MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 17 - 18
SONGA NAYO......
Mdada mie nikaanza kupiga ukelele wa furaha na bila kujigikiria mara mbili mbili nilimkumbatia Anfrey mwamba naye ni kama alitegemea hivyo maana alinipokea tena kwa hamu kubwa
"Anfrey asante asante ansante, sijui hata nikupe nini Anfrey ..."
Niliongea huku tukiwa bado tumekumbatiana pale, machozi yalikuwa. Yanatoka kama mvua, yani mimi ni mwepesi wa kutoa machozi kuna yale ya furaha, huzuni na njaaa 😂
Basi mimi ni shwaaa michozi hiyo 😂 niliwahi kuambiwa eti natumia machozi vibaya siku nikipata msiba wa baba au mama yangu nikilia machozi hayatatoka ng'o 😂 sasa sijui ni ukweli au uongo 😁
"Mira mama, we kuwa na amani nimekupa hii zawadi kubwa kwa sababu wewe ni mfano wa kuigwa yani sijui hata niseme nini tu ili unielewe.."
Alivyoongea hivyo nikajitoa kifuani kisha nikamtazama usoni, akakwepesha macho na kupeleka pembeni.
"Vipi unaonekana kama hauko sawa..??"
Nilimuuliza, akageuza shingo na kuniangalia kishaakazungumza
"Mira niambie ukweli Bless ni mtoto wako..??"
Nikashtuka kidogo kisha nikamuuliza
"Wewe ni nani aliekwambia..??"
"Aaaah nijibu kwanza, Bless ni mtoto wako..??"
"Hapana.."
"Kwahiyo ni mdogo wangu sio..??"
"Ndio.."
"Mira sijui hata nikupe nini kwa shukrani, maana naona kama gari ni zawadi ndogo sana ila usijali mungu akinijalia nitafanya kubwa zaidi ya hili.."
"Aaah basi bwana inatosha.."
Nilisema huku nikitaka kugeuza mazungumzo
"Hivi Mira wewe ni binti wa aina agani ambaye unaweza kukaa na kitu kizito kiasi hiki, yani najiuliza toka jana nimefahamu kuwa Bless sio mtoto wako huwezi amini siku nzima nimekaa nakuwaza.."
( 🙄 uniwaze kwani nimekuwa mpenzi wako au.?? )
"Kawaida tu si unajua tena me nilikuwa kule kama mdada wa kazi tu so haviingiliani na hayo.."
"Haviingiliani kivipi Mira, kumbe siku zote hizo hujawahi kuniambia kama Nasrat oooh Bless ni mdogo wangu na unakaa kimya kabisa hiviiii my God.. "
Anfrey alikuwa anaongea kwa uchungu sana, ikabidi nimtulize kidogo maana mwamba alikuwa anaumia sana kumuona mdogo wake namna ambavyo aliteseka sana
"Lawama zote hizi zinatakiwa ziende kwa madam maana yeye ndie chanzo, mimi sio kama nilikuwa sitaki kukwambia hapana Anfrey me nilikuwa naogopa mno kumpoteza Bless maana nilikuwa nampenda
Lakini pia Bless alikuwa mdogo sana so ikabidi nifanye hivyo kwa ajiri ya kumlinda maana madam alikuwa akinipa vitisho.."
Nilisema huku machozi yakinitoka dah, basi mwamba akanikumbatia pale huku akinipiga piga mgongoni 😂 nicheke kwanza mimi mtoto wa mama Mira
Kumbe kumbato lenye hisia ndani yake huwa ni zuri sana na hamniambii mpaka kumkataa mkaka wa watu 😊 lile kumbato lake lilikuwa zuri sana iseee 🥰
Msinione maraya ila ukweli huyu mkaka alinivutia toka ile siku ya kwanza kabisa ninamuona kwenye laptop, so mdada mie naweza kusema huyu mkaka nilikuwa namtamani mda sana
😂 Sasa nimewaambia ukweli kuna wengine mnafurahi kimoyo moyo my zangu niambieni kama nimepatia kuchagua au niachane nae tu nitafute mtanzania mwenzangu..
Basi siku hiyo ikapita siku nyingine ikashika nafasi niliamka na kujikuta juu ya kifua cha mwamba 🥰 nilishtuka walah kidogo nikimbie ila nilishangaa zaidi baada ya kujikuta ndani ya gari
Inamaa usiku wa jana huba lilituzidia sana mpaka tukajikuta tukalala ndani ya gari, kuna namna nilifurahi ila nilipokumbuka kuwa huyu mkaka anapendwa na wadada wengi
Nikamsukuma huko kwa kumkanyaga na teke kwenye kifua 😅, aaah niseme tu ukweli huyu kaka akitoka kuamka anakuwa mzuri hatari 🥰, badala ya kuendelea kumkanyaga nikajikuta nabaki kumshangaa
Kile kifua chake sasa na zile Sixpack zilinipagawisha mimi 🥰
"Mbona unanishangaa hivyo..??"
Aliniuliza, ndio nikakurupuka sasa baada ya pepo la uzinzi kunitoka,, ndio hapo kidogo fikra zikanijia kuhusu usiku wa jana bwana
Yani usiku wa jana ulikuwa usiku wa malove love, hamuwezi amini ndugu zangu usiku huo ndio usiku ambao mimi na Anfrey tulivunja amri ya sita tena kwennye gari wazinifu sie
Mira mimi nilichakazwa haswa😅 sema tu kilichonisaidia ni kwammba sikuwa bikra, mnashangaa nini bikra yangu ilitolewa kitambo sana na ex wangu
Huyu mwanaume popote ulipo ulaaniwe wewe na ukoo wako wote maana ulikuja kwenye maisha yangu na kuchukua bikra yangu, haya sasa nitamwambia nini huyu mwarabu
Unajua kiasi gani huyu mwarabu ataniona mimi matako yake 😅 popote ulipo wewe Gerald nakuapia nikikushika natoka na .......
Basi siku hiyo bwana ndio siku ambayo sitaisahau kabisa kwenye maisha yangu maana maisha yangu yalibadilika kwa kiasi kikubwa sana
Hamuwezi amini ndugu zangu, yale ambayo nilikuwa nikimuomba mungu kwa mida mrefu sana aliyatimiza, amini tu yale ambayo unamuomba mungu wako na mungu anakufanyia siku ambayo hitegemei kabisa
Yani anafanya kitu kuwa kama surprise kwako, ninachokuambia ndugu yangu mtumaini mungu kwa kila hatua unayoipiga na pia usache kumshukuru kwa kile kidogo unachokipata
Hamuwezi amini jamani maisha yangu yalibadilika, maisha yangu yalikuwa yenye furaha tele pamoja na mume wangu kipenzi ANFREY ambaye mwanzo nilimkataa
Hii ni kali walahi, yani mwanaume nilimkataa lakini leo hii anakuja kuwa baba watoto wangu nyiee....
ITAENDELEA........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni