TIPWA TIPWA NA MR MARVEL. SEHEMU YA 13
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋
Dakika chache baada ya Noela kuondoka, Salmon aliingia akiwa anatoka jasho. Alimtazama Iris na kusema “Nimesikia Noela alikuwa hapa”
“Nani amekuambia hivyo?”😳
“Nina watu wangu kila mahali, hivyo niambie ukweli, alikuwa hapa?”
“Ndiyo, alikuwa hapa”😠
“Kwa nini huku niambia kwamba alikuwa hapa?”
“Sikuona kama hilo ni jambo muhimu kwako kujua. Pia, alikuja kuchukua nguo zake na vitu vyake vyote”
Salmon akashangaa “Unamaanisha nini?” 😳
“Namaanisha Noela ameondoka hostel. Na ninavyoona, kuna mwanaume nyuma yake. Aliletwa hapa na gari kubwa la bei kali. Nafikiri ni huyo huyo mwanaume aliyemnunulia zile zawadi”
Salmon akafura kwa wivu, Akakasirika mpaka akaenda kupiga ngumi ukutani.
“Una akili sawa kweli? Unapiga ukuta kwa sababu yake? Kwa sababu ya yule tembo?” Iris alitoa macho
“Huyo tembo ni muhimu sana kwenye maisha yangu kuliko unavyoweza kufikiria. Sitakubali kumpoteza kirahisi, Iris. Na yote haya yametokea kwa sababu yako. Nimepoteza mtu muhimu sana kwangu….”🥺
“Lakini mimi pia ni muhimu kwako”
“Kila mtu kwenye maisha yangu ana umuhimu wake, lakini Noela ni wa kipekee. Huwezi kuelewa” Baada ya kusema hivyo, Salmon akaondoka zake.
Hili lilimuumiza sana Iris. Alifanya kila kitu ili Salmon ampende, lakini haikufanya kazi. Kila siku hali ilizidi kuwa mbaya zaidi💔.
Akaona kama kwa Salmon ina gonga mwamba, basi hana namna zaidi ya kumkwapua mwanaume anayemhudumia Noela kwa sababu anaonekana ana pesa. Akimpata huyo hata Salmon hatakua na maana tena kwake. Ila Iris🙌
Basi Wiki hiyo, Noela alianza kuingia darasani. Alikuwa analetwa chuo na dereva wa Mr. Marvel na akimaliza masomo, anaingia kwenye gari na kurudishwa nyumbani.
Na apo Salmon alikua anajaribu sana kuzungumza naye, lakini hakupata nafasi kwa sababu alimkosa mara kadhaa. Hakujua kabisa kama Noela alikua analetwa chuo kila siku na gari la baba yake.
Sasa Siku moja, akaamua kusubiri nje ya darasa la Noela. Baada ya vipindi kuisha, Noela na wanafunzi wengine walikuwa wanatoka nje. Hapo ndipo Salmon alipata nafasi ya kumshika mkono Noela na kumvuta pembeni ili wazungumze.
Noela kwa hasira akafoka “Unataka nini?”🗣️
“Nataka kuzungumza na wewe maana umekuwa ukinikwepa kwa muda mrefu”
“Salmon hakuna cha kuzungumza. Kumbuka tayari tumeachana”
“Hakuna sababu ya kuachana, Ilikuwa ni kutoelewana tu. Tunaweza ku fix na kuendelea na uhusiano wetu”
“Hilo haliwezekani”
“Kwa nini haliwezekani? Au kwa sababu tayari una mwanaume mwingine?”
Noela akatabasamu “Ni kwa sababu ulinisaliti na rafiki yangu wa karibu. Ingekuwa afadhali kama ungecheat na mwanamke mwingine, lakini umefanya na rafiki yangu Iris. Hukuwa na hata aibu??”
“Najua nilichofanya ni kibaya sana. Samahani Noela, kweli najuta. Sikuwahi kufikiria mambo yatafika hapo momy pleasee”🥺
“Hakuna kurudiana Salmon! Asante kwa kila kitu ulichonifanyia kwenye maisha yangu”
“Please usifanye hivyo……….Nakupenda………Nakupenda, please…….usiondoke”
Noela hakusema chochote, Aliutoa mkono wa Salmon na kuondoka bila hata ya kugeuka nyuma.
Yote haya yalionwa na Iris Aliejaa hasira, alikasirika sana na akaanza kupanga jinsi ya kuharibu maisha ya Noela.
Unajua nini kitatokea baada ya hapo?
Nakuja…………
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni