Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

NAKUPENDA BILA MIPAKA 26 - 35
Gonga94 · Stories

NAKUPENDA BILA MIPAKA 26 - 35

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.

:26
Nikacheka na kusema “Muanko ana muda sasa, hacheki na yeyote, yaani tabasamu lake tangu nifike pale sijaliona dada hivi unanielewa.”

Alinitazama akisema “eenh chaupole wangu nipe nipe.”
Nilimtazama na kusema “wewe tena ukishaamua kunijaza. Sasa sikia dada Dee. Kuna huyu wa kuitwa Dokta Kabale. Kwanza dada ananata balaa, dada ana deka muda wote, kujifanya mzungu muda wote, huyu sasa ndiyo naona tatizo, yaani sijui nikuambie nini.”
Alinitazama Dorice akiuliza “ana uzuri?”

Nilitabasamu na kusema “ndugu yangu watu wanaoga, kama kuoga tu watu wanajua. Dada ni mzuri, dada ana ngozi safi, dada anavutia haswa ila sasa anaonekana mkali sana.

Masharti kibao utadhani yeye ndiyo mwenye nyumba, au na yeye ni mtu wa pale, maana ananichosha mimi. Ila sio mbaya nitajua namna ya kuishi naye maadamu mimi na mgonjwa tunashibana.”

Dee alitabasamu na kusema “hilo sasa ndiyo uliloliacha, hiyo ni sehemu nzuri kipenzi. Jikaze, si unaona maisha ya nyumbani yalivyo eenh, hapo shoga yangu tunza kihela chako mwisho wa siku tufanye vitu vya maana na sisi tuheshimike.”

Nilimtazama na kusema “hilo nalo neno, lakini watoto wa maskini sie vinatunzika.” Akacheka akisema “tena shooo weka mbali haswaa.” Halafu akapunguza sauti na kusema “mara shwaaaa Baraka kapita nayo si unajua akili zake.”

Tulijikuta tunacheka halafu nikawa namuuliza “vipi mama Dorice sijamuona wiki sasa hapa nilipo nishamkumbuka.”

Akacheka akiinuka na kusema “si ndiyo uje sasa, una muulizia mama ukiwa mbali hivi binti. Uje yeye mwenyewe kidogo tu anakutaja ameshakumiss mtoto wake mzuri maana anaona mimi chenga muda wote. Haya sasa kipenzi mimi naenda, shemeji yako alisema anakuja mpaka sasa simuoni keshanikera tena.”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:27
Nilimtazama na kusema “wewe tena na kudeka, sina neno mie.”
Alitabasamu akicheka huku anatoka, na mimi nikawa natoka. Tulikuwa na furaha sana.

Waliongea mawili matatu pale akawa anamuaga mama, mama sasa anacheka akisema “wewe Dori bhana haya mwanangu karibu tena, msalimie mama.”

Dori anavyocheka akisema “na usikute mshaonana leo sasa namsalimia nini mama.”
Mama alicheka akisema “na kweli tushaonana, wewe msalimie tu.”

Tulicheka tena, huku mama akisema “yaani Dorry ni mchangamfu sana.”
Nilitabasamu na kusema “saana mama, ana roho nzuri pia.”

Mama alitabasamu, akanitazama akisema “eenh niambie mwanangu habari za kazini?”

Nilimtazama mama na kumjibu kwa upendo nikisema “kusema kweli mama namshukuru sana Mungu, Mungu ni mzuri mama. Nimekutana na mgonjwa mzuri na tunaelewana vizuri.”

Mama yangu akanitazama anatabasamu na akisema “jamani anaumwa nini maradhi haya.”

Nilisema kwa upole “wacha tu mama. Amelala tu hapo kitandani hawezi lolote lile zaidi ya kuzungumza tu kwa sauti ya huruma na kula nayo nimeambiwa leo ndiyo amekula.”

Mama alitabasamu na kusema “mwanangu, Mungu amekupendelea. Wewe una kibali sana ch kukubalika Mungu azidi kukufungulia milango si unaonaga hata hao maboss zako wengine wanakutafuta ni vile wagaigai.”

Nilitabasamu nikisema “ni kweli mama, ni kweli namshukuru Mungu kwaajili ya hilo. Mama vipi mjukuu wako, hapa najikaza akili yote kwake.”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:28
Mama alicheka akisema “wewe nikiwa napiga simu zangu za hofu unaanza ooh mama ni msumbufu, mama usijali nipo sawa, mama akijua haupo sawa na upo mbalo anapigapiga simu kama nini.”

Nikacheka na kusema “lakini na wewe mama umezidi jamani nisiseme.”
Mama alicheka akisema “huo ndiyo uchungu nakuambia, bila uchungu wewe kuweza. Mjukuu wangu kihoma tu naona kilikuwa kinamnyemelea ila usijali, atakuwa tu sawa mwanangu, kama nikiona kesho ameamka na joto tena nitawahi hospitali haraka.”

Nilitabasamu na kusema “mama, leo nimepata elfu 30 hii hapa, lakini wewe shika 20 kwanza kapunguze punguze madeni huko dukani, halafu sasa kesho tutaona tufanye nini.”

Mama alinitazama na kutabasamu akisema “mwanangu, ni mshahara wako wa kwanza jifanyie hata jambo.”
Nilitabasamu, halafu ndiyo nikasema “mama ndiyo najifanyia jambo sasa si unaona hata wewe.”

Mama alitabasamu, kisha alipokea akisema “mwanangu Nazwi, utulie mwanangu, tulia ufanye kazi. Nafasi kama hizi za kupata pesa haziji mara mbili tena pesa hujawahi kupata. Nakuomba sana binti yangu”

Nilitabasamu nikisema “ondoa shaka mama, ngoja nikamuone binti yangu.”

Mama alikuwa ananitazama kwa furaha unajua tena eenh, na mimi nikawa tu nina amani Ingawa nimechoka lakini lazima nifanye ya hapa nyumbani.

Nakumbuka nikaingia chumbani na kukuta mwanangu amelala, nilikaa pembeni yake, unajua kila nikimuona mwanangu ni kama napata nguvu ya ajabu sana.

Machozi yalinitoka huku ndani yangu nikimwambia binti yangu nikiwa nimeshika mkono wake mdogo “binti yangu mzuri Priya, mama yako nimepata kazi.

NAKUPENDA BILA MIPAKA:29
Upande mwingine ni kazi ya ndoto zangu. Imepitiliza matarajio yangu. Kiukweli nimefurahia sana. Tafadhali binti yangu, usiache kumwambia Mungu nataka zaidi.

Kwasababu natamani upate maisha mimi mama yako sikuyapata pengine binti yangu hutokosea namna hii na huu ndiyo ukweli, natamani upate maisha bora, vile sikuwahi pata wewe upate, uwe bora sana binti yangu. Nakupenda.”

Nikasikia mama akisema “usije niamshia mtoto huko.”
Nilitabasamu tu, unajua bila mama yangu kuna muda nawaza ingekuwaje.

Mama anafanya maisha yangu yawe rahisi sana haswa kwa malezi. Ni kama mwanaye vile kumbe ni mjukuu, aliumia sana mimi kupata mtoto kabla ya mambo muhimu.

Ila alinipokea mimi na binti yangu kwa upendo na hajawahi hata siku moja ongelea hili kwa nia mbaya zaidi ya kunikanya kutorudia kosa na kukaa mbali na huyu mwanaume.

Nampenda sana mama yangu, Mungu ampe maisha marefu pengine siku moja nitafanikiwa na yeye atakuwa sehemu ya kula jasho langu kwa furaha.

Nikarudi kwa mama, mama aliniambia ameniachia chakula, nilienda kutazama na kusema “kaka Baraka hajarudi tu.”

Mama alisema “Mungu tu anisikie natamani sana kaka yako abadilike, natamani. Ni kijana mzuri tu ila sasa.”

Nikasikia vibaya sana ndani yangu, roho iliniuma, mimi tu mtoto kaumwa kidogo nimeumia sasa vipi mama anayeona mtoto wake anapotea. Nilisema kwa upole “mama usijali, ni suala la muda tu kaka atakuwa mtu makini sana.”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:30
Mama aliguna na kusema “haya mwanangu mimi naingia chumbani.”
Nikawa sina namna, mimi nikawa sasa napata muda nachezea simu yangu huku nakula, baada ya hapo binti nikaanza msaidia mama yangu kazi walau asubuhi akiamka nyumba iwe safi ahangaike na biashara yake sio huku Mjukuu, huku kazi hii, huku vile na mama mwenyewe afya yake kuumwa umwa hivyo sitaki kabisa achoke.

Vile nafanya kazi mama aliita “Nazwiii!!, mwanangu unafanya nini?, kwani hujachoka?”

Nilimjibu kwa upendo “kuchoka kawaida mama ila sio kivileee, halafu mama nakusaidia ili na wewe usiteseke. Si unajua asubuhi kazi nyingi huku mtoto, huyu biashara huku nyumba chafu hapana, sitaki uumwe na mimi niwe sababu.”

Mama alitoka chumbani, alinifuata nilipo.Alinitazama kwa upendo sana, akanishika mabega yangu kwa upendo na kisha nywele zangu.

Sijui pengine alikuwa ananitamkia baraka sijui, ila alipokuwa anafanya hivyo kuna raha ilikuja ndani yangu, amani na utulivu wa hali ya juu sana.

Nilikuwa nafurahia sana halafu akaniambia “nashukuru sana binti yangu. Ukaoge upumzike sasa. Inaenda saa tano sasa.”


Nilimtazama mama kwa furaha na kusema “uwe na usiku mwema mama, Mungu akulinde.”
Alitabasamu na kusema “uweke alarm sasa nakujua wewe.”
Nikacheka tu.

Basi nilioga vizuri, nikapanda kitandani. Nikiwa kitandani nikashusha pumzi ndefu. Nikakumbuka yule mama mgonjwa.

Yupo kitandani anaumwa lakini bado anakumbuka kusali halafu mimi binti mdogo kusali naona taabu eenh, nilitabasamu na kusema “nitajifunza kuhusu Mungu, kama hata watu wanapesa, wana maisha mazuri kiasi kile wanamuomba Mungu. Mama yule anaumwa bado anamuomba Mungu.

NAKUPENDA BILA MIPAKA:31
Halafu mimi umri huu, sina chochote cha maana kwenye maisha zaidi ya binti yangu na pumzi lakini sijaona umuhimu wa Mungu. Haiwezekani.”

Nikajikuta natabasamu, na kusema “asante Mungu, leo ni siku nzuri sana kwangu. Naomba siku nzuri zaidi.”

Nikacheka kidogo na kujiuliza “sasa ndiyo nafanya nini.Mungu anajua nilicho maanisha.”

Nikajilaza, huku nakumbuka vile nimefika pale, mambo ya pale, mimi nikawa nashangaa tu kila kitu kinavutia. Sasa suala la Mr Gallen.

Nikawa najikuta nacheka.Nikajiambia tena “oooh!!, wewe binti naona unachanganyikiwa muache muanko wa watu.”

Nikaweka simu pembeni, na kuamua zangu kulala.

Unajua tena ukiwa umechoka zako. Unapata usingizi mzuri sana hiki ndiyo kilinitokea. Nilikuwa nimepata usingizi mzuri. Nimeamka, nakuta mama tayari ameamka yupo zake ana andaa vitu vyake.

Nilimsalimia nikisema “ni kama umewahi sana leo mama?”
Mama akanitazama na kusema “mwanangu biashara ikiwa nzuri unapata mood ya kazi, wateja wamekuwa wengi basi nazidiwa acha tu.”

Nilitabasamu na Kusema “Mungu atusaidie mama. Ningekuwepo ningekusaidia.”
Alinitazama na kusema “upo mwanangu, uwepo wako upo sana. Fanya ujiandae sasa uwahi eenh.”
Nilifurahi sana kuzungumza na mama asubuhi hii.
Nilianza kujiandaa.

NAKUPENDA BILA MIPAKA:32
Sasa vile najiandaa maandazi ya mama yananukia. Maandazi haya huwa mazuri sana. Mama yangu anajua kuyatengeneza, najua pia lakini yeye akipika tofauti na mimi, yake kama matamu sana.

Na kwa mtaani hapa ameteka.Watu huyapenda sana wengine hununua mengu utasikia “nitanywea soda mchana, au haya jioni na maharage niwekee mama Nazwi.”
Haya yote kwetu ni furaha.

Nikiwa sasa naendelea kujiandaa, huku ile harufu nzuri ya maandazi ikinisumbua. Nilijikuta namkumbuka yule mama anayeumwa alivyo sisitiza. Nilitamani sana kubeba lakini nikikumbuka maneno ya Dokta maringo. Naona tu nisije poteza kazi yangu.

Nilijiambia ndani ya moyo wangu “sitabeba, nisije beba mama wa watu akaugua bure. Sitafanya hivyo.Mambo yenyewe hajazoea. Hapa nile mie tu mengine hapana maana huyo Dokta atanifukuza hata kazi yenyewe.”

Basi nikaendelea kujiandaa, nikavaa zangu vizuri kabisa. Baada ya hapo nilitoka na kusema “mama yangu, mimi naenda. Lakini huko situmii simu kabisa. Kama kuna lolote nitumie hata ujumbe, kuna ule muda wa kula nitachungulia kidogo uniambie tu anaendeleaje. Halafu sasa naomba nitafune andazi maana linanukia balaa.”

Mama alicheka akisema “wewe tafuna tu utalipia.”
Nikacheka na kusema “mama hadi mimi?”

Akacheka akisema “sasa ni biashara, kwenye biashara ukiendekeza ndugu, marafiki, sijui wananifahamu mbona utafunga. Hata mimi nikija kwa biashara yako nidai pesa mengine tutajuana nje ya kazi.”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:33
Nikacheka nikisema “mama unajua pesa wewe mama nini, haya mama yangu kazi njema. Byeee!!”
Mama nilimuacha anacheka tu.

Nilienda kupanda zangu gari huku nakula barabarani wala sio shida zangu. Safari ilikuwa ni ya taratibu siku hii mpaka nikawa naona hapa nachelewa. Ila nitafanya nini ndiyo usafiiri tena.

Nilishuka nikaanza kutembea, na kwa bahati nikiwa naenda nilikutana na yule boda siku ya jana alinibeba na kunipa habari.

Aliponiona tu alisimamisha akisema “sisteri nikupe lifti.”
Nilimtazama na kusema “ni wewe tena, asante sana jamani.”

Akasema “vipi palepale pa jana, mimi kuna mteja wangu namfuata maeneo hayohayo.”
Nikapanda huku nikishukuru, alianza kuendesha akisema “umepata kazi sisteri?”
Nikatabasamu na kusema “ni kweli namshukuru sana Mungu.”

Akaniambia akiwa na furaha “hongera sana dada, sio watu wote haswa mabinti wazuri kama wewe hivyo wanapenda kazi. Nakupongeza. Sasa huku kazi gani?”
Nilitabasamu na kusema “mimi ni Nesi, hivyo nakuwa nashinda na mgonjwa.”

Akasema akicheka “aanh kumbe nipo na nesi sasa nikiumwa ninaye wa kumsumbua.”
Nikacheka na yeye alijitambulisha akisema “mimi naitwa Baraka dada yangu.”

Nilitabasamu, kwasababu ana jina la kaka yangu na kusema “una jina la kaka yangu nyumbani.”
Akacheka akisema “unaona sasa kwahiyo mimi nishakuwa kaka tayari.”

Tulijikuta tunacheka, na mimi nikamwambia “naitwa Nazwi.”
Aliniambia “nafurahi kukufahamu sisteri, sasa tushafika mimi naendelea mbele. Nakutakia siku njema.”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:34
Nilitabasamu na kusema “nashukuru sana, umeniwahisha.”
Basi akawa ana ondoka zake, mimi tena na kengele yangu kama kawaida mlinzi akanifungulia.

Vile nimeingia, nimesign pale mlangoni na nikaanza kufuata mjengo. Mbele yangu namuona dokta kapendeza mwenyewe ana mavazi yake ya kisasa haya na vile ana rangi safi basi nakuambia hapo bado hajaweka koti juu.

Halafu jana huyu Boss alivaa Suti, leo kavaa kawaida fulani hivi na chini kapiga raba fulani basi nasema “mmh wanapendeza sana.”

Niliwafikia, mimi nawaona ni wakubwa zangu, niliwasalimia kwa heshima “Shikamoni.”
Dokta alinitazama na kujibu “marahaba Nazwi.” Kisha akafuata huyu Mr Gallen “marahaba.”

Halafu wakaendelea, nilipiga hatua chache kuelekea ndani. Nikasikia Dokta anasema “Nazwi natumai jana ulinielewa eemh?”
Nilitabasamu kidogo na kusema “bila shaka Dokta.”

Hakuongeza neno, nilimuelewa yeye alizungumzia maandazi sijui anaona ni uchafu sijui. Laiti angejua watu wanavyo gombaniana huko we muache tu. Waliendelea na mazungumzo yao. Mimi nikaingia ndani.

Nikafika ndani nilikutana na dada Maria akiwa na mambo yake. Nikamsalimia vizuri na yeye aliniitikia akisema “karibu sana nesi.”
Nilitabasamu.

Kisha nikaingia kwa chumba changu cha kubadilisha, halafu baada ya hapo nikaingia chumbani kwa mama. Niligonga na kuingia. Mama alikuwa tayari ameamka.

Nikatabasamu na mwa furaha nilimsalimia nikimuuliza “eneh unaendeleaje mama yangu mzuri eenh?”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:35
Mama huyu alitabasamu na kusema “nilikukumbuka sana, natamani kama ungekuwa unalala hapahapa. Sijui ni kwanini binti yangu, uwepo wako unanipa furaha sana.

Labda ni kwasababu wewe ni mrembo sana. Kuna namna nikikutazama ninajisikia. Karibu sana mwanangu, sasa niambie mjukuu wangu anaendeleaje?”

Nilitabasamu na kusema “ooh mama, ni homa tu za hapa na pale si unajua. Nimeacha amelala nimemwambia mama wanijulishe itakuwaje.”

Akatabasamu na kisha nikaingia bafuni kwa lengo la kuandaa maji nimsafishe kwanza, nisafishe chumba na kicha apate na dawa na kula.

Nilipomfikia akanitazama na kusema “eenh niambie umeniletea?”
Nilishusha pumzi tu na kusema “mama kwasasa siwezi kufanya hivyo nijipe muda kidogo.”

Huyu mama akatazama pembeni akisema “dokta huyo najua, ni yeye.”
Nilitabasamu na kusema “ni sawa mama, ila ukipona utakula sana.”

Huyu mama hakuwa na furaha tena niliona hilo kwa uso wake. Wakati sasa ndiyo naanza tu nimpunguze nguo, Dokta alifika. Nikasikia mama huyu na sauti yake ya upole akisema “Nazwi unaweza kutoka mara moja.”

Nilitabasamu tu, na hapa nasikia Dokta akisema “kuna nini tena mama yangu?”
Sikusikia alijibiwa nini. Lakini ninachojua nilitoka na kusimama mlangoni. Nikawa nimehakikisha hakuna mtu ameniona nikarudi mlangoni.

Nilisikia huyu mama akisema “wewe ni dokta wangu. Najua kuwa natakiwa kuheshimu kile unachosema. Lakini huna haki ya kunipangia nile nini kutoka wapi. Labd uniambie kuwa nisile kabisa ila sio siruhusiwi kula vitu vya nje.

Maoni

You're not logged in


Tangazo - from bangi to baby fully stories 1 to 21
from bangi to baby fully stories 1 to 21
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NAKUPENDA BILA MIPAKA 26 - 35


:26
Nikacheka na kusema “Muanko ana muda sasa, hacheki na yeyote, yaani tabasamu lake tangu nifike pale sijaliona dada hivi unanielewa.”

Alinitazama akisema “eenh chaupole wangu nipe nipe.”
Nilimtazama na kusema “wewe tena ukishaamua kunijaza. Sasa sikia dada Dee. Kuna huyu wa kuitwa Dokta Kabale. Kwanza dada ananata balaa, dada ana deka muda wote, kujifanya mzungu muda wote, huyu sasa ndiyo naona tatizo, yaani sijui nikuambie nini.”
Alinitazama Dorice akiuliza “ana uzuri?”

Nilitabasamu na kusema “ndugu yangu watu wanaoga, kama kuoga tu watu wanajua. Dada ni mzuri, dada ana ngozi safi, dada anavutia haswa ila sasa anaonekana mkali sana.

Masharti kibao utadhani yeye ndiyo mwenye nyumba,...

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/nakupenda-bila-mipaka-26-35

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle #BeautyBattle #AfricaVsWorld #Tanzania #Kenya #Congo #Rwanda #Burundi #SouthAfrica #USA #VoteNow #DebateTime #Trending <br>

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi nakupenda-bila-mipaka
NAKUPENDA BILA MIPAKA 1 - 12
NAKUPENDA BILA MIPAKA 1 - 12
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

*MY HOT PILOT* (rubani wangu🔥) EP 15.

*MY HOT PILOT* (rubani wangu🔥) EP 15.

342
SHAMIRA 82 MPK  86

SHAMIRA 82 MPK 86

318
SHAMIRA 87 MPK. 91      (SEASON FOUR)

SHAMIRA 87 MPK. 91 (SEASON FOUR)

236
SHAMIRA 79  MPK. 81.    (SEASON 4)

SHAMIRA 79 MPK. 81. (SEASON 4)

209
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 6

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 6

156
ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY 1 ---- 5

ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY 1 ---- 5

150
*BILLIONS OF LOVE💓💓*  "1__5"

*BILLIONS OF LOVE💓💓* "1__5"

149
SHARON 1 mpka 5

SHARON 1 mpka 5

148
NAKUPENDA BILA  13 - 25

NAKUPENDA BILA 13 - 25

125
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 7

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 7

123

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.78K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.49K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.85K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.34K
MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

2.95K
MY WANGU❤️ sehemu ya 108

MY WANGU❤️ sehemu ya 108

2.93K
MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

2.75K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.73K
MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

2.67K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.6K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
NAKUPENDA BILA MIPAKA 26 - 35 Post Mpya
NAKUPENDA BILA MIPAKA 26 - 35
@majario LIVE

:26 Nikacheka na kusema “Muanko ana muda sasa, hacheki na yeyote, yaani tabasamu lake tangu nifike pale sijaliona dada hivi unanielewa.” Alinitazama akisema “eenh chaupole wangu nipe nipe.” Nilimtazama na kusema “wewe tena...

NILIKUTANA NA MAREHEMU MKE WANGU AKIWA KWENYE GARI LA TAJIRI MKUBWA  ​Episode 1 Post Mpya
NILIKUTANA NA MAREHEMU MKE WANGU AKIWA KWENYE GARI LA TAJIRI MKUBWA ​Episode 1
@majario LIVE

​Mvua ya rasha rasha ilikuwa ikidondoka jijini Dar es Salaam, ikichanganyika na moshi wa magari na kelele za wapita njia. Nilikuwa nimesimama kando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, nikisubiri...

BILLIONS OF LOVE💓💓   SEHEMU YA "6"💓😽 Post Mpya
BILLIONS OF LOVE💓💓 SEHEMU YA "6"💓😽
@majario LIVE

"BY BABIE LOVE" Basi bwana kakabaki ka laki na nusu nikasema hatakama kesho sipiki lazima tu niende road nikatafute chakuniinguzia pesa Mnakuja nn 😂😂😂 vitoto vya mskini sisi akili ni...

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 7 Post Mpya
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 7
@majario LIVE

🐓 Mwandishi:lissa mwalla Reyhan kwel ananifanyia mm hiv?niliumia sana huku nikimuangalia ivan anaonfoka zake.reyhan akasema imeisha hio huwez nifanyia mm umalaya ww,unanijua unaskia?sasa uneshakua malaya kweli washkaj malizaneni nae m najikataa.aliongea huku...

NAKUPENDA BILA  13 - 25 Post Mpya
NAKUPENDA BILA 13 - 25
@majario LIVE

MIPAKA:13 “Keti tafadhali.” Nilimtazama, yeye hapo hata hajainua uso wake. Nilimeza mate nikaketi hapo moyoni najisemesha “wenye hela wana ringa jamani kwani si anitazame hata.” Nilipoketi aliniinua uso wake na kunikabidhi karatasi akisema...

SHAMIRA 87 MPK. 91      (SEASON FOUR) Post Mpya
SHAMIRA 87 MPK. 91 (SEASON FOUR)
@majario LIVE

🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀 SHAMIRA Sehemu ya 87 Mwandishi; lissa wa huru media Siku iyo sasa nimeenda kazini. Ile nimefika tu asubuh love akainiita mh nikaogopa nikahisi au nimeharibu sehemu.mana kufika na kufika nimeitwa.nijaenda kisha ...

JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 6 Post Mpya
JOGOO WA KIENYEJI sehemu ya 6
@majario LIVE

🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓 Mwandishi:lissa mwalla Sasa hapo ndio nimekwisha sasa,uwiii,niliogopa nikamsukuma ivan,akasema nani huyo?nikasema ni ticha,akasema ticha wako ndio anakufata mpaka huku?mm nikatoa tu macho,ivan akasema subir hapa,nikasema sawa,akanyanyuka akavaa nguo akatoka mm name...

SHAMIRA 82 MPK  86   Post Mpya
SHAMIRA 82 MPK 86
@majario LIVE

(SEASON FOUR) (HURU MEDIA) 🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀 SHAMIRA Sehemu ya 82 Mwandishi; lissa wa huru media Basi shoga yenu maisha yakaanza dodoma sasa. Nikawa nipo na kiakiba changu ndo kinanisapoti naendesha maisha mdogo mdogo. Apo...

ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY 1 ---- 5 Post Mpya
ISABELA NA WATOTO WA BOSSLADY 1 ---- 5
@majario LIVE

SEHEMU YA KWANZA Ni majira ya jioni ikiwa ni muda mfupi tokea ametoka bafuni kuoga kwa ajiri ya kujiandaa aweze kurudi nyumbani mara baada muda wa kazi kuisha, Isabela akiwa...

SHAMIRA 79  MPK. 81.    (SEASON 4) Post Mpya
SHAMIRA 79 MPK. 81. (SEASON 4)
@majario LIVE

(HURU MEDIA wababe wa hili Game) 🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀🏀 SHAMIRA Sehemu ya 79 Mwandishi; lissa wa huru media Nimawa nagoma kutoka .uku nalia nikawa nasema mama usinizalilishe plsss .yule mama akasema nisikuzalilishe nini...

*MY HOT PILOT* (rubani wangu🔥) EP 15. Post Mpya
*MY HOT PILOT* (rubani wangu🔥) EP 15.
@majario LIVE

Nilikaa na kimimba changu kilimpenda, king Yani akikawia tu kuludi nyumbani najikuta naanza kulia, mpaka majilani nawapa Malala Miko napita Kwa majilani Yani mpaka king aje ndo naakubali kulejea nyumbani,...

*BILLIONS OF LOVE💓💓*  "1__5" Post Mpya
*BILLIONS OF LOVE💓💓* "1__5"
@majario LIVE

SEHEMU YA "1"💓😽 BY BABIE LOVE "Alikuja kama muuza chai kumbe ni Billionea💵" Nyie njooni niwaambie kitu ……… mnazijua chapati? Sambusa je ? 😂😂 nani hazijui halfkeki ? Wote mnazijua ? Ona sikilizeni...

Nargis and Sunil Dutt were not just legendary stars of Hindi cinema, but also one of the most respected and inspiring couples in Bollywood Post Mpya
Nargis and Sunil Dutt were not just legendary stars of Hindi cinema, but also one of the most respected and inspiring couples in Bollywood
@majario LIVE

. Nargis was known for her natural acting and powerful screen presence. Films like Mother India made her a timeless icon, and even today she is remembered as one of...

SHARON 1 mpka 5 Post Mpya
SHARON 1 mpka 5
@majario LIVE

🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺 *SHARON* Sehemu ya 1 Kwa majina naitwa sharon hillary, mm ni mtoto wa 3 kuzaliwa katika familia ya watoto watatu, so mm ni wa mwisho kuzaliwa wa kwanza ni kaka yetu anaitwa...

Mwamuzi wa mchezo wa Esparance dhidi ya Al Ahly,Issa Sy 🇸🇳 Post Mpya
Mwamuzi wa mchezo wa Esparance dhidi ya Al Ahly,Issa Sy 🇸🇳
@majario LIVE

Mara baada ya filimbi ya mwisho akatoa kadi yake nyekundu,anataka kumuona mtu amfuate kuhoji maamuzi yake. Kuna afisa mmoja wa benchi la Al Ahly alitaka kwenda,baada ya kuona kadi nyekundu imeshikwa...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest