*LECTURER NIKIKUPA HUTONINANII* Chapter 12 Niliingia ndani, mama alikuwa ananisubiri kwa hamu kweli maana
"Haya Famrish na Hemed nendeni ndani nataka niongee na huyu dada yenu mjinga mjinga yaani leoo nataka anijibuuu kila swali langu" Famrshi alimchukua Hemed na kwenda nae ndani yeye akabaki na mimi sebuleni "Enhee humu ndani kwangu siku hizi nafuga makahaba sio watu. ambaoo wanawatongoza wanaumee za watu si ndio?, mama yako nilikuwa ndioo nina mambo mengi ila sikuwahi kumtongoza mwanaume kwenye maisha yanguu upo hapo, haya nataka majibu yanguu wewe mpuuzi, tena nijibu haraka ipasavyoo maan naweza kukuuuwa kw ajinsi nilivyo ninahasira na wewe mtoto mjinga, Fatha kanielezea kila kitu mpuuzi wee, na bado ukaenda kutembeea na lecturer wenu si ndioo hivi wewe mtoto umeenda shule kufanya umalaya si ndio?" alikuwa anaongeaa mama hapuziki mimi sikutaka kumkatisha kwa maswali yake nikamuacha tu aseme maana ndio nahisi hasira zake zitaishia hapo mimi japo nilikuwa najua mama yangu ili hasira zake ziishe lazima anibutuee kisawa sawa yaani mpaka maji niyaitee mmma
"Huna majibu ya kunijibu sio, na bado nataka nijuee jana ulilala wapi wewe mshenzi hivi hao wanaume wamekusaidia nini mpaka leo si upo kama mama yako hap nilivyoo, hivi hapa ndio unapata mimba kwa mfano si unakuja kuongeza mizigoo wee mshenzi wewe, yaani wanaume wako wa maana ni mmoja tu na ninahisi pia ni mwanaume wa mtu wewe mjingaa hivi kwani..... hakumalizia sentensi akanirukia na kuanza kunipiga, jamani alinipga miguni akaona haitoshi akachukua fagio alijua kunipiga jamani nilipigwa mimi kha nilivimbaa jamni mpaka kuna mahala alinichana alinipiga mpaka akahakikisha ameridhikaa akaniacha siwezi hata kutembeaa hapo ni ninaliaa mpaka sauti ikakauka alikuja Famrish akaninyanyuaa taratibu akanipeleka chumbani kwangu nikapumzikee, ilikuwa ni majira ya saa 12 sasa maan chuo nilitoka saa 10 nililala sikutaka kusumbuliwa kabisaa nililala yaani kiufupi sikutaka fujo masikioni mwangu maana hata simu ilipoitaa sikupokeaa ila nilishtuka saa 6 usiku nikakuta aliekuwa akipiga ni lecturer nilijaribu kumpigia hakupokeaa, nikajua tu atakuwa amelala
Asubuh ilifika na mdogo wang Famrish alienda shule na mimi nikabaki zangu chumbani nimelala hata mama alijua tu kwamba leo. sitoenda chuoo, maana alikuwa amenipiga vikali mama yangu huwa ana huruma sana alikuja na maji ya motoo akaanza kunikanda huku akinichamba ila hakuwa ananichamba kwa kufoka alikuwa ni kama ananipa ushauri, hii ilinifanya niwe huru kumuelezeaa mama yangu kila kitu, kuhusu hyo video huyo sama, mpaka huyo lecturer na jinsi alivyonisaidia maana jumatatu nilikuwa naanza kazi rasmi
"Anaonekana ni mtu mwema na hana mambo mengi, ila wewe nae mjinga unawezaje kwenda kukutana na mwanaume bila kujua historiaa yake wewe vipi hata kama nilikuwa nimechangamka wakati wangu ila nilikuwa sikutani na mwanaume bila kumjuaa historia yake" alisema mama nilicheka tuu etty alikuwa kachangamkaa mhh mama naee hapana kazidi " sawa mama nitamuuliza" nilimjibu mama" ila wanaume sio watu wa kuwamini kabisa mwanangu japo alipokuja asubuhi alinipattia 400k shga angu, hhh hapa mpenzi umepata ila sasa awe mpenzi wa mtu uabishwe tena hhh ntakucheka" alisema mama nilimtizma tu maneno yake yalikuwa yameniingia japo aliongea kiutani, "haya pumzika sasa usikilizie maumivu alisema mama huku akitoka nje kwenda kuandaa chakula,ile anatoka tu na lecturer akapiga tukaongeaa nikamuhadithia kila kitu alinionea huruma na aliahidi kuja kuniona
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
