VYOTE NDANI GONGA94
MZUNGU TULIA MOYO HAUNA RANGI SEHEMU YA 4
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
"Fredy, nini kuvutana bana!" Sada aliongea kwa maumivu mkononi...
"Sada, nisikilize: tabia ya kumpiga Kasie bila kosa lolote acha! Kuna siku utakuja umpige upate balaa!" Fredy alilalamika...
"Khaaaa! ๐ Nicheke ninenepe mie! Kwanza huyo Kasie nimpige mimi wa umri wangu huu? Halafu tena, kama ningempiga wala asingesema lakini hajapigwa analeta shobo," Sada aliongea akiwa anautikisa mwili wake.
"Shenzi (Fredy alimtwika kibao da Sada), pumbavu wewe! Nisikilize: nikirudia kusikia umempiga Kesie utaujua undani wangu upoje," Fredy aligeuka akitaka kuondoka... Lakini na mimi nilimuwahi nikamuweka mtama kama alivyomuweka da Sada.
"Ukome kabisa! Da Sada, twende ndani!" nilimshika mkono da Sada tukaingia ndani.
"Kaka! Amekupiga ๐ณ! Usikubali kaka," Kasie alisema huku akitaka kunifuata... Hapo nikamsukumiza da Sada ndani, kisha mimi nikasimama mlangoni.
"Unasemaje sasa! Sogea nikuchavue huo uso! Na kwavile umejichubua basi ndio hutokaa upone kenge wa njano! Ebu sogea uone!" nilisema nikiwa tayari kwa vita.
"Kasie, tuondoke!" Fredy aliongea huku akimvuta mdogo wake... Alikuwa akinitazama... Nadhani ni kwasababu hakuamini kuwa ningefanya kama nilichokifanya.
Niliingia ndani nakuta Sada kavuta mdomo... Nikakaa nae ili kujua shida...
"Da Sada, usiwe hivo nishalimaliza bana," nilisema kumgeukia Sada...
"Hivi Love: umepata aje ujasiri wa kumpiga Fredy? Yani uhhh
unawezaje kumpiga?" da sada alifoka sana
"Dada, nisingejizuia kuona anakudhalilisha mbele ya hiko kitoto bana!" nilisema nikiwa na hasira.
"Ugomvi wetu tuachie wenyewe!" da Sada alisema kisha akajitupa kitandani na kulala.
Asubuhi tuliona gari mlangoni wakati tunataka kwenda kazini. Mi nilijua tu huyu ni boss bana. Haya nikaona bora nichukuwe bajaji. Da Sada hakunielewa, ila nilimvuta kwenye tax tukaanza mwendo sasa. Alikuwa akitaka kuongea, ila mi niliona gari likianza kutufuata sasa nadhani alikuwa na maswali mengi: leo taxi mimi Love mmh maajabu.
To be continued......๐ฅ
Umesoma kwa utulivu ยท dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi mzungu-tulia-moyo-hauna-rangi-sehemu-ya