TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 11
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Noela alipoondoka hakujua hata aende wapi. Alitembea polepole barabarani, machozi yakimtoka na wala hakujali. Aliumia kwa sababu alisalitiwa na watu wawili muhimu sana kwenye maisha yake💔.
Alikumbuka dalili alizowahi kuona kwamba kuna kitu kinaendelea kati ya Iris na Salmon lakini alikuwa anazipuuza tu😭.
Kisha mwishoni akakumbuka maneno ya Mr. Marvel aliyomwambia muda mfupi uliopita. Akagundua kuwa kuna uwezekano Mr. Marvel alikuwa anajua ukweli tangu mwanzo.
Kwa hasira Akatoa simu yake na kupiga ile namba ya mwisho ambao ilikua ya Mr Marvel.
Wakati huo, Mr. Marvel alikuwa amelala lakini alipoona anayepiga ni Noela, alipokea simu haraka.
Kwa utani akasema “Umenimiss tayari?”
“Kumbe ulijua mwanao analala na rafiki yangu wa karibu halafu hukuniambia?” Noela alisema huku analia
Sauti ya Noela akiwa analia ilimpa ukichaa Mr Marvel mpaka usingizi wote ukamuisha
“Uko wapi sasa?”
“Sijui hata niko wapi! Ila ninachojua ni kiwa Nataka tu kufa…… haya maumivu ni too much”😭
“Uko wapi Niambie, Nakuja hapo sasa hivi”
Noela akacheka kwa uchungu “Nooooo usije. Kwa nini uje? Kwanza ukija Nitakuwa tayari nimeshakufa. Siwezi kuona rafiki yangu na mpenzi wangu pamoja. Inauma sana”😭
Baada ya kusema hivyo, Noela akakata simu na kuizima kabisa.
Aiseee Hilo lilimfanya Mr. Marvel apanic. Hakuwa tayari kumpoteza Noela kwa gharama yoyote. Aliposikia anataka kujiua, akachanganyikiwa kabisa.
Akaamka, akabadilisha nguo then akachukua bodyguards wake na magari kadhaa, akaanza kumtafuta. Alitaka kumpata kabla jambo baya halijatokea.
Wakati huo, Noela alikuwa tayari amefika darajani. Alisimama pale akiangalia maji yalivyo tulia. Maumivu ya usaliti yalikuwa makubwa sana na kitu pekee kilichokuwa akilini mwake ni kujiua ili asisikie maumivu tena💔.
Alidhani Salmon alimcheat kwa sababu yeye ni mnene, mkubwa na si mrembo vya kutosha. Na sio mara ya kwanza kwa watu kumsema vibaya kisa mwili wake.
Alijichukia kwa kuwa mnene kiasi kile. Akaangalia mwili wake akahisi mpaka kichefuchefu.
Basi alitupa pochi yake pembeni kisha akaweka mguu wa kwanza, kisha aweke wa pili ili ajitupe. Mungu bariki kuna mtu alifika nyuma yake akamdaka kwa nguvu.
Hakua mwingine bali ni Mr Marvel! Hamuwezi amini alitumia almoast milioni 3 ili afanikishe kumpata Noela kwa mda mchache! Na kama
Sio yeye tungekua tunaongea mengine kuhusu Noela
Sasa ivi🥺
“Usiniguse!…..Niachie!……Nataka kufa!……Niachie!” Noela Akaendelea kupiga kelele lakini Mr. Marvel hakumuachia.
“Unataka kujiua kwa sababu ya mapenzi? Kwani Wewe ni wa kwanza kuchitiwa???”
Noela akalia kwa sauti “Inauma sana… haya maumivu ni too much……inaumaaa……”😭
“Najua inauma lakini maumivu yanatufanya tuwe na nguvu. Kama kila mtu alie chitiwa angejiua, dunia ingekuwaje? Ivi Umefikiria kuhusu familia yako? Ndugu zako? Unajiua kabla ya kutimiza ndoto zako, kwa sababu ya watu wasiostahili uhai wako???”
“Kama ningejua mapenzi yanauma hivi nisinge jihusisha nayo. Etii amenicheat kwa sababu mimi ni mnene, si mzuri! Hata rafiki yangu amediriki kuniita mimi nguruwe”😭
“Wewe uko perfect ulivyo. Kuwa mnene kunaongeza uzuri wako. Mimi napenda ulivyo, na machoni pangu wewe ni mwanamke mrembo sana! Maisha ni mazuri sema hujakutana tu na mtu sahihi. Mimi nipo na nitakuonyesha ninafaa kwako. Please tulia…….”
Maneno hayo mazuri yalimtuliza Noela. Akamkumbatia Mr. Marvel huku analia na Mr. Marvel akamwacha alie juu ya kifua chake🥰.
Baada ya Noela kutulia, wakaingia kwenye gari na Mr. Marvel akampeleka kwenye nyumba nzuri sana. Nyumba hiyo aliijenga kama sehemu ya kupumzika pale anapokuwa na stress au anataka kutulia.
Nyumba ilikuwa nzuri, simple na classic. Ilikuwa karibu na bahari, hivyo upepo wa bahari ulikuwa unasikika vizuri kabisa👌.
Walipofika Mr. Marvel akampa chumba Noela ili apumzike kwanza maana hapakua hata na haja ya maongezi.
Noela akakubali, akaingia chumbani kulala. Sio kwamba alilala kwa raha??? Hapana, kila aliposhtuka kilio kilianza upyaa mpaka kunakucha.
Jua lilipo chomoza Noela aliamka akaenda hadi jikoni akamkuta Mr Marvel yupo busy anaandaa Breakfast.
Alisimama mlangoni akimtazama kwa muda mrefu huku akimchunguza. Sio siri Mr Marvel ni handsome kinoma hata mtoto wake Salmon hajaurithi u-handsome wa baba yake kama inavyotakiwa maana ingekua balaa zaidi ya hili.
Pia aligundua ni mpole alafu anajali mno, sasa akashindwa kuelewa kwa nini Salmon si kama baba yake🥱
“Hujachoka kuniangalia?” Sauti ya Mr Marvel ilimshtua Noela mpaka akaona aibu
“Sorrry”🙈
Mr. Marvel akatabasamu “its okay! unaweza kuniangalia mpaka uchoke”
“Sipaswi kufanya ivo! By the way Unapika nini?”
“Nakuandalia breakfast”
“Ila mimi Sina njaa” Noela akajitetea
“Izo ni stress tu ndio maana huna hamu ya kula. Unatakiwa Kula hata kidogo ni nzuri kwa afya yako”😊
Noela akajibu “Sawa”
Kisha Mr. Marvel akaandaa meza yenye vitafunwa vichache kama soseji, mayai na sambusa.
Walikaa pamoja mezani wakipata kifungua kinywa huku Noela akila kidogo tu kwa sababu kila akifikiria yaliyotokea jana hamu ya kula inapotea.
Baada ya chai alimshukuru sana Mr. Marvel kwa kumjali kwa muda mfupi waliokuwa pamoja
Mr. Marvel akamuuliza “Mpango wako ni upi?”
“Sijui, Sijisikii kurudi chuo sasa hivi”😔
“Mpaka lini?”
“Sijui! Sitaki hata kumuona Salmon wala Iris. Itauma sana”
“Kwa hiyo unataka kujificha?”
“Ndiyo, Kama hakuna shida, ningependa kukaa hapa siku chache mpaka nitakapokuwa sawa” Noela aliomba🥺
“Unaweza kukaa hapa kwa siku zote utakazo but kumbuka lazima usome. Familia yako inakutegemea”
“Najua! Nahitaji tu muda wa kupona kama wiki moja au mbili tu zinatosha”
“Sawa, no problem”
“Acha niende chumbani” Noela alinyanyuka akarudi chumbani na hapo kilio kikaanza upya.
Alikua anaogopa kulia mbele ya Mr Marvel kwaiyo alijiificha ili alie vizuri. Uzuri Mr Marvel ni mtu mzima anajua kupona kidonda cha mapenzi sio rahisi. Ila
Kwakua yeye yupo, atahakikisha Noela anakua sawa kabisa.
Basi Mchana akaenda kugonga mlango wa chumba cha Noela. Alipofunguliwa, alimuambia Noela
Kuwa kamuandalia Suprise, jambo
Ambalo Noela hakua analitegemea kabisa.
“Nini? Siko tayari kwa surprise” Akatabasamu kidogo😊
“Ni lunch tu. Pia nimekununulia nguo chache, Natumaini zitakutosha” Akampa mifuko yenye nguo na viatu.
Noela akashukuru “Asante”
Baada ya hapo Mr Marvel akaondoka akimpisha Noela ajiandae. Noela alipofungua ile mifuko akakutana na magauni mazuri na pamoja na viatu. Na vyote vilikuwa size yake, imagine hata nguo za ndani zilimtosha. Akashangaa Mr. Marvel alijuaje size zake na yeye ni tipwa tipwa🙈🙈
Basi kwenye yale magauni, alichagua gauni moja jeupe ambalo ndilo alilovaa. Na lilimpendeza sana mpaka Mr. Marvel alipomuona, alijisifia kuwa anajua kuchagua🥰.
So Pembezoni kidogo mwa ile nyumba palikua pameandaliwa special kwaajili yao. Kulikua na vyakula, vinywaji na kulipambwa pakapambika.
Mr Marvel alifanya vile kwa matumaini ya kumfuraisha Noela na kweli alifanikiwa kwani Noela alikua hakaukwi na matabasamu usoni.
Tena hasa U-gentleman wa Mr. Marvel ulimvutia mno. Kulikuwa na mambo aliyomfanyia ambayo Salmon hakuwahi kumfanyia kabla..
Sasa Wakiwa wanakula, Noela akamuuliza Mr Marvel swali la kizushi
“Mkeo yupo wapi?”
“Mke gani?”😳
“Si Mama Salmon?”
Mr. Marvel akatabasamu “Ooooh…”
“Hautaki kuniambia? Niko interested maana sijawahi kumsikia Salmon akimzungumzia”
“Yeah! Ni kweli Lakini tule kwanza, Tukimaliza nitakuambia kila kitu unachotaka kujua kuhusu mimi. Sawa, msichana wangu?”
Noela akasema “Sawa”
Wakaendelea kula kimya kimya huku Noela akimtazama kwa siri siri. Kadri walivyoendelea kuwa pamoja ndivyo alivyozidi kuvutiwa na Mr Marvel bila yeye kujua.
Baada ya kumaliza kula, Mr. Marvel akamshika mkono wakaenda kutembea ufukweni. Walitembea, wakacheza na maji kidogo, wakakimbizana kama watoto. Ilikuwa moment nzuri sana👌.
Walipochoka na kupumzika, ndipo Mr. Marvel akaanza kumwambia ukweli kuhusu mama yake Salmon.
“Miaka michache iliyopita, nilikuwa na mke mzuri sana niliyempenda. Lakini wakati huo sikuwa na kitu licha ya kuwa msomi mwenye Degree ya Engineering. Hata milo mitatu kwa siku sikuweza kumudu. Nilifanya kazi kwa bidii but mapenzi na juhudi hazikutosha. Wife Alitaka maisha ya kifahari, pesa na mimi sikuwa navyo. Aliamua kuniacha lakini akagundua ana mimba ivyo akahairisha kuniacha kwa mda! Alivumilia mpaka alipojifungua Salmon ndipo akaondoka na kuniachia mtoto”
Noela akashangaa “Nini?”😭
“Ilikuwa ngumu sana kwangu, kufanya kazi na kulea mtoto mchanga kwa wakati mmoja”
Noela akauliza “Halafu nini kilitokea?”
Unajua nini kitatokea baadaye?
Nakuja………
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni