NAISHIWA PAWA๐ซ SEHEMU YA "4_5" ๐ Ujumbe ule mfupi wa mandishi niliotumiwa na Boss Hance ulisomeka kama ifuatavyo..... ""Hello Pink
Nilimuitikia ikabidi niamke nikajiandaa chapu kisha nikaondoka kuelekea ofisini......nilifanya kama alivyonielekeza Boss Hance niliwapokea wageni wake nikawaomba wamungoje ndani ya muda mfupi tu atakuwa kaishafika...... na kweli baada ya Dakika 45 Boss Hance aliingia ofisini akaniomba nimwandalie kikao na hao wawekezaji wawili waliokuwa wanamungoja pale ofisini niliandaa kikao haraka baada ya Hance kuingia kwenye kikao wafanyakazi wote pale ofisini tuliitwa na mama yake Hance kama nilivyokwisha waambia kwenye kampuni niliyoajiriwa ni kampuni ya kifamilia inayoongozwa na Boss Hance kama Mr C.E.O baba yake Hance ambaye ndo manager wa kampuni bila kumsahau mama yake ambaye yuko katika kitengo cha uhasibu......mimi nimeajiriwa pale ofisini kama secretary wa Boss Hance.......Madame Laura ambaye ni mama mzazi wa Boss Hance alikuwa akitutaarifu juu ya birthday ya kijana wake wa pekee ambaye ni Boss Hance.....
Madame laura alisema ya kwamba Weekend ijayo itakuwa ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa mtoto wangu Hance natamani tuungane staff wote tufanye kitu kwa ajili ya Boss Hance na awamu hii natamani sherehe yake iwe ya tofauti na sherehe zingine...... naombeni mawazo yenu kipi kifanyike?!......staff members walianza kuchangia mawazo juu ya birthday ya Boss walipendekeza iwe ni birthday ya tofauti kidogo.....na kwa kuwa hiyo birthday iliangukia siku ya Weekend siku ambayo hatuendi kazini staff wote tulikubaliana tukutane katika eneo tulilolichagua tupike aina ya vyakula mbalimbali ikiwemo keki tulipanga kufanya wenyewe kwa mikono yetu kwa ajili tu ya kumfurahisha Boss aone ni kwa kiasi gani tunavyomjali madame Laura alifurahi sana alitushukuru na kutuambia kuwa sisi ni kama familia yake...... siku zote nimekuwa nikioda kila kitu kuanzia vyakula keki na kila kitu kwa ajili ya birthday ya mwanangu kiukweli hii itakuwa birthday ya tofauti sana kwake na nina imani ataifurahia sana aliongea madame Laura huku akiwa anatuhug kila mtu......
Sasa bwana pale ofisini kuna wafanyakazi kutokea nchi mbalimbali kila mfanyakazi alipendekeza kupika chakula cha kikwao kisha tuone Boss Hance atapendelea chakula cha nchi gani ๐คฃ๐คฃ๐คฃhii tuliifanya kama challenge ๐คฃ๐คฃ๐คฃlol mie mtoto wa kihaya niliwaza nipike nini au niagize senene kutoka Bukoba๐คฃ๐คฃ๐คฃhahahaaaa tutajua bwana kumbuka zimebakia siku tatu tu kufika birthday ya Boss.....madame Laura alituomba staff members wote kila mmoja aandike jina lake katika kikaratasi pamoja na aina ya chakula atakachopika tulifanya hivyo kwa bahati mbaya chakula cha kiafrica nilichokichagua kukipika kilichaguliwa na staff members mwenzangu ambaye yeye anatokea nchini Kenya๐ซ๐ซ๐ซilibidi nimuachie apike yeye kwa sababu hapakutakiwa kupikwa chakula cha aina moja na watu wawili basi mie niliombwa nipike keki nyieeeeeee๐คฃ๐๐คฃ hiyo keki sijawahi hata kuipika lakini nilikubali tu sikutaka madame ajue kuwa mimi sijui kupika๐ฉ๐ฉ๐ฉ
Jioni ya siku hiyo nilipokuwa njiani kurudi nyumbani Jordan alinitumia sms alikuwa akinijulia hali tu......aliniandikia hello Pink how are you Doing?! Nikamjibu I'm fine niko poa Jordan๐๐.......but natamani kuongea na wewe kuhusiana na jana kushindwa kuja kuonana na wewe๐๐๐ its okay Pink naelewa kuwa boy Friend wako ni wa muhimu kuliko kitu chochote usijal......mmmhhh Jordan what are you talking about๐๐๐ I don't have a boyfriend yule ni Boss wangu na hakuna chochote kati yetu๐ฅบ๐ฅบ.... sorry Pink nilihisi huenda akawa boyfriend wako kwa sababu hata tembea yenu ni kama mtu na mtu wake vile mlivyokuwa mmeshikana mikono yenu ilionekana kama watu mnaopendana niambie ukweli kwa sababu sitaki kuwa msumbufu nikajaonekana kama vile ninataka kukuvunjia mahusiano yako....... hapana Jordan wala hata haiko hivyo......naomba tuonane leo....... ni sawa Pink lakini kwa leo naomba upange wewe maana mimi naweza nikapanga ukashindwa tena kutokea nitajisikia vibaya tena kama jana๐๐๐..... its okay ngoja nikifika nyumbani nitakwambia wapi tukutane.....tulikubaliana kukutana.....
Niliendesha gari kwa kasi huku nikiwa nimeachia tabasamu murua lol Jordan anaonekana mwenye wivu sana hahahaaaa hata hivyo mwanaume mwenye wivu ndo mwenye upendo wa kweli natamani Jordan angekuwa mzima ili tuweze kupendana mimi na yeye๐ฐ๐ฐ nahisi ni kama moyo wangu unafeel kitu juu yake au namhurumia tu kutokana na ulemavu wake kiukweli hata sijielewi๐จ๐จ๐จ nilipofika nyumbani nilimtafuta soo_ha nilitaka anisaidie kuchagua sehemu tamu na tulivu kwa ajili ya mimi kwenda kukutana hapo na Jordan hahahaaa we mbwa ushapenda hebu nitambulishe nimjue shemeji yangu nisije kumdangia๐น๐น๐น soo_ha ni mkorea lakini anaongea huyo kama mbongo๐คฃ๐คฃ๐คฃ soo_ha mimi ni wifi yako kwa Leeminho nataka tu kutoka na rafiki yangu kuna ishu tunaenda kupanga mara moja ok nipe dakika chache nikutafutie sehemu nzuri๐ฅฐ๐ฅฐ alloh thank you my friend that's why I love mwaaaaaaa๐๐๐๐ nilimkiss chaumbea wangu kisha nikakata simu baada ya kukata simu dakika chache ikaingia msg kutoka kwa soo_ha alinitumia jina la pub maridhawa iliyotulia akaniambia hiyo
itanifaa sana na mtu wangu ninayeenda kukutana naye......
Nilimtumia Jordan jina la sehemu tunakokutana na kweli usiku mida ya saa mbili tukakutana hapo nilikuta tayari kaishafika ananisubilia tu mimi nilipofika alinipokea nilimkumbatia mimi kwa sababu yeye kusimama hawezi......alikuja akiwa na ile zawadi aliyoninunulia alinipatia lakini akaniomba nisiifungulie pale pub alitaka niifungue nikiwa Peke yangu๐๐๐ tulipata vinywaji pamoja na dinner bila kusahau story za hapa na pale...... usiku huo Jordan aliniambia kuwa siku yake ya kuzaliwa imekaribia na anatamani siku yake hiyo aisheherekee akiwa pamoja na walemavu wote wa miguu walioko katika mazingira magumu alisema kuwa anatamani kuwanunulia baiskeli walemavu kadhaa wanaokosa uwezo wa kutembea kutokana na ulemavu wa miguu pamoja na miguu ya bandia kwa watoto wa kike baadhi wenye uhitaji wa miguu bandia..... lakini pia Jordan alitamani sana namimi niwepo katika sherehe yake hiyo ya birthday......wow Mungu akubariki sana Jordan kiukweli una moyo wa utoaji ubarikiwe sana lakini pia usijali kuhusu mimi nakuahidi nitahudhulia na nitachangia chochote kitu kwa ajili ya walemavu birthday yako ni lini kwani?!....... kiukweli nitaufurahia sana uwepo wako Pink birthday yangu siyo mbali zimebakia siku tatu tu...... haaa๐ณ๐ณ๐ณ
Unamaanisha nawe birthday yako ni weekend ijayo?!..... ndiyo Pink birthday yangu ni jumamosi ijayo......duh birthday ya Boss Hance na Jordan zimegongana๐๐๐
Je kati ya birthday ya Hance na Jordan Pink atahudhulia birthday gani?! Kumbuka birthday zote zimeangukia siku ya jumamosi...... ni Jordan au Hance?!
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni