MY CRAZY BOSS 10
ENDELEA
Nilirejea ndani huku nikiwa na bashasha ya kuangalia ni nguo za aina gani zilizopo ndani ya mfuko huo
"Khaa!!! Kumbe sina taa jamani , hata siwezi kuona ni za rangi gani, acha tu nilale pakikucha nitaziangalia na vile kesho ni weekend itakuwa poa sana, nilizungumza, kisha nikaweka mfuko pembeni na kulala."
Asubuhi iliwadia kama kawaida ya uswazi saa kumi na moja asubuhi huku ni saa sita mchana, nilijiamkia zangu nikafagai fagia😁chumba chenyewe cha kufagia nnacho sasa🙌🙌ni huzuni kweli.
"Mama ashrafu shikamoo".
"Mqrhaba ". Mbona wanikodolea macho ?? Sema kilichokuleta na kama ushalitibua huko utajua weye mie hata vyombo huvigusi leo.
😁😁Kheee we mama wewe!!!! Alokwambia ninekuja kuosha vyombo nani?? Kwanza sio shida zangu , em nipe mapupu mie na chapati.
Halooo👌👌kweli watu mmepanda hadhi hehehe hya panua miguu panuu nikuwekee supu ujinywee.
Sikujali wala nini , uswazi ndo nilipokulia maneno nimeyazoea, nilijinywea supu halafu huyo nikarudi zangu geto , tumbo ndi.
Halafu nimekumbuka kwanza🙌🙌em ngoja nijaribu hizi nguo kabla usiku hujaingia , mie sasa🥰🥰japo kioo sina lakini sikuacha kujisifia, japo hazikuwa nyingii za kushangaz ni kagauñi na viblauzi viwili ila si haba vilinitoa.
Nikiwa sina hili wala lile simu yangu ilianza kuita, niliiangalia kwa mbali ndipo nilipogundua ni boss aliyekuwa akipiga.
Haraka niliipokea .
"Haloo boss".
"Yes joy upo powa."
Nipo powa kabisa boss. Nilijibu.
Oooh okay samahani kwa kukusumbua najua ni weekend , nilikua naomba tukutane leo usiku kuna mambo nahitaji kuyaweka sawa kwako, boss alizungumza.
Nilikaa kimya na kuwaza kwa muda mfupi , akili yangu iliwaza nini boss angehitaji kuniambia
"Ni sawa,haina shida. Nilijibu.
Asante sana Joy , nitakupitia Saa mbili usiku naomba ujiandae.
" Sawa . "Niliitika misha nikakata simu
" Hivi boss anataka kuongea nini na mimi leo?? Mmmmh sijui ni kwanini huu moyo unaenda mbio ? Mmmh joy wewe embu sanuka🤣sijui nna nini mimi au mnahisi nna nini??
Masaa yalizidi kwenda hatimae saa mbili iliwadia, nikiwa nimevalia gauni jipya jeusi nililoletewa na boss pamoja na raba nyeupe, kwa muda huo nikiwa nimekaa juu ya kitanda akili na macho yote yakiwa simuni, ni wazi nilikuwa nikisubiri simu ya boss Erick. Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu natolewa out ukiachilie zile mbwa ex outing za vichochoroni hii inaonekana ya bei kali😜😜
"We joy wewe!!!! Joy!!!!!!" Nilisikia nikiitwa.
Nini tena mama ashrafu usikuu huu vipi???
"We acha tu mwenzangu , nna ubuyu hadi roho yataka kutoka".
Khe !!!mama ashrafu wewe ubuyu gani huo?? Ebu nipashe.
" Si yule bwana anaekufataga , kaja yupo hapo nnje leo kawanunulia chakula watu wote hapo nnje na mie kanipa afu hamsini, eti kasema niishi vizuri na weye".Shoga usiliache danga lile danga haswa🙌🙌🙌we shoga angu wa maana nakupenda mwaa😘😘
" Makubwa haya , leo hii mama ashrafu unanipenda mie? Sio wewe ulonfukuza juzi sijui jana?? Anyway tuachane na hayo acha niwahi".Niliongea hayo huku nikitoka nnje
Baada ya muda nilifika hadi alipopaki gari boss.
" Umependeza sana Joy".
" Asante boss🤣huku nikichekacheka mwenyewe".
" Ingia twende mrembo".
Boss alizungumza.
" Asante boss"
Basi safari ilifana , hadi nnje ya hoteli kubwa ya kifahari ipo huko masaki, jina silijui nahisi ni la kichina lile kama sio la kijapani.
Kwa mara ya kwanza boss alinishika mkono kisha tukaelekea hadi hotelini humo.
🙌🙌🙌Nyie nilijihisi kama nipo Shangai China huko🤣🤣.Baada ya kukodoa kodoa na ushanba wangu , muhudumu alikuja sikuelewa hata nini alionhea na boss zaidi ya kusikia " Shishoshungu shwi shwa shwo".Si mnajua kichina tena.
Haikuchukua muda mrefu, chakula kililetwa, jamani🙌🙌tambi si tambi na mimaji maji , na bakuli lenye mchuzi mwekundu na kijiko🤣
Nikabaki nakodoa😳😳😳kheee nini hiii ??? Anhaaa buanaa sitaki kuonekana mshamba miee acha nijikaze🤣🤣
Nikavuta bakuli la mchuzi waaah nikamix na tambi nikajiweka sawa mtoto wa kike na kuanza kula😁😁.
"Kho khokho khokho". Pilipili si pili pili jamani🙌🙌na ushamba wangu nilidhani ni mchuzi kumbe ni pilipili acha nianze kukohoa kama mwizi .
"Upo sawa Joyce?? Boss aliuliza
Nipo sawa tu, Nilijibu huku nikishushia maji macho mekundu jamani ushamba huu🙌🙌🙌
Basi tukamaliza kula pale mie nipo hoi tumbo lipo moto sana jamani🙌.
" Joy kuna jambo nahitaji kukwambia naomba unisikilize".Boss alizungumza.
" Ni sawa, nakuskiliza boss".Nilijibu.
" Nimetokea kuvutiwa sana na wewe Joyce, ukubwa wa masikio yako kama ungo, rangi nyeusi ya mdomo wako, pamoja na udogo wa miguu yako imenivutia sana Joyce".Boss alizungumza.
😁😁😁Kheee🙌🙌🙌jamani mbona sikuelewi unachokiongeleaa, ko umeniita hapa kunitusi sio?.
" Hapana Joyce, nachomaanisha nakupenda sana,nimevutiwa na wewe kwa muda mfupi tu, si wewe tu bali na kila kiungo cha mwili wako nimevutiwa nacho".
" Upo sawa kweli boss Erick? Nahisi haupo sawa em ngoja nikakutafutie dawa, pharmacy bado zipo wazi niliongea huku nikinyanyuka kuelekea nnje".
Gafla nilishikwa mkono na kuvutwa, kwa kasi iliyonifanya nifunge macho kwa uoga😔.
Midomo ya boss iligusana na yangu pumzi yake niliisikiaa
" Nakupenda sana Joyce usinifanyie hivyo tafadhali, boss alizungumza".
" Nakupenda pia ni muda tu,nilijibu."
" Unasema kweli??".Eti Joyce ??
Hapo ndipo nikashtuka na kujitoa kwenye mikono ya boss" hivi nimesema nini mimi lakini??"ila mbona kama sijutii nilichokisema kabisa??
Itaendelea
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni