AIBU YA KUCHELEWA KUOLEWA ILINIFANYA NIKAOLEWA NA JINI ????????
Sehemu ya Tatu ( 3 )
*************
@Kila Mtu
????????????????????????????????????????????????
Taratibu niligeuka na kupiga hatua hadi lilipo gari nikapanda na kuondoka , njia nzima nilikuwa nalia kwa uchungu sana . Kumbu kumbu za matukio yangu na Adam zilijirudia kichwani na kunifanya nizidi kuumia , kwa neema ya Mungu nilifika nyumbani salama na kupitiliza moja kwa moja chumbani kwangu. Sikutaka kuongea na mtu hivyo nikajifungia na kubaki nikilia mwenyewe, nililia na kumuuliza Mungu kwanini ameruhusu niumizwe kila siku.Maana kila mahusiano ninayoingia yanaishia njiani na kuniachia maumivu makali moyoni. Nililia na kulala bila hata kuweka kitu chochote tumboni, kesho yake asubuhi niliamka mapema kama kawaida nikajiandaa na kwenda kazini. Siku hii nilitoka nyumbani nikiwa nimevaa miwani kuficha macho yangu maana yalivimba na kuwa mekundu kwasababu ya kulia sana . Bila kuchelewa nilifika kazin nikasalimia baadhi ya wafanyakazi wenzangu kisha nikaingia ofisini kwangu, nilikaa na kabla sijaanza kufanya kazi sm yangu ikaita.Kuangalia mpigaji ni dada yangu ambae ni wapili kuzaliwa, niliiangalia sm kwa mda na kupokea kinyonge sana . "Hello dada " "Yes mambo" "Poa vp familia inaendeleaje?" "Tuko sawa ,nimekupigia kukwambia nataka kuonana na wewe jioni ya leo" "Aaaam samahani leo sitakuwa na nafasi labda tufanye siku nyingine ""Oooh sawa haina shida" aliongea na kukata sim bila hata kuniaga, kinyonge niliweka sm pembeni na kushusha pumzi kisha nikaendelea na kazi. Jioni ilipofika niliweka vitu sawa na kirudi nyumbani, ajabu nilifika na kumkuta dada akiwa amekaa sebleni. Nilimsalimia huku nikionesha mshangao na kusema " Da Candy! kulikoni uko hapa mda huu?" "Mbona unauliza kwa mshangao hivyo, kwani kuwa hapa ni kosa ama ? Sikia sina mda wa kupoteza nimekufuata ili tuongee vizuri maananaona ukiambiwa kuhusu kuongea unajifanya uko bize." Nilimuangalia bila kujibu kitu nikaenda chumbani na kubadilisha nguo kisha nikarudi na kukaa ,baada ya kukaa Candy akasema . "Elena! Nimechoka kusumbuliwa na baba kila siku ,hivi unampango gani na maisha yako maana unatuweka tumbo joto kila iitwapo leo" "Mpango kuhusu nini na baba anakusumbua kuhusu nini?" "Muone unavyo niuliza kama vile hujui kilichonileta hapa""Aaaa! Sasa nitajuaje ile hali sijaongea na wewe au naonekana Malaika so ninajua mambo hata kabla ya kuambiwa ?" "Acha maigizo yako ,niko hapa kutaka kujua unaolewa lini?" Kauli yake ilinikata maini na kunifanya nibaki namuangalia bila hata kuongea,Candy alikaa kimya kwa mda na kuniuliza tena . "Elena naongea na wewe unaolewa lini?" Nilimuangalia Candy kwa sekunde kadhaa na kumjibu kinyonge " sijui ""Heee! hii ni ajabu ,hivi unajiona mtoto sana si ndio ? Maana kila unapoulizwa jibu lako ni sijui. Elena we ni mtu mzima una miaka 30 sasa nasio 21, hivi huoni aibu au kujisikia vibaya kuona wasichana walika lako wote wameolewa na wanafamilia zao?" "Candy! Hivi kwanini mnanifanya nijione sifai?" "Acha upuuzi nani kakufanya ujione hufai, sisi kuambiwa ukweli ndo kukufanye ujione hufai, au unataka tukae kimya huku ukienda kuwa ajuza bila hata ndoa?"Nilishusha pumzi ndefu na kusema " Candy! Swala la ndoa ni swala nyeti sana na si kila mtu anaolewa kwa wakati anaotaka yeye. Naombeni mniache tafadhali na mda ukifika nitaolewa kwani shida iko wapi?" "Oooh unataka kusema wewe hapo ulipo hujafikia umri eeh mda bado, dada unataka kuolewa ukiwa na miaka mingap 50 au 60 ?" Maneno yake yalinichukiza na kunifanya nimjibu kwa hasira sana ,"sitini haitoshi ongeza 40 , kwani shida yenu ni nini? kwanini msifocus na maisha yenu.
Kila siku kunipigia makelele olewa olewa nitaolewa na majani au nyoka ?" "Acha ujinga wewe hutaki kupigiwa kelele olewa, na Sikia Elena hili swala halitakaa liachwe kuzungumzika hadi pale utakapo fanya maamuzi" "Sawa endeleeni kuongea siku mkichoka mtakaa kimya wenyewe" "Mmmmmm! Poa " Candy aliongea na kuchukua pochi yake akaondoka kwa hasira sana , niliinamisha kichwa chini na fumba macho.Machozi yalinitoka bila kikomo na kuzidi kunifanya nizidi kuumia . ...???????? Nyieeeee....Mambo ni ya motooo.???? Kwani wewe auogopi Usipite bila kulike na kukomeniti fanya ku share kabisa ili sehemu inayofuata isikukose maana ndiyo sehemu balaaa????????????????????????????????
..ITAENDELEA...... Hii ni bonge la simulizi isikubali ikupite.
@wafuasi
#itaendelea_story_ni_kali_sana?
Mkiwa wavivu kucoment namimi nakuwa mvivu kupost hivyo comment kwa wingi jamani ili mnie mizuka
# PIA USISAHAU KUNI FOLLOW MIMI KULUTI MC ILI USIWE UNAPITWA NA STORY ZANGU FAIDA YA KUNI FOLLOW NI KUWA WA KWANZA KUPATA STORY KILA NINAPO POST
@everyone.