Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

MKASA: NILIWEKA LIMBWATA KWENYE CHAKULA CHA MUME WANGU, ILA KWA BAHATI MBAYA CHAKULA AKAKILA BABA YAKE SEHEMU YA 02

1st Jul, 2025 Views 63


Rayuni alisimama mlangoni akiwa kama sanamu. Mikono yake ilitetemeka, mdomo wake ulikuwa wazi kama anataka kupiga kelele lakini sauti ikamkataa. Macho yake yalishikilia sura ya mzee anayemwita baba mkwe—mtu ambaye sasa alikuwa anakula chakula alichowekewa limbwata.
“Ee Mungu! Hii ni nini sasa?” alijisemea kwa sauti ya ndani huku moyo ukipiga mbio kama anayeandaliwa kuchinjwa. Alitamani akimbie, apokonye chakula hicho kutoka mikononi mwa mzee, lakini mwili wake haukumtii.
Mara Aga alitoka jikoni akiwa na sahani nyingine mkononi, akaketi karibu na baba yake na kuanza kula. Wote wawili walionekana kufurahia chakula kile—kama vile hawajawahi kupata kitamu kama hicho.
Rayuni hakusubiri kuonekana. Alichepuka kimya kimya kama paka, akakimbilia chumbani huku macho yakiwa yamejaa hofu, aibu, na maswali mazito yasiyo na majibu.
Alijilaza kitandani lakini usingizi ulikuwa mbali naye. Macho yake yaliangalia dari la chumba kama yanatafuta msaada kutoka juu. Sauti ya mzee na Aga ziliendelea kusikika sebuleni wakiongea na kucheka.
Aga alienda kuandaa chumba kwa ajili ya baba yake, sawa pengine mkewe angepaswa kufanya hivyo lakini hakuona haja ya kumsumbua akijua amelala, akatandika shuka safi chumba cha wageni kisha akamuambia baba yake akalale
Baada ya ya hapo, Aga alikuja chumbani, akidhani kuwa mkewe tayari kalala. Alijilaza pembeni, akavuta shuka, na ndani ya dakika chache, alisikia pumzi ya mkewe ikiwa nzito, akahisi analala. Lakini hakujua... Rayuni hakuwa amelala.
________________________________________
Asubuhi ilipofika, Aga aliamka mapema kama kawaida yake. Aliangalia saa ya mkononi na kugundua amechukua muda mwingi, hivyo alifunga viatu haraka, akasogea mlangoni mwa chumba cha baba yake, akamsalimu kisha akamuaga na kuahidi atarudi mapema waje wafanye mipango iliyomleta mjini. Kisha akatoka kwenda kazini.
Rayuni naye aliamka, lakini hakuwa yule mwanamke wa jana. Alionekana amechanganyikiwa, mwenye uso wa wasiwasi na moyo mzito. Akaenda jikoni kuandaa chai, huku mikono ikitetemeka kila alipogusa kikombe au kijiko. Kisha akaanza usafi wa kawaida, akipiga deki sebuleni kwa kuchoka.
Alipokuwa ameegemea chini akisugua kona ya ukuta kwa kitambaa, ghafla alihisi kiuno chake kimedakwa kwa nguvu za kiume. Alishtuka sana! Alinyanyuka haraka, moyo ukidunda kwa kasi, akageuka na kukutana uso kwa uso na baba mkwe—mzee aliyevaa kaptula, akiwa ametabasamu kwa utulivu usiokuwa wa kawaida.
“Baba... shikamoo!” Rayuni alisema kwa sauti ya hofu, akijinyoosha na kujaribu kumuepuka mzee huyo.
Lakini mzee huyo alicheka kisha akasema, “Shikamoo ya nini sasa? Au unaninyima zawadi? Hivi unajua wewe ni mzuri ajabu? Wanangu wana bahati sana…”
Rayuni alijikuta amekosa cha kusema. Akanyamaza. Machozi yakaanza kujikusanya kwa haraka machoni mwake.
Baba aliinua mkono wake na kumpapasa shavuni kwa upole lakini kwa hisia nyingi, “Mwanangu amepata chombo, anaenjoy sana. Na mimi natamani nife na radha hiyo hiyo… hata kidogo tu.”
Rayuni alijikuta anatetemeka. Akasema kwa sauti ya chini, “Ee Mungu nisaidie…” kisha akakimbilia chumbani na kujifungia ndani.
Hakujua afanye nini. Alikuwa na hofu ya kufichuka siri yake, aibu ya kumsaliti mume wake, na fedheha ya kuwa katika hali ya aibu kiasi kile na baba mkwe.
Dakika chache baadaye, mzee huyo alijitokeza mbele ya mlango wa chumba akiwa anashikilia bahasha.
“Rayuni... mpenzi, shika hii laki tano tu. Sitaki kingine... hata tukumbatiane tu… tafadhali!” Alizungumza kwa sauti ya huzuni na macho yalijaa machozi, lakini pia tamaa.
Rayuni aliinama chini, alishindwa kuvumilia. Akachukua simu yake na kumpigia Ashura.
“Ashura... limbwata limeenda kwa baba mkwe wangu! Ameanza kunitamani! Ananipa hela! Na sijui nifanye nini!” aliropoka kwa sauti ya kukata tamaa.
Ashura alishtuka lakini hakukosa jibu, “Ni lazima turudi kwa mzee Kijivu! Tuone kama anaweza kuondoa madhara!”
Rayuni alisema kwa huzuni, “Sina hata nauli... sina hela kabisa!”
Ashura alikuna kichwa, kisha akajibu kwa sauti ya haraka, “Basi chukua hiyo laki tano. Mkumbatie tu kama alivyoomba... halafu twende moja kwa moja kwa mganga kabla hajazidi kuchanganyikiwa!”
Rayuni alikaa kimya kwa sekunde chache. Macho yakimwagika. Kisha kwa mkono mzito akafungua mlango. Baba mkwe alikuwa bado amesimama, machozi usoni, na bahasha mkononi.
Rayuni alikumbatia baba mkwe kwa nguvu za kujilazimisha. Baba aliinua uso wake, akambusu kwa huba, na kwa haraka akaanza kumnyonya denda kwa pupa huku akisema, “Nitakupa unachotaka. Nitakununulia hata gari. Mradi uwe wangu…”
Rayuni aliweka mkono kwenye mdomo wake kumzuia zaidi. Akachukua bahasha ya hela. Kwa haraka akaingia ndani, akavaa nguo zake vizuri, kisha alimpigia Ashura wakapanga safari.
________________________________________
Baada ya saa moja walikuwa njiani kuelekea Vikindu. Mioyo yao ikiwa na matumaini kuwa mganga atarekebisha limbwata ile iliyokosea mlengwa.
Lakini walipofika... walikuta kilinge kimeteketezwa, miti iliyokuwa imepambwa kwa hirizi ilikuwa imeangushwa, na kibanda hakikuwapo tena.
Waliposogea kwa majirani na kuuliza, waliambiwa,
“Mzee Kijivu? Hah! Alitangaza jana kuwa ameokoka. Amesalimisha kila kitu, ameanza kumtumikia Yesu. Hasa baada ya ndoto ya ajabu aliyoiita ya maono.”
Rayuni alitetemeka kwa mshtuko. Akashika kichwa kwa mikono yote miwili.
“Yaani... nimerogwa na sasa sina msaada?”
________________________________________
ITAENDELEA...
Je, Rayuni atafanya nini sasa baada ya mganga kuokoka? Baba mkwe ataishia hapo au atazidi kuchanganyikiwa kwa limbwata? Je, penzi la ndoa litavunjika? Fuatilia sehemu ya tatu ya simulizi hii kali!
KWETU morogoro __.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MKASA: NILIWEKA LIMBWATA KWENYE CHAKULA CHA MUME WANGU, ILA KWA BAHATI MBAYA CHAKULA AKAKILA BABA YAKE SEHEMU YA 02  >>> https://gonga94.com/semajambo/mkasa-niliweka-limbwata-kwenye-chakula-cha-mume-wangu-ila-kwa-bahati-mbaya-chakula-akakila-baba-yake
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

GIGY MONEY DAH😭

majario rewards 100 Comments 0
 

YOUNG AFRICANS,

majario rewards 100 Comments 0
 

BAKORA VILLAGE

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 7...8

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA EPISODE 2

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE...5...6

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 3...4

majario rewards 100 Comments 0
 

HUYU KAKA 1

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈21

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈20

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 8

majario rewards 100 Comments 0
 

DADA WA KAZI EPISODE 7

majario rewards 100 Comments 0
 

Life in a Year (2020)

majario rewards 100 Comments 0
 

Kenya, Tanzania, Congo

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 40

majario rewards 100 Comments 0
 

POSHY QUEEN:

majario rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 39

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈19

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈18

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈17

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH 💋🙈16

majario rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈15

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 05 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 04 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 03 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 02 ❤❤.

majario rewards 100 Comments 0
 

HAIZIMI 01 ❤❤.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NIPE YOTE DADY 34

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈14

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DAAAAAAAH💋🙈10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

TUWASHUKURU KINA BABA

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest