πΊπππππ πππππ ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 95
Yaani mwenzenu hata ile meme inatembeaga kwamba ukitekwa mpenzi wako akikutafuta ndiyo umeokolewa mimi mwenzenu mnitoe huko. Maana nitatekwa kwa sekunde. Akiwa busy sana nusu saa. Stewart hajawahi kuwa ametingwa kwangu na ikiwa hivyo ananiambia na namuelewa.
Hivyo nami nilimjibu βAm sorry jamani. Mr Tarick hajapeperusha njiwa wako. Nilichoka sana nikajilaza bahati mbaya ndiyo nashtuka hapq. Pumzika kesho mapema nitakuja kukuona.β
Hapohapo akajibu βtotoo usifanye hivyo tena kamwe, usifanye hivyo mimi utaniua nakuambia utaniua.β
Nikacheka na kujibu βndiyo unitumie meseji zote hizi na simu kunipigia kama unanidai figo.β
Akaniambia βmuone huyu, nakudai penzi Ndeana kwanza huwezi amini nimekumiss eti, kwani siwezi kuja kukuchukua hata nusu saa tu.β
Nikacheka nikisema βmara hii, wewe jamaa. Jikaze kidogo basi.β
Akacheka eti βnina nguvu hizo basi, una bahati nasinzia. Nasinzia sana My sweet person.β
Nikasema βsitaki!!β
Akaniuliza βsasa unataka nini totoo!!β
Nikasema βnataka honey pot.β
Akacheka akisema βNdeana wangu. Asante sana. Nakupenda.β
Nami nikamjibu βNakupenda.β
Sasa wakati namjibu hivyo, nikawa nasikia sauti ya mtu analia. Ilinibidi niinuka kitandani. Kutazama vizuri ndiyo naona huyu rafiki Joan amekaa chini kajikunja analia kwa uchungu sana na kilio cha kwikwi.
Niliita βJoan!!, Joan!!β
Joan alilia kwa uchungu akisema βNdeana nateseka sana, nateseka mwenzako.β
Niliuhisi uchungu wake. Ilinibidi nishuke kitandani na kwenda kumkumbatia. Nikamwambia βLia sana Joan, lia mno uchungu wote ukuishe na kisha uniambie nini kinakusumbua ninaweza kuwa na njia moja ama nyingine.β
Ninatamani ungemuona alivyokuwa analia, alilia kwa uchungu sana na hata akawa anatoka jasho. Nami nilimkumbatia na kumfuta machozi yake. Ninakumbuka sana, aliniita akisema βNdeana, niahidi itakuwa kati yetu.β
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 96
Nikamtazama na kusema βnakuahidi.β
Akanitazama na kuvuta kamasi kisha alisema tena huku akilia kwa uchungu kwani hakuweza nyamazaβmimi sielewi nianzie wapi ila nilianza kuona tofauti baada ya kuwa dada mkubwa na kuanza mapenzi na kutafuta kazi yangu.
Ndeana mimi hapa, hakuna mwanaume nalala naye akanirudia. Hata kama alikuja na mapenzi namna gani, nikivua nguo tu. Siku hiyo hiyo anabadilika hanitaki tena. Tena bora hata hao ambao wanafanya mapenzi na mimi.
Mfano Boss ndiyo hata aibu Ndeana. Aliishia kunitazama tu na kisha aliniacha na yeye akaondoka. Ndeana mimi mwenzako sijawahi kufanikiwa katika maisha yangu. Ninaweza kuwa nafanya kazi.
Ninapata pesa, ninapata sana pesa kama unavyojua kazi zetu, ila pesa hizo hazikai, na pesa ikikaa sifanyi kitu cha maana yaano inapotea tu. Tangu nianze pambana mimi sasa najua ningekuwa na biashara yangu ila wapi.
Pesa mwisho wangu ni kulipa pango tu zaidi ya hapo mimi sina cha maana. Nikawa najitahidi kufuatilia madarasa ya kutunza pesa ila hayajawahi kuwezekana, mimi kwangu pesa haikai sina hata kitu cha maana zaidi ya unavyoniona hivi. Wanaume nikikuhesabia umri huu ambao nimewahi kulala nao ni ajabu, huwezi kuniamini.Ni wengi wengi wengi mno.
Ndeana ninawaza hao wanaume wamebeba nini kwangu hata wananiacha najiuliza sipati majibu. Mimi ni mama, ninaye mtoto mmoja. Miaka kadhaa nyuma kabla ya hii kazi nilikutana na mwanaume mmoja.
Huyu ndiyo mwanaume pekee ambaye nililala naye na hakuniacha. Nikabeba mimba yake, hakutaka kabisa niteseke mwenyewe. Alinichukua kwa upendo na kuanza kuishi pamoja naye. Ulikuwa ni muujiza sana, nilifurahia sana maisha pamoja naye.
Maisha yangu yalikuwa mazuri, nilianza kupendeza zaidi na zaidi. Mwanaume alinipenda sana, alinijali, alinitunza na aliniamini sana. Ila huwezi kuamini Ndeana, mwezi mmoja tu kukaa naye. Kila kitu chake kilianza kupukutika.
Alifukuzwa kazi, aliishiwa pesa. Mwanaume alikuwa ni wakulia na kuhuzunika. Mimi nilikuwa hata nikimshauri vipi haiwezekani. Alikuwa anahangaika kutafuta kazi hapati. Na akianza hata biashara ndogo ndogo ambayo na mimi nitamshika mwenzangu haichukui muda inakufa.
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 97
Alikuwa analia ana mkosi gani, alikuwa analia kwanini anapitia mambo hayo. Tulianza kuchakaa, tulianza kuchoka. Na hata kodi tena tulikuwa hatuwezi kulipa kabisa. Ilitubidi twende nyumbani kwao mkoani.
Nilikaa pale wiki tu. Nakumbuka mama wa mpenzi wangu aliniita alisema βBinti, sijawahi kukuchukia. Ila nakuambia kwasababu nataka maisha mazuri kwa kijana wangu. Joan nimehangaika kujua tatizo la mwanangu na nimejua tatizo ni nini?β
Nilimgeukia na kumuuliza mama βeenh mama tatizo ni nini?β
Ndipo yule mama alisema βtatizo ni wewe, tatizo ni wewe Joan. Ili mwanangu arudi kwenye ubora wake kaa naye mbali kabisa. Na wala usikutane naye. Kama unampenda mwanangu muache na maisha yake na wewe uishi maisha yako.β
Nilishangaa na kusema βkivipi mama mimi nampenda sana.β
Mama alisema βhata yeye pia. Ila kamwe wewe huwei kuolewa. Kwani nikuulize wewe si wanaume wanatembea na wewe wanakuacha?β
Nikashtuka, nikamuuliza βmama umejuaje?β
Akanitazama na kusema βhuyu ni kijana wangu, siwezi kukaa naona anapotea. Ina maana wewe humuhurumii. Yeye ndiyo nategemea kutoka kwake. Leo hii anakaribia kuchanganyikiwa. Cha kukusaidia, ni wewe kuondoka hapa. Na ukae ukijua kuwa...β
Nikamtazama machozi yakitoka na kumuuliza βkuwa nini mama?, niambie tafadhali?β
Huyu mama alisema βni ngumu sana ila wacha nikuambie. Wewe ni msichana mzuri sana, ila hutokuja kuolewa, wala kufanikiwa na mwanaume yeyote atakaye kuwa karibu yako hatakuja kufanikiwa kabisa.
Kwasababu mwanangu wewe una laana, mwanangu wewe una vitu vya ajabu. Mimi sina mengi sana ila rudi kwenu kabisa, kaulize nao watakuambia ukweli. Ila utahangaika sana kutafuta mchawi, na vitu kama hivyo.
Ila kwenye maisha yako mchawi ni laana za ukoo wenu na wala sio wewe tu fikiria huenda hata wengine wapo hivyo. Nimeongea na mwenzako, hawezi kukuambia na mimi sina msaada mwingine. Naomba uondoke nyumbani kwangu.β
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 98
Sikuamini Ndeana, baada ya kuhangaika kote kote. Nimepata mwanaume wa kunisitiri na mimba juu naambiwa mimi ni laana niondoke pale. Ninampa mikosi, nuksi na balaa mtoto wao. Nikasema kwa uchungu βmama naomba nisaidie. Nisaidie mwanao. Nitafanya nini sasa na hii mimba mimi. Nakuomba mama.β
Huyu mama alisema βkuwepo kwako hapa ndiyo mabalaa yanaongezeka. Wewe hutufai. Nenda ukapambane na matatizo yako. Chukua nauli hii hapa. Kesho asubuhi uondoke.β
Nililia sana Ndeana, nililia mno, mbaya zaidi mwanaume sikumuona pale nyumbani kumbe yeye karudi Dar na hata hajaniaga. Mama yake aliniambia kuwa mwenzio kaondoka wewe hapa utabaki na nani ondoka tu. Usiku ule ulikuwa ni mchungu sana. Ilinibidi niondoke, niliondoka nikiwa na maumivu makali sana. Inawezekana vipi mimi kuwa laana, mkosi na kubeba mabalaa. Ina maana mimi nina peso filisi au kitu gani.
Mambo yalikuwa mageni kwangu. Nilisafiri mimi mpaka nyumbani. Nilifika nyumbani kwa mama yangu. Sijui utanielewa vipi ila baba yangu na mama yangu wanaishi kila mtu kwake ila hawajatengena. Yaani wanaishi hivyo tu. Hata sisi hatuwaelewi ila wanaishi hivyo.
Na wakika pamoja hata mara moja ni ugomvi na matatizo kibao. Kwahiyo mama atapika huku anapeleka chakula, baba atalala huku ataondoka. Ni ndoa ya ajabu eenh!!, ila ndiyo tumezoea kwa maana hata sisi watoto tumekua hivyohivyo mara huku na mara kule.
Na kweli yapo mambo niliyawaza wakati nikiwa safarini. Ni kweli kabisa, kwenye ukoo wangu hakuna mtu aliyefanikiwa na wala hakuna aliyeolewa, hakuna kabisa. Mimi sitaki kuwa mmoja kati yao. Ninakumbuka mama alinipokea.
Aliponipokea tu nilianza kulia kwa uchungu sana nikisema βmama ni wewe tu, ni wewe unaweza kuniambia ukweli wa maisha yangu. Kwani mimi nina kitu gani. Maisha yangu hayaeleweki. Tafadhali mama niambie.β
Mama alivuta pumzi na kunitazama akisema βacha kulia mwanangu, futa machozi yako. Nakuomba sana.
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 99
Nami nilimwambia mama yangu βnitanyamaza ukisema ukweli tu, nimechoka kuwa laana, nimechoka kuhangaika. Tazama mama hali yangu unataka na huyu mtoto aje kuishi maisha yangu. Nini kinaendelea, mama usiponiambia ukweli hutoniona tena kwako, hutoniona.β
Mama alivuta pumzi na kusema βHuna cha kufanya mwanangu, hii ndiyo hatma yetu wote. Hata mimi sikutaka haya yawakute. Ila ipo njia kwenye haya. Sikia mwanangu. Mimi wakati nakutana na baba yako sikujua kuhusu yeye sana. Na kumbe familia yake ni watu wa mila na sadaka za mizimu.
Hapo ndipo mambo yalipoanzia. Nimekuja kujua hilo tayari ni mtu mzima, mambo yangu yalipoanza kwenda tofauti. Kwasababu nilipaswa kwenda njia moja na baba yenu. Nilikataa na tayari ninyi wanangu mlishazaliwa.
Babu yenu akawa ananichukia sana na kuona naenda kinyume na ndiye ambaye alisema yeyote anayekataa kutumikia mizimu yao hatofanikiwa kwa lolote na amelaanika wala hakuna mwanaume wa kumtamani. Sikujali mimi nikasema wanangu hawatatumikia mizimu. Ulipofikisha miaka kumi na nane.
Walinifuata tena na kusema binti yangu mkubwa ambaye ni wewe, mizimu ya kweni imekuchagua kuwa kiongozi wa ibada hizo.β
Nikashtuka na kusema βunasemaje mama, umri huu, miaka hii na mizimu wapi na wapi?β
Mama alinitazama akatokwa machozi akisema βnatamani nisingekutana na baba yako. Ameharibu maisha yangu. Nalaani siku aliyoniona nami nikakubali. Miaka yangu yote mpaka uzee huu nahangaika kuvunja hizo roho za madhabahau chafu juu yenu na ndiyo maana nilikuondoa ila naona bado. Mwanangu hakuna zaidi ya kukataa roho hizi. Naomba usikae hapa, wakikuona tu wataanza mambo yao. Jitahidi kesho uondoke hapa. Nakuomba mwanangu.β
Familia zina mambo Ndeana. Miaka yote hiyo sijawahi kujua mama yangu anateseka, machozi yake yaliniuma. Naenda kwetu mama yangu anaogopa hata nisionekane. Acha tu. Alinipa nauli, usiku uleule nilitafuta kwa kulala nikiwa na maumivu sana. Nalia mno. Ndipo nikarudi Dar. Nikaomba msaada kwa rafiki yangu. Nikatafuta kazi maisha yaliendelea nikiwa na mzigo mkubwa moyoni.
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 100
Nilianza kwenda makanisa ya mitume na manabii. Sikuwahi kufanikiwa hata kidogo Ndeana sijui labda sijui kuomba. Ila naomba sana kusema ukweli.
Baada ya miezi miwili tu nikaja kusikia mwanaume wangu karudi kazini, yaani yupo safi kabisa bila mimi.Roho iliumia sana. Nikalia sana. Ningefanya nini zaidi ya kusubiri nijifungue.
Nikapata mtoto wa kike mrembo kama mimi mama yake. Ila bado hali haijanitoka. Baba mtoto wangu hajawahi nitafuta hata kuulizia damu yake. Hakuna mwanaume ananitaka baada ya kulala na mimi.
Kuna muda hata hela ya ada ya mwanangu elfu 30 tu nashindwa. Nimechoka sana, natamani kuvunja hizi roho, natamani kuzivunja na laana itoke kwenye familia yangu kwani hata wadogo zangu watakuja pitia haya.
Usiku naota ndoto za mizimu tu, naota nipo naimba na kucheza kwenye mti mkubwaZ Naota ndoto mbaya. Huwa naogopa kulala usiku, nalia na kuteseka sana.
Nimechoka sana mimi, nami nataka kuwa kama wengine, nataka wanaume waliokutana na mimi wajiondoe na laana zangu pengine watahamishia kwa watoto wao. Naogopa na nimechoka sana. Nimechoka Ndeana. Natamani kupiga hatua na mimi, mbona nafanya kazi, napata pesa sasa kwanini haya. Nimechoka mimi.β
Alilia kwa uchungu akinikumbatia. Hakika dunia ina mambo mengi sana. Na asilimia kubwa ya mambo hayo mlango wake ni mapenzi. Mungu wangu asante kumbe mimi Ndeana nina bahati sana.
Nilimuacha alie nikimbembeleza na kisha nilimwambia. Nilimwambia Joan kwa utulivu nikimtazama usoni βJoan, kipenzi umelia sana, nyamaza. Kuna kitu kimoja nataka kukuambia. Mimi sijui sana kuhusu Mungu.
Ila nampenda sana namna anafanya sana kazi zake. Tena natamani sana kumjua zaidi. Kama ulivyosema umeomba sana, umezunguka sana, huoni mabadiliko. Ni kweli, na wala hupaswi kukata tamaa.
Maombi ni akiba amini hilo. Ndiyo maana kuna wakati Mungu anakufanyia jambo mpaka unashangaa uliomba lini kumbe kuna siku uliwaza hata moyo na Mungu akafanya. Ni jambo moja tu Mungu hawezi kulifanya. Hawezi moja, nalo ni kushindwa.
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 101
Sijui ukubwa wa tatizo lako mbele za wanadamu. Ila mbele za Mungu hilo ni dogo sana. Mungu anakufungua, mimi sijui sana ila nikuambie kitu. Niliona lakini kwenye filamu. Unajua nini, yule muhusika alikuwa na matatizo mengi sana.
Ila siku ile alijikuta akiita jina la Yesu mara nyingi awezavyo. Tunaweza fanya na sisi kwa imani. Muamini Mungu, amini Yesu atatembelea maisha yako. Tena usichoke. Soma maandiko majibu ya maswali yetu yote yapo huko.
Youtube kuna maombi mengi kwa watumishi wengi, chagua wakukuongoza, nami nitakusaidia kutafuta. Unajua kwanini nakuambia hivyo, jifunze kujiombea rafiki yangu, omba mwenyewe, ita jina lake zuri kwenye maisha yako, kataa roho chafu, vunja masanduku ya maagano, vunja, toa sadaka nenda kanisani kwako Mungu Yupo.
Huwezi ukaombewa kila siku tu na wewe hujiombei. Omba rafiki yako. Naamini ukienda kanisani utapewa na muongozo mzuri sana. Vita hii kwa binadamu ni ngumu, ila mbele za Mungu ni rahisi sana. wewe utakuwa wa kwanza kuolewa kwenye ukoo wako, utakuwa wa kwanza kufanikiwa. Usikate tamaa, jipambanie na silaha yako ni maombi. β
Nikachukua simu yangu, na kuanza kumuonesha baadhi ya watumishi wa Mungu, nikisema βhuyu ana maombi mazuri, huyu yaani kesho ukitoka mapema nenda kanisani. Elezea kila kitu utapata msaada mzuri sana.β
Joan alinikumbatia akilia sana, kwa pamoja tulianza kusali tukiwa tumeshikana mikono. Tulilia huku Joan nikimuambia arudie kusema βYesu karibu kwangu, Yesu karibu kwangu, Yesu karibu kwangu.β
Zilikuwa ni hisia chungu sana, Joan alikuwa anaumia mno. Hakika nilimuonea huruma. Mpaka mimi napanda kitandani, Joan alibaki akiita Mungu akaribie ndani ya Moyo wake tena kwa uchungu.
Ipo sababu ya kusema asante Mungu umezaliwa kwa familia hiyo. Zipo familia zina mengi magumu, zipo familia zina mila za ajabu, zipo familia za kichawi, zipo familia za kishirikina.
Kila unapomvulia mtu nguo zako, fikiria pia nini unachoenda kubeba kutokwa kwake. Kitu gani kitasafirishwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Nataka kusema Tusivue nguo ovyo mbali na matamanio ya kibinadamu. Tusali sana kwa kila tunachofanya.
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 102
Asubuhi ilifika, Joan aliamka aliniambia βrafiki yangu asante kwaajili ya jana. Hakika leo nimeamka mwepesi. Hapa leo tukimaliza kazi mapema nitaenda kanisani. Kisha nitakuambia kinachoendelea. Umenitia moyo na nguvu. Ninaanza upya na nitapambana kukataa vifungo vya familia hii. Nakupenda Ndeana.β
Nilitabasamu nikisema βAsante kipenzi. Pandisha imani yako na uamini kila jambo litakuwa sawa.β
Basi kama kawaida mimi na baby wangu tuliwasiliana na tuliendelea na kazi. Nataka kusema kuwa mimi kazi hii nilikuwa naipenda sana. Ni ndoto yangu. Nikiwa huku hata simu nikawa naingia nayo sasa nikimaliza kazi nachukua video, napiga picha naandika na ujumbe mzuri naweka mtandaoni. Na mimi mwenyewe pia nilikuwa ninajiweka na sare zangu, ninavyopendeza na rafiki yangu alinipiga picha. Ila nilihakikisha simu haingilii kazi. Na kwakuwa wakati huo tulikuwa na kazi hii kubwa sikutaka chochote kipite. Yes niliweza. Siku hii tulimaliza.
Usiku Joan alirudi na alikuwa anatabasamu akisema βnimeongea na mchungaji. Kuna sadaka nitatakiwa kutoa. Pia nimeongozwa maombi na natakiwa nianze kuhudhuria. Unajua huu uzuri wangu wote hata sionekani kisa uchawi uchawi tu. Ndeana nitafanikiwa na nitakukumbuka maisha yangu yote maana sikuwa najua naanzia wapi.β
Nilimkumbatia kwa furaha sana. Kisha alikula, akaoga, mimi nikawa nawasiliana tu na My boss, nacheka, natabasamu na vitu kama hivyo yaani sielewi. Penzi limenikaba.
Penzi langu na Boss lilizidi kunoga. Alinipenda mno. Kumbe ule mwili niliwaambia si mwembamba si mnene sio wangu mjue, ile ngozi niliona nzuri nayo wala sio yangu. Kule kupendwa, kujisikia raha na furaha. Nilizidi kupendeza, nilizidi kuwa mzuri, nilizidi kunawiri, ngozi yangu ilzidi kuwaka kama taa. Hata Joan rafiki yangu ambaye alikuwa anaendelea na maombi na kufuatilia mambo yake aliniambia hivyo. Kupendwa ni tiba ya matatizo mengi sana. Kupendwa raha sana.
Upo wakati Boss alikuwa anakuja kuja kule ukumbini. Tunagongana macho anatabasamu tu. Mimo naye saluni kwa Aunt sasa nimezoea. Nimezidi kuwa mzuri sana.
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 103
Sasa wakati watu wanatoka Mr Tarick alinifuata tena kwa maana nilikuwa ninamkwepa sana. Alinitazama na kutabasamu akisema βHello Beutiful, unanikimbia kwanini?β
Nikatabasamu. Akaniambia βNilikupa namba hujanitafuta. Vibaya hivyo.β
Nikatabasamu tu na kusema βnilitingwa sana. Tumefurahi kuwa nanyi hapa.β
Kabla sijajibu nikasikia Mr Tarick akisema βOoh Mr Stewart, nipo na Ndeana. Hakika una wafanyakazi makini sana.β
Boss wangu alisogea, huku mimi nikishangaa tu kumbe washatafutana wanajuana.
Mr Tarick aliendelea kunisifia mbele ya Boss wangu. Boss wangu akawa ananitazama kwa jicho la wizi kisha baada ya sifa zote zile yeye alinijibu βNdiyo maana nataka kumuoa. β
Nikashtuka na Mr Tarick pia akauliza βAre you...Are ... Eeh Mr Stewart.β
Akatabasamu na kusema βYes, she is beutiful. Nampenda sana. Ni mpenzi wangu huyu. Anytime soon nitakupa mualiko. Tuombee tu. Kisha alinitazama na kutabasamu akisema βBaby Asante kwa huduma nzuri sana. Wateja wetu wamefurahi.β
Nikatabasamu tu. Kisha Mr Tarick kwa aibu akawa anajikanyaga tu akisema βwaooo!!, waooo!!, Nice couple. She is beutiful. Hongera sana. Nawatakia kila jema. Nimefurahi kusikia hivyo.β
Boss akatabasamu na kusema βNashukuru, ninaweza kumchukua sasa right?β
Mr Tarick alijibu βYes!!, Yes!!, no problem.β Tena huku akikuna kichwa chake. Natamani ukiniona hapo nnavyotamani kucheka. Boss ana wivu huyu, anapeperusha madanga yangu. Nikawa namtazama nacheka tu. Ananiuliza βunacheka unaona sifa, muone kichwa kama Mr Tarick. Umependa nini kwanza, au vile hana ndevu na mimi ninyoe. Unanichanganya ujue.β
Nikacheka tu, tena yeye hakujali, alinishika mkono tukitembea haraka kuelekea ofisini kwake. Nikasema kwa furaha β taratibu basi utaniumiza si unajua mimi mtoto laini sana.β
Akacheka na kunisukumia ndani. Nilipoingia ofisini alikuja mbele yangu tena. Nikawa namuuliza βnini sasa!!β
Anazidi kusogea na kusema βwewe mwanamke wangu mzuri kuliko wote. Sikia nataka nikushukuru leo. Kumbe kuna ndoto ambazo unaweza kuzishika.β
ππππππ ππππ ππ πππππ ππππ πππ: 104
Nikashangaa na kuuliza βndoto unaweza kuishika?β
Akaniambia akinitazama βunajua ulichokifanya kwa hii Hotel. Ndeana umefanya kubwa na kwa taarifa yako tumepata kazi zingine nyingi kwaajili ya hili la kwanza.
Ndeana, Toto, My sweet person. Nataka nikushukuru kwa kuwa ndoto, ndoto ambayo ninaiota na ninaweza kuishika sasa. Nataka nikushukuru kwa kuwa umenifundisha kuwa kuna watu wazuri, wenye moyo mzuri, mapenzi ya dhati, wapole, watulivu, wenye akili na hekima kama wewe Ndeana.
Asante kunifanya niamini kuwa mapenzi ya kweli na dhati yako na ni kweli kuna malaika duniani wanaoishi kama malaika. Ndeana wewe ni mzuri sana kwangu. Yes Love is beutiful Thing in the world, i currently admit.
Waooo!!!!, nikamtazama kwa upendo na nikauliza βkuna ule msemo unasemaga, unasema When two souls understand each other....β
Yeye akaniambia kwa mahaba βwhen two souls understand each other, everything becomes sweet.(Nafsi mbili zikielewana, kila kitu kinakuwa kizuri.)
Nikatabasamu na yeye akasema akinitazama usoni βI love what we have together.β
Nikatabasamu tu, akanibusu. Kisha nikasema βNakupenda.β
Akacheka akasema βMr Tarick kidogo alie, hawezi kukupata. Wewe ni wangu.β
Nikacheka tu. Mara simu yangu ikaita. Haraka nikatoa, alikuwa ni dada hata nikasema βkanimiss nimemwambia leo narudi.β
Nikapokea, kwa bahati mbaya nilipopokea dada yangu alikuwa analia sana, alilia kwa uchungu akisema βNdeana, baba, baba ameanguka njoo haraka, anaumwa sana nampeleka hospitali. Njoo tusaidiane mdogo wangu.β
Nikajikuta natetemeka. Nikaachia simu ikaanguka. Boss alinitazama akiuliza βtotoo!!, tatizo nini babyπππππ
Naaaam
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005


Maoni