NAKUPENDA BILA MIPAKA 96 - 100 MWISHO SEASON TWO
:96
Yeye akawa tu anaendesha kama vile hakuna kitu amezungumza. Mimi hapo tena naona tu kesho ifike tu nipelekwe tu hiyo sehemu.
Sijui hata ni kuchinjwa au nikutekwa mimi tayari tu nipo tayari kwa lolote hata sielewi. Alinifikisha, mpaka nyumbani, nyumba ile pale, mimi huyu hapa.Nilimtazama na kusema “asante sana, nashukuru.”
Alisema kwa upole “kwenu pazuri, kumechangamka sana.”
Nilitabasamu na kusema “karibu sana.”
Sasa hapo nje naona mama na mjukuu wake kwa mbali unajua eenh, akaniuliza “yule ni mama yako?”
Nilimtazama na kusema “ndiyo, na yule mtoto ni binti yangu.”
Akawa ana bonyeza simu, baada ya muda nikasikia “mpe mama.”
Nikasikia mama akisema “eenh mwanangu, umemfikisha mpaka nyumbani?”
Mr Gallen alinitazama na nikajikuta nacheka kidogo halafu ndiyo akajibu “ndiyo tajiri, naweza kurudi sasa.”
Mama alisema “hapo sawa, bado yupo ameondoka.”
Akajibu “ameshashuka mama.”
Nilitabasamu, mama akasema “ni sawa mwanangu, ni sawa ila nitamuuliza kama amefikishwa mpaka nyumbani.”
Gallen alicheka akisema “hakuna shida tajiri, dereva nishamaliza kazi nasubiri malipo yangu.”
Mama alicheka kisha Gallen akakata simu akisema “si umesikia, ulitaka unipe kesi bure. Unaweza kwenda sasa.”
Basi natamani abaki tu, mlango wenyewe wa gari nafungua haufunguki, akanisaidia ushamba wangu tena ila sasa nitafanyaje. Vile ndiyo nashuka akaniambia “Napenda tabasamu lako, una tabasamu zuri sana.”
Sijui kama sijafanya kwa raha leo, nikazidi kutabasamu tena kwa furaha kubwa sana. Basi niliposhuka, nilianza kuelekea nyumbani, yeye bado hajaondoka bila shaka alikuwa ananitazama.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:97
Basi na mimi tena na mwanangu, kisha nikaenda kukaa alipokaa mama. Ndiyo nikaona gari ile inaondoka. Mama wala hakuuliza kitu, pengine hakujua mimi ndiyo nimeshuka pale pengine au ndiyo ana mambo yake.
Akaniuliza “leo umechelewa mwanangu kwema lakini?”
Vile nilivyo na raha kama nimsimulie mama ila ndiyo siwezi, nikamjibu mama yangu “nipo salama kabisa mama.”
Akanitazama, halafu akasema “unanukia vizuri leo, halafu hilo tabasamu sijaliona zamani sana, vipi una nini leo?”
Nilicheka tu nikisema “mpelelezi kazini mama jamani, nimefurahi tu.”
Mama alicheka akisema “nafurahi kuona una furaha mwanangu mzuri. Haya karibu nyumbani. Halafu mwenzako yupo chumbani kwako, hana hata raha.Hataki kuzungumza nimemuacha tu apumzike.”
Nikawa nashangaa na kuuliza “una maanisha nini mama?”
Mama akaniambia “Dorice, lakini nishamwambia mama yake kuwa Dee yupo huku.”
Nilishusha pumzi na kusema “wacha nikamuone au kagombana na shem huyu.”
Mama akacheka akisema “mambo yenu sasa.”
Basi nikacheka na mwanangu pale, ile namshusha niingie ndani namuona kaka Baraka huyo anarudi, kaka Baraka amenyoa, amenyoa nywele zake zilizokuwa zimesokotana.
Amependeza sana. Nilishangaa, huyu sasa naona ndiyo amekutana na Mungu. Ni kama vile familia yangu imetembelewa na Mungi. Furaha kwa nyumba, mimi nashangaa mama hadi alisimama. Nilishuhudia mama akiita “Baraka!!!”
Kaka Baraka kwa maumivu aliitikia “mamaaa!!”
Jamani walikumbatiana kwa furaha sana. Kaka alikuwa akilia hata na mimi nataka kulia akisema “mama nisamehe kwa machozi niliyowahi sababisha ulie.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:98
nakuahidi mama, hutowahi kulia juu yangu, hutowahi kulia sababu nikawa ni mimi. Nitahakikisha nakufurahisha. Nakupenda mama.”
Mama yangu alilia akimshukuru Mungu, nikaona huu wakati usinipite. Sisi wote tulikumbatiana. Hata safari mimi ya kwenda kwa Dee iliisha. Tulikaa hapa, tunahamu ya kujua muujiza uliotokea. Nakumbuka saana.
Alinitazama na kusema “dada unakumbuka nilikwambia nimekutana na mtu anamuhubiri Mungu mtaani. Usiku wa jana sijalala, nilikuwa nasoma Biblia na kutafakari sana.”
Mama akauliza “Biblia?”
Kaka Baraka akajibu “ndiyo mama, ni ya dada. Wakati nasoma nilikutana na kifungu ambacho nikatamani nisome tena na tena. Nilitafuta kalamu na karatasi nikaiandika maana ni ndefu na sikuwa naweza kuweka kichwani. Akaanza kujikagua mfukoni halafu akatoa, na kusoma “Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami.
Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie.
Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.
Waaibishwe, wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya.
Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini.
Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa Bwana akiwafuatia.
Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.
Uharibifu na umpate kwa ghafula, Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe; Kwa uharibifu aanguke ndani yake.
Na nafsi yangu itamfurahia Bwana, Na kuushangilia wokovu wake.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:99
Mifupa yangu yote itasema, Bwana, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini na mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
Mashahidi wa udhalimu wanasimama, Wananiuliza mambo nisiyoyajua.
Wananilipa mabaya badala ya mema, Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa.
Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia.
Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.
Nalijifanya kama kwamba ni rafiki au ndugu yangu, Naliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.
Lakini nikijikwaa hufurahi na kukusanyana, Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua, Wananipapura wala hawakomi.
Kama wenye mzaha wakikufuru karamuni Wananisagia meno.
Bwana, hata lini utatazama? Uiokoe nafsi yangu na maharabu yao, Na mpenzi wangu na wana-simba.
Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi.
Walio adui zangu bure wasinisimange, Wanaonichukia bila sababu wasining’ong’e.
Maana hawasemi maneno ya amani, Na juu ya watulivu wa nchi huwaza hila.
Nao wananifumbulia vinywa vyao, Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona.
Wewe, Bwana, umeona, usinyamaze; Ee Bwana, usiwe mbali nami.
Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu.
Unihukumu kwa haki yako, Ee Bwana, Mungu wangu, Wala wasinisimangize.
Wasiseme moyoni, Haya! Ndivyo tutakavyo; Wasiseme, Tumemmeza.
Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu.
Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe Bwana, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.
Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa.
NAKUPENDA BILA MIPAKA:100
Kila nikisoma nikawa naona kama mimi nipo kwenye vifungo, nikawa narudia tena na tena. Lakini nikaendelea, nikakutana tena na kifungu ambacho kinanirudisha tena hukohuko Isaya 49:25 namna nilikuwa naisoma nikaiweka kichwani “Naam, BWANA asema hivi, Hata mateka wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka wake aliye katili wataokoka; kwa maana nitapambana na yeye abishanaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.
Nilijikuta namwambia Mungu naomba nisaidie, kupitia haya maneno yako, mimi sikujui, sijawahi kukuomba, sijawahi kukufuatilia lakini naona nipo mateka, naona mimi ni mfungwa, nifungue, nitoe kwenye laana, nisaidie niwe huru, adui zangu waniachie ili nikutumikie wewe, nisaidie Mungu, nitumie, niwe rafiki yako.
Asubuhi ndiyo nilipata usingizi na kidogo nikachelewa kuamka, nilipoamka, mama nimeenda kwenye harakati zangu nakutaka na yule muhubiri tena ananihubiria habari za mateka, na kuwa na Mungu ili niwe huru na kufurahia maisha.
Mungu aoneshe kilichopo ndani yangu. Nikakumbuka usiku wangu, nikaona sio kawaida ni Mungu, akaniuliza kama nipo tayari Kumpa Mungu maisha yangu nikakubali, nilipotubu tu mama na kukubali kuwa yeye Yesu aliye hai ndiyo mwokozi wa maisha yangu nilianza kuona mambo tofauti.
Kwahiyo kuanzia leo mimi nitamtumikia Mungu. Amenielekeza kanisa analo sali, na mimi nitaanza kwenda huko nina furaha sana.Kesho naenda kanisani.”
Tulijikuta tunafuraha sana, nilisema “hongera sana kaka kusema kweli nina furaha sana. Zawadi yangu kwako sasa kaka yangu hii hapa.”
Nikatia Biblia niliyopewa na mama mgonjwa nimpe, kaka yangu alifurahi sana. Alifurahia sana.
Mama alikuwa tu anamtazama mwanaye anakumbatiana naye, hapo Priya sasa na anko wake yupo mwilini. Nilikuwa na furaha sana, nikaona mama na kijana wazungumze na mimi nikamsikilize rafiki yangu. Vile nainuka, kama akasema “dada yangu, unanukia kitajiri.”
Nikacheka huku moyoni naona raha, aanh bwana kunukia raha asikwambie mtu.
NAAAAAAAAAAAAAAM
HAPA NDIYO MWISHO WA SEASON TWO
SEASON THREE INAPATIKANA
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni