TIPWA TIPWA NA MR MARVEL SEHEMU YA 17 - 18
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Siku iliyofuata, Noela alipofika chuoni alihisi hali si ya kawaida. Watu walikuwa wanamuangalia kwa macho ya ajabu, wengine wakinong’ona pembeni yake. Alijaribu kupuuza lakini hali ilikuwa mbaya zaidi alipoingia darasani😭.
Mwishowe, rafiki yake mmoja akamwonyesha picha zilizosambazwa kwenye magroup. Aliona picha zake pamoja na maneno ya kumdhalilisha. Hapo ndipo alielewa kwa nini kila mtu alikuwa anamtazama vile.
Alishindwa hata kusoma siku iyo, Akaamua kuondoka chuoni na kurudi nyumbani😭.
Tukija kwa mama Salmon, alikuwa akiwaza sana ombi la mwanae. Alikuwa na hisia bado kwa Mr Marvel, lakini kurudiana naye haikuwa rahisi kwa sababu Mr Marvel hakumtaka tena.
Baada ya kufikiria kwa muda, akaamua kurudi Dar ili akajaribu bahati yake huenda akarudi kwa mumewe kama zamani.
Jioni Mr Marvel aliporudi nyumbani, alimkuta Noela analia. Haraka akamsogelea Akamuuliza, “Kuna nini?”
“Chuo kizima kinanicheka. Wanasema nimetembea na baba na mtoto”😭
Mr. Marvel akakasirika, akidhani ni Salmon ndiye aliyesambaza maneno yale. Akamkumbatia Noela na kusema “Usijali. Haya mambo yataisha”
“Siwezi kwenda chuo tena. Sina amani mimi”🥺
“Pumzika nyumbani kwa siku mbili. Baadaye utaendelea kwenda chuo, kama utaona bado hali ni ngumu, nitakutafutia chuo kingine! Sawa”
“Sawa” Noela akakubali huku Mr. Marvel akimbembeleza ili ajisikie vizuri🥰
Kusema kweli Hata Noela alikuwa ameanza kuwa na hisia kwa Mr. Marvel lakini kwa jinsi mambo yaliyokuwa yanaendelea, hakuona kama anaweza kuanzisha uhusiano naye tena💔.
Basi Siku iliyofuata, Salmon alifika ofisini kwa baba yake. Lakini hakuwa peke yake, alikuwa pamoja na mama yake, Grace.
Mr. Marvel akashangaa kuwaona pamoja. Akamuuliza “Grace, umefika lini?”
Grace akajibu “Nimefika muda si mrefu”
“Okay karibuni mkae” Wote wakakaa ili kuzungumza. Salmon ndie alikua wa kwanza kuongea
“Dad! Sitaki kukuona na Noela”
“Ninamjali na nampenda Noela. Ni ngumu kuwa mbali naye”
Salmon akakasirika “Siwezi kukubali hilo”😡
“Kwanini huwezi kukubali??? Nilikutana na Noela kabla hata sijajua kuwa una mahusiano nae! Kabla hata hujanitambulisha kwake! Na toka siku hiyo nilimpenda mpaka leo” Mr Marvel alikua mgumu kuelewa.
Kuona kuna uwezekano baba na mtoto kupigana, Mama Salmon akamuomba Mr Marvel kama mzazi mwenzake
“Tafadhali achana na mpenzi wa mtoto wako. Tujaribu kurudiana na kujenga familia yetu tena! Huu umri sio wa kuhangaika na vibinti Marvel”🥺
“Siwezi kurudiana na wewe. Sababu sina mapenzi na wewe! Moyo wangu na hisia zangu anazo Noela tu! Huyo ndo mwanamke ninae taka kuwa nae” Mr Marvel aliongea kwa hisia kiasi kwamba Mama Salmon akaona kweli anamaanisha anachokisema.
Pia akagundua jinsi gani Mr. Marvel anampenda Noela. Aliona anampenda sana kuliko hata alivyo mpenda yeye zamani💔.
“Ooooh unampenda sana??? Basi Chagua moja Mimi mwanao au huyo mwanamke” Salmon alisema kwa uchungu.
Maskini Mr. Marvel akabaki kimya kwa muda. Anampenda sana mwanae kuliko kitu chochote na upande mwingine anampenda Noela kwaiyo kuchagua ni ngumu.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni