MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 16
SONGA NAYO.......
Basi ikabidi waniache, nikaingia ndani nikawa nimeloa chepechepe na binti angu nae vile vile hakunibanduka kabisa mikononi mwangu
"Karibu sana baba karibi, jisikie upo nyumbani.."
Nikiwa chumbani navaa niliweza kumsikia mama yangu akiongea huko, nilijua bila shaka anamkaribisha Anfrey, basi mama Bless mie nikabadili nguo kisha nikatoka
Mkumbuke kwamba sikuweza kupokea funguo za gari, nilisogea na kuketi moja ya sofa. Mama alimuandalia Anfrey chakula.
Basi wakaati Anfrey anakula Hakim alikuja kumchukia Bless huku akinikonyeza nitoke nje, mimi ni nani nikatae na huku umbea ndio maisha yangu, chapu nikatoka nje
"Dah sis, unajua wewe una nyota kali haya tuambie yule nani..?,"
Baada ya kufika nje, kaka zangu wakarundikana wote hapa wanataka kumjua Anfrey kama ni mchumba wangu, Hebu ngoja kwanza niwatambulishe kaka zangu maana toka mwanzo sijawaambia kabisa
Okay love, kama nilivyosema awali sie tumezaliwa watoto nane na wote tupo hai na kibaya zaidi tunaishi kwa wazazi waetu 😂 ikiwa mamalao ndio kabisa ninaongoza kwa kukaa nyumbani
Kaka zangu wote wameshamaliza elimu ya msingi na secondary so wapo nyumbani ila wanafanya vibarua vidogo vidogo ambayo vinaweza kuwaingizia pesa
Sasa ngoja niwatambulishe majina yao ili kama kuna wadada mmevutiwa nao muwatafute kabisa ili mimi npate mwanamke mwenzangu wa kumuita wifi 🥰
Sasa mimi ndio wa kawanza, naitwa Mira yes Miranda 🥰 wa pili anaitwa Eliazar, na number tatu Eliakim ila tumezoea kumuita Hakimu na dume la nne Elisha 🥰 nyie huyu mkaka yuko 🔥
Yani Elisha ni muhandsome pia ni mtulivu sana bro wangu, hanaga papara na anahuryma sana kaka ayangu huyu mungu azidi kumuinua na sio yeye tu bali wote
Anafuatia huyu pasua kichwa wa familia 😆 Ezra, yani Ezra bwana sijui akili zake zina matope au mayai, maana huyu dogo akili zake anazijua mwenyewe walah
Kuna siku huyu dogo bwana tulikuwa tumekaa nje wanafamilia ila baba ndio hakuwepo, punde bana akapita mdada flan hivi huyo dada ameolewa na ana maumbile ya kawaida sana
Yani maumbile yake, yako hivi ni mwembamba wa wastani hana shape ila tako ndio analo lakini ni gumu 😂, sasa siku hiyo mdada wa watu sijui aliweka nini maana tako lilikuwa limelainika ile mbaya
Ezra atabaki kuwa Ezra bwana, si akajikuta anaongea tena mbele ya mama
"Yani tako la mama mussa huwa halieleweki kabisa, leo unaliona gumu kesho laini saivi hapo limetepeta na halina muelekeo kabisa.."
Nilicheka sana hii siku, mama akawa analalamika kuwa simfundishi Ezra tabia njema, sasa kama mtu amechagua maisha yake ya nini kumfatilia na sio kama ni mfundishe mimi
Ezra ni kijana mkubwa na ninamuheshimu mno so kuwa nakaa na kuanza kumueleza huku jamaa linajua zuri na baya....
Haya sasa anafuata huyu hapa Six boy Emmanuel, nyie wazazi sijui walipania kwenye kuita majina maana madume yote herufi zao za mwanzo zinaanza E kasoro mimi tu
Tabia ya Emmanuel ni mzee wa totozi, 😂 kuzaa watoto wengi hasara tupu maana hawakosi vibaka hata jambazi lazima litakuwemo
So me nimejiwekea mipango ya kuwa na watoto watatu tu huku bless ndio akiwa mtoto wa kwanza, basi bwana maneno mengi ya nini, tuendelee sasa linafuata hili domo zege la familia Eliya
Ila Eliya 😂 yani Eliya acheni aitwe Eliya maana ni muoga harafu ako na aibu huyu kijana na sijui kama ana mchumba kweli maana kutongoza tu hawezi
Hata mimi dada yake kunitazama tu aibu 😅 huyu kijana kuna mda huwa ananikera sasa, yani muda wote yeye ako ana aibu tu kama mwanamke vile dah nachoka mimi 😆
Sasa kuna hili la mwisho yani hili dogo hasara tupu, huyu dogo ni mbea yani hakikisha siri zako humwambii huyu dogo la sivyo unazikuta zishafika kwa mama Mira,...
Nazani mmewajua kaka zangu bwana, basi tuendelee pale tulipoishia aaah tumeishia wapi kweli yes nimekumbuka bwasi bwana nikamtazama hawa kaka zangu maana ni waongo sana
"Umbea tu ndio unawasumbua hebu nipisheni mimi.."
Niliongea huku nikitaka kuingia ndani, nikavutwa tena nikajikuta niko katikati yao 😂 kuwa na kaka raha sana maana muda wote watakuwa wanakulinda tu
Basi wakawa wananisisitiza niseme
"Ni mtoto wa boss wangu.."
"Mh mtoto w boss na akuletee zawadi ya gari..??"
Eliudi kama kawaida yake akaongea
"Eti..??"
Na wenzake wakadakia
"Sikilizeni nyie, yule ni mtoto wa boss wangu na hatuna mahusiano yoyote baina yetu , hizo zawadi hata huko Oman alikuwa akiniletea sana so naomba mkae kwa kutulia.."
Niliongea kisha nikarudi zangu ndani, basi msaa yalisogea hatimae muda wa Anfrey kuondoka uliwadia, so ikabidi nitoke nikamsindikize lakini nilishangaa baada ya kufika kwennye garai akanikabizi fungo za gari..
"Za nini hizi..??"
Nilimuuliza
"Ni zako mama Bless.."
Majiraniiii itaneni huku mje muone nimepewa funguo za gari, niliwehuka pale pale na kuanza kulembelea kidole kimoj 😂 maana kupewa gari tena lenye bei kubwa kiasi kile ni bahati bwana tena kubwa......
ITAENDELEA........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni