MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 19 - 20
SONGA NAYO.........
miezi kama miwili ilipita huku nikiishi Tanzania pamoja na wifi yangu kipenzi BLESS 🥰 yes amekuwa wifi yangu badala ya mtoto wangu lakini nimemfanya kama bjnti yangu nampenda huyu mtoto never and ever 🥰
Kipindi hicho Bless amefikisha miezi 11, nilianza kujihisi tofauti kabisa, mara nimchukie bless kuna mda nilikuwa nakapiga kabisa bila sababu 🥹
"Kwahiyo hiyo mimba ndio inakufanya umpige mwanao sio..??"
Siku moja mama aliamua kunitolea uvivu baada ya kuona nampiga sana Bless bila sababu
" unaongea kuhusu nini mama..??"
Nilimuuliza
"We binti acha kunifanya mimi kama matako yako sawa.."
Ila mama 😅 yani hiyo Kauli atakuwa kaitoa wapi kama sio kwangu maana mimi kitu kidogo basi lazima niseme hilo neno
"Acha kuwaza vingine aambavyo havipo kabisa.."
Nilimwambia
"Acha ujuaji nikuulize hiyo miezi ya nyuma umeingia perido..??
Mama aliniuliza swali ambalo lilinifanya kidogo nishtuke maana kweli hiyo miezi miwili sijaona siku zangu, na huwa ninkawaida Sana kwa mimi kupitulia mwezi au miezi bila kuona period
"Ukweli sijaona siku zangu, lakini niko hivi toka zamani sana.."
"Sawa mkuu.."
😁😁 mama huyu alinijibu kisha akaja kumchukia Bless ambaye alikiwa analia baada ya kumfinya, basi maisha yaliendelea na kabinti kangu kakawa kanakuwa vizuri tu
Bless alikuwa mrembo nyei, yani alikuwa mzuri mpaka kuna mda nikawa namuonea wivi sasa, na kipindi hicho cvote bless ananijua kama mama
Sitaki kumwambia chochote mpaka pale atakapokuwa mkubwa, ndio nifunguke mwanzo mwisho maana kumwambia akiwa na umri mdogo inaweza kumuathiri kisaikolojia
********
Bandugu, hebu itaneni kutoka mashariki , magharibi, kaskazini na kusini mje muone siku yangu mhimu sana, hii siku ndio siku ambayo nilivaa gauni la harusi
Hii siku ndio siku ambayo niliiheshimosha familia yangu kwa miaka yote ambayo nimeishi nayo, siku ambayo kipenzi changu Bless alifikisha mwaka mmoja 🥰
Nyie hivi mnaijua ile hisia ya kufurahia kitu ambacho kimekuja katika siku ambazo ni siku muhimu sana,?? Basi naweza kusema mimi nilikuwa miongoni mwao
Siku hii nilikuwa na furaha sana na sababu kuu ya kuwa nilijijua nina ujauzito wa miezi minne, 😅 nicheke mie yani siku zote hizo sikuwa najijua ila siku ya harusi yangu ndio nikajua kama nina mimba
Tena mimba ambayo iliingia kwa siku moja tu kwenye gari tena siku ya kuzaliwa kwanngu aloooo 🤣🤣🤣 yes najivunia mimo acha nitambe dunia nzima ijue ni kiasi gani najisikia furaha..
Basi bwana ndoa yangu ilipita na ilikuwa ndoa kubwa sana kuwahi kutokea hapo buza, maana kulikuwa na kila aina ya chakula watu wallikuwa mpaka wengine wakawa wanabeba kwenue vikoba vyao
Na siku hiyo ndio siku ambayo watu wengi walizini na kutenda dhambi 😅😅 ni kweli maana kulikuwa na mkesha wa siku mbili arafu ukatae kuwa hakukuwa na uzinzi kweli 😅
Anyway niachane na hayo All in all niwashukuru sana kwa kuwa nami mwanzo mpaka mwisho wa mkasa huu, ninaamini kuna kitu umejifunza kupitia hii story
Amani, upendo na heshima humfanya mtu kufika mbali na katika jambo ambalo hulitarajii kabisa mungu anaamua kukuonyesha miujiza yake
Mfano mzuri ni Mira yes binti alikuwa na mungu ambaye alikuwa akimuongoza eeeh niache ulokole bwana 😅 kufika hapa sina la ziada tena ninawatakiwa furah, amani na upendo katika maisha yenu
MWISHOOOOO
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni