa kazi...
Boss: msijali anawaletea msosi hapo chap....
Basi kiroho safi nikaenda kuwapa habari mafundi nao wakaanza kubadilisha na kuvaa ovaroli zao na kuchukuwa vitendea kazi kuweka tayari...
Kimsingi ilikuwa ni kazi ya siku mbili tu kulingana na idadi ya mafundi na uwezo wao wa kazi ila nikiwa kama kiongozi wa kazi niliamua kutengeneza mazingira ya kupata chochote kitu cha zaidi lakini kuhakikisha kazi inaenda vyema kabisa..
Basi kwa kuwa sikuwa na kipengele chochote siku ile basi na Mimi nikaamua kubadilisha nguo na kushika spana pia baada ya muda mrefu..........
Baada ya kama nusu saa nikasikia naitwa na mlinzi huko kwa nguvu...
Nikaweka spana chini na kwenda...
Nilitoka na kofia yangu kichwani na huku na ovaroli nililokuwa nimevaa na buti zangu za kazi...........
Sehemu 3
Ile kufika mlangoni hivi nikakutana na meneja na kadada kengine kadogodogo hivi wananiita kwenye gari..
Kufika wakanielekeza kuwa wao Wana haraka sana hivyo tushirikiane kushusha kile chakula wao waondoke zao...
Nikasema sio shida ...
Basi chap tukashusha msosi na mlnzi pale ghafla nikasikia Cony njoo huku dirishani kwangu.....
Nikasikia...I'm sorry sikujua kama ulikuwa unaulizia chakula muda ule..
Nikamwambia.. poa usiwaze sisi mafundi tushazoea ..
Akauliza.. mmezoea nini...
Nikamwambia.. kujibiwa vyovyote tu.. si unajua kazi ngumu hazina heshima..
Akajibu... Hapana, usiseme hivyo Cony najisikia vibaya.. ni vile leo nimekuwa bize siku nzima nimekuwa nikiongea na mtu mmoja mmoja na kama unavyojua wengine sio waelewa kabisa...
Nikamwambia.. yameisha hayo, Kama vipi karibu tuguse msosi kidogo wote..
Akajibu.. hapana, labda kesho.. saa hizi naenda shopping kidogo na mtoto wa mzee hapa kesho anaenda zake chuoni Arusha..
Basi tukaagana kiroho safi nikaenda kuwaita mafundi tule kisha tuendelee na kazi...
Msosi ulikuwa wa nguvu na kweli ile siku tukapambana na ile kazi mpaka saa 2 hivi usiku..
Tukafunga mageti, tukakubaliana kesho kila mtu afike saa nne pale kazi iendelee............
Sehemu 4
Asubuhi saa 3 nikaamka nikaanza kujiandaa chap, nikapiga jeans yangu nyeusi, tshirt na raba nikawasha pikipiki yangu na kuanza mwendo...
Saa nne kasorobo nilikuwa nimefika kiwandani nikamkuta Jane ameshafika na anaendelea kumalizana na walinzi na watu watu wa kutunza mazingira...
Mpka kufika saa nne na robo team yangu ilikuwa full na kazi ikaendelea kama mchwa yaani..
Tulifungua mashine na kuzipanga vizuri kwenye makasha ya mbao tayari kwa ajili ya kuzisafirisha..
Ghafla Jane akaja kwangu, nikasema moyoni huyu mama Kuna kitu anataka sio bure.. nikamsogelea...
Niambie boss...
Aaah usiniite boss tena .. si unaona kazi ndio kwishnei hii.. saa hizi ni wanakijiji tu hapa..
Nikamwambia: hapana siwezi kuacha kukuita boss wangu kwa sababu Bado nipo kazini au hujui nikipata shida hapa saa hizi inahesabika nipo kazini....
Akacheka kidogo akasema .... anyways vyovyote tu, ila nina bahasha yako hapa kutoka kwa mzee hapa anasema ni chai yenu ya leo na kesho... Chakula cha mchana mtaletewa kama jana, leo na kesho....
Nikamwambia; Asante.. ngoja niendelee na kazi morali iko juu Bado ...
Akasema :poa endelea....
Basi kwa kuwa kila fundi nilikuwa na uhakika amekunywa chai nyumbani kwake nilikaa kimya tu km hamna nililoambiwa na meneja...
Tulipiga kazi mpka saa Saba hivi msosi ukawa umeletwa kweli...
Tuligusa msosi kisha kazi ikaendelea mpka saa moja kasoro hivi ambapo mashine zote zilikuwa zimeshafunguliwa na kuwekwa kwenye makasha yake...
Hapo ndio nikawaambia kuhusu mzigo wa chai uliotumwa asubuhi, kila fundi akalamba 20 yake safi tukaagana kuwa kesho tufika kama leo ila kazi itakuwa ni ndogo tu ya kuhakikisha mashine zinatoka kiwandani salama...........
Sehemu 5
Asubuhi siku ilyofuata nilivaa zangu jezi yangu nyeupe kali ya Madrid nikiwa na jeans ya blue na sendo tu..
Nilijua kabisa sio siku ya kazi Bali ni kuzuga tu Kwan tuliwaambia wanaokuja kuchukuwa mashine waje kuanzia saa tisa hivi ndio tutakuwa tumemaliza kazi yetu..
Basi tukafika kitengo na kuhakiki mashine zote na kujaza fomu zote za makabidhiano za ofisi na kukabidhi vifaa vingine kwa mtu wa store na meneja..
Basi shughuli zote zikafanywa kwa uangalifu na utaratibu mpaka kufikia saa Saba tukaanza kupiga story na kucheza draft kama kawaida..
Basi kwa kuwa nilikuwa ndio fundi mkuu nililazimika kusaini fomu zangu wa mwisho kwenye kila idara hadi kufikia kwa meneja mkuu...
Mpka nafika kwa Jane basi nilikuwa nimechoka kuongea, nikamwekea form mezani afanye kushusha Saini yake tu...
Nikasikia ....Cony vipi unaumwa?
Nikajibu.. hapana..
Jane: vipi Sasa mbona kama kinyonge...
Nikajibu... Hamna, Kuna mtu tu kaniboa huko.. we nisainie nitoke nikacheze hata mchezo mmoja pale chini...
Jane: huyo aliyekuboa kakuboa na nini??
Mimi: aah anadai spana moja hivi nimemwambia ipo kwenye gari boss hataki kunielewa...
Jane: aah kumbe vitu vidogo namna hiyo ndo vinakuboa jamani??? Eem acha hizo be happy.. nitashughulikia hilo usijalii Cony..
Nikamwambia, poa.. Fanya hivyo..
Basi akaanza kunipa maelekezo mengine ya kazi akaniambia kesho kutwa asubuhi saa 3 kutakuwa na kikao na boss..
nikamuuliza cha nini tena sasa??
Akaniambia ni kikao cha wakuu wa idara wote mameneja na mkurugenzi na boss mwenyewe.. Kuna maelekezo ya ziada kwetu..
Nikamjibu poa nitakuja, nisainie form zangu niende nikacheze draft.. akaniambia hapana form zote za watu wa kesho kutwa zinabaki ofisini hadi hicho kikao kipite....
Nikakubali nikamwambia, vipi naweza kwenda??
Akanijibu, yes unaweza kwenda baada ya kunywa glasi moja ya maji...
Akanyanyuka na kuielekea friji ndogo iliyokuwepo ofisini kwake pale na kunipa chupa ndogo ya maji na glasi...
(Nilikuwa namwangalia kwa kuibia vile anavyotembea kwa madaha huku yupo peku peku na suruali yake ya kitambaa)
Nikamwambia.. haya mambo ya glasi sio mambo yangu kabisa.. usisahau Mimi ni fundi.. ustaarabu ni nadra kwangu..
Jane: hahaha fundi bhana una nongwa wewe.. hivi mkeo si kazi anayo huko nyumbani??
Nikajikuta nimemjibu... Mwanamke wa nini Mimi saa hizi, sitaki stress zisizo na utaratibu mimi....
Akauliza...
Unasemaje...?????
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni