KANUNI 31 TAKATIFU (BRO CODES)
1. Usimdhuru mwanamke kwa njia yoyote ile – hasa kingono.
2. Mwanaume halazimiki kupika vyakula vitamu kila mara, lakini siyo kosa kujifunza.
3. Ni vyema wanaume wawili kutokuwa uchi pamoja – heshimu mipaka ya mwili.
4. Mwanaume wa kweli huogelea kwa maji ya baridi; anaulinda uzalendo wake.
5. Mwanaume wa kweli hujua muda wa kuondoka bila kuambiwa.
6. Usimuulize Mwanaume jina lake kila mara – mkiitana “Bro,Chef, Kiongozi inatosha
7. Nguo zako zikitoa harufu kali, unapaswa kujijali – usitumie hilo kama sifa, Mwanaume hasifiwi kwa uchafu
8. Ukiona mpenzi wa Mwanaume mwenzako yupo, jiondoe bila kusubiri kuambiwa.
9. Usimchekelee Mwanaume mwenzako ili kuwapendeza wanawake.
10. Mwanaume wa kweli halipi pesa ili kupata mapenzi , kamwe.
11. Mpenzi wa Mshikaji wako wa zamani, nawe ni wa zamani – ni mwiko kumtamani , acha kabisa hii tabia chafu.
12. Mwanaume Tafuta hela kwanza kabla ya kutafuta mapenzi.
13. Mwanaume wa kweli hakikisha Kama hupendi filamu fulani, ni sawa – lakini usiwadharau wanaoziangalia.
14. Dada wa Mshikaji wako ni kama dada yako pia – Muheshimu sana.
15. Tazama maudhui yenye maana, lakini usihukumu wanachokitazama wengine . ( Mfano kama unatazama movie nzuri inayoelimisha wengine wanatazama katuni pembeni yako achana nao usihahukumu )
16. Ukifanikiwa, Usimtupe yule aliyekuwa nawe – mbadilike pamoja kimaisha wote mfanikiwe.
17. Usifanye majukumu ya mume kama mwanamke huyo bado ni demu wako tu wa kawaida ( hujamuoa ).
18. Mwanaume wa kweli hakati tamaa – anapumzika na kuendelea kupambana.
19. Ukiambiwa na mwanamke wewe ni dunia yake, kumbuka dunia inazunguka – usijisahau.
20. Mwanaume Usichukulie mapenzi kwa uzito kuliko maendeleo yako binafsi.
21. Usisaliti Mwanaume mwenzako kwa mwanamke wake – uaminifu ni msingi.
22. Mwanaume Ukipewa siri, iwe siri milele.
23. Mwanaume wa kweli hujali usafi na muonekano wake.
24. Usibishane na Mwanaume mwenzako hadharani – mzungumze faraghani myamalize kiume.
25. Mwanaume huinua Mwanaume mwingine – si kumporomosha.
26. Usimtangazie kila mtu matatizo ya Mwanaume mwenzako– mlindie heshima.
27. Mwanaume wa kweli huomba msaada, haoni aibu kusema “sina” au “nisaidie”.
28. Msichana akimkataa Mwanaume mwenzako, wewe pia huna nafasi – ni heshima.
29. Usivunje uhusiano wa Mshikaji wako kwa umbea au fitina.
30. Mwanaume mwenzako si adui, hata mkikosana – mshikamane bado.
31. Kuwa Mwanaume wa kweli si jina, ni matendo.
Kama unakubaliana na hizi kanuni react hapa wewe ni Mwanaume wa nguvu 👊💪.