Wimbi la single mothers linaongezeka kutokana na sababu mbalimbali baadhi ni za kihisia, kijamii, kiuchumi, na kimaadili. Hivyo Ili kulikabili wimbi hili linalozidi kukua na kukita mizizi katika jamii zetu, tunahitaji hatua za kina ambazo zinaweza zikatusaidia kupunguza kama sio kukomesha tatizo hili.
Ili kupunguza wimbi la single mothers, ni lazima:
1.Kuhamasisha ndoa za halali na zenye misingi bora; Watu wafundishwe thamani ya ndoa si harusi ya kifahari, bali maisha ya kujenga pamoja.
Vijana wahimizwe kuoa/kuolewa mapema kwa njia halali badala ya kuishi kama wapenzi bila mwelekeo.
2.Elimu ya malezi, ndoa, na uhusiano ipewe uzito; Shule, misikiti, makanisa, na jamii zifundishe kuhusu uhusiano wa kiafya, heshima, majukumu, na mawasiliano katika mapenzi.
Wengi huingia kwenye mahusiano bila kuelewa majukumu yao jambo linalosababisha kutengana kirahisi.
3.Kupinga vikali tabia ya 'kuchezea' wasichana kisha kuwaacha wajawazito
Vijana wa kiume wafundishwe kuwa waaminifu, wawajibikaji, na kuheshimu maisha ya wanawake.
Sheria na jamii ziwawajibishe wanaume wanaotoroka majukumu ya watoto wanaowapata nje ya ndoa.
4.Kuwawezesha wasichana kielimu na kisaikolojia; Wasichana wakipewa elimu, maarifa ya kujitambua, na ujasiri wa kusema “hapana” kwa mahusiano yasiyo na tija wataepuka mimba na ndoa za kiholela.
Elimu huwapa uwezo wa kuchagua vyema.
5.Kuzuia mahusiano yasiyo rasmi (u-boyfriend/girlfriend usio na mwelekeo)
Wapenzi wa “kupotezeana muda” ndio chanzo kikubwa cha mimba zisizotarajiwa na watoto wa nje ya ndoa.
Vijana wafundishwe kutafuta uhusiano wa dhati unaolenga ndoa, si starehe tu.
6.Kufuta dhana potofu kuhusu ndoa
Baadhi ya wasichana hukataa ndoa wakiamini wanaume ni “mateso” au hawafai, kutokana na machungu ya wengine.
Lakini suluhisho si kukataa ndoa bali ni kuchagua vyema, na kujifunza kushirikiana.
7.Jamii iimarishe mfumo wa kulea na kushauri:; Familia, wazazi, na wazee wa mtaa wawe walezi wa vijana watusaidie kushauri, kuunganisha, na kupatanisha.
8.Maongezi ya kweli badala ya hukumu
Tuwasikilize mama wa watoto pekee, sio kuwalaumu tu. Wengine hawakuchagua hali hiyo, ila waliingia kwenye dhoruba za maisha.
Kuwasaidia kujijenga upya ni sehemu ya suluhisho pia.
Kwahiyo, tukifundisha maadili, heshima, uhusiano wa dhati, na kuwajibika, tutapunguza idadi ya single mothers. Lakini pia tukiwaheshimu na kuwasaidia walioko kwenye hali hiyo, tutajenga jamii yenye huruma na matumaini.
Sufian Mzimbiri.