SHAMIRA 82 MPK 86
ππππππππππππππππππππππππππππππππ
SHAMIRA
Sehemu ya 82
Mwandishi; lissa wa huru media
Basi shoga yenu maisha yakaanza dodoma sasa. Nikawa nipo na kiakiba changu ndo kinanisapoti naendesha maisha mdogo mdogo. Apo nilikuwa ni mtu wa ndani tu na kwenda dukani mala moja .nikiludi nakuwa ndani kwangu .sikutaka ata mazoea na majirani sana zaidi ya salamu. Na sikuwa nataka mazoe na watu kabisa. Wala sikuwa mtu wa story sana na watu apa. Nilikuwa nawaza sana nafanya nini ambacho kitanibust na aya maisha mimi daaah .mana sielewi kabisa na akiba itaisha tu ni vyema kama nitatafuta kitu cha kufanya jamani.
Basi siku moja nikiwa ndani kwangu sasa .nikamsikia mkaka wa chumba cha pili anaongea na simu. Akiwa ndani kwake.mana pale nilipopanga ni hakuna singboard kwa juuu kwaiyo huwa nasikia sana maongezi yake uyu kaka .mana ndo jirani yangu wa karibu. Na uyu kaka wal sikuwa nimemzoea zaidi ya salamu .na anaonekana ni kijana mstaarabu sana tu. Alikuwa anaongea na simu anasema sawa dada ntajalibu kutafuta ao watu watatu . Tutaongeza hakuna shida . Nikawa namsikia na uyo dada anasema sawa nakutegemea sana pascal jitahidi sana .mimi nakuaminia sana wewe. Kwaiyo naamini pia utaniletea watu waaamini na wastaarabu wanaoweza kuwahudumia wateja vizur .simu yake bila ya shaka aliweka loud kwaiyo nikawa nadikia mazungumzo ya pande zote mbili.
pascal akasema sawa sister kuwa na amani kabisa na wala usijali sister ntakutafutia ao wstu watatu ma kazi wataliga freh .mh nikaona mbona kama deal la kazi hili.na mimi nishakaa dodoma mwezi sasa bado sijpata kazi .nikaona ebu niongee na uyu kaka japo sijamzoea ila atanielewa tu
Basi pascal aliongea sana na yule dada ila nilielewa ni kama kazi ya kuuza duka hivi nikaona wee najifyatua mimi.nikatoka nje kisha nikaenda kumgongea pasacl na katika ile nyumba tulikuwa wapangaji wawili tu ndo tunaishi uwani . Mimi na pascal .ila kwa nyumba kubwa kulikuwa na vyumba vingi na mwenye nyumba hakuwa anaishi apo so wote tulikuwa wapangaji.
Basi pascal akatoka akasema aha jirani vp kuna shida .nikasema ahaa pascal ebu naomba tuongeee kidogo. Akasema ndio nakusikiliza . Nikasema nimekusikia unaongea kuwa utafuta vijana 3 wakafanye kazi. Mimi nahitaji kazi piah. Mh akaniangalia kwanza akasema utaweza kazi yenyewe mana ni supermarket kubwa. So kuzulula na wateja na kuwaonesha bidhaa utaweza mana hakuna kukaa iyo. Nikasema haraka pascal naweza yani naweza kabisa. Akasema sawa mshahara laki 2 na 50 kama utaweza kesho amka mapema. saa 12 uwe umeamka saa 1 tunaenda ni apo mjini centre .kama unaona unaweza ni sawa. Nikasema pascl naweza kuwa na amani kabisa na mimi. Akasema sawa amna shida .
πππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππ
SHAMIRA
Sehemu ya 83
Wassap; 0742443214
Mwandishi; lissa wa huru media
Basi nikaludi chumbani kwangu nikawa na amani.nikaona mh laki 2 na 50 sio ndogo .mimi itanitosha na ntafanya mambo yangu itanisapport tu. Basi kweli kesho yake saa 12 .nikafanya kazi zangu chapu chapu nikajiandaa nikawa nipo tu kwenye godoro langu namngoja pascal.na kweli pascal akanistua .kisha tukaongozana mpka dom mjini.
Jamani ilikuwa bonge ya supermarket ni kubwa kweli kweli.yani floor nzima ya ghorofa na ilikuwa na kila kitu. Yani woow kubwa mno.mh yani mpaka rahaa na kulikuwa kuna wafanyakazi wengi tu kila mtu kasimama kona yake. Nami pascal akanipeleka mpka kwa mdada mmoja mrembo kweli na kapendeza mno .yani yule mdada ukimuangalia tu unajua apa pesa ipo .alikuwa amekaa sehemu ya kupokea pesa na kufanya mahesabu . mimi chapu nikawa nimeelewa kuwa uyu ndio boss sasa.
Badi nikamsalimia vizuri na wala hakuwa mkubwa san yani kama kunipita umri uyu alinipita kidogo sana.ila si unajua tena mwenye pesa sio mwenzio. Basi pascal akasema madame uyu anaitwa shamira ni mpangaji mwenzangu na ni mchapakazi sana nikaona nimlete apa . Ili apige kazi.yule dada akaniangalia kisha akatabasamu akasema shamira karibu sana.na karibu kazini.woow ni kanaongea vizuri alafu anaonekana yupo simple uyu dada wala hana mashauzi. Basi nikamjibi asante madame
Akasema sawa sasa shamira apa sisi tuna sale zetu ntakupa na ntakupa mtu wa kukuelekeza kazi. Na ndo umekuwa ushaanza kazi sawa.naomaba uwe maikini an kazi.na hasa mdomo.naomba uwe na kauri safi na wateja sawa.nikasema sawa.hakuna shida .basi yule madame alinambia yeye anaitwa madame loveness au wengi wamezoea kumuita love.basi bwana madame love akamwambia pascal mpeleke changing room na kweli pascal akanipeleka mie nikaongia kwa wanawake yeye akaingia kwa wanaume.kule nikakutana na mdada hivi .akanambia nimepokea simu yako kwa boss wewe sindo shamira nikasema ndio akanmbia sawa chagua t shirt linalokutosha apo.basi nikaangalia nikaona nikavaaaa.
Akanmbia aya nifate sasa. Basi nikamfata nikaingia dukani sasa. Akanipeleka kwa mdada mmoja akamwambia bos kasema uwe beneti na uyu binti ni mfanyakazi mpya anaitwa shamira so umsaidie na kumuonesha majukumi yenu na manafanyaje kazi .akasema sawa kisha yule madame akaondoka na yule dada akajitambulisha kwangu anaitwa mile .nikasema saawa na mimi kama nikamwambia naitwa shamira akanambia sawa.
πππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππ
SHAMIRA
Sehemu ya 84
Wassap; 0742443214
Mwandishi; lissa wa huru media
basi bwana wateja wakawa wanakuja.na wateja walikuwa wengi mana hii sehemu ilikuwa center kabisa. Kazi wala haikuwa ngumu kabisa .ni kimsikiliza mteja kwa anachokitaka na kumpeleka pale asipoina bidhaa asiyoitaka. Na kumsaidia kumbebea bidhaa zake .hatukuwa tunapokeaa pesa kabisa. Na pesa zote anapokea mwenyewe madame love. Sisi kazi zetu mdo hizo tu .kulipia anaenda kwa madame love
Na ata pascal alikuwa nafanaya kazi apa. Ila yeye nilikuwa naona ni kubeba mizigo ya wateja kuwapeleke kwenye usafiri. Basi bwana siku ya kwanza nilipata ugumu kidogo mana sikuwa nimezoea kazi kabisa. Na pilika pilika zilikuwa nyingi mno.ila baada ya week 2 nilizoea kazi kabisa .na nilikuwa naenda na pascal kila siku kazini.aseee pascal ni kijna mwenye adabu sana yani alikuwa ananichukulia kama dada yake .ni kijana mwenye heshima sana mnikaona uyu katulia sana na ndo mana madame love anamuamini anamwambia mpka amtafutie wafanyakazi
Basi bwana maisha mdogo mdogo yakawa yanasogea kama masihara. Mshahara wangu wa kwanza nilivyopata nikanunua na kitanda changu ili kujishikizia . Na nikawa naendelea na kazi vizuri mno japo wateja wengine changamoto maraya maraya sana yani mpka wanakwaza kiukweli. Mtu unamsikiliza ili umuhudumie anaanza kukutongoza.basi tunamalizana nao kikubwa .mana ukijibu vibaya kazi huna. Madame love hakuwa anataka masihara ata kidogo na wateja wake. Kwake mteja ni zaidi ya mfalme uwa anasma hivyo
Basi bwana nikawa naendelea kuongea sana na shoga yangu husna . Na tulikuwa tunapuga sana story na alikuwa akinitia moyo kuwa nipambane tu mungu atanifanyia wepesi na maisha yataenda inshalla. Sassa iyo siku madame love akaniita akanambia shamira ebu kaniletaa choclate 5 kule . Hizo choclate alizoniagiza moja inauzwa elfu 5. Mimi wala sikutaka kuuluza nikaenada kumchukulia nikampelekea. Akasema mh bola leo niziweke mapema nikampelkee aunt yangu mana nasahaaugi inakuwaga moto analia mno. Nikasema ahaaa ni mtoto wa nani yako kwani madame.akasema ni mwanangu mtoto wa kak yangu.yani mpka kinaoza meno kwa kupenda hizi choclate .ila kinapenda balaa nakuwaga nambebea tu japo baba yake hataki .ila nafanyaje sasa na mwenyewe anapenda. Namvutaga chumbani kwangu nampa meno yakioza yote ndo kitaelewa.aseee nilicheka tu kisha nikakumbuka mbali sana.nikasema kama mtoto wangu angekuwwepo kwa sasa angekuwa na miaka 4 mpka mitano kasoro daahπππππ
πππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππ
SHAMIRA
Sehemu ya 85
Wassap; 0742443214
Mwandishi; lissa wa huru media
Basi bwana nikasema anaonekana mtundu aunt yako.love akacheka akasema sana yani mtundu mno alafu anaongea sana yani ana maswali kama mtu mzima mpka namkimbiaga mda mwengine.nikacheka tu .nikajikuta na hamu ya kutaka kusikia story za uyu mtoto zinakuja. Na alafu uyu boss wetu mzungu ni yupo fair sana. Labda umkwaze sana na asa ugombane na mtaja ndo ata kuzingua.ila hana shida wala.nimkamuuliza anaitwa nani akasema anaitwa gift. Ni kamalkia chetu bwana kasumbufu kweli kweli yani sana anapilika pilika mno. Nikacheka tu nikasema sawa siku uje nae nimuone basi. Akasema weee unazani kutakalika apa. Baba ake alikuwa anamleta nyuma uko anakuwa nanalikia kila kitu. Sasa si shida oyo .nikawa nacheka tu.akasema na ana fujo mno gift weee ana kelele. Yani balaaaa ila kana upendo sana japo kadogo. Akikuona kama haupo saww anakuja anakukumbatia namshaangaaga yule mtoto kama mtu mzima vile.nikacheka tu
Akanmbia alafu unajua nini shamira kuna jinsi naona umefanana sna na binti yangu. Nikacheka nikasema uyo gift akasema ndio yani watu wawili wawili. Ni vile nimebadili simu ningekuonesha picha zake.siku nikimpiga ntakuonesha umuone mrembo wangu.nikacheka tu kisha nikasem sawa madame.kisha nikaludi kuendelea na kazi zangu. Kiukweli kwa uo mda sikupanga kabisa kujiingiza katika mahusiano ya mapenzi mimi.nilikuwa natongozwa sana ila nilishaona wanaume hawana deal lazima nijitambue bila ya hivyo ntazalilishwa sana mimiπππππππππππ
Basi bwana ikakata miezi 3 .nipo dodoma nafanya maisha yangu.mshahara wangu ulitosha sana kufanya mambo yangu. Alafu nilipata sana bahati uyu love alikuwa ananipenda sana. Kuna mda ata ananipa mikate sijuh masoda ananipa tu. Ananambia nimekupa sababu unafanana na mwanangu .nakuwa nacheka yu na kupokea . Yani damu zetu ziliendana sana.ata nikichelewa kazini hafoki sana kama anavyowafokea wafanyakazi wemgine.basi bwana siku iyo nipo busy kweli kweli na kazi zangu. Akaingia mkaka handsome mno jamni anawaka vibya sana kapiga pensi tu na t shirt ya blue. Ila amekaa kitajiri alafu kaingia tu mimi nilikuwa mbali nae ila nilikuwa nasikia harufu ya pafyumu yake daaha ananukia mno
πππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππππ
SHAMIRA
Sehemu ya 86
Wassap;0742443214
lissa wa huru media
Ila nikaona kaenda moja kwa moja kwa love.na nikWa naona wanaongea sana uku love akicheka. Yani kama yule kaka alikuwa anamuhadithi kitu love. Nikahisi huenda ni mwanaume wake .nikiwa busy na kazi. Masdame love akaniita niende pale. Nikasogea mpaka pale .nikamsalimia yule kaka . Akaningalia kisha akaniitikia ila hakunichangamkia sana.aliitikia ile kawaida tu. Ahaa watu wenye vipesa vyao wanalingaga kama hawanyi vile khaaaaaπ π π π π π π π π π π π π π π π π
Love akasema sasa shamir kaniletee zile biskuti 5 .si unaona gift leo kamsumbua baba yake .yupo shule analia uko hatki kusoma mpka aletewe biskuti khaaaa ndo kaja kumfatia baba yake apa .akampeleekee shule aache kulia asome.nikacheka tu mana uyo mtoto wao anaomekana ana visa sana. Nikasema sawa madame nkaenda mubeba biscut nikamletea mpka palw.na Nikampa zile biskuti uyu kaka sasa. Apo ndo aliniangalia nilishanga kaganda anainagalia mno.mh mpka nikashangaa au aliona picha zangu napigwwa uchi kipindi kile mbona kaningalia sana. Yile kaka akaniuliza unaitwa nani.nikasema shamira .akasema ooh wewe dodoma ni mgeni .nikasema ndio .akaniuliza umetokea wapi nikasema arusha.nilidanganya akasema sawa umefanana kidogo ma binti yangu.nikacheka tu nikasema madame love aliwah kunambia pia. Love akasema ni kweli broo ata mimi niliwahi kumwambia hivyo si unajua watu wawili wawili duniani .nikajua aahaa kumbe uyu sio bwana ake ila kaka yake
Basi broo wake akasema powa kisha akatoka nje. Uo mkoko alopark apo nje mh sio powa watu wana pesa jamani khaa. Basi love akanmbia yani gift anajua kimpelekesha baba yake anamsumbua mno. Na kaka anampemda sana yule mtoto yani kuna mda mpka mimi ndo namwambia anmlea vibaya yani mtoto anamtuma baba yake. Badala ya baba kumtuma mtoto et ana muona mdogo mtotl anakalibia miaka 5 ni mdogo shamira? Nikasema hapana ni mkubwa tu akasema basi kaka yangu mie anamuona mdogo kweli kweli . Kumbe ana kialibu. Nikacheka nikasema mapenzi yamemjaa sana kwa mtoto ndo mana.akasema yaa ni kweli lakini.nikasema au anaye uyo uyo. Akasema ndio ndo uyo uyo basi anamlea kama jicho.nikawa nacheka tu. Kisha nikaenda kuemdelea na kazi zangu
Basi bwana maisha yakawa yanenda ila nilikuwa namuona sana yule kaka yake na love anakuja sana dukani kwa dada yake.na kuna mda usiku tukishafunga tukiwa tunaondoka tunaona gari yake amekuja kunchukua dada yake. Niliona ni ndugu wanaopendana sana.nikawa nasikia awa wafanya kazi wenzangu wana sema yule kaka ana pesa mno ni hakimu mkubwa sana apa tanzania . Na ata ile super market ni yake .sikuwa nayafatilia san mana ayanihusu mimi muhimu naenda kazini nipiga kazi nalipwa basi maisha yanaenda
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni