THE KING'S SON (MTOTO WA MFALME ) Sehemu......ya.......01 ANZA NAYO........ Ni vita kubwa iliyokuwa ikiendelea kati ya falme mbili, ufalme wa AZENI na ufalme wa PADALA.
Walianza kukimbia ila kabra hawajafika mbali walizungukwa na maadui zao.
"Mfalme nilikwambia huna uwezo wa kushindana na mimi kwa usalama wako inatakiwa unioneshe ni wapi hazina zilipo"
"Siwezi kukuonesha hazina zilipo ila kama ni ufalme nipo tayari kukuachia. naomba unipe nafasi ya mimi kuondoka na familia yangu twende tukaishi mbali"
"Hiyo haitawezekana, najua lazima utarudi kunisumbua siku moja wewe pamoja na familia yako, kama haupo tayari kunionesha hazina zilipo basi leo lazima upoteze maisha wewe pamoja na familia yako" pale pale alitoa amri kwa vijana wake kuishambulia familia ya Mfalme wa PADALA aliyefahamika kwa jina la Mfalme Gideoni.
Mfalme Gideoni alijaribu kujitetea lakini hakuwa na uwezo huo kwani aliuliwa na kupoteza maisha pale pale. Mkewe aliyefahamika kwa jina la Malikia Maria naye alipoteza maisha kwa kuuliwa huku mtoto mdogo akiwa kwenye mikono yake.
Mwanajeshi mmoja aliweza kumuona mtoto aliyekuwa ameshikwa na Malikia Maria aliyekuwa amepoteza maisha tayari,
"Mfalme mtoto wao bado yupo hai" asikari yule aliongea na kumpa tarifa Mfalme wake.
"Kwakuwa baba yake kakataa kunionesha hazina zilipo basi hatakiwi kufa huyo mtoto mbebeni tuondoke nae nitamfanya kuwa mtumwa wangu" Mfalme aliyefahamika kwa jina la Mfalme Balaki aliongea na kuwafanya asikari wake wamchukue mtoto nakuondoka nae huku kila mmoja wao akiwa na furaha kwa kupata ushindi japo walishindwa kujua ni wapi hazina zilipo.
Safari yao iliwapeleka kwenye ufalme wao wa AZENI na walipofika kila raia siku hiyo alikuwa na furaha ya kuwapokea mashujaa waliokuja na ushindi kwa kuwashinda maadui zao. Mfalme Balaki alielekea kwenye jumba la kifalme na kupokelewa na Malikia aliyefamika kwa jina la Malikia Rebeka.
Mfalme Balaki alifika kwa Malikia Rebeka na kupokelewa kwa furaha na mkewe,
"Hongera sana kwa ushindi ulioupata Mfalme"
"Asante ila huu ni ushindi wa AZENI sio wangu peke yangu na ata hivyo nimekuja na mtoto wa Mfalme Gideoni kwenye ufalme wangu huu" Mfalme Balaki aliongea lakini maneno yake yalimfanya Malikia Rebeka ashangae.
"Mfalme...!?, huoni kama akikua atatuletea matatizo hapo baadae hasa akija kugundua kuwa tuliangamiza familia yake...!?" Malikia Rebeka aliongea akiwa na hofu ya hali ya juu.
"Hawezi kugundua pia nafanya ivi kwakuwa Mfalme Gideoni alikataa kunionesha hazina zilipo, na yoyote atakayefungua mdomo wake kumwambia basi kifo kitakuwa halali yake" Mfalme Balaki aliongea ila licha ya yeye kuongea bado Malikia Rebeka hakufurahishwa na kitendo cha Mfalme kumuacha hai mtoto wa Mfalme Gideoni.
Miaka ilisogea na kila kitu kilikuwa kimebadilika ndani ya ufalme huo wa AZENI kwani Mfalme Balaki alipata watoto wawili, Prince Yoramu na Princess Miriamu.
Mtoto wa Mfalme Gideoni aliyeuliwa na Mfalme Balaki alikuwa ameshakuwa mkubwa na alifahamika kwa jina la Yoashi na aliishi kama mtumwa ndani ya ufalme huo. maisha ya Yoashi ndani ya ufalme wa AZENI yalikuwa niya kitumwa kama watumwa wengine walivyokuwa wakiishi ndani ya ufalme huo.
Malikia Rebeka alimwita Prince Yoramu na kumweleza ukweli wote unaomhusu Yoashi huku akimwambia awe makini nae asije kugundua kama familia yake iliuliwa na Mfalme Balaki kwenye vita vilivyopigwana hapo nyuma, Prince Yoramu alimwahidi mama yake atamfanya Yoashi awe mtumwa wake na hata gundua chochote kile.
Prince Yoramu siku hiyo alijiandaa kwa ajili ya kwenda mawindoni. Yoashi aliitwa na Prince Yoramu na alifika mda huo huo baada ya kusikia akiitwa na mwana wa Mfalme,
Alifika na kuinama karibu na Farasi na kumfanya Prince Yoramu apate sehemu ya kukanyaga. Alikanyaga mgongoni mwa Yoashi na kupanda kwenye Farasi,
"Inuka na uongoze njia mpaka mawindoni" Prince Yoramu aliongea na kumfanya Yoashi atii maagizo yake.
Alinyenyuka nakuanza kutembea kuwaongoza njia kuelekea polini kwenye mawindo. wenzake walikuwa wamepanda kwenye Farasi ila yeye peke yake alikuwa akikimbia kwa miguu na maisha yale alikuwa ameshayazoea.
Prince Yoramu aliona kama Yoashi anawachelewesha,
"Ongeza mwendo wa kukimbia wewe unatuchelewesha" Prince Yoramu aliongea na kumfanya Yoashi aongeze kasi ya kukimbia mpaka pale walipofanikiwa kufika.
Prince Yoramu alishuka kwenye Farasi wake na kuanza kuzunguka kwenye poli hilo akiwa na walinzi wake huku Yoashi akiwa ni muongoza njia, walitembea na walipofika mbele Prince Yoramu alimuona swala nakuandaa upinde wake ukiwa na mshale kwa ajili ya kumpiga swala ila badae aliamua kuacha na kumtazama Yoashi aliyekuwa amesimama kwa utulivu,
"Mkimbize huyo swala na uje nae hapa akiwa mzima" Prince Yoramu aliongea akimwambia Yoashi.
"Prince...!!,atawezaje kukimbizana na swala..!!?, mimi naona sio vizuri kumpa iyo kazi ya kumkimbiza swala" Mlinzi wake aliongea huku akionesha kumuonea huruma Yoashi kwa kazi aliyoambiwa afanye.
Prince Yoramu alimtazama kwa hasira Mlinzi aliyeongea na kumtetea Yoashi,
"Natengua kauli yangu niliyosema hapo mwanzo, basi na wewe utaungana naye, wote mnatakiwa mfanye hiyo kazi na ole wenu swala awakimbie mtanieleza vizuri" Prince Yoramu aliongea na kumfanya Mlinzi aliyejaribu kumtetea Yoashi ajute.
Yoashi na Mlinzi wa Prince waliungana kumkimbiza swala walioambiwa wamfatilie ila bahati mbaya ilikuwa kwao kwani hawakufanikiwa kumpata na walirudi wakiwa mikono mitupu mbele ya Prince Yoramu.
Prince Yoramu alikasirika baada ya kuwaona wakiwa mikono mitupu bira kuwa na swala,
"Niliwaambiaje..!?"
"Tusamehe Prince, ametukimbia" Yoashi aliongea kwa unyenyekevu.
"Twendeni kwenye jumba la kifalme mkapate adhabu yenu" Prince Yoramu aliongea na Yoashi alijua nini kitakachoenda kutokea mana hayo maisha alikuwa ameshayazoea toka akiwa mdogo ndani ya ufalme huo.
Walipofika kwenye jumba la kifalme Prince Yoramu alitekeleza kile alichowaambia kule polini kwani alifanya miili ya wenzao kuwa sehemu ya yeye kufanyia mazoezi, Yoashi pamoja na Mlinzi walikuwa wametuliza miili yao huku Prince Yoramu akiwapiga lakini pale pale aliweza kufika Princess Miriamu,
"Kaka utaacha lini kumpiga Yoashi..!?" Princess Miriamu aliongea.
"Kaa pembeni haya kuhusu haya" Prince Yoramu alimjibu huku akiendelea na kile alichokuwa akikifanya na hakutaka kusikiliza maneno ya dada yake.
Princess Miriamu aliamua kwenda na kumpa tarifa zile Mfalme Balaki aliyekuja mda huo huo,
"Nilishakwambia mwanangu haina haja ya wewe kuwapiga watumwa ovyo, emu acha unachokifanya" Mfalme Balaki aliongea na kumfanya Yoramu asitishe kile alichokuwa akikifanya na kuondoka pasipo kuongea neno lolote kwa baba yake mzazi.
Mfalme Balaki alimwangalia Yoashi na alikili kuwa mtoto huo alifanana na Mfalme Gideoni karibu kila kitu aliyemuua miaka kadhaa iliyopita nae aliondoka akiwa na Princess Miriamu nakuwaacha Yoashi na Mlinzi wakiugulia maumivu.
**********************************
Ndani ya ufalme wa PADALA, ufalme uliopoteza mvuto tangu Mfalme Gideoni alipofariki hakukuwa na watu waliokuwa wakiishi kwenye ufalme huo, nyumba zilikuwa zimechakaa na mazingira yake yalikuwa niyakutisha kutokana na mifupa ya binadamu iliyokuwa imeenea karibu kila sehemu kwenye ufalme huo.
Ndani ya jumba la kifalme, alionekana bibi aliyechokeana, na maisha yale alikuwa ameshayazoea ya kuishi kwenye ufalme huo bira kuogopa mafuvu na mifupa mbalimbali ya binadamu iliyokuwa imezagaa. Alinyenyuka na kushika jembe lake nakuondoka. alifika sehemu nakuanza kuchimba kwa tabu na alipomaliza alienda kuchukua baadhi ya mifupa ya binadamu na kuja kuifukia mahali alipokuwa amechimba,
"Licha ya umri wangu kwenda nimeifanya hii kazi kwa miaka mingi ya kuzika ndugu zangu...ee mwenyezi MUNGU ikumbuke PADALA na utuletee mtu wakuja kuurudisha ufalme huu uwe kama mwanzo ulivyokuwa" yalikuwa ni maneno ya bibi aliyeongea kwa uchungu huku akiendelea kuzika mifupa ya ndugu zake.
**********************************
Prince Yoramu alimfata Mfalme Balaki nakumkumbusha kuwa siku mbili zijazo ni siku yake ya kuzaliwa hivyo angetamani kuwe na sherehe siku hiyo. Mfalme Balaki alimsifu kwa kumkumbusha na alimkubalia kijana wake mana ndiye mtoto wake mkubwa na anayetegemea kwa badae aje awe mlithi wake, kila mfanyakazi ndani ya jumba hilo alipatiwa tarifa za sherehe hiyo na maandalizi yalianza kufanyika siku hiyo hiyo.
Prince Yoramu alimfata Princess Miriamu nakunza kumuongelesha,
"Huwa unapenda kumtetea sana Yoashi ngoja tuone utawezaje kumtetea siku ya sherehe yangu" Prince Yoramu aliongea na kuondoka.
Princess Miriamu baada ya kuachwa peke yake alifikilia maneno ya kaka yake na alihisi huenda kuna kitu kibaya alichopanga kumfanyia Yoashi alitoka na kwenda kumtafuta Yoashi lakini hakufanikiwa kumpata kwa wakati huo,
"Mmmh...!! kaka kapanga kufanya nini tena, mana ana roho mbaya isiyo ya kawaida" Princess Miriamu aliongea nakuendelea kumtafuta Yoashi aone kama atafanikiwa kumpata.
Siku ilipita bira Princess Miriamu kumpata Yoashi kwani siku hiyo Yoashi hakuwa ndani ya jumba hilo la kifalme.
Siku iliyofata maandalizi yalikuwa yakiendelea kama kawaida, Princess Miriamu alibahatika kumpata Yoashi asubuhi hiyo,
"Yoashi inakupaswa uondoke na uende mbali nje ya huu ufalme"
"Kwanini Princess..!?"
"Kwa sababu kuna jambo Yoramu alilopanga kukufanyia hivyo nakuonea huruma huenda ukaja kuingia kwenye matatizo zaidi" Princess Miriamu alimaliza kuongea na kumsikiliza Yoashi aone atajibu kitu gani.
Yoashi alifikilia nae pia alikuwa ameshachoka maisha ya kunyanyaswa na Prince Yoramu aliamua kukubali ushauri aliopewa na Princess Miriamu.
Haraka alianza kufanya maandalizi kwa ajili ya kutoroka wakisaidizana na Princess Miriamu na baada ya kila kitu kuwa tayari alitoka ndani ya ngome ya kifalme ili atoroke.
Bahati mbaya ilikuwa kwake kwani alishangaa kumuona Prince Yoramu akiwa kasimama mbele yake tena akiwa na walinzi wakutosha.....ITAENDELEA.
Prince Yoramu alijuaje kama Yoashi anataka kutoroka?. na amepanga kumfanyia nini Yoashi siku ya sherehe yake?. Tukutane sehemu ya pili
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni