AIBU YA KUCHELEWA KUOLEWA ILINIFANYA NIKAOLEWA NA JINI ????????
Sehemu ya Tano ( 5 )
*************
@Kila Mtu
????????????????????????????????????????????????
Hakuwa mwingine bali ni Penina ,huyu ni rafiki yangu wa toka utoto naweza kumuita best friend maana amekuwa na mimi kwenye nyakati zote.Na ndo mtu pekee ananielewa tena naweza kusema kuliko hata dada zangu, basi Penina alitembea huku akiongea. "Wema unataka kumwambia nini mrembo wangu ,ajaribu kumtafuta ili iweje ?" Aliongea na kukaa pembeni yangu na kunishika kwenye paji la uso kama vile ananipima joto, Wema kuulizwa vile kajibu. "Unauliza amtafute ili iweje kwani hujui akili ya Adam anaweza kusema hivyo kesho akarudi ""Arudi kwamba kuna kitu kasahau?, kwanza usitake kuniambia hujaona kama amempost mpenzi wake mpya" "Nimeona na ndo maana nikawa nampigia sm mgonjwa wetu ila hakutaka kupokea naona heartbreak inamfanya akose nguvu ya kuongea na sm" "Kumbe umeona ila ukawa unamuenjoy mwenzako?maana ulivyokuwa unamuuliza nikama hujui kitu" "Aaah jamani sasa mimi najua nini ? Me nimeona jamaa kampost mtu na makopa kwa wingi nikasema nimuwahi ndugu yangu asije kujipiga kitanzi.Bahati nzuri nimekuta mzima wa afya sema amelia sana hadi uso umejaa , sema nini pole ndugu yangu me naamini amefanya hivyo kwa hasira tu akiwa sawa mtaongea ." Aliongea Wema Penina akataka kumjibu nikamuwahi na kusema . "Hakuna penzi tena kila kitu kimeshakufa, sasa niwakati wa kuanza safari mpya" niliongea kwa huzuni sana Wema akanijibu. "Hizo safari ambazo umekuwa ukianzisha na kuishia njiani wallah zinachosha ,lakini haya yote unayataka wewe"Wema alivyosema hivyo Penina alikunja uso na kumuuliza" Wema unataka kusema nini?" "Aaah nimesema anayataka mwenyewe,kama angekuwa hataki angefanya maarifa wala hili penzi lisinge kufa kizimbe namna hii" Baada ya Wema kusema hivyo penina alitaka kuongea nikamzuia na kumuuliza Wema . "Wema! Sikuelewi unataka kusema mimi nimetaka iwe hivi?""Ndio ,kwani ni mara ngap nilikwambia mtengeneze ukaona oh nimambo ya kishirikina haya kaondoka . Sasaivi unaanza upyaa sa sijui huchoki au mwenzetu unaona sawa tu" Nilicheka kinafki na kumuuliza " Wema unataka mimi nimroge mwanaume ili iweje kwa mfano? Yaani kwanza naanzaje kwenda kwa mganga ?" "Aaah unaanzaje!? endelea kuuliza hivyo hivyo ,utakapo fika miaka 40 bila ndoa ndo utaelewa , we unafikili watu wote waliopo kwenye ndoa wameingia kwa mwanaume kupenda?.Dada watu wanaroga sasa we shanga shangaa tuone utafika wapi" "Nahisi bado sijakupata, kwahiyo unataka kusema ili ni olewe natakiwa kumpiga mtu libwata si ndio?" "Eeh kwa nuksi uliyonayo shoga angu unahitaji msaada ,laa sivyo utachunda shost " Nilimuangalia Wema nikawa kama vile simuelewi vile ,unajua kauli ya kuwa nimroge Adam hajaanza kuisema leo. Lakini mara zote nilijua anatania ila leo naona kweli ana maanisha anachokisema .Nilishusha pumzi ndefu na kumwambia "Wema! Katika vitu ambavyo sitakaa nikafanya kwenye maisha yangu nikumwendea mtu kwa mganga. Na sio kumwendea tu bali sitakaa mimi Elena nikakanyaga kwa mtu anaeitwa mganga iwe ni kwashida yoyote ile sitawahi. Kuhusu ndoa naelewa kwamba wenzangu mmepata bahati hiyo mapema na mnaenjoy, hongereni ni bahati kwenu. Ila mimi nitasubiri hata ipite miaka mingapi bado nitasubiri, unajua kwanini ? Namuamini Mungu, najua anampango mwema juu yangu.Maana ananiwazia mema ,na kamwe hawezi kuniacha nikaaibia hivyo basi niacheni nionekane mkosi au vyovyote vile mnavyoniona ila mda wangu waja." "Mmmh haya maneno si mageni kwako toka mwaka jana unasema hivyo hivyo ila leo tunaenda kumaliza mwaka ukiwa single singula singwengwe. Sema kwakua umeamua poa ,lakini hii ndio njia pekee iliyobaki kwako ,hata hivyo sioni kama ni shida kwasababu huendi ili kumuua mtu ila unatengeneza kesho yako.""Kesho yangu haitengenezwi na mtu Wema , nitasubiri na nina Imani nitapata hitaji la moyo wangu kwa wakati sahihi" "Wakati gani ambao utakuwa sahihi kwako?, dada usiji sahaulishe na kujifanya kama unamiaka 20 my dear una miaka 30 tena sio 30 tu soon unaingia 31. Sasa niambie hiyo miaka 31 huna mahusiano ya kueleweka na unajifariji eti wakati sahihi , haya tusema sawa ndoa sio fungi lako zaa basi . Maana mda si mrefu utaacha kuona siku na ukishaacha kuona tu jua habari yako itakuwa imeishia hapo utakufa ukiwa huna mtoto wala mume.Na unajua ukiondoka kwenye dunia hii bila kuacha alama ni mwezi tu tunakusahau mazima , so chagua maana maisha niyako" Wema amekuwa ni mtu wakuongea maneno makili au kuropoka bila kufikilia nini anaongea na nilimzoea na kuona ndivyo alivyo. Lakini leo uongo dhambi amenikwaza,si mimi tu hata Penina alikwazika sana na kuanza kujibishana huku kila mmoja akipandisha sauti. Nilikaa kimya huku nikiwaangalia tu, wakajibizana na walipochoka wakanyamanza .Wema hakutaka kukaa tena alichukua pochi yake na kuaga kisha akaondoka . Baada ya Wema kuondoka Penina alinisogelea na kunikumbatia akanambia ,"Usilie wala kuumia jipe moyo huku ukiamini Mungu atakwenda kukupa hitaji la moyo wako. Na usiweke moyoni maneno yote wanayo kwambia ila muangalie Mungu kwa moyo wa imani sawa mpendwa wangu" Maneno ya Penina yaliniingia na kujikuta nikianza kulia , nililia sana na kumwambia " Penina nahisi kuchoka ,ndio natamani sana na mimi kuwa na ndoa yangu.Lakini nitafanya nini ikiwa bado Mungu hajaruhusu hili kwangu, familia yote wananisema na kunifanya nijione kama mdhambi. Wanashindwa kuelewa kuwa sijapenda kufikia umri huu bila ndoa au mahusiano ya kueleweka ,naumia na kuchoka pia . Natamani wanielewe walau nitapata nguvu ya kutembea kwenye njia ya matumaini ila kadri wanavyo nizonga nahisi udhaifu ndani yangu " "Hapana usiruhu kuchoka ,najua ndio unaumia ila kaa ukiamini kuwa utapokea ,na kingine hujachelewa kwa Mungu hakuna kuchelewa.Wala hakuna mahari kuliko andikwa kwamba kila binti anatakiwa kuolewa akiwa na umri flani no, kila mtu anamuda wake ambao Mungu alimpangia kwamba ufikapo mda huo utaingia kwenye ndoa. Hivyo kipenzi changu omba natena ikibidi acha kuomba bali mshukuru Mungu kwani tayari ameshasikia maombi yako kilichobaki ni kupokea sawa" Niliitikia ndio akanifuta machozi na kwenda jikoni kuniandalia chakula ,kilipokuwa tayari alinilisha mwenyewe huku akinipigisha story za kufurahisha ... ...???????? Nyieeeee....Mambo ni ya motooo.???? Kwani wewe auogopi Usipite bila kulike na kukomeniti fanya ku share kabisa ili sehemu inayofuata isikukose maana ndiyo sehemu balaaa????????????????????????????????
..ITAENDELEA...... Hii ni bonge la simulizi isikubali ikupite.
@wafuasi
#itaendelea_story_ni_kali_sana?
Mkiwa wavivu kucoment namimi nakuwa mvivu kupost hivyo comment kwa wingi jamani ili mnie mizuka
# PIA USISAHAU KUNI FOLLOW MIMI KULUTI MC ILI USIWE UNAPITWA NA STORY ZANGU FAIDA YA KUNI FOLLOW NI KUWA WA KWANZA KUPATA STORY KILA NINAPO POST
@everyone.