MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 8
SONGA NAYO......
Madam hakuwa na maneno mengine ya kuongea zaidi alijiinamia kama mtu anaefikiri kitu, ili kuepuka kesi mtoto wa mama Mira mie nikaamka na mwanangu haoo mpaka chumbani kwetu na kumuacha madam akiwa amekaa pale.
Muda wa party ulifika naweza kusema bwana party ilifaa na kufaaana yani ilikuwa kama sherehe maana watu walijaa karibia ukumbi mzima, na wageni waalikwa wengi walikuwa wadada ππ
Yani wadada walikuwa wengi na mishangazi nayo haikukosekana kabisa ππ mimi nilikuwa nacheka bwana kila nikitazama namna mabinti walivyokuwa wakijipendekeza kwa Anfrey ndio kabisa nilihisi kuchoka
Unakuta kidada kimevaa kinguo kifupi yani imebakia kidogo tu kalio lionekane hapo ikitokea ameinama awee nyeti zote zinabaki hazarani π€£π€£
Yani ilikuwa tafran tupu maana wadada kila muda walikuwa wanaenda kule mbele ambako alikaa Anfrey na sababu yenyewe haina maana eti tuchukue photo ππ
Kila muda ilkuwa photo mpaka nilichoka kutazama upuuzi, nikiwa na mtoto wangu nilinyanyuka pale nilipokaa ili nielekee chumbani nikapumzike maana muda ulikuwa umeenda sana..
"Mira.."
Nilisikia kuitwa, ikabidi nigeuke nione nani alieniita, bwana si nikakuta ni madam yani huyu mwanamke sijui ananitafuta nini mimi
"Naenda kupumzika mara moja nitarudi.."
Niliongea na sikusubiri hata aongee chochote nikasepa zangu, nimefika chumbani kwangu juu ya kitanda nilikuta boksi yani lilionekana kama kuna zawadi ndani yake namna lilivyokuwa limefungwa
Kwanza nilimshusha mtoto nikamlaza, nilipomaliza nikalichukua lile boksi na kwenda nalo mpaka chooni ili kama kuna kitu kibaya kinitokee mimi na sio mtoto wangu
Basi kufika chooni ndio nilianza kufungua kwa tahadhari kubwa, macho yalinitoka baada ya kukutana na boks la simu, kwanza nilitoka chooni ili nikaangalie vizuri
Kufika chumbani niliwasha taa hata zile ambazo nilikuwa situmii nazo niliwasha π , basi nikiwa na furaha kweli lilikuwa boksi la simu na simu yenyewe ilikuwa simu janja
Aweee kuna furaha niliipata aiseee maana toka nizaliwe sijawahi tumia simu kubwa na nilitamani siku moja nije nitumie smartphone.
Na leo ni kama bahati imejileta mwenyewe , sijui ni nani kanipa hii zawadi basi bwana sikupoteza muda niliweka sim yangu charge kisha nikatoka nje, kwenda kuangalia party namna inavyoendelea.
"Mbona unaonekana una furaha sana..??"
Swatii aliniuliza, kweli nilikuwa na furaha tena kubwa maana kumiliki simu sio mchezo tena hujanunua kwa pesa yako bali umepewa kama zawadi awee furaha zilikuwa zimezidi kiasi kwamba zikaanza kutokea kwenye masikio sasa ππ
"Dah sijui hata niseme nini ili unielewe.."
"Mh nambie kwani kuna nini...??"
"Nimekuta kuna zawadi nimewekewa chumbani na sifahamu nani ameniwekea nilipofungua nikaku..."
Sikuweza kumaliza kuongea hii ni baada ya Naina kufika pale tulipokuwa tumekaaa.
"Mira mama anahitaji kuongea na wewe.."
Baada ya Naina kufika hapo tulipo aliniambia naitwa
"Kuna nini kwani..??"
"Wewe nenda utajua mbele kwa mbele.."
Nikaona isiwe kesi nikashika njia mpaka alipokuwa amekaa madam, alikuwa amekaa na wamama watu wazima na pia hata Anfrey alikuwepo, basi baada ya kufika pale nilipewa kiti nami bila ubishi nikakaa
"Mira kwanza samahani kwa kukuita hapa.."
Alizungumza mwanamke mmoja wa makamo akiwa ananitazama sana, basi mimi sikujua nini wameniitia hapo zaidi nilibaki naitikia tu
"Mira tumependezwa na ufanyaji wako wa kazi, lakini pia tunapenda kukuomba ukubali ombi letu.."
"Ombi gani...??"
"Samahani tupo hapa kuwakutanisha wewe na Anfrey..."
Nikanyanyuka kwa jazba nyie, hawa watu wananiona mie matako yao sasa maana kama mtoto nimekubali kumlea lakini kwa hili siwezi kuwakubalia aisee.
"Mira hebu kaa kwanza.."
Madam aliniambia, nikakaa huku nikiwa nimenuna wakati yote hayo yanaendelea Anfrey alikuwa kimya kabisa akitazama tu namna wazazi walivyokuwa wananiforce.
"Mira sio kwa ubaya lakini.."
Madam alizungumza kisha akaweka kituo me nilikuwa namchora tuu huyu mama.
"Naweza kusema kwamba wewe ndie mwanamke ambaye nimekuona unafaa kuwa mke wa kijana wangu, lakini sikuforce ni maamuzi yako binafsi."
Hapo nikapumua kwanza kisha nikachukua moja ya Glas ya wine iliyokuwa hapo juu ya meza nikanywa kisha nikasimama huku nikiwa nimechachuka balaa.......
ITAENDELEA......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni