Baba Celena alistuka kumuona mkewe ameanguka , huku akitoka na mapovu mdomon ,haraka na upesi akaita wafanyakazi na kusaidiana kumkimbiza hospital, Celena alikuwa analia tu nakuita mamaa ,mamaa ,
Walimuwahisha hospital na haraka na upesi akapatiwa matibabu ya kuuwa sumu kwenye mwili na akalazwa akiwa bado hajitambui ,
Baba Celena alikosa majibu aliwaza mke wake amepatwa nanini hakujua kabisa kuwa ni ile soda ndo chanzo ,
Alirudi nyumbani akiwa na mtoto wake Celena pamoja na wafanyakazi wake ,
Baba Celena alikuwa na mawazo sana ,aliwaza kilichomkuta mkewe na hajui kama atapona na aliwaza kuhusu hawa watoto wawili pamoja na mkewe Celina na hakupata jibu la moja kwa moja ,
Alipitiwa na usingiz na asubuhi na mapema alijiandaa na kuwahi kule hospital , na akaambiwa bado mkewe hajapata nafuu maana sumu ilikuwa Kali sana ,
Akatoka na kwenda kazin , ila bado alikuwa na mawazo sana , muda wa jion akatoka na kabla hajaenda kwa mkewe hospital akaamua aende kule kwa kina Stefano ili akamuone Celena kichaa na ikibidi amuone vizuri yule mtoto aliefanana na mwanae ,
Alifika mpaka kwa kina Stefano na kweli alimuona Celina kichaa akiwa nje ya nyumba hiyo , akapaki gari na taratibu akashuka na kumsogelea pale alipo , alimuangalia vzr akajikuta machozi yanamtoka ,aisee ni kweli huyo ndie mkewe Celina, mke aliedumu nae kwenye shida na Raha , leo amekuwa kichaa , alijikuta analia na kumstua Celina kichaa ,
Celina alipogeuka akamuona haraka na upesi aliamka akaokota jiwe na kulirusha likamkosa mumewe,
""Usinisogelee ,,kaa mbali namimi,,""
Celina aliongea huku akinyanyua jiwe lingine ,
Kule ndani alikuwa mama Stephano na baba Stefano pamoja na Celina akiwa na Stefano,
Waliposikia Celina kichaa anaongea kwa ukali wakatoka nje wote na kushangaa baba Celena akiwa kasimama mbele ya Celina kichaa na Celina kichaa kashika mawe ,
"Mke wangu subili basi tuongee mimi ni mume,,,,
"Hebu funga domo lako nisijenikakuharibu sura na mawe,""
Balozi alitaka kujitetea lakini alikatizwa na Celina kichaa,
Eti mumewe ,,"?au nimeskia vibaya ,,""?
Mama Stefano alimuuliza mumewe aliesimama pembeni akiangalia ule mpambano,
"Celina hebu kajaribu kumtuliza mama yako tuone kama anaweza kutulia,""
Baba Stefano badala ya kujibu swali ye akamtuma Celina,
"Baba subili kwanza tuone na Leo atafanya nn maana anaonekana akiwa kwenye hali hii akili kama zinarudi ,"
Aliongea Celina na wote wakaona ni sawa ,
Balozi akasogea tena ili am bembeleze Celina lakini Celina akarusha jiwe lingine likampata la mgongoni ,
"Nimesema usinisogelee ,kaa mbali na mimi""
Celena kichaa alijibu tena kwa hasira ,
Kumbuka mama stefano na mumewe hawamjui barozi na ndio maana wanamshangaa mala amuite Celina kichaa mkewe , na ni mala ya pili sasa anakuja na kugombana na Celina kichaa ,na hawakujua kama huyu ndio mumewe ,
Celina mtoto anamjua barozi kuwa ndie baba yake na celena sasa hapa kinachomshangaza kwanini anamuita mama yake mkewe,
"Mama inatosha nazani unajua ninavyojiskia nikikuona upo hivyo ,,""
Celina alijalibu kumtuliza mama yake,
"Mwanangu Celina niache tu ,ungejua alichonifanyia huyu mwanaharamu ,basi ungeniacha nikalia mpaka nichoke mwenyewe,""
Celina kichaa alimkumbatia mwanae nakuanza kulia tena kwasauti ,
Baba Stefano akamfuata barozi nakumwambia aondoke na aje siku nyingine maana leo hawawezi kuelewana ,
Barozi alimwangalia baba Stefano akamfananisha yaani nikama alishawahi kunuona mahali ila hakumbuki ni wapi,lakin pia baba Stefano na mama Stefano wamefanana na Celena yaani kama mtoto wao ,
S"amahani naomba nikuulize hivi yule nimwanae kweli au,,""?
Barozi aliuliza , huku akimwangalia Celina mtoto jinsi alivyofanana na mwanae Celena ,
"Ndio ni mtoto wake wa kumzaa kabisa ,,""
Baba Stefano alimjibu barozi,
Inamaana Celina alikuja akapata mtoto,,"" ?
"alizaa nanani,na imekuwaje ,"
Balozi aliwaza huku anapanda kwenye gar yake nakuelekea nyumbani kwake,
Alipofika kwake akajitupa kwenye sofa huku akiwa na mawazo tele,
Sasa itakuwaje au nimrudie mke wangu ,?
Au niongee ukweli kuwa mtoto huyu sio wangu,?lakin watu watanionaje,na baba wa hawa watoto ninani,?
Shkamoo baba ,,"
Celena alikuja na kumsalimia baba yake ,lakini baba alikuwa mbali kimawazo na hata hajaskia salamu ya mwanae,
Babaa,,"
Celena aliamua kumtingisha baba yake na barozi akastuka kumuona Celena
Vipi mwanangu umekuja mudaee ,,"
Barozi aliongea huku anamkagua mtoto wake maana bado alikuwa haamini kama niyeye alijua niyule Celina kule ndio kaja,
Hakyamungu hawa watoto ni mapacha ,,"
Aliwaza barozi wakati anamkagua Celena ,
Baba mbona unaniangalia sana ,,"?
Aah hakuna mwanangu ,ulisema unamjua yule mama kichaa ,"?
Barozi alimuuliza mwanae,
Ndio baba namjua tena ni mama yake na na yule msichana tuliefanana sana ,""
Celina aliongea bila kujua anamchanganya baba yake kabisa,
Kama nikuchanganyikiwa baba huyo alichanganyikiwa haswa,
Alijiuliza siku huyu mtoto akigundua kuwa hapo sio kwao itakuwaje,na mama yake atakuwa katika hali gani,?
**
"Huyu baba itakuwa ni mume wa yule dada aliekuja juzi na kama ni mkewe basi Celina atakuwa ni mtoto wao , sasa swali je mbona kama hawamjui huyu Celina ,"?
Walijiuliza mama na baba Stefano bila kujua kuwa huyo Celina ni mtoto wao wenyewe na wanaishi nae kama kumpa msaada tu yeye pamoja na mama yake kichaa ,
Celina mtoto alikuwa anam bembeleza mama yake huku mama huyo akilia huku anakumbuka mbali sana,
Celina kichaa alikumbuka mbali sana sema ndio hivyo kumbukumbu zake hazidumu ,siku hiyo alikumbuka kuna siku aliamka asubuhi na alitapika sana ,unajua celina alikuwa anajitambua japo alikuwa kama zezeta na viungo vyake kukakamaa kama mtu aliepooza,
Sasa anakumbuka siku hiyo alijitapikia sana na asubuhi yake akanikokota mpaka nnje nia yake ni kumuona barozi amwambie yeye anajihusi kama mjamzito ,
Na kweli alifanikiwa kutoka na kwabahati barozi nae alikuwa anatoka kwenda kazini kwake ,wkakutana mlangoni ,celina alikuwa hawezi kuongea vizuri kutokana na mdomo wake kwenda upande ,hivyo alianza kumuoneshea kwa ishara kuwa mbona kama anjihisi mjamzito ,lakini barozi alimwangalia kwa zarau ,na akampita kama hamjui ,celina akaona nibora aende akamzuie getin wakati anatoka na gari ili amuelezee ,
"Nitakugonga mshenzi wewe toka hapo ,,""
Barozi alimwambia celina wakati celina anamuoneshea kwa ishara tu kwamba anahisi yeye ni mjamzito na pale alipo anaumwa,
"Wee yakobo hebu mtoe huyo ,,"
Barozi alimwita mfanyakazi wake ili aende akamtoe celina pale getini ,yakobo alishindwa maana hata yeye alimuonea sana huruma celina ,
"Mariaaa ,,njoo umtoe huyu mi nipite,""
Baada ya yakobo kushindwa barozi alimwita maria na maria alipokuja na jinsi anavyomchukia akamshika mkono na kum buruza kama anaburuza mbuzi ,huku anampiga makofi yanguvu na barozi hakujali ndo kwanza aliwasha gari lake na kuondoka zake,
"We unajifanya unamimba wewe ,mpuuzi kabisa yaani unajitapisha ili uonewe huruma ,heheheeeee,,haloooo,,,kwataarifa yako tu mi nakwambia mimi ndio nitamzalia mtoto barozi ,sio wewe mpuuzi ,""
Maria alisema huku anampiga mateke ya tumboni ,maskini celina alijihisi maumivu sana sikuhiyo alilia sana ,na hakujua afanye nini ,kitu pekee alichokiona kuliko kuteseka hivi nibora anywe sumu tu ajifie zake ,
Jioni yake barozi aliporudi ,celina alijikokota tena na safari hii aliingia mpaka sebuleni akawakuta wamekaa wamekumbatiana yaani maria na barozi ,
Celina aliomba asikilizwe japo dakika moja ,lakini maria alisimama na kumsukuma na teke mpaka nnje huku barozi akicheka cheka tu ,
"Bora umemtoa maana hali yahewa ilishaanza kubadilika hapa ,""
Barozi aliongea huku akimimina wain kwenye grasi,
Celina akarudi tena na safari hii aliambulia kipigo tena mbele ya mumewe ,
Nimekwambia usiwe unaingia humu kwanini huelewi ,"sas ukiniona niko na mume wangu naomba usisogee eneo hilo sawa,,"??
Maria aliongea kwa sifa na akamalizia kumpiga na teke latumbo ,
Celina alisikia maumivu kupita kiasi na damu zilianza kumtoka ,maria bila hata ya huruma akam buruza na kumtoa nje ili asichafue mazuria meupe ya mule ndani ,celina alipofika nje akili ikamruka yaani hapo ndipo uchizi ulipomuanza ,hakuelewa tena kama damu zinamtoka ,hakujua tena kama pale alipo niwapi ,cha ajabu aliweza kusimama na kuanza kuzurula hovyo ,
Balozi alijona hali ile lakini hakujali na celena alipopata upenyo alitoka nje na kuzurula huku nakule ,na ndio ukawa mwanzo wa ukichaa ,hakujua tena ile mimba iliendaga wapi nakama ilitoka ilitoka vipi maana akili ilihama kabisa,
Aisee tuishie hapa mi machozi yananilenga lenga ,😭😭
Kumbuka story hii utaipata yote mwanzo mwisho kwa elfu moja tu,
Namba ni 0655772653 NJOO WHTSAP.
Maoni