TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 6
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Kwaiyo Mr Marvel akahairisha kwenda eneo la pool, badala yake akamfuata Noela nyuma na kumuona akiingia chooni.
Huko ndani Chooni, Noela alikua anatoa tu machozi kama hana akili nzuri. Moyo ulimuuma sana sio mchezo, tena mbaya zaidi ni namna ambavyo Salmon alikua akishikana shikana na wanawake wengine akiwemo Iris💔.
“Sipaswi kulia, labda kalewa tu ndo maana anafanya vile…..” alijifuta machozi taratibu akijipa moyo.
Dakika zile zile mlango ukafunguliwa na Mr Marvel akaingia. Kitu cha kwanza alicho kifanya ni kumkumbatia Noela kwa nyuma.
Kwa akili za Noela alidhani ni Salmon kaja kumuomba msamaha kumbe hata sio. Alichogundua ni kwamba siku hiyo alihisi msisimko sana aliposhikwa tofauti kabisa na siku nyingine ambazo Salmon humshikaga.
Akageuka taratibu ndipo hapa alipohisi kuzimia baada ya kukutana na Mr Marvel. Hata yeye hakuwai kumsahau kabisa hasa kwa kile alichomfanyia.
“Wewe…. Wewe….. ulini…….” Hakupata hata mda wa kumaliza sentensi yake.
Kwanza Mr Marvel alimtuliza kwa busu moja zito kuonyesha ni kiasi gani alimmiss. Na kuna namna lile busu likamchanganya Noela, lilikua tamu alafu pili Mr Marvel hakua na papara. Yani slowly slowly sio kama Salmon.
Noela alitamani sana kama wangeendelea ila kwakua yeye ni mpenzi wa mtu, hakupaswa kufanya vile! Alikusanya nguvu za kutosha na kumsukuma Mr Marvel pembeni.
“Kaa mbali na mimi please”🗣️😡
“Why??”
“Mimi ni mpenzi wa mtu, na ninampenda mpenzi wangu sana tu kwaiyo tuheshimiane. Kwanza hujui ni kiasi gani nakuchukia kwa kile ulicho nifanyia”
“First, sijali kama una mpenzi, also I know sikufanya kitu kizuri and i am sorry! Uliposema hautaki nilipaswa kuacha ila haikua ivyo”
“Kama umetambua kosa lako vizuri” Noela alitaka kutoka kule chooni ila Mr Marvel akamzuia maana hakua kamaliza kuongea nae.
“Unaenda wapi sasa wakati bado hatujamaliza kuongea?”
“Kuna kipi kingine cha kuongea?”😡
“Kuhusu sisi!”
“Sisi na nani?? Hakuna chochote baina yetu!”
“Hahaha! Do you think kwamba ni rahisi namna iyo?? No! Sijawai kuwa interested sana na mwanamke mwingine zaidi yako kwaiyo please nielewe”
“Mbona unakua mgumu kuelewa? Nimesema ivi sitaki mazoea na wewe!”
“Sijuagi hapana katika maisha yangu, kaa ukijua ilo” alimpisha Noela atoke huku akiwa anatabasamu😊
Apo Noela alikua kachukia balaa, alirudi chumbani kwa Salmon, akavua ile swimming suit akavaa nguo zake za kawaida.
Baada ya hapo akarudi kule kwenye party akiwa anaona aibu vibaya mno. Bado watu hawakuacha kumtazama na kumsema. Yani alikua kama topic kwenye midomo ya watu.
Salmon alipomuona alimfuata akiwa kachukia
“Ndo nini sasa kuaibishana Noela??”😡
“Nimekuaibisha vipi wakati ile nguo ni wewe ndie umeni nunulia??”
“Kwaiyo? Kama haikua inakutosha si usinge vaa!”
“Nisinge vaa ili uje unikasirikie tena?? Nilivaa kwaajili yako na sikutaka ujisikie vibaya kwenye birthday yako!”
“Ni bora mara mia usingevaa kuliko kuja kuniaibisha na limwili lako ilo kama fenesi”🗣️
“Umesemaje Salmon??!” Noela alishangaa maana hapo mwanzo Salmon hakuwai kumkosoa mwili wake hata kidogo iweje leo afanye ivo?🤔
“Kwani umesikia nini?”
Kabla Noela hajajibu walisikia sauti nyuma yao. Ile sauti ilimfanya Salmon ageuke haraka akiwa ana wasiwasi
“Dad! Umerudi……”
“Yes and hiki ni nini???” Alisema Mr Marvel kwa kufoka na hapa ndipo tunajua kuwa Mr Marvel ndie baba mzazi wa Salmon🔥
Kuona vile Noela akaishiwa nguvu kila mahali, unajua lazima upate presha maana sio kwa kile kilichotokea baina yake na baba mkwe! Aiseee😰
“Ni Party!…….Ni birthday party yangu”
“Ndo ufanye nyumbani??? And unajua kabisa sipendi kelele pindi ninapo rudi nyumbani kupumzika! So please Party its over! Watoe watu wako” Mr Marvel alifoka akiwa bado hajamuona Noela
“Sorry Dad nimeelewa! Also nataka kukutambulisha mpenzi wangu yuleee nilie kuambia! Anaitwa Noela” Salmon alimshika Noela mkono akamgeuza upande aliokua kasimama Mr Marvel, so wakakutana uso kwa uso.
Hakuna kitu kilicho mchoma Mr Marvel kama kugundua kuwa mwanamke anae uchanganya moyo na ubongo wake ndie mpenzi wa Mtoto wake.
Alimuangalia Noela pasipo kummaliza huku akichemka ndani kwa ndani kwa wivu💔.
Je nini kitaendelea?
Nakuja……….
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni