Simulizi za john
0789 824 178 ,
1000
Nikasema, βMama, hakuna chochote, baba alikuwa anaangalia vidonda tu.β Akasema, βUnasemaje? Baba? Baba gani? Babako yule? Unamudu ili unibadilishe uishi kwenye ghorofa hii, si ndiyo? Unaona ninafaidi, unataka kuwa mke mwenza, si ndiyo? Ulimuonyesha nini huko chini?β Nikasema, βMama, mbona unaniambia maneno ambayo sielewi? Unanionea!β Akasema, βNani anakunea?β Alinishika, akanibamiza ukutani, akasema, βNitakuua!β Nilipasuka kichwani kisogoni, damu zikamwagika. Mama hakustuka, akaendelea kunipiga, kisha akasema, βToka kwangu, toka!β Akanisukuma nje huku navuja damu, nalia, bila kusema nisameheβnilishaamua kuondoka, bora nikafie mbali.
Nikimkumbuka mama na bibi yangu, nilitamani kurudi, lakini baba yangu ni mkatili, ataniua. Nje ya nyumba kuna kibaraza chenye ngazi, akanisukuma, nikabiringika kama mzigo, nikatua chini. Masai aliona, akaja akikimbia, lakini mama aliniokota, akaanza kunipiga tena, akisema, βOndoka kwangu, mshenzi!β Nikaskia sauti, βMama Zawadi, mshenzi wewe, mwache mtoto wa watu!β Alikuwa Baba Zawadi. Masai alinishika, nikiwa navuja damu puani na mdomoni, bila nguvu. Baba akasema, βMasai, kampakie kwenye gari haraka! Na wewe, mwanamke mkatili, nikirudi nisikukuteβuna roho mbaya kama paka!β
Masai alinibeba, nikatolewa nje ya geti kwenye gari la baba. Baba alipanda, akasema, βMasai, hakikisha nikirudi simkuti yule mwanamke, nitamuua!β Aliwasha gari. Nakohoa damu, baba akaogopa, akasema, βZawadi, nakupeleka hospitali, sawa?β Sikuweza kusema. Alipita kwa polisi, akachukua karatasi, tukafika hospitali. Alinibeba, akipiga kelele, βNesi, daktari, nisaidieni mtoto huyu!β Walinipokea, nikawekwa kwenye kitanda cha emergensi. Nilitibiwa, lakini sikusikia maumivu, kama sielewi kinachoendelea. Nilipopewa dawa, nikapitiwa na usingizi.
Niliamka niko kitandani, bila nguo, nimefunikwa shuka. Nikajiona niko hospitali, chumbani chenye vitanda vinne, lakini hakuna mtu. Nilianza kukumbuka yaliyonipata, machozi yakanitoka. Nesi akaja, akasema, βMuda wa dawa, binti mzuri, umeamka?β Nikasema, βNdiyo.β Akasema, βUnajisikiaje?β Nikasema, βNafuu.β Akasema, βKakako anakuja, yupo njiani.β Nikashangaa, βKakangu gani?β Nikauliza, βKaka?β Akasema, βYule aliyekuleta, kwani sio kakako? Si babako, bado mdogo.β Nikajua ni Baba Zawadi. Nikakaa kimya. Alinipa dawa, nikanywa, drip liliisha, akaweka lingine, akatoka.
Nikiwa na mawazo, βMama akirudi, itakuwaje? Bora nitoroke.β Nilitamani kumtafuta Neema, lakini sikuwa na mawasiliano naye. Nikapanga kutoroka nikipata nafasi. Nikiwa nimelala, Baba Zawadi akaniita, βZawadi!β Nikaitika, βAbee,β nikafumbua macho. Akasema, βUnajisikiaje?β Nikasema, βNaendelea vizuri.β Akasema, βPole sana.β Nikasema, βAsante, baba.β Akasema, βNimekuletea nguo uvae, ile ilichafuka, ilitupwa.β Nikasema, βBaba, asante, lakini nitaifua.β Niliongea nalia.
Baba alinishika, akasema, βZawadi, naomba unisamehe kwa yaliokufanyia mke wangu. Alikufanyia kitu cha kinyama. Nitafanya kila kitu kwa ajili yako, nitakupa chochote unachotaka. Nina watoto, nawaza kama sipo, wataishije? Nisamehe, nitakulea kama mwanangu.β Nikasema, βBaba, naogopa, siwezi kurudi, yule mama ataniua.β Akasema, βHayupo, hatorudi kabisa kwangu. Uwe na amani, nitakusaidia, nitatafuta msichana wa kazi, sawa? Naomba unipe muda.β Nikasema, βMmmh, nifanyaje? Nimepigwa hadi nakohoa damu, safari hii ataniua. Je, ni kweli hatorudi?β Nikawaza, βNikubali au iwaje?β Itaendelea.