Mnamo Machi 8 mwaka 1957 katika jiji la Wilmington lililopo jimbo la Delaware nchini Marekani ndipo alipozaliwa. Akaja kukulia Pennsylvania, akaja kujifunza mapigano akiwa na miaka 13 tu.
Huyu ndiye Cynthia Rothrock ambaye alishikilia rekodi ya ubingwa wa dunia kwenge mapigano ya kawaida na kutumia silaha. Ikiwa ni miaka mfululizo kuanzia mwaka 1981 hadi 1985 alipoamua kustaafu. Akiwa ameshiriki mivhuano zaidi ya 100 ya mashindano pasipo kupoteza.
Alikuja kuingia kwenye uigizaji mnamo mwaka 1985 akicheza filamu iitwayo Yes Madam akiwa na Michele Yeoh. Kuanzia hapo ikawa ni historia kwenye filamu za mapigano, alipowavutia wengi kuanzia waigizaji, watayarishaji hadi watazamaji.
Huyu ni mama wa mtoto mmoja wa kike. Hivi sasa ana miaka 68 akiwa na mikanda meusi saba ua michezo tofauti ya mapigano. Ikiwemo dan ya nane ya Tang soo do, Taekwondo, Eagle claw, Karate, Wu Shu, Northern shaolin na Pai Lum Tao kung fu.
Kaacha alama kwenye sanaa ya mapigano na uigizaji. Je unamkumbuka kwa filamu ipi hasa?
#Mambosreview.