MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 15
SONGA NAYO.......
Mira mie nikaanza kupiga maombi ya kuteketeza roho ya umauti niliomba sana, jasho lilikuwa likinitililika na kulowanisha kifua Changu
Nilikuwa nimezama kwenye ulimwengu wa roho nikifanya maombi, ni sauti ya mtoto ndì iliyonirudisha kwenye ulimwengu wa mwili
Nikafumbua macho na kutazama, nilifirahi baada ya kumuona Nasrat akiwa amefumbua macho akinitazama kwa furaha niliyokuwa nayo nikamkumbatia ila kwa tahadhari kubwa
Kuepeuka kutonesha jeraha lake, kilichofuata hapo ni asante yesu, ambazo zilitawalla karibia chumba kizima
"Nasra binti yangu kuanzia leo hutaitwa tena Nasra nakubadili hili jina kwa sababu mungu amejidhihirisha kwako na kuonyesha nguvu zake kwahiyo kuanzia sasa utaitwa Bless..."
Nilitamka hayo basi Nasrat au Bless akatabasamu, kitendo kilichonifanya na mimi nitabasamu eeh kuashiria hili jina binti yangu amelipokea...🙏🙏
Kwa uwezo wa mungu binti yangu aliendelea kuimarika siku mpaka siku, hata kile kitovu chake kiliacha kabisa kutoa usaha, amani ilirudi tena kwenye moyo wangu
"Bless niachie jamani uwiiiiiii..."
Ni kelele ambazo nilikuwa nikipiga ni baada ya Bless kunivuta nywele wakati nikiwa nimembeba mabegani, 😂 binti yangu ni mkorofi nyie huu ukorofi ameupata baada ya kufika bongo yani kabadilika ile mbaya
Bless ni mtoto mtundu sana, amepata watu wa kucheza nae nakwambia kamechangamka muda ote kanatabasamu tu na uso wake ulionekana kuwa na nuru 🥰
Nilikuwa niko zangu ndani na ka binti kangu tena nyumbani kabisa huku buza 😅 ndio makao makuu ya Mira na nimecheza sana hiyo mitaa hata miguu na utumbo wa kuku nimeula sana
So huku ni nyumbani nimecheza sana rede nakwambia..😅
"Da Mira kuna mtu anakuita huko nje.."
Basi mdogo wangu Eliudi, alikuja kuniita, Eliudi ni mdogo wangu na ndie rast born wa familia ya mama Mira. Basi nilitoka huku mikononi nikiwa nimempakata Bless
Kweli nipotoka nje nilikuta kuna gari nzuri sana tena ile ya gharama achana na hizi za million moja, ile gari ilikuwa ikiwaka waka balaa
Nilitembea mpaka kwenye hilo gari nikajaribu kuita lakini hakukuwa na mtu.
"We Eli, huyo mtu ambaye ananiita yupo wapi..??"
Nilimuuliza Eliud huku nikipiga hatua za kuondoka maeneo yale, sasa bana sijui huyo mtu alitaka kunishtua maana alikuja nyuma angu na kuniziba macho
"Otea nani..."
Nilisikia sauti ya mdogo wangu mwingine huyu ni wa tatu kuzaliwa na bado anaishi hapa hapa nyumbani sasa kitendo cha kumsikia anaongea nikajua ni yeye tu huyu dogo
"Hakim si uniache basi we nae, yani hutaki kuniona nikuwa na amani..."
Nikawa naendelea kulalamika lakini sikuachiwa
"Hakim nitakupiga ujue, harafu mikono yako inanuka umeshika nini..??"
Niliposema mikono yake inanuka akaniachia nikageuka ili kumpiga kofi lakini nilistop hii ni baada ya kumuona Anfrey ndie aliekuwa nyuma yangu
Na kibaya zaidi alikuwa akijinusa mikono hii ni baada ya kusema mikono yake inanuka 😆 maskin kaka wa watu alikuwa anajinusa tu😂😂🙌🏾
Niliona aibu hatari nikageuka kuangalia pembeni nikamuona hakim ananichekea, watoto wa mama Mira hasara tupu kijana amekuwa yule lakini ana mambo ya kitoto sana
Ikabidi nigeuke nimuombe radhi Anfrey lakini nilishangaa akinikabizi fungo za gari, macho yalinitoka nikajua labda huu mkaka ananitania bwana
"Aah ni yangu..??"
Niliuliza huku nikiwa natetemeka nyie, yani kumiliki gari sio mchezo wengine huwa wanazimia kabisa kwa furaha, nilishangaa zaidi ni baada ya ndugu zangu wakiniimbia wimbo wa happy birthday ndio nikajua kuwa leo ndio siku yangu ya kuzaliwa
Kwanza nilimuangaliaa Anfrey kisha nikawaangalia kaka zangu, katika maisha yangu sijawahi kifannyiwa surprise nzuri kama hii ambayo kwa namna moja au nyingine
Ilinifanya nijisikie furaha sana lakini pia na kujiona kuwa hata mimi ninapendwa bwana.
"Happy birthday my sis.."
Kaka zangu wwaliniambia, nilifurahi balaa nikasogea na kuwakumbatia huku Bless nae yumo humo humo 😂, basi baada ya kukumbatiana na hawa ndugu ambao tunashea damu ya kunguni
Nikamgeukia Anfrey maana wakati yote yanendelea alikuwa akitutazama tu, kitendo cha kugeuka tuliangaliana sana ndio tukaja kushtuka ni baada ya mimi kumwagiwa maji 😂
Makaka zangu walikuja na ndoo zilizojaa maji na kunimwagia hawakujali kama Bless nilikuwa nae, Bless alinifanya nicheke maana wakati namwagiwa na yeye alikuwa anchekelea yani furaha yake ni kuona anamwagiwa maji..
"Jamani imetosha sasa khaaa.."
Ni sauti ya mama ilisikika hata sijui alitokea wapi maana aliaga anatoka kwenda kwenye vikoba vyake huko, sasa sijui alifika sangapi.....
ITAENDELEA......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni