*************
@Kila Mtu
*SEHEMU YA KWANZA*
Ikiwa ni siku ya juma mosi siku ambayo nilipaswa kuhudhulia harusi ya mdogo wa rafiki yangu, siku hii nilikuwa na huzuni sana.
Kwanzia asubuhi hadi inafika saa nane sikuwa nimeshuka kitandani ,zaidi nilijilaza huku nikizama kwenye ulimwengu wa mawazo. Macho yangu yalivimba kwa kulia huku mafua na sauti za kwi kwi ya kilio ndio zikisikika chumbani humo, dakika zilisogea ikafika saa tisa kasoro mara simu yangu ikaita. Iliita kalibia mara tatu bila kupokelewa mwisho nikanyosha mkono na kuangalia anaepiga nikaona ni Rafiki yangu, kinyonge nilipokea na kuongea. "Hello "
"Elena uko wapi wewe mbona unatuvuruga hivi?, jana tumeongea na kupanga kila kitu lakini hadi mda huu haujatokea wala hupokei sm. Vp kuna tatizo au?" Wema aliongea kwa kupanick sana , nilishusha pumzi ndefu na kumjibu" samahani mpenzi nitafika mda si mrefu" "Utafika mda si mrefu ! ,hivi unajua saizi ni sangap na haujafika hata salon""Wema! Nielewe nakuja " sikutaka kuongea tena nikakata simu na kuweka pembeni, taratibu niligeuza uso wangu upande wa pili na kuangalia picha iliyokuwa ukutani. Picha hii ilikuwa ni mimi na mwanaume aliebeba maisha yangu, kadri nilivyozidi kuiangalia picha ile ndivyo maumivu yalizidi kuutafuna moyo wangu. Kwa sauti ya chini nikajiambia(" Elena utakuwa sawa" ) niliongea na kushuka kitandani nikaingia bafuni na kujiweka safi kisha nikatoka . Nilisimama kwenye kioo na kujiangalia kalibia dakika mbili mwisho nikafuta machozi nakuachia tabasamu ,tabasamu ambalo lilionesha uchungu wa hali ya juu. Basi bila kupoteza mda nilijiandaa vizuri na nilivyomaliza nikachukua pochi pamoja na funguo ya gari nikatoka chumbani. Nilifika sebleni na kukutana na msichana wangu wa kazi, tukasalimiana kisha nikatoka na kumuacha akiniangalia kwa uso wenye maswali mengi. Haraka niliingia kwenye gari na kuondoka kwa mwendo mkali sana, sasa wakati nikiwa katika mwendo mkali simu yangu ilita taratibu nikapunguza mwendo na kupokea sm."Hello Mama ,Shikamoo" "Maharaba, uko wapi maana tumeshafika kanisani lakini sikuoni" "Mama niko njiani nitafika mda simrefu" "Uko njiani utafika mda si mrefu,hivi unajua Elena utakuwa na roho ya uchawi ndani yako?. Binti wewe toka asubuhi huonekani sm hupokei, ni kwamba hujui kama unatakiwa kuwepo ili usaidizane na mwenzako au wivu ndo unakusumbua?""Mama nakuja "niliongea kinyonge na kukata sm , nikashusha pumzi na kuweka umakini mbele. Dakika 25 zilinitosha kufika nje ya njengo kubwa la kanisa , taratibu nialiangalia sehemu sahihi ya kupark gari langu nikapark na kushuka. Nilipiga hatua za haraka huku nikitoa uso wa huzuni na kuweka tabasamu, nikafika waliposimama kina Wema pamoja na ndugu na baadhi ya marafiki na kuwasalimia. Kila mtu aliniuliza nilikuwa wapi ,nikadanganya nilipata kikao cha dharura hivyo nilikuwa ofisini.Nilivyojibu hivyo walinielewa na kunisifia kuwa nimependeza , niliitikia kisha nikamfuata bibi harusi ambae alikuwa pembeni akiongea na mama yake . Kwa furaha nikampa hongera na kuitikia wito wa mama ambae alidai anataka kuongea na mimi. "Ndio mama kuna nini ?" Nilimuuliza baada ya kutoka mbele za watu, mama aliniangalia juu chini na kuniuliza. "Kwa hiyo umeona nisawa kuja hivi?" Swali lake lilinifanya nikajiangalia jinsi nilivyo vaa na kujibu."Yeah!, kwani kuna shida au naonekana vibaya?" "Unauliza kuna shida ,eeh shida ipo, Elena hii ni harusi sio birthday party, unajiwekaje simple namna hii ? Embu angalia wenzako walivyowaka wamependeza make up zimewakaa vizuri halafu wewe umekuja kama unakuja kusimamia ubatizo. Kwani shida yako nini haswa uniaibishe au ? siku kama hizi unatakiwa utumie pesa na muda kujiweka vizuri ili walau uonekane.Na sisi tuondokane na aibu lakini hapana ,unavaa vile unavyoona ni sawa na kutoka halafu unategemea kijana wa mtu aje kukuposa . Nani atae poteza mda wake kukufuata ile hali unajiweka kama house girl mwenye anaelea mapacha. Sikia baada ya ndoa kufungwa hakikisha unajiweka vizuri ndo uingie ukumbini,sio uje kama unaomboleza msiba wa bibi yako. Me habari za kuwekwa vikao na baba yako kila siku nimechoka, kwanza hivi huoni aibuu wenzako wamesha olewa na sasa wanaolewa wadogo zao.Wewe raisi wa mishangazi upo tu huoni haya ? Mfyuu " Mama alimaliza kuongea na kuondoka huku akinisindikiza na sonyo kali, niliangalia chini kwa sekunde kadhaa na kushusha pumzi kisha nikageuka kuwaangalia rafiki zangu. Nyuso zao zilipambwa na furaha huku mikono yao ikipendezeshwa na Pete zilizo kuwa zikiwaka vidoleni mwao. Nilitabasamu na kuficha maumivu niliyokuwa nayo moyoni na kuwafuata, kufika tulipiga selfie kidogo na kuingia kanisani kwani mda wa ibada ya ndoa ulikuwa umefika.Basi ibada ilianza na mda wote nikawa nawaangalia maharusi huku nikitokwa na machozi, watu walihisi machozi yale ni ya furaha lakini haikuwa hivyo. Nilitokwa na machozi ya uchungu, moyo wangu ulikuwa umejaa maumivu ma kubwa huku kiu na shauku ya ndoa ikiwa ndio uvuri wangu. Ndoa ilifungwa na baada ya hapo watu walipata picha na baada ya picha maharusi wakaenda kupumzika huku sisi wengine tukisubiri mda wa kuingia ukumbuni ufike.
*SEHEMU YA PILI*
... Ili kuepuka maneno ya mama ilinibidi nijiweke vile anavyotaka , na mda wa kuingia ukumbuni ulipofika tukaingia na sherehe ikaanza.Siku hii sikuwa sawa hata kidogo, nilijitahidi sana kuonesha furaha ili nisije kuonekana mtu wa ajabu kwenye harusi za watu. Basi sherehe iliendelea mimi nikawa nimekaa huku nikichukua picha na video ,mara mama akanambia " Nipe hiyo simu" "Nikupe simu yangu unataka kumtafuta mtu ama?" "We nipe sio uniulize ulize maswali ya kijinga " Sikuongea neno nikampatia akapokea na kusema "haya inuka ukajichanganye nawenzako, sio kukaa kaa hapa kama unaumwa miguu ya uzee" Sikutaka kubishana nae ,niliinuka huku nikiweka tabasamu fake na kwenda kuungana na wenzangu. Mda ulienda hatimae sherehe ikaisha nikaagana na wenzangu kisha nikaelekea ilipo gari langu ili niondoke , sasa wakati nikiwa nakalipia kufika alikuja mbaba na kunisimamisha. Kwa heshima nilisimama huku nikiwa na tabasamu pana usoni, mbaba yule alisogea karibu na kunisalimia."Habari yako mrembo" "Ni nzuri " "Okay, bila kupoteza naweza kupata namba yako tafadhali?" Alivyosema hivyo nilimuangalia kwa sekunde kadhaa huku nikijishauri ni mpe au nisimpe, ajabu wakati najifikilia kuhusu jambo hilo alikuja mama na kufika anampa namba yangu. Ukweli sikupendezwa na kitu alicho fanya mama , baba yule alipokea mama akajichekesha pale baba wawatu akashukuru na kuniaga kisha akaondoka .Baada ya baba huyo kuondoka mama alinishika mkono kwa nguvu na kutembea kwa haraka hadi kwenye gari langu na kuniachia mkono. "Mama ! Ndo unafanya nini sasa?" Nilimuuliza huku nionesha kutopendezwa na kitu alichofanya. Mama aliniangalia kwa jicho kali na kunambia" Unaniuliza ndo nini kwani nini usichoelewa?, nimempa namba zako " "Mama ! Hujafanya vyema, nani kitu cha aibu sana unawezaje kufanya jambo kama hilo?""Eeeh !sijafanya vyema ila wewe umefanya vyema si ndio? Sikia Elena, nitahakikisha napambana hadi unaolewa , hivi huoni aibu au kujisikia vibaya kuona wenzako waolewa wewe upo tu na komwe lako kama kibalaza cha kanisa. Mtu unajua kabisa age go bado unaringa kutoa namba,dada unataka kuoelewa na mizimu ya kwenu?" "Mama please" "Please nini Elena, unajua shida yako nini dharau ,eeeh hiyo elimu na pesa ulizo nazo zinakufanya uwe na dharau kiasi cha kujiona huitaji ndoa.Sasa siko tayari kukaa kimya nikiona unafanya au kuchagua maisha ya kipuuzi namna hii, elimu na vipesa kidogo tu ushaona huitaji mwanaume kwenye maisha yako. Mimi mbona nimeolewa au una elimu kunishinda mimi? Au unaona nimefanya kitu cha kijinga " "Mama! Naomba hii mada uiache tutaongea tukiwa nyumbani " "Kuongea nyumbani? Ni mara ngapi umeitwa ili tuweze kuzungumza na hukutokea ?"Nilishusha pumzi ndefu na kusema "mama nakuahidi kesho nitakuja " "Huna haja ya kuahidi hata usipokuja nitakula na wewe sahani moja hadi siku nitakayo kuona ukija na kijana nyumbani " Aliongea na kuondoka ,nilibaki na muangalia huku machozi yakinitoka . Kinyonge niliingia kwenye gari na kuondoka , baada ya mda kadhaa nilifika nyumbani nikapark gari na kuingia ndani.Nilifika chumbani na kujitupa kama mzigo, kichwa kilijaa mawazo huku moyo wangu ukifunikiwa na wingu la huzuni. Taratibu mda ulienda nikajikutaka nikipitiwa na uzingizi mzito, nakuamka kukiwa tayari ni asubuhi. Haraka nialiamka na kujiandaa nilipamaliza nikaenda kazini, kufika huko nikafanya kazi kama kawaida ilipofika mda wa kutoka nikaweka mambo yangu sawa na kuondoka. Sasa wakati nikiwa njiani nikaona nimtafute kitunguu wangu na bila kuchelewa nikampigia, bahati mbaya hakupokea sm zangu .Nikaona isiwe shida kikubwa najua unaishi wapi ,basi nikabadilisha safari badala ya kwenda nyumbani nikaenda kwa huyo kitunguu. Yes kitunguu maana kwa namna anavyofanya nalia kila siku hili jina linamfaa kabisa , basi bwana nilifika kwake nikapiga honi lakini sikufunguliwa. Nilipata hasira na kushuka nikagonga kawaida mlinzi akatoka na kunambia boss wake kamzuia asinifungulie, kusikia hivyo nikaona nishuke ,maana kama nikitumia hasira basi sitaingia.Kweli nilivyoshuka na kumuomba kwa upole alinielewa na kunifungulia , nami bila kupoteza mda nikaingia chapu kisha nikapark na kugonga mlango wa kuingia ndani. Niligonga kama mara nne bila kuitikiwa nikachukua sm ili nimpigie ila kabla sijapiga mlango ukafunguliwa, niliinua macho yangu na kumuangalia kipenzi cha roho yangu. Adam aliniangalia kwa macho yenye hasira kali, bila kuongea nilibaki nikimuangalia namna alivyokuwa akitokwa na jasho jingi mwilini. Kichwani nikajiambia please isiwe kama ninavyowaza ,maana mpenzi wangu huyu huwaakiwa kwenye shughuli zile za kikubwa ndo huwa anasweat hivi. "Madam! Umekuja nyumbani kwangu kufanya nini ?" Aliongea Adam tena kwa sauti iliyojaa dharau, kinyonge nilitabasamu na kumjibu. "Aaaamh nimekuja kukuona na pia ningeomba tuongee " "Kuongea? Mimi na wewe tuna kitu cha kuongea?" "Adam please naomba usinifanyie hivi ,unajua kabisa siwezi kukaa na amani ile hali hatuko sawa ""Sikia Elena mimi na wewe hatuna cha kuongea ,na unatakiwa kuelewa kwamba tumeshamalizana " "No Adam hatuwezi kuishia hapa,kumbuka tuna ndoto nyingi na safari yetu bado changa, so please kama kuna kosa lolote nililofanya naomba sana nisamehe. Lakini usivunje hili penzi nakuomba sana mpenzi wangu " Niliongea kwa uchungu huku machozi yakinitoka ,Adam aliniangalia kwa dharau na kutaka kuongea ila akasita na hii ni baada yakuitwa na mdada ambae alitokea chumbani kwake huku akiwa amejifunga kanga . Tena kanga yangu , bidada yule alisogea karibu na kuuliza " babe nini kinaendelea mbona umekaa sana huku" Neno babe lilipenya kama mshale wa moto masikioni mwangu, nilimuangalia yule dada na kurudi kumuangalia Adam na kwa sauti ya upole nikamuuliza. "Adam unanisalit!!??" Kuuliza hivyo kijana akajibu ."Nakusaliti kivip mimi na wewe tuna mahusiano hadi nikusaliti?" "Hatuna mahusiano? Adam nakuuliza mimi na wewe hatuna mahusiano?" "Sikia we boya usitake kunichanganya, hivi kwanini hutaki kuachika nimeshasema sikupendi wala sikuhitaji kwanini huelewi?" "So safari hii una maanisha kweli? " "Sio sasa, siku zote nilikuwa nikimaanisha" "Kosa langu kwako ni nini hadi ufikie hatua ya kukatisha kila kitu?"Nilivyouliza hivyo aligeuka na kutaka kuondoka bila hata kunijibu, kwa hasira nilimshika mkono na kumrudisha ,bibie akapanick na kutaka kuanzisha fujo. Kwa sauti iliyojaa hasira nikamwambia" we kinda kaa mbali na hili, mh Adam mkaka mwenye mabawa yako hivi unafikilia ni rahisi tu kuingia kwenye maisha yangu na kupotea kwa wakati unaotaka wewe?. Sikia haya mahusiano hayafi kama unavyotaka ,kama kuna lolote ambalo haliko sawa tutakaa na kuliongea ila kuua kila kitu no siwezi kukuruhusu ufanye hivyo. "Adam alicheka kwa dharau na kusema" Okay embu nambie unataka kufanya nini?, maana unajitoa akili " "Acha nijitoe akili ila siwezi kukaa na kukuangalia ukiharibu mahusiano ambayo tumetumia mda na nguvu kuyajenga. Adam wewe ni wangu sio sasa ni jana, leo kesho na hata milele ,hivyo kama unajitadanga kuwa unaweza kuniacha hiyo ni ndoto wewe ni wangu na utabaki kuwa wangu." Adam alicheka sana na kunambia" sikuwahi kujua kama nilikuwa na date na kichaa kama wewe ,sikia binti mimi Adam siwezi kuwa na wewe maisha yangu yote.Una muona huyu ,huyu ndio mwanamke wa ndoto yangu nasio wewe usie na mbele wa nyuma " "Mwanamke wa ndoto yako!, wala si mimi nisie na mbele wala nyuma, leo hii nimekuwa sina mbele wala nyuma si ndio?. Yaani baada ya kila kitu saizi nimekuwa kama makapi? No hatuwezi kuishia hapa. Adam kumbuka tulikotoka mimi na wewe ,kumbuka ahadi zako kwangu nasio kufuata tamaa ambazo hazina mbele wala nyuma.Adam nakupenda na wewe unalijua hilo so please naomba sana usiuvunje moyo wangu please Adam" "Sikia, moyo wako ,maisha yako sijui tulikotoka hivyo vyote havina umuhimu kwangu, na nikwambie sijawahi kukupenda na kama nizile ahadi potezea hakuna hata moja iliyokuwa ya kweli . So unahitaji kuelewa na kuniacha na maisha yangu ili niweze kuenjoy na mwanamke nimpendae" Maneno ya Adam yaliniumiza sana nikatamani kuongea lakini nikakosa hata neno la kuongea ,bila kuangalia nyuma Adam alimshika mwanadada mkono na kuongozana ndani. Nilibaki nimesimama huku macho yangu yakibubujikwa na machozi, (nimeachwa tena ) ... Nyieeeee....Mambo ni ya motooo. Kwani wewe auogopi Usipite bila kulike na kukomeniti fanya ku share kabisa ili sehemu inayofuata isikukose maana ndiyo sehemu balaaa
..ITAENDELEA...... Hii ni bonge la simulizi isikubali ikupite.
@wafuasi
#itaendelea_story_ni_kali_sana?
Mkiwa wavivu kucoment namimi nakuwa mvivu kupost hivyo comment kwa wingi jamani ili mnie mizuka
# PIA USISAHAU KUNI FOLLOW MIMI KULUTI MC ILI USIWE UNAPITWA NA STORY ZANGU FAIDA YA KUNI FOLLOW NI KUWA WA KWANZA KUPATA STORY KILA NINAPO POST
@everyone.