Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

NAKUPENDA BILA MIPAKA 76 - 86 SEASON TWO
Gonga94 · Stories

NAKUPENDA BILA MIPAKA 76 - 86 SEASON TWO

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.

:76
Nazwi niambie kuna tatizo, unagombana tena na dokta wako?”
Nilitabasamu na kusema “mimi kugombana na dokta?, kwanini?, Hapana kuna vitu alikuwa ananielekeza tu.”

Alinitazama, Nadhani aligundua kitu mimi sijui Ila sikuwa nimempa hiyo nafasi, aliniambia “nimeona kila kitu, niambie ukweli.”
Mimi nilitabasamu, na kusema “hapana, alikuwa ananielekeza kitu kuhusu mama.”

Alinitazama, nami nikawa najikaza kwelikweli, lakini moyoni naona raha niaje, bosi ananijali, bosi hataki nigombane, natamani Kama nafasi Kama hizi zitokee Tena na Tena na Tena lakini sasa ndiyo hivyo, Kwahiyo mimi niliingia ndani na moja kwa moja jikoni. Sikumkuta dada Maria, nikachukua sahani na kuingia zangu chumbani.

Kusema ukweli nilikuwa nimekasirika sana, nilikuwa nimechukia mno upande wa Dokta Kabale, lakini upande mwingine Leo nina furaha mno. Usiniambie umesahau, mimi nimepewa manukato, sio nimepewa tu na yeyote.

Ni Mr Gallen kaenda dukani fikiria, halafu kanunua kwaajili yangu niambie hii si hatua kubwa jamani. Ni Kama naelekea ushindi vile. Nikajipulizia kiasi. Waooooo!!, waoooooo!!, waooooo!!! Unajua inanukia vizuri, inanukia helahela nasikia raha mwenzenu sijui niseme nini.

Baada ya hapo nikachukua Yale maandazi na kuingia chumbani kwa mama. Mama aliponiona alitabasamu, alinitazama nami nikasalimia. Mama aliniitikia halafu akasema “mwanangu, umechelewa sana leo ulikuwa wapi?”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:77
Nilimtazama na kusema “nisamehe sana mama, naomba nisamehe.”
Mama aliniambie “wewe Nazwi wewe, emu sogea hapa.”

Vile anaongea kwa upole halafu ni Kama ananishangaa, nikajiuliza “nini Tena tatizo hapa jamani mbona naitwa hivi.”

Nilisogea mama akaniuliza “haya manukato mwanangu umetoa wapi?”
Niliinamisha kichwa tu, aibu naona mimi nitasemaje ni Gallen amenipa. Mama alicheka, alicheka kivivu akisema “nina uhakika huyu ni Gallen, nakuambia haya manukato mume wangu alikuwa anayapenda sana Kwahiyo mimi enzi zangu hii ndiyo ilikuwa harufu yangu. Gallen mkorofi sana.

Leo mmenikumbusha mbali sana. Nilipokuwa mtu mzima nikaona ya kisichana sana nikabadilisha eti nipate yakupoa zaidi. Jamani nimefurahi sana. Unanukia sana mwanangu.”

Wakati mama anacheka na mimi nikajikuta nacheka, dokta akaingia akatukuta tunacheka. Mimi nikasema “karibu sana Dokta.”

Alivyo mnafiki kwa mama sasa alikuwa mwenye furaha akimkumbatia mama akisema “mama yangu, nimekukumbuka sana, nisamehe Jana sikuweza kufika lakini maelekezo yote nilimpatia Nazwi bila shaka upo salama.”

Mama alikuwa tu na furaha akisema “usijali mwanangu, yaani sikuhizi Hakuna hata shida, Nazwi ananihudumia vizuri sana hata sikuwa nakumbuka Jana hukufika, lakini niambie binti yangu mzuri kwema?”

Sasa ungemuona vile mama amesema alikuwa hakumbuki kuwa hakufika, nilitazama pembeni kucheka.Mama anaumwa Ila ana mdomo na mafumbo kama nini, angekuwa mzima huyu ungekuwa ni balaa.

Mimi nikaona mambo yasiwe mengi, nilimtazama mama Kisha nikasema “mama, mimi nina kazi kidogo nje, nitarudi. Dokta tafadhali mama bado hajapata dawa mnaweza mkaendelea.”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:78
Dokta aliniambia “usijali Nazwi nitampa tu, vipi unataka kula nini?”
Mama akasema “nitakula maandazi haya hapa mwanangu kaniletea, na chai.”

Mimi sasa nikawa natoka, nilipofika mlangoni mama alisema kwa upole “harufu yako mwanangu, natamani ukae karibu muda wote. Nimekumbuka mbali sana.”
Nilitabasamu na kusema “Asante mama.”
Halafu nikatoka.

Sasa nilitoka nikawa naona tu niwapishe sikuwa nataka kuendelea kukwazana na Dokta. Nikaona tu nikakaa jikoni na dada Maria. Nilipofika nilikuta anakatakata mboga za majani.

Nilitabasamu na kusema “dada Maria unaonekana unapenda sana kazi hupumziki?”
Alinitazama na kusema “haya ndiyo maisha yangu naanzaje kuchoka.”

Nilitabasamu na wakati huo simu yake inaita. Dada Maria ana simu yake nzuri tu kunishinda hata Mimi. Akawa anaongea anasema “Amen, hakuna shida nashukuru sana, Amen mchungaji.”

Baada ya muda alikata simu. Nilimtazama na kusema “lakini leo unaonekana Kama haupo sawa.”

Alinitazama na kusema “Unajua Nazwi haya maisha wakati mwingine yanaumiza sana.”
Nilikaa na kumuuliza “kwani nini shida dada yangu eneh?”

Alinitazama na Kisha niliona kama anataka kulia. Nilimuhurumia.

Halafu nilitazama Kama Kuna mtu anakuja, akaniambia “Boss ameondoka, lakini haonekani kuwa sawa. Inaonekana Dokta amemkera.”

Nilimtazama na kusema “tuongee kuhusu wewe, hili utaniambia wakati mwingine. Tatizo nini?”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:79
Alishusha pumzi na kusema “unaniona hapa nilipo, nina miaka zaidi ya 20 sijawahi kwenda kwetu. Kwenye hii nyumba, namaanisha kwa huyu mama nimeishi naye kwa zaidi ya miaka 20 sijui hata Kama unanielewa.”

Nilishangaa na kusema “wewe dada Maria, miaka yote hiyo upo hapa, una mtoto au watoto Labda?, samahani swali limeniponyoka.”

Alitabasamu na kulia kwa wakati mmoja, baadaye alibaki analia tu. Nikajuta kuuliza swali lile.

Huyu dada alianza kulia, alilia akisema “moyo wangu ni mzito sana Nazwi, kuna muda nashindwa kupumua, kuna muda nashindwa kuishi vizuri, kuna muda naogopa kila mtu na kila kitu. Na upo wakati nashindwa kusema nini kinanisumbua kwasababu naona nitabaki peke yangu, peke yangu mimi.

Mimi hapa unaponiona naogopa hata kurudi nyumbani, na sio Kama nimefanya kosa huko wala hata sijafanya kosa lolote lile Labda kosa langu mimi ni kuzaliwa tu. Tumezaliwa wanne lakini mimi ndiyo naonekana kuwa sawa.

Yaani dada yangu wa kwanza ni kichaa, dada yangu wa pili kukicha anaanguka maradhi ya ajabu bila hata sababu ya msingi, kaka yangu sasa ndiyo sielewi mtu wa namna gani anateseka, Mke wake kila akizaa watoto wanakufa, wanakufa wote, anaacha huyu anaoa Yule ni yaleyale.

Ndiyo mimi mama yangu alinitorosha nikiwa bado binti mdogo. Na yote ni kwasababu mama natakiwa kurithi mikoba Yao ya uchawi, mimi siwezi kuwa mchawi kabisa siwezi.

Hata hivyo mimi hapa nilipo sitamani hata mwanaume, mwanaume akinisogelea naona Kama mdudu, natukana, nawakwepa kwa gharama zote.

NAKUPENDA BILA MIPAKA:80
Jitihada zangu za kuokoka hazijasaidia kabisa, naona nimechelewa, miaka 37 sasa nakaribia 40 nani atanitaka mimi, nani ananipenda, nitaishia kuwa dada wa kazi za ndani za watu tu.

Tazama hapa mama yangu ameanguka na kupooza, natuma pesa lakini haitoshi kipenzi, natamani kuwa na mama lakini siwezi. Yote haya no Shangazi yangu, ni mchawi balaa, kijiji chote ukitaja tu jina lake anajulikana.

Nazwi, mjue sana Mungu, hii dunia Ina mambo mengi ya kutisha huyaoni, kuna roho zinatufuatilia za ajabu na hatujui.

Ukipata Neema ya kukutana na Mungu mkumbatie usimuache. Ukijua vitu napambana navyo utanihurumia, natishwa, Hakuna usiku mimi nimelala vizuri. Acha tu kipenzi, naumia.

Haijawahi kuwa rahisi, ni maombi, ni kufunga, ni kusali. Namshukuru sana huyu mama, aliniweka karibu na Mungu wakati huo nafika mambo yalikuwa mabaya sana. Ndiyo naendelea jipambania, ipo siku Mungu ataachilia uhuru wote wa maisha yangu, namuamini sana ndiyo maana sichoki.”

Huyu dada alilia sana, alilia akaumia sana. Niliyahisi maumivu yake, nilihisi namna anajisikia hata na mimi nikajikuta naumia sana. Nilimkumbatia kwa nguvu.Alinikumbatia pia.

Sikuwa hata na neno zuri la kumfariji eenh jamani mtu amekimbia kwao, kisa wanataka awe mchawi, anateseka, dada mkubwa namna hii hata mwanaume hataki kweli mambo ya kutisha.

Hayo anakutana nayo kwakweli sitaki hata kujua mimi mwenyewe naona tu maisha yangu yanatisha. Lakini zaidi ameniambia nikikutana na Neema ya kumjua Mungu nisiachie dunia Ina mambo mengi hayaonekani.

Sasa nikasikia Kama anacheka, Nikamtoa mwilini, huku wote tunalia nikamuuliza “sasa unacheka nini?”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:81
Akawa anafuta machozi akisema “nesi unanukia vizuri, Tena hii harufu Kama sio ngeni lakini sina hakika.”
Nikatabasamu, na wakati Huo dokta alifika pale akisema “eenh wenzangu kuna nini hapa?”

Maria alitabasamu na kusema “kutakuwa na nini tena dokta wangu mrembo, Hakuna jipya kipenzi. Hongera umependeza sana leo.”

Dokta alitabasamu akisema “Maria ushaanza mambo yako, hii si ni kawaida yangu.”
Maria alicheka akisema “na uzuri unachangia au unasemaje binti.”
Maria alicheka tu, akachukua alichofuata.

Ukimuona dokta utasema hapa ni kwake, anajifanya anajua kila kitu kilipo hivi unanielewa sijui. Nakuambia anajishaua Kama nini, mimi nipo hapo tu namtazama.

Basi vile anaenda ananiambia “Nazwi kipenzi, ukimaliza mambo yako uje kuna maelekezo.”
Niliitikia kwa upole “sawa Dokta.”


Vile kaingia tu chumbani, Maria alisema “Binti anamtaka Boss kwa nguvu zote, umewahi kusikia haambiliki.”
Nilimtazama na kusema “Ina maana Tajiri hamtaki?”

Alicheka akisema “hivi unamfahamu Yule wewe. Niulize mimi. Hana mambo hayo kabisa, aliwahi kupenda hapo kabla, halafu mwanamke wake wakiwa kwa process za ndoa alifariki.

NAKUPENDA BILA MIPAKA:82
Binti alipendwa Yule, sisi wote tulimpenda alikuwa mzuri, mpole sana. Basi unafikiri alikuwa hata anataka mwanamke mwingine, najua ni mwanaume Labda anakula anatema anaendelea zake na maisha si unajua wanaume. Ila tangu hapo hatujawahi tambulishwa Tena. Hata mimi dada yake wa karibu hajawahi.”

Nilimtazama na kusema “Ina maana Hana hata mtoto wala mpenzi?”
Alitabasamu na kusema “kuna muda namtania anacheka tu.”
Nilishangaa nikisema “wewe unamtania Yule anavyonuna vile.”

Akacheka akisema “watu wengi wanamuogopa, lakini kwangu ni Kama Kaka unajua. Ni mtu serious tu Ila ana upendo sana. Ndiyo maana bishost anataka ndoa leo kesho.”

Nilitabasamu tu na kusema “story zitakolea hapa wacha niende kwa mama.”
Hapo mimi moyoni nasema “Kabale unanisumbua bure kumbe kutakwa kwenyewe hutakwi una kazi ya kunisumbua tu sasa Subiri nitakunyoosha wewe endelea tu kunichokonoa.”

Nikawa natembea kuelekea chumbani kwa mama.Ingawa ndani yangu kuhusu Maria naumia sana, inawezekana vipi yaani mimi nimezaa watoto wangu vizuri, eenh halafu mtu tu kutoka huko alipotoka anasema lazima uteseke na watoto wako au laah uchawi huu hapa.

Ningekuwa mimi ndiyo mama Maria sijui ningemfanya nini huyo Shangazi mchawi kuniharibia wanangu, hii ni mbaya sana na haikubaliki.

NAKUPENDA BILA MIPAKA:83
Nilipofika chumbani mama alikuwa zake tu anatabasamu. Aliponiona alizidi kutabasamu na dokta sasa na unafiki wake ni kama vile ananipenda sana. Kumbe anatamani nifukuzwe hapa muda wowote ule.

Nilimtazama, na yeye alikuwa akinipa maelekezo kwa upendo sijui ndiyo mama ajue kuwa tunaelewana. Halafu alipomaliza alisema akitabasamu “Nazwi unanukia vizuri sana, Nimependa sana harufu yako.”

Nilitabasamu na kusema “asante Dokta, unanukia zaidi.”
Akatabasamu akisema “inaitwaje hii, ni nzuri sana.”
Nilimtazama na kusema “sijui bei yake dokta wala hata sijui jina lake.”

Alitabasamu na kusema “ni sawa kipenzi, mimi naenda sasa. Tafadhali hakikisha unafanya kama nilivyokuelekeza nakuomba Nazwi eenh. Kama ukisahau nipigie muda wowote.”

Nilitabasamu tu, na kisha alienda akambusu mama paji la uso na kusema “mama, baadaye, nitakuona baadaye kipenzi changu.”

Mama alitabasamu na kusema “Mungu akutangulie mwanangi mzuri.”
Dokta alijibu “Amina mama.”
Mama alitabasamu na dokta kuanza kuondoka zake akionekana kuwa na furaha sana.

Alipo ondoka alinitazama, nikajikuta sasa natabasamu. Mama aliniambia kama kawaida yake “mwanangu jamani asante sana, unajua haya maandazi ni matamu sana, nafurahia sana.”

Nikacheka kidogo na kusema “mama ina maana utashukuru kuhusu maandazi mpaka saa ngapi jamani. Mama usinambie umemaliza maandazi.”

Mama alicheka akisema “yaani mwanangu, wewe acha tu. Unajua saizi mama yako nimelala tu hapa eenh, siwezi kufanya lolote basi nafanyiwa utapeli hapahaoa. Ni huyo Boss wako Gallen, amekula na yeye pia.

Anayapenda sana haya maandazi akila haachi kuyasifia, basi na yeye alikuja hapa akabeba zake yake na kukimbia nayo.”
Nikacheka nikisema “Boss Gallen kala maandazi?”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:84
Mama akatabasamu akisema “kwanini asile sasa, tena anapenda vitu vitamu yule balaa. Unajua mwanangu ni kijana mzuri sana, hana mambo mengi sana, kwa namna mimi namjua.

Sio kama namsifia mtoto wangu ukaanza ooh mama ana mnadi mwanaye, lakini namjua yule akitaka jambo lake ametaka na lazima apate kwa namna yoyote ile na asipotaka ni hataki.

Kuna wakati maamuzi yake yananiumiza mpaka mimi. Yote kwa yote ni kijana wangu nampenda sana, natamani siku apate familia, sijaona akifurahi miaka mingi sana wakati mimi najua ni mtoto mwenye furaha sana.

Tangu kifo cha mchumba wake kipenzi amebadilika kabisa. Lakini atakuwa sawa si ndiyo mwanangu.”

Nilimtazama mama, nikasogea karibu na kusema “usilie tafadhali mama, usilie.”
Akaniambia akitabasamu akisema “usijali mwanangu, unadhani nalia kirahisi. Hapana hata hivyo namshukuru sana Mungu ananipenda sana mama yake, ananiambia mengi, nazungumza naye mengi sana.”

Nilitabasamu na kusema “eenh hapo kwenye mengi mama na huwa unanisema mama.”

Mama alicheka, alicheka na kusema “akuuuu!!, wewe mtu akuulize kitu kuhusu rafiki yako, embu kwanza niambie una rafiki yako unampenda?”

Nilitabasamu na kusema “ninaye, anaitwa Dorice.”
Akaniuliza kwa upole “ni mtu wa aina gani hata mnaelewana hivyo?”

Nilitabasamu na kusema “eenh yaani mama, Dorice kwanza ni mcheshi sana, halafu ana upendo mno. Unaweza kuamini yeye ndiyo alinitafutia hapa kazi. Mimi napenda sana moyo wake.”

Mama alisema “kabla hata sijaendelea akasema “kumbeee, nadhani Dorice anahitaji zawadi maana amenipa rafiki mzuri sana. “

NAKUPENDA BILA MIPAKA:85
Tukacheka halafu akaniambia “sasa enh ndiyo kama hivyo, na yeye huwa ananiuliza maswali kuhusu wewe.”

Eenh, ndani yangu nasema “jamani, ni mimi huyi nauliziwa na dokta Gallen au nachanganyikiwa mimi. Natamani nimuulize mama ananiuliziaga nini ila ndiyo siwezi.”

Hapo huku naendelea na kazi huku tunapiga story za hapa na pale. Akaendelea “unajua mwanangu mimi nakupenda sana kwasababu nakuona kabisa wewe ni msichana ambaye unampenda Mungu, una hekima, unyenyekevu, upole na una moyo mzuri sana.

Basi mwanangu anapenda sana niwe na amani, akiniuliza kidogo nami namuelezea. Hata mimi sijui kwanini anapenda sana kuuliza kuhusu wewe, au mwanangu, au.”

Mama alianza kucheka na mimi nikamtazama nikisema “mama ushaanza hivyo au nini?”

Mama alisema “leo nina furaha sana, lakini lazima nipate majibu, mwanangu ameenda dukani, akanunua pafyumu yangu ya zamani sana akakupatia wewe hapa kuna jambo, kuna jambo kuna jambo sio bure nasema.”
Nikacheka na kusema “mamaaaa!!, upoje lakini.”

Mama alicheka na kusema “nimefanya nini sasa mwanangu, tena nilitaka nisahu mwanangu nina umbea. Lakini sitakwambia sasa kwasababu natakiwa nilale. Ila nikiamka nitakusimulia wotewote. Lakini sasa kabla sijalala niambie kuhusu Biblia.”

Nilimtazama mama na kusema “mama lakini si unaona unavyonifanyia, hiyo wala sio tabia nzuri. Unaniweka roho juu juu mwenzako, ungesema basi huo umbea eenh.”

Mama alicheka akisema “mwanangu kwa umbea sasa, nitakuambia mwanangu. Unajua dawa zilivyo eenh, wewe acha nilale niamke nikiwa sijachoka sasa hata kuongea siwezi.”

NAKUPENDA BILA MIPAKA:86
Nilitabasamu na kusema “sawa mama, basi pumzika halafu ukiamka tutaongea. Kuhusu Biblia mwenzako hata sijaweza sielewi nianzie wapi mama. Lakini nakuahidi nitaweza.”
Alitabasamu. Hakusema kitu zaidi alianza kufumba macho yake.

Itaneni itaneni itaneni jamani, niamshieni Dokta Kabale, dokta Kabale aamshwe au naota mimi. Mr Gallen ananiulizia mimi?, mimi Nazwi nauliziwa na Mr Gallen, mbona hii ni miujiza, haya ni maajabu.

Kumbe mimi nikiondoka huwa ana kaa na mama yake wanasimuliana weee. Kama naona mama anavyonisifu mimi. Sasa hili la kuuliziwa ni dogo, amekula maandazi yangu.

Nahisi joto, mapigo ya mbio yanaenda moyo uwii nachanganyikiwa samahani jamani ni mapigo ya moyo yanaenda mbio, au ananipenda.

Au, mh hapana, mimi ni mdogo kwake lakini sasa, sasa itakuwaje, au anaona mdogo hawezi niambia. Lakini hapana, au wanapendana na Dokta kabale, ni wivu au nini mbona nahangaika mimi jamani.

Nipo hapa moja haikai mbili haisogei, nawaza nakuwazua mengi jamani. Naona hata mama na yeye haamki, anipe huo umbea. Basi ikabidi tu nitoke niende nje kidogo nipunge upepo. Nilipotoka nje, nilikuta dada Maria amekaa na juisi yake pembeni halafu anasoma Biblia.

Nilitabasamu na kusema “unasoma Biblia?, bila shaka utanifundisha.”
Alitabasamu na kusema “ni rahisi sana, ni kutenga tu muda tena ukizoea unakuwa huwezi pitisha siku.”
Nikatabasamu.

Akanitazama na kusema “karibu mdogo wangu, eenh niambie.”
Nilitabasamu na kusema “sina hata la kusema dada Maria.”
Akanitazama na kusema “asubuhi nimekuona bustanini na dokta.”

Nilimtazama, halafu akaniambia “Kaka Gallen aliwaona pia, akatoka haraka akiniuliza “wanafanya nini?”
Nikamwambia “lakini tulikuwa tunaongea tu.”
Alinitazama na kusema “unanificha mambo yako eenh.”

Maoni

You're not logged in


Tangazo - My true love mwanzo Hadi Mwisho
My true love mwanzo Hadi Mwisho
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NAKUPENDA BILA MIPAKA 76 - 86 SEASON TWO


:76
Nazwi niambie kuna tatizo, unagombana tena na dokta wako?”
Nilitabasamu na kusema “mimi kugombana na dokta?, kwanini?, Hapana kuna vitu alikuwa ananielekeza tu.”

Alinitazama, Nadhani aligundua kitu mimi sijui Ila sikuwa nimempa hiyo nafasi, aliniambia “nimeona kila kitu, niambie ukweli.”
Mimi nilitabasamu, na kusema “hapana, alikuwa ananielekeza kitu kuhusu mama.”

Alinitazama, nami nikawa najikaza kwelikweli, lakini moyoni naona raha niaje, bosi ananijali, bosi hataki nigombane, natamani Kama nafasi Kama hizi zitokee Tena na Tena na Tena lakini sasa ndiyo hivyo, Kwahiyo mimi niliingia ndani na moja kwa moja jikoni. Sikumkuta dada Maria, nikachukua sahani na kuingia zangu chumbani.

Kusema ukweli nilikuwa nimekasirika sana, nilikuwa nimechukia...

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/nakupenda-bila-mipaka-76-86-season-two

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama #fblifestyle #BeautyBattle #AfricaVsWorld #Tanzania #Kenya #Congo #Rwanda #Burundi #SouthAfrica #USA #VoteNow #DebateTime #Trending <br>

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi nakupenda-bila-mipaka
NAKUPENDA BILA MIPAKA 1 - 12
NAKUPENDA BILA MIPAKA 1 - 12
NAKUPENDA BILA MIPAKA  36 - 45
NAKUPENDA BILA MIPAKA 36 - 45
NAKUPENDA BILA MIPAKA 26 - 35
NAKUPENDA BILA MIPAKA 26 - 35
NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO
NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 80

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 80

1.21K
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 81 na 82 enjoy Sunday

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 81 na 82 enjoy Sunday

1.06K
NAKUPENDA BILA MIPAKA 76 - 86 SEASON TWO

NAKUPENDA BILA MIPAKA 76 - 86 SEASON TWO

193
NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO

NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO

189
IN LOVE WITH ZURI*   Chapter 7

IN LOVE WITH ZURI* Chapter 7

186
LETICIA 15:16

LETICIA 15:16

184
CHUMBANI KWETU 💚   Sehemu   ya   10

CHUMBANI KWETU 💚 Sehemu ya 10

143
ROWAN (Mine alone) 1 - 5

ROWAN (Mine alone) 1 - 5

133
CHAGUO LA MOYO ❣️ SEHEMU YA 01--- 05

CHAGUO LA MOYO ❣️ SEHEMU YA 01--- 05

107
Poor Orphan Got Pregnant With Twins & Was Kicked Out By Her Stepmom -Unexpectedly Baby's Dad Was CEO

Poor Orphan Got Pregnant With Twins & Was Kicked Out By Her Stepmom -Unexpectedly Baby's Dad Was CEO

13

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.92K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.62K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.87K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.42K
MY WANGU❤️ sehemu ya 108

MY WANGU❤️ sehemu ya 108

3.02K
MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

2.99K
MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

MY WANGU❤️ sehemu ya 116 na 117

2.83K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.78K
MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

2.7K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.66K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
NAKUPENDA BILA MIPAKA 76 - 86 SEASON TWO Post Mpya
NAKUPENDA BILA MIPAKA 76 - 86 SEASON TWO
@majario LIVE

:76 Nazwi niambie kuna tatizo, unagombana tena na dokta wako?” Nilitabasamu na kusema “mimi kugombana na dokta?, kwanini?, Hapana kuna vitu alikuwa ananielekeza tu.” Alinitazama, Nadhani aligundua kitu mimi sijui Ila sikuwa nimempa...

USIKAE KWENYE NYUMBA MOJA YA KUPANGA KWA MUDA MREFU. Post Mpya
USIKAE KWENYE NYUMBA MOJA YA KUPANGA KWA MUDA MREFU.
@majario LIVE

Tena ikiwezekana katika hizi nyumba za kupanga uwe na limit ya muda wa kukaa, mtu unakaa miaka na miaka kwenye hiyo nyumba mpaka unaonekana kama wewe ndiye mwenye nyumba. Inafikia...

LETICIA 15:16 Post Mpya
LETICIA 15:16
@majario LIVE

💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍💍 LETICIA Sehemu ya 15 Mwandishi;LISSA Yule dada alikuwa mcheshi dakika mbili tushazoeana ,nilikuwaga namuona tu kijijini ila hii siku ndio nikamjua vizuri .alinambia anaitwa rehema. Tulipiga story mno akanipa na namb yake...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 81 na 82 enjoy Sunday Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 81 na 82 enjoy Sunday
@majario LIVE

Mwandiishi; LISSA Basi bwana sasa siku iyo nakumbuka nilikuwa kwa jalia , nikamuuliza jalia mbona huna tumbo alafu mimba si itakuwa na miezi 2 , akanmbia mh naona...

CHAGUO LA MOYO ❣️ SEHEMU YA 01--- 05 Post Mpya
CHAGUO LA MOYO ❣️ SEHEMU YA 01--- 05
@majario LIVE

MTUNZI RITHA STORIES WHATSAPP 0754380244 AU 0680992844 SONGA NAYO................. Mpenzi msomaji Leo na kuletea kisa hiki Cha mapenz ambacho Kita kufunza mengi na kukusisimua,kukufurahisha, na kukuhuzunisha pia Karibu tuende wote👇 Unaweza kuniita Sonia...

Poor Orphan Got Pregnant With Twins & Was Kicked Out By Her Stepmom -Unexpectedly Baby's Dad Was CEO Post Mpya
Poor Orphan Got Pregnant With Twins & Was Kicked Out By Her Stepmom -Unexpectedly Baby's Dad Was CEO
@majario LIVE

If you don't leave my house right now, I will cut you into pieces today. Mrs. Helen screamed, waving a big sharp cutlass in the air. Grace backed away, her...

CHUMBANI KWETU 💚   Sehemu   ya   10 Post Mpya
CHUMBANI KWETU 💚 Sehemu ya 10
@majario LIVE

Nilifurahi sana❤😘nikaletea mtoto wangu nikamuona nililia kwa furaha nikamshukuru sana Betty maana amekuwa msaada sana kwangu🙏❤ asubuhi ya siku iliyofuata mume wangu nae akaja kumuona mtoto nae alifurahi sana...

ROWAN (Mine alone) 1 - 5 Post Mpya
ROWAN (Mine alone) 1 - 5
@majario LIVE

MTUNZI: Mr Burudan Sehemu ya: 01 ANZA NAYO.... Niite Vee, jina la kifupisho cha jina langu la Vera, Vera ndio jina langu halisi nililopewa...

NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO Post Mpya
NAKUPENDA BILA MIPAKA 66 - 75 SEASON TWO
@majario LIVE

:66 Mimi nilitoka nikiwa na furaha sana, Niliondoka hapa ni Kama nimezaliwa upya. Moyo wangu ulikuwa umechangamka mno. Ingawa nilifika kwa kujivuta sana lakini siku imeisha na tabasamu pana kwenye uso...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 80 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 80
@majario LIVE

🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈🦈 Basi nikaludi ndani sasa , nikamkuta zena ana mawazo sana, nikasema zena naomba nikupe chakula kwanza kisha tutaongea tu nitakuelezea kila kitu mke wangu, zena akanmbia sawa, wala hakuwa na...

IN LOVE WITH ZURI*   Chapter 7 Post Mpya
IN LOVE WITH ZURI* Chapter 7
@majario LIVE

SONGA NAYO..... Kitendo cha mimi kuongea kwa ukali kiasi hicho kiliwashtua sana Idress lakini pia na Ethan, Ethan yeye mpaka alinyanyuka na kuja sehemu niliyokaa kisha akachukua hiyo chai ambayo nasemea...

IN LOVE WITH ZURI* *Sehemu YA SITA* Post Mpya
IN LOVE WITH ZURI* *Sehemu YA SITA*
@majario LIVE

SONGA NAYO..... Kimya kifupi kilipita hii ni baada ya mimi kusikia kuwa Zuri ni mke wa mtu nilikuwa naumia sana sio siri jamani ila sema nilijikaza mbele ya mama asigundue "Unamaanisha kwamba...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 78 na 79 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 78 na 79
@majario LIVE

Basi ikawa hivyo, na ikakat mwez amani ndani hakuna kabisaa, zena ni kanuna , yani hacheki na mm kabisaa, hatuna story ata, na mala nyingi nikiludi nyumbana namkuta kashalala et...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 77 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 77
@majario LIVE

Mwandiishi; LISSA Nikasema.mm ndo nanukia ayo malashi mke wangu, akanmbia ndio.kwani apa si nipo mimi na ww. Nasikia marashi ya kialabu, mh nikajinusa sasa na mm. Eeh ni.kweli aya ni...

NAKUPENDA BILA  SEASON TWO 51 - 65 Post Mpya
NAKUPENDA BILA SEASON TWO 51 - 65
@majario LIVE

NAKUPENDA BILA MIPAKA:51 Nilitoka nikiwa nishapendeza hata mama alishtuka na kusema “kulikoni tena? Nilishusha pumzi na kusema “Acha tu mama ndiyo nishaitwa.” Mama alinitazama na kusema “huna namna nenda. Sasa vipi pesa ya...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest