Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

NIMEKUSAMEHE ILA SITASAHAU SEHEMU YA 01 "uuuwiiiii Diana mambo gani hayo ya kumwagiana maji mdogo wangu??!

17th Sep, 2025 Views 21

" nililalamika lakini siyo kwa kumaanisha au kwa kutokupenda ila ni kwa sababu maji yalikuwa ya baridi aliyokuwa ananimwagia mdogo wangu Diana

"hakuna cha mambo gani wala mambo gani hapa unaoga maji tu Happy birthday to you my sister!!" Diana aliniambia huku akinimwagia maji kwa mpira alioninyang'anya wakati nikiwa namwagilia bustani asubuhi, mimi mwenyewe sikukumbuka kama ni siku yangu ya kuzaliwa, niliamka tu na kuanza shughuli zangu za kila siku, Diana mdogo wangu aliyekuwa amejiandaa kwenda chuoni ndiye aliyenikumbusha kama kuna sikukuu yangu ya kuzaliwa leo

"kumbe ni my birthday leo uuwiii jamani nimesahau kabisa mdogo wangu asante!" nilimwambia nikitaka kumkumbatia
"we we we dada ishia hapo hapo unamkumbatia nani?" alininyooshea kidole
"jamani kwani dhambi kukukumbatia?"
"na ulivyolowa hivyo naenda chuoni mwenzako nimeshajiandaa utanilowesha bure!"

"hahaha si nimesahau na ningekulowesha kweli usistaduu wote ukuishage"

"thubutuu!!" nakuvuta nywele
"huweze wapi"
"haya dada mimi naenda ila baadae nakuletea kitu kizuri nikirudi chuoni"
"kitu gani jamani?"
"supriseee we subiri tu utaona"
"jamani nidokeze hata kidogo yaani hapa unanipa kimuhemuhe"
"wait and see my dear sister (subiri uone dada yangu mpendwa)" aliniambia akinibusu shavuni na kuondoka mbiombio akiita bodaboda na kuondoka akiniacha natabasamu tu peke yangu nikiwa nimelowana chapachapa asubuhi asubuhi na ndipo niliposikia hatua za viatu nyuma yangu nilipotazama nikamuona mume wangu George akiwa ametoka amejiandaa anaelekea kazini nikamfuata kimahaba na kumshika begani

"taratibu utanichafua" alinizuia nisimshike begani
"ni maji tu mume wangu mpenzi ndo umeshajiandaa hivyo, mbona umebadilisha shati nililokuvalisha na tai yake umevaa shati jingine?"

"nimeamua tu tutaonana baadae!" alinijibu na kulifuata gari
"mume wangu" nilimfuata
"nawahi kazini Rebecca tutazungumza nikirudi"
"leo ni siku gani unakumbuka?"
"ni ijumaa leo"
"kuna tukio gani?"
"Rebecca baadae unanichelewesha"
"ni birthday yangu jamani mume wangu"
"happy birthday to you" aliniambia huku akifungua mlango wa gari
"ndo ya juu juu hivyo jamani?"
"nikirudi Rebecca" alinijibu akawasha gari nami sikuwa na cha kufanya nilimuaga tu kwa kumpungia mkono wakati akiondoka na gari akionekana anawaza mbali mimi kama namsumbua tu lakini nilijua ni uchovu tu wa jana maana alichelewa kurudi alirudi saa tano usiku akiniambia kulikuwa na kikao cha dharura ofisini kwao

"mama"
"mumy!" watoto wangu waliokuwa wameshaandaliwa na dada wa kazi waliniita wakiwa tayari kwenda shule na sare zao na mabegi yao mgongoni

"naam wanangu wazuri!"
"happy birthday to you happy birthday to you happy birthday dear mamy happy birthday to youuu!" waliniimbia na kunikumbatia na dada wa kazi aitwae Aisha karibia waniangushe chini

"asanteni sana wanangu wazuri"

"haya bye mamaa!"
"mniletee zawadi"
"haya mama" walinijibu wakienda barabarani kusubiri gari lao la shule (school bus) nilikuwa na watoto watatu, wa kwanza Theresia akiwa darasa la saba, Robert darasa la nne na binti yangu mdogo Leticia akiwa chekechea

Waliondoka na dada wa kazi wote wakisoma shule moja, nami nikaendelea kumwagilia bustani nje ya nyumba yangu

"hodi hodi humu ndani"
"karibu sana" nilimwitikia mgeni huyo ambae alipishana na watoto wangu getini hakuwa mwingine ila ni mwanamama Magritha, rafiki yangu wa karibu ninayesali nae kanisani na tukiwa wote kwenye Saccoss moja ya wanawake

"naona vijana wanaenda shule"
"eeh karibu sana namimi namwagilia bustani hapa"
"Rebecca unachekesha kweli yaani badala ungepanda mboga mboga ule wewe unamwagilia bustani ya maua uwafaidishe nyuki mimi siwezi kazi kama hiyo"
"nyumba inapendeza bibi wee karibu kiti barazani"
"hapa pananitosha siwezi kuingia ndani huko asubuhi yote hii sitaki chai za watu ndokwanza saa kumi na mbili" aliniambia akikaa kwenye mawe ya bustanini

"enhee za asubuhi"
"njema Rebecca za kwako na familia?"
"safi kabisa nipe habari naona asubuhi asubuhi"
"nimekuja uniazime elfu hamsini tu shoga yangu wala nisizunguke zunguke nipo vibaya mwanangu anadaiwa shuleni ameshindwa kwenda leo yaani"

"mh Magreth sina hata akiba humo ndani"
"jikung'ute tu shoga yangu naaibika mwenzio, nitakurudishia jumapili kanisani kuna hela yangu kwenye Vicoba tunavunja jumapili"

"sawa ngoja nikakuchukulie hela fulani ina kazi nyingine ila kazi yake ni ya wiki ijayo"
"nashukuru sana"
"usijali tumetoka mbali sana" nilimjibu nikiinuka kutaka kwenda ndani

"Rebecca!" aliniita
"abee" nikageuka
"mumeo yupo?"
"ameenda kazini"
"mmh jana alirudi saa ngapi?"
"kwanini unauliza?"
"nauliza tu kuna ubaya?"
"alirudi saa tano hivi na nusu karibia saa sita usiku"
"ohoo na mdogo wako yule Diana alirudi saa ngapi?"

"mbona maswali jamani Magreth rafiki yangu?"
"swali la mwisho tu hili"
"alirudi kama saa tano hivi na yeye walipishana kidogo tu na shemeji yake ila Diana alitangulia kama robo saa hivi kabla ya shemeji yake"

"vipi hujahisi kitu chochote kutokana na maswali yangu na hiyo mida niliyokuuliza?" Magreth aliniuliza nikabaki njiapanda nikishindwa kumuelewa anamaanisha nini kuniuliza maswali hayo

"hapana nifafanulie"
"jana nimewaona mumeo na mdogo wako pamoja kwenye mazingira nisiyoyaelewa elewa!!"

"unasema???!!"....

Vipi wewe msomaji umehisi nini?!

Full Story TSH1000 tu,
Njoo Whatsapp 0675137453 ujisomee

Inaendelea.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIMEKUSAMEHE ILA SITASAHAU SEHEMU YA 01 "uuuwiiiii Diana mambo gani hayo ya kumwagiana maji mdogo wangu??!  >>> https://gonga94.com/semajambo/nimekusamehe-ila-sitasahau-sehemu-ya-01-uuuwiiiii-diana-mambo-gani-hayo-ya-kumwagiana-maji-mdogo-wan

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest