WEWE NI WANGU SEHEMU YA 7
SONGA NAYO......
Hatimae mda wa vipindi ulianza na siku hii nilikuwa na kipindi cha asubuhi kwa kidato cha tatu nilikuwa natakiwa kwenda kuwafundisha geography
Basi nikaelekea darasani, kufika humo nakuta wanafunzi hawatulii wanapiga kelele yani ndio kwanza asubuhi darasa lilkuwa chafu karatasi zilizagaa kila sehemu
Nilicbukia sana nikamuita monter na montress wapite mbele, kweli wakaja kuangalia vizuri monter ni ka toto kadogo ila sura imakakamaa dah π
" we ndio monter...??"
Nilimuuliza yule dogo.
"Ndio sir.."
Alijibu kwa sauti ya bes jamani sauti ambayo hata mimi kijana wa miaka 25 sina ila huyu dogo anayo dah π
"Kwanini darasa lako ni chafu..??"
Niliendelea kumuuliza
"Sio hivyo sir..."
"Sio hivyo nini sasa..??"
Nilimuuliza huku nikimchapa chapa na fimbo begani, ila mimi nae nimezidi sasa, yani sina hata week tayari nimeanza kuchapa wanafunzi π
Jamani niseme tu ukweli sikuwa na mpango wa kuchapa mtu, ila monter ndio alikuwa ananiforce nimpige kwa sababu alikuwa ananijibu kama anaongea na mshkaji wake jambo lililopelekea kuchapa darasa zima ππππΎ
Hasira hizi acheni tu, nikiwa nachapa chapa pale tena fimbo za mgongoni nikakutana na sura ambayo naijua kabisa, nikastopi kisha nikamtazama huyo binti
"Kwani wewe una pacha wako..??"
Nilimuuliza baada ya kuona anafanana sana na Lizy, hata ile tabia ya kuinamisha uso na huyu alikuwa nayo..
"Hapana mwalimu huyu Lizy ameletwa huku na dada yake Leah.. "
Kuna mwanafunzi aliropoka, hii tabia siipendi kabisa nauliza mtu mwingine ila najibiwa na mwingine nilichofanya ni kumpiga fimbo ya mgongoni yule ambaye aliropoka ππππΎ
"Namuuliza huyu arafu we unajibu inamaana unamfanya mwenzio hajui kuongea au..??"
Nilimuuliza yule binti ambaye alilopoka basi binti akakaa kimya nikamgeukia tena Lizy
"We si nakuuliza..??"
"Hapana ni mimi, ila huku nimeletwa na Leah.."
"Kwani wewe huwezi kukataa au huna nguvu za kumpiga..??"
Nilimuuliza kwa ukali maana huyu binti kuna muda anakera sana yani amekaa kinyonge nyoge ndio maana anaonewa, nilichofanya hapo ni kumshika shati lake na kumtoa nje
Huku nikimsisitiza aende kwenye darasa lake kisha nikarudi darasani na kufunga mlango, π basi somo lilianza rasm nikaanza kufundisha sasa
Nilikuwa nafundisha maada ya maziwa makubwa yanayopatikana barani Africa, kwahiyo hapo nikauliza swali
"Ni maziwa yapi yanayopatikana barani Africa je mnaweza kunitajia baadhi ya majina..??"
Kuna mwanafunzi akanyoosha mkono, nikamchagua akasimama na kusema
"Maziwa ya ng'ombe..."
πππππΎ nilikuwa nimekasilika ila kwa hili lilinifanya nicheke walah, sio mimi tu hata wanafunzi wengine walicheka sana, hako katoto kalikonijibu kalikuwa kadogo dogo harafu kafupi nyie π
Katika siku ambayo nilicheka ni hii siku walah π dah kuna wanafunzi wengine ni pasua kichwa, basi somo liliendelea na hatimae kipindi changu kiliisha nikatoka nje, nafika nje sasa namuona mwalimu anamchapa mwanafunzi
Kwa kuwa mimi ni mbea nikajifanya nazuga ili kwenda kutazam nijue amekosea nini, maana mimi sipendi kuona mtu anaoneawa kabisa
"Ooh madam Penina.."
Nilimuita baada ya kufika hapo maana alikuwa kanipa mgogo, akageuka na kunitazama kitendo kilichonifanya nimuone huyo mwanafunzi ambaye alikuwa anamchapa
Dah niliumia sana sijui kwanini baada ya kumuona Lizy ndie ambaye alikuwa anachapwa.
"Mh asubuhi asubuhi umeshika stick vipi amekosea nini huyo..??"
Nilijisogeza ili kumtetea huyu binti sasa π kwa kuwa huyu madam ni bongowazi akanijibu
"Mijitu mingine bwana, badala ya kuwa darasani muda huu yeye anazunguka tu huku nje na yupo form four kabisa sijui ana shida gani huyu..??"
"Dah, sasa madam wewe nenda ukaendelee na masomo niachie huyu nitamalizana nae.."
Nilizungumza, kweli yule madam aliondoka nikabaki mimi na huyo msichana sasa, alikuwa bado amepiga magoti vile vile nikasogea karibu kabisa na alipokuwa.
"We si nilikwambia uende darasani mbona hukusikia..??"
Nilimuuliza
"Sir sio hivyo kusema ukweli darasa zima naonewa sio kama siwezi hapana naweza sana ni vile tu nikileta ubishi naweza nikachomwa mikasi maana mle darasani wanafunzi wengi ni wazambuli ..."
( ππ³ inamaana nimekuja kwenye shule ya wazambuli...??")
Nilijiwazia
"Mh sasa binti hayo niachie mimi nitamalizana nao mimi, dah sasa si masomo yanakupita lakini..??"
Mwanaume nilijikaza ili nionekane na mimi ni mwanaume kweli π lakini ukweli ni kwamba mimi naogopa mno tena ni muoga sana kwenye haya mambo ya vibaka aweee naweza kuacha kabisa simu yangu ili niokoe roho yangu
Basi ikabidi nimwambie anifuate ili nimpeleke huko darasani, basi mtu mbili tuliongozana haooo mpaka darsani nafika darasani bana bana π³
Nakuta baadhi ya wanafunzi wamepanda juu ya meza wanakatika huku wavulana wanawabambia huku nyuma, kifupi darasa liligeuka kuwa jumba la mziki na kwa mbali kulikuwa na redio inalia..
Nilivyoingia wote wakashuka chini na kukaa tena wakatulia kama sio wao, nikabaki nawatazama hawa wanafunzi na shule yao khaa π©
Ety ndio nasikia kuwa inafaulisha wanafunzi vizuri tu ndio kwa staili hii, aah hapana kwa kweli huenda kuna michezo michafu inafanyika ili kufaulisha wanafunzi.....
ITAENDELEA.......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni