Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya โ€“ Gonga94 Semajambo

*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO* *1-5* *
Gonga94 ยท Stories

*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO* *1-5* *

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
__________________________________*

*SEHEMU YA KWANZA*

Naitwa Nelly ni mtoto wa kwanza kwa baba yangu wazazi wangu hawakuwahi kuishi pamoja hivyo niliishi na mzazi mmoja tu ambaye ni mama .

Niliishi na mama yangu hadi nilivyofika kidato cha kwanza mama akaanza kuugua hatimaye MUNGU alimpenda zaidi mimi nikakosa mtu wa kukaa nae ndugu wa mama wengi wao maisha yao yalikuwa chini sana ikabidi nikaishi na baba yangu muda huo alikuwa tayari ana familia nyingine. Walibahatika kupata watoto wawili wa kiume mapacha na mwingine binti mkubwa alimkuta kwa mkewe tulipishana miaka mitatu yeye alikuwa mkubwa kwangu nilimkuta yupo kidato cha tatu alikuwa anaitwa Victoria.

Wenzangu walikuwa wanasoma shule za kulipia yaani shule za magari ya njano Victoria yeye boarding ila mimi nikapelekwa shule ya kata ,
Mwanzoni tuliishi vizuri kimbembe kilianza nilivyofika kidato cha nne kazi zilikuwa haziishi nyumbani na hivi nilikuwa nasoma shule ya kutwa ndio kabisa nilikuwa sipati muda wa kujisomea vizuri. Mungu alisaidia hivyo hivyo nikamaliza masomo yangu nikwa nasubiria matokeo ila kipindi nipo nyumbani๐Ÿก cha moto nilikiona kwa kweli .

Hapo binti yake yupo chuo watoto wake wanarudi jioni sana hapo walikuwa wanasoma darasa la saba kwahiyo nilibaki peke yangu nyumbani ๐Ÿก muda mwingi.
Nelly wewe Nelly hebu amka unalala hadi sasa hivi una raha gani kwa mfano ufanye uamke hapo nje kuna mikazi kibao sauti ya mama ilisikika ikiniamsha na hapo jana yake nilikuwa nimechelewa kulala kisa kazi hizohizo.
Niliinuka taratibu mama jamani usiku wote huu niliongea nikaangalia saa ilikuwa ni saa kumi na moja alfajiri nikatoka nje kufanya usafi nilimaliza kazi zote hadi mida ya saa tatu za asubuhi nilikuwa tayari nishamaliza kila kitu.Mama alitoka nje akanikuta nimekaa ukiwa kwangu lazima kazi ufanye hakuna cha bure kama unataka kudeka uende ukadeke kwenu.

Mama unanifanyia hivi ni kwa sababu unajua sina pa kwenda niliongea kwa upole.
๐Ÿ˜„wewe huyo huna pa kwenda si uende ukakae kwa ndugu zako mama yako kwani hakuwa na ndugu, lazima uishi hapa na sisi yaani naomba matokeo yatoke hata kesho uondoke huko shule na kwa hizo akili zako sijui kama utafaulu mtoto unanikosesha amani kweli wewe na ndoa yangu .

Nilibaki nimenyamaza kimya namsikiliza tu maana ningemjibu angeona najibizana nae kuishi na mama wa kambo ni kazi sana basi tu japo mimi alinikuta tayari nimeshazaliwa sijui chuki zinatokea wapi.

Itaendeleaโ€ฆโ€ฆ

*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹๐Ÿ™Œ02*
๐Ÿ’‹
Niliingia chumbani nikajifungia mlango nikaanza kulia ๐Ÿ˜ญ nirifikiria mengi huenda mama yangu angekuwepo yasingetokea haya mateso ila ndio hivyo ndugu wa mama nao maisha yao hayakuwa mazuri sana ningeenda kuishi hata kwao .
Siku matokeo yametoka nilikuwa sijui mama ndio aliniambia kuwa matokeo yametoka nimtajie namba yangu ya mtihani ili tujue . Nilimtajia namba yangu nilikuta nimepata division four nilijikuta nakata tamaa ๐Ÿ˜” kabisa lakini cha ajabu mama alikuwa ananicheka ๐Ÿ˜‚ yaani wewe nilijua tu huna akili bora hata baba yako hajakupeleka shule ya kulipia mbona angepata hasara tu ufanye uolewe ale hata mahari usije ukazalia nyumbani ๐Ÿก ukazidi kututia aibu.mitoto kama hii huwa inawazaga urithi tu wazazi wafe wapate mali Mama aliongea kama kameza cd mimi kama kawaida yangu nilibaki nimenyamaza kimya . Siku hiyo sikuwa hata na hamu ya kula kabisa nilienda๐Ÿšถ kujilalia zangu chumbani .
Kuna ule msemo unaosema ukimpiga chura teke umemuongezea hatua sasa ndicho kilichonikuta mimi mwenyewe alijua ananikomoa kumbe ananifundisha maisha ni nini ๐Ÿค” .
Mida ya jioni mama alikuja kuniita chumbani kwangu kuwa anataka aniagize hapo kwa jirani ambaye ni rafiki yake na mama niende nikamchukulie mzigo . Sikujua ni mzigo gani niliamka nikaenda hadi hapo aliponiagiza hapakuwa mbali na nyumbani ๐Ÿก kwetu ni nyumba ya tatu kutoka nyumbani kwetu. Nilifika nikagonga geti likaja kufunguliwa na mlinzi, karibu unamuulizia nani binti mlinzi aliniuliza? huku akinitazama usoni kwa umakini.

Karibu unamuulizia nani binti ? Mlinzi aliniuliza namuulizia mama Denis mama kaniiagiza kwake nije nichukue mzigo
Sawa karibu ndani bosi katoka kidogo ila atarudi muda sio mrefu utamsubiria kidogo hapo nje kwenye kibaraza. Sawa nilimjibu yule mlinzi nikaenda kukaa kibarazani nikawa namsubiria huyo shoga yake mama.
Kichwani nililkuwa na mawazo mengi sana kuhusu hatma ya maisha yangu yatakuwaje baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari matokeo ndio yamekuja mabaya.
Nikiwa katikati ya mawazo nje gari ๐Ÿš— ilipiga honi mlinzi alifungua geti likaingia ndani nilijua ni mama Denis lakini hakuwa yeye alishuka mkaka๐Ÿง walisalimiana na mlinzi akawa anakuja ndani akanikuta kibarazani nimekaa .
Nilimsalimia aliitikia akaingia ndani baada ya dakika kadhaa alitoka nje akanikuta bado nimekaa.
Mbona umekaa nje muda mrefu ? Namsubiria mama Denis nimeagizwa kwake nilimjibu huku nimetazama chini .
Ingia ndani mama hayupo ila atakuja muda sio mrefu karibu ndani.

itaendelea

*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹๐Ÿ™Œ03*

Asante nilisimama nikaingia ndani , Dada mpatie maji mgeni anamsubiria mama mimi naondoka akija utamwambia nilikuja sina nafasi nitamsalimia siku nyingine.

Sawa kaka Denis dada wa kazi alimjibu hapo ndipo nikagundua huyu ndie Denis mwenyewe.Aliondoka nilikaa kama nusu saa ndipo mama Denis alikuja .
Shikamoo nilimsalimia , marahaba umekuja muda Nelly nilikuwa na kikao kazini mwanangu mama yako kakuagiza uje uchukue mzigo?

Ndio ,Mama Denis alienda chumbani kwake akaniletea bahasha . Hiyo mpelekee mama yako nilichukua nikampelekea mama , alikuwa amekaa sebuleni akaenda chumbani baada ya dakika kadhaa akatoka tena sebuleni huku ile bahasha akiwa ameifungua akakaa kwenye sofa akampigia mama denis .
Simu๐Ÿ“ฑ iliita baada ya sekunde kadhaa ilipokelewa. Alooh shoga mbona hela haijatimia hii ? Nimetoa hela yote mbona kwani ipo kiasi gani ? mama Denis aliuliza . Nimekuta milioni na laki tatu tu laki mbili hakuna mama alijibu mimi nikawa namsikiliza tu mama alikata simu๐Ÿ“ฑkisha akanigeukia umepeleka wapi hela nyingine wewe mtoto ?.
Hela gani mama hiyo bahasha nilivyopewa ndivyo nilivyoleta.

Umeiba hela Nelly hizi hela sio zangu ni za baba yako kwahiyo sasa mtajuana wenyewe ngoja ninyamaze kimya mimi, lakini mama mimi sijaiba hela yoyote ile.
Shhs ๐Ÿคซkimya usiniambie chochote kile utakuja kumwambia baba yako maana nikiongea mimi nitaonekana nakuonea kulea mtoto wa mtu kazi sana . Mama aliondoka sebuleni akaenda chumbani kwake nilibakia sebuleni nisijue cha kufanya . Niliamua niende zangu kulala tu usiku baba alikuwa ametoka safari aliyoenda nilienda kumpokea ila sikuwa na furaha๐Ÿ˜” kabisa . Wewe vipi tena hauna furaha una shida gani๐Ÿค” ? baba aliniuliza lakini kabla sijajibu kitu mama alikuwa tayari ameshakuja akadakia mwambie makosa uliyofanya baba yako ajue yaani mwanao siku hizi kawa mwizi na hela sijui anapeleka wapi? pia matokeo yametoka amefeli wastani kapata mbaya .

Nelly anayoongea mama yako ni kweli๐Ÿค” baba aliniuliza nilikuwa na machungu sana moyoni mwangu nilishindwa kujibu baba alinitandika kofi ๐Ÿ‘‹ moja nilihisi nyota nyota . Mimi sijaiba nilipewa hela nimeleta kama zilivyo . Kwahiyo unataka kusema mama Denis ni muongo huyu inabidi nimkague itakuwa tu kaiba kweli. Mama aliongea huku akielekea chumbani kwangu baada ya dakika kadhaa kweli alitoka na hela nilikuwa nimehifadhi kwenye mfuko wa sketi yangu ya shule.



*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹๐Ÿ™Œ04*

Hizo hela zilikuwa zangu mimi mwenyewe nilikuwa nazitunza kipindi nasoma ili nije ninunue simu nahisi mama aliziona akaamua anifanyie mchezo ijulikane nimeiba hela mimi .........

Baba mimi sijachukua hizo hela , hizo hela ni za kwangu nilikuwa natunza . Unatunza hela unazitoa wapi kama sio kutuibia sisi ,mama alidakia.
Kwanza umefeli , pili unaiba hela nimekuchukua kukulea kama msaada tu kwa sababu mama yako amefariki ila sina shida na watoto tena mtoto mpumbavu kama wewe msaada wangu ulipofikia unatosha kusanya kila kilicho chako kesho nakupeleka kwa mama yako mkubwa ukaishi huko ndicho ulichokuwa unakitaka. Baba aliongea hakutaka hata kunisikiliza aliingia ndani nilibaki nimesimama sina cha kufanya.

Si ukakusanye virago vyako au hujaelewa mama aliongea huku akicheka ๐Ÿ˜‚ akaingia ndani na yeye. Niliingia ndani nikaenda kupanga nguo zangu taratibu, mara mama alikuja kusimama nyuma yangu tena ngoja nije nikuangalie usije kuiba nguo za binti yangu bure maana mwizi ni mwizi tu .

Sikujibu kitu nikawa naendelea na kazi ya kupanga nguo hadi nilivyomaliza nilitoa begi nje ndipo mama na yeye akatoka nje nilikaa sebuleni nikawa namsubiria baba , Moyoni nilikuwa na machungu ๐Ÿฅฒ sana ila niliona bora niondoke tu manyanyaso niliyachoka. Baba alitoka chumbani vipi ushakusanya vitu vyako tayari? Baba aliniuliza nikamjibu ndio nimeshakusanya haya twende kwa mama yako mkubwa labda mtawezana kwa hizo tabia zako.

Kwa kuwa baba alikuwa ana usafiri wake tulifika mapema nyumbani ๐Ÿก kwa mamkubwa , alipaki gari ๐Ÿš™ tulishuka bahati nzuri mamkubwa alikuwa amekaa njee alishangaa kuniona nipo na mizigo. Enhee ๐Ÿ˜ณ kulikoni tena na mizigo ghafla tena bila taarifa ๐Ÿค” mamkubwa aliuliza. Nimemleta mwanao ili tusaidiane kulea siku hizi amekuwa na tabia za hovyo mimi sikai sana naomba niende .
Baba aliaga kisha akaondoka zake nikabaki na mamkubwa pale nje.

Nelly unaona maisha yalivyo magumu unapata nafasi ya kulelewa bado unaleta ujinga kwanini ? Mamkubwa aliniuliza , mamkubwa unanifahamu mimi vizuri sina hizo tabia mama mwenyewe ndio ana matatizo ananisingizia mimi vitu ambavyo sijawahi kufanya .

Sasa kama hujafanya kwanini umekubali kosa nimpigie simu ๐Ÿ“ฑbaba yako sasa hivi hapa nimwambie kama umesingiziwa, Hata ukimwambia haisaidii hana kauli kwa mke wake kwanza mimi mwenyewe nishaingiwa na kinyongo siwezi kurudi tena pale.

Mhh๐Ÿค” haya ila mimi maisha yangu ya hapa ni magumu sana nifanye vibiashara ndio nile na kusomesha mwanangu utaweza kuishi na mimi kweli? Kwanini nisiweze wakati wewe ndio mama yangu nitakaa na wewe hivyohivyo bora ugali dagaa kwenye amani kuliko wali nyama vitani.

*SEHEMU YA TANO*

Haya karibu Ingia mizigo yako ndani huko kisha uje usonge ugali tule nimeshanunua fungu la dagaa mchele tutalumagia tu.
Niliinuka nikaingiza mabegi yangu ndani kisha nikatoka nje nikaenda jikoni kusonga ugali, Huyu ni mama yangu mkubwa anaishi kibaha loliondo ndipo alipojenga nyumba ๐Ÿก yake ya vyumba viwili na sebule sehemu nyingine alikuwa hajamalizia . Akitoka yeye ndie anafuatia mama yangu kisha mdogo wao wa mwisho wa kiume nae alishaoa mama yangu mkubwa alijaliwa mtoto mmoja tena alichelewa kuzaa kweli ndio kwanza yupo shule ya msingi darasa la sita. Niliivisha chakula๐Ÿดnikaandaa ili tule bahati nzuri na mwanae alikuwa asharudi shule tukala pamoja.
Kesho yake asubuhi ๐ŸŒ„ na mapema mamkubwa aliamka ili aende kwenye biashara yake na mimi niliamka , Na wewe kuamka mapema asubuhi ๐ŸŒ„ yote hii kulikoni mamkubwa aliniuliza, Nataka nikusindikize kwenye biashara yako nikusaidie kuuza nilimjibu. Haya kwa kuwa umetaka mwenyewe mimi nauza karanga na korosho pale stendi ya magari mbezi na huo usista duu wako sijui kama utaweza ๐Ÿค”.
Mamkubwa usidharau mtu unaweza kukuta mie nikauza hadi ukashangaa kila mtu na nyota yake. mhh๐Ÿค” ngoja tuone mtu mwenye nyota yake leo. Mtoto wake alienda shule na sisi tukaenda mbezi kuuza korosho na karanga ana meza magari yakipita naenda kuuza nilijitahidi kuuza hadi mamkubwa alinisifia .Giza lilipoingia tukarudi nyumbani kweli uliniambia una nyota leo nimeuza sana kuliko siku zote shika elfu mbili hii utanunua chochote . Mamkubwa hata usijali hiyo hela tutanunua hata mboga nashukuru ๐Ÿ™ sana niliirudisha ile hela tulipika zetu ugali na matembele tukajilalia zetu .
Kesho niliamka asubuhi ๐ŸŒ„ nikafanya usafi tukaenda zetu kwenye biashara kama kawaida yangu nikawa nikiona magari au daladala naenda kuuza, Mamkubwa akawa anauza kweli ulipita mwezi nikawa nimeshazoea kuuza . Siku hiyo kuna gari ๐Ÿš™ lilipita karibu na sisi likasimama inaonekana mwenyewe alikuwa anataka akanunue vitu mimi tena nikaona mteja si ndio huyu nikaenda kupeleka korosho na karanga. Karibu korosho kaka niliongea tulivyotazamana na yule kaka wote tukabaki tunashangaana nikajisemea nisitoke kwenye reli hapa nikajikausha , Kaka korosho tamu hizi grade one kutoka mtwara kuna mbichi na zilizokaangwa unataka zipi๐Ÿค”. Dada samahani nakufananisha kama nimekuona mahali hivi ๐Ÿค” yule kaka aliniuliza , utakuwa umenifananisha . Sawa naomba korosho za elfu kumi. ๐Ÿ˜ณ nilibaki nimeduwaa za elfu kumi tena . Mbona unashangaa niletee hizo korosho nilienda kuchukua alibaki ananiangalia hadi nilivyokuwa narudi akanipatia hela, nikaondoka nikarudi kukaa maana sikuwa na ujasiri hadi alivyoondoka yule kaka na gari ๐Ÿš™ lake.
Mbona kama umepoa ghafla ? mamkubwa aliniuliza , Hapana mama nipo sawa tu nilimjibu kisha nikachukua korosho nikaenda kuuza giza ๐ŸŒƒ lilipoanza tulirudi nyumbani ๐Ÿก usiku ๐ŸŒƒ kucha nikawa namuwaza ๐Ÿค” yule kaka.
Kesho yake mamkubwa akaniomba niende mwenyewe yeye hajisikii vizuri sikuwa na hiyana nikaenda kuuza mwenyewe nikiwa nimekaa sina hili wala lile nikasikia mtu ananiita jina langu Nelly niligeuka nikaitikia nilimkuta ni Denis yule kaka ambaye nilikutana naye jana .

MWISHO WA KIONJO

Maoni

You're not logged in


Tangazo - SHUKRANI โ€“ Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
SHUKRANI โ€“ Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
SHUKRANI โ€“ Emidee ft. Mbacho Wizzy (Official Lyrics Video) ? Produced by: Gift Record ? Released: 20
Wimbo wenye ubunifu imechanga kiarabu kiswahili na amapiano wimbo wa kushukuru kwa maisha na upendo Sasa sikiliza na ku download hapa gonga94.com
Sikiliza Wimbo Kamili
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO* *1-5* *

__________________________________*

*SEHEMU YA KWANZA*

Naitwa Nelly ni mtoto wa kwanza kwa baba yangu wazazi wangu hawakuwahi kuishi pamoja hivyo niliishi na mzazi mmoja tu ambaye ni mama .

Niliishi na mama yangu hadi nilivyofika kidato cha kwanza mama akaanza kuugua hatimaye MUNGU alimpenda zaidi mimi nikakosa mtu wa kukaa nae ndugu wa mama wengi wao maisha yao yalikuwa chini sana ikabidi nikaishi na baba yangu muda huo alikuwa tayari ana familia nyingine. Walibahatika kupata watoto wawili wa kiume mapacha na mwingine binti mkubwa alimkuta kwa mkewe tulipishana miaka mitatu yeye alikuwa mkubwa kwangu nilimkuta yupo kidato cha tatu alikuwa anaitwa...

๐Ÿ‘‰ Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/ila-boss-anajua-kupeleka-moto-1-5

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle #BeautyBattle #AfricaVsWorld #Tanzania #Kenya #Congo #Rwanda #Burundi #SouthAfrica #USA #VoteNow #DebateTime #Trending <br>

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu ยท dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi ila-boss-anajua-kupeleka-moto
๐Ÿ’‹ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹ 6 na 7
๐Ÿ’‹ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹ 6 na 7
 ๐Ÿ’‹ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹ 8,9,10
๐Ÿ’‹ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹ 8,9,10
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 68

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 68

1.25K
AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 69

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 69

933
AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž 70 Hadi 72

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž 70 Hadi 72

639
SHAMIRA 99 na 101

SHAMIRA 99 na 101

331
SHAMIRA 102 kwa 104

SHAMIRA 102 kwa 104

298
SHAMIRA Sehemu ya 97&98

SHAMIRA Sehemu ya 97&98

237
SHAMIRA 105 na 106

SHAMIRA 105 na 106

225
SHAMIRA 107 Hadi 109

SHAMIRA 107 Hadi 109

225
NAKUPENDA BILA MIPAKA  36 - 45

NAKUPENDA BILA MIPAKA 36 - 45

190
JOGOO WA KIENYEJI 9 na 10

JOGOO WA KIENYEJI 9 na 10

187

ZIMESOMWA ZAIDI

โ€ŽTUNDA LA  DADA โ€Ž โ€ŽSEHEMU YA KWANZA

โ€ŽTUNDA LA DADA โ€Ž โ€ŽSEHEMU YA KWANZA

11.8K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.53K
๐Ÿ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA๐Ÿ”ฅ  sehemu ya tisa.  ๐Ÿ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...๐Ÿ‘‡

๐Ÿ™„ NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA๐Ÿ”ฅ sehemu ya tisa. ๐Ÿ‘‰ Akaanza kunipamp sasa...๐Ÿ‘‡

3.85K
๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ  Sehemu ya sita.  ๐Ÿ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...๐Ÿ‘‡  Shemeji inauma utanichana.

๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ Sehemu ya sita. ๐Ÿ‘‰ Aaaaaaaaa chomoa...๐Ÿ‘‡ Shemeji inauma utanichana.

3.35K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 119 na 120.

2.97K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 108

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 108

2.95K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 116 na 117

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 116 na 117

2.78K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ  Sehemu ya 20.  ๐Ÿ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...๐Ÿ‘‡

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ Sehemu ya 20. ๐Ÿ‘‰ Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...๐Ÿ‘‡

2.74K
MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 106 na 107

MY WANGUโค๏ธ sehemu ya 106 na 107

2.68K
๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ  Sehemu ya 16.  ๐Ÿ‘‰ nakupenda pia...๐Ÿ‘‡

๐Ÿ”ฅ UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa๐Ÿ”ฅ Sehemu ya 16. ๐Ÿ‘‰ nakupenda pia...๐Ÿ‘‡

2.61K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
KAMA ULIZALIWA BAADA YA MWAKA 1995 HAYA MAMBO YALIKUPITA: Post Mpya
KAMA ULIZALIWA BAADA YA MWAKA 1995 HAYA MAMBO YALIKUPITA:
@majario LIVE

1. Kupakwa GV kwenye kidonda 2. Kung'olewa jino kwa uzi 3. Ubwabwa kupikwa jumapili tu 4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetesakrin 5. Kupamba kadi na pamba sebuleni 6. Ukumbi wa sherehe kupambwa...

SHAMIRA 107 Hadi 109 Post Mpya
SHAMIRA 107 Hadi 109
@majario LIVE

Sehemu ya 107 Wassap; 0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Akasema acha na masuala ya mtoto bwana apa nipo mimi na wewe plsss mpenzi . Nikajikuta nacheka tu akanmbia daah ukicheka...

Jamie Carragher baada ya Senegal๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ณ kuinyangโ€™anywa(na CAF)ubingwa na kuitangaza Morocco๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ kuwa mabingwa wapya:๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ๐ŸŽ™ Post Mpya
Jamie Carragher baada ya Senegal๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ณ kuinyangโ€™anywa(na CAF)ubingwa na kuitangaza Morocco๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฆ kuwa mabingwa wapya:๐Ÿด๓ ง๓ ข๓ ฅ๓ ฎ๓ ง๓ ฟ๐ŸŽ™
@majario LIVE

โ€œSawa, subiri kidogoโ€ฆ kwa hiyo Senegal wanashinda fainali ya AFCON, mashabiki wanashangilia, wachezaji wanainua kombe, kila mtu anasherehekea halafu sasa wanaambiwa: 'Hapana, samahani, Morocco ndio washindi 3-0!' Unatania?" "Yaani, hii ndiyo...

 ๐Ÿ’‹ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹ 8,9,10 Post Mpya
๐Ÿ’‹ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹ 8,9,10
@majario LIVE

O8 Unamaanisha hii simu๐Ÿ“ฑni yangu ๐Ÿค” nilimuuliza , Ndio ni yako lete nisevu namba yangu baadae nataka tuongee kuhusu kazi . Sawa nashukuru ๐Ÿ™ sana kaka Denis Mungu akubarikii ulipotoa akuzidishie....

๐Ÿ’‹ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹ 6 na 7 Post Mpya
๐Ÿ’‹ILA BOSS ANAJUA KUPELEKA MOTO๐Ÿ’‹ 6 na 7
@majario LIVE

O6 Umekuja tena ? nilimuuliza . Ndio kwani ni vibaya kuja kukujulia hali wakati wewe ni jirani yangu sasa kwanini jana ulikataa kuwa sio wewe wakati nakufahamu vizuri hadi nimeenda kumuuliza...

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž 70 Hadi 72 Post Mpya
AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž 70 Hadi 72
@majario LIVE

Sehemu ya 70 Siwafichi umaraya sikuwa nimeacha ila.nilipunguza sana, yani sanaaaaaaa , yani nachepuka sawa ,ila kwa kutokezea sana, nilitulia na awa wake zangu wawili, ata ibraa alinambia nimechange...

LETICIA 1 MPAKA 6 Post Mpya
LETICIA 1 MPAKA 6
@majario LIVE

๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’ LETICIA Sehemu ya 01 Mwandishi; LISSA Kwa majina naitwa leticia sabasi, wengi wanapenda kuniita leti,kwenye familia yetu ya mzee sabasi tumezaliwa mabinti wa wawili ,mimi ni mtoto wa mwisho kuzaliwa anaanza dada...

SHAMIRA 105 na 106 Post Mpya
SHAMIRA 105 na 106
@majario LIVE

Sehemu ya 105 Mwandishi; lissa wa huru media Nakuuliza wewe hivi shamira una shida gani na uyu mtot eeh kwanini unampiga piga. Mimi mwenyewe sijawahi kumgusa ata siku moja uyu...

AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 69 Post Mpya
AFANDE MILLAN๐Ÿ˜Ž Sehemu ya 69
@majario LIVE

๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ๐Ÿฆˆ Nikasema sawa kama umemfahamu zena sasa, nimemuoa sasa na yeye ni mke wangu pia, jalia akaniangalia sana kisha akasema sawa mimi nimeshajua kuwa umemuoa uyo zena, yeye anajua kuhusu mm,...

SHAMIRA 102 kwa 104 Post Mpya
SHAMIRA 102 kwa 104
@majario LIVE

99. MPK 104 (NARUDIA KUSEMA HURU MEDIA WABABE๐Ÿ˜‚) ๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€ ๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€๐Ÿ€ SHAMIRA Sehemu ya 102 Wassap; 0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Basi walivyomaliza kula love hakuniuliza kitu ata...

JOGOO WA KIENYEJI 9 na 10 Post Mpya
JOGOO WA KIENYEJI 9 na 10
@majario LIVE

๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“ sehemu ya 9 Mwandishi:lissa mwalla Alikua ni Ivan, sikuamin mana sura yake haikubadilika japo alikua amekua, tulitizaman huku mm nikiwa sijui nimsalimie au nimshangililie lkn huyu anajua siri yangu mm nikichofanyiwa kipindi...

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 8 Post Mpya
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 8
@majario LIVE

Mwandishi:lissa mwalla Babaaa! Niliita kwa mstuko, baba akasema tayla wee taaaay... Kabla hajamaliza niligeuka nyuma na kuanza kuondoka, kumbe DA frida alikua anatembea na babangu siku zote hizi? Baba kampangia anaishi...

BILLIONS OF LOVE๐Ÿ’“๐Ÿ’“   SEHEMU YA "7_8"๐Ÿ’“๐Ÿ˜ฝ Post Mpya
BILLIONS OF LOVE๐Ÿ’“๐Ÿ’“ SEHEMU YA "7_8"๐Ÿ’“๐Ÿ˜ฝ
@majario LIVE

"BY BABIE LOVE" Huyu kashaliwa huyu tena usiku kuchaaaa Mama Samson sasa kwa aibu akanipita bila hata kunisalimia Mara zee mapumba hili hapa linatoka likiwa alinafunga xipi yake vzr loooh ๐Ÿคฎ...

SHAMIRA 99 na 101 Post Mpya
SHAMIRA 99 na 101
@majario LIVE

Sehemu ya 99 Mwandishi; lissa wa huru media Mh shoga yenu nikawa ata sijielewi elewi .mala simu yangu ikaingia sms.nikavuata simu .nakuta sms nimetumiwa imeandikwa .asante kwa penzi tamu shamira siajajutia...

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kuwavua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco, Post Mpya
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kuwavua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco,
@majario LIVE

Kufuatia uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wa kuwavua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco, mshambuliaji wa Senegal, Sadio Manรฉ, ameonyesha kusikitishwa na...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest