REGINA(1);Habarini jamani, naomba niwasimulie na mimi kisa changu,Vivian kanikumbusha story ambayo huwa siipendi kiukweli
Mimi ni mtoto wa kwanza kwa mama yangu,ambapo tumezaliwa watoto wawili tu lakini kwa baba yangu tupo wengi. Mama yangu na baba hawakuoana,Mimi nililelewa na mama,baadae nikapelekwa kwa bibi,bibi yangu alikua anaishi kijijini na mama yangu alikua anaishi mjini. Baba yangu pia alikua anaishi sehem nyingine mjini lakini wote ni mkoa mmoja. Nikaanza shule,namshukuru Mungu darasani nilikua vizuri,ikifika likizo nilikua naenda kwa mama.
kama mnavyojua maisha ya kijijini yalivyo,basi ninapotoka kule kwa mama alikua anahakikisha ananinunulia kila kitu Cha shule na nilikua msafi kweli,wengine walikua wakienda peku shule lakini mie nilikua naenda nimevaa viatu,begi safi,kwetu tunakunywa chai na bibi yangu anaongea kiswahili maana alikuaga mtanga ikiwa Kijiji kizima wanaongea kilugha. Ilikua ikifika Ile saa sita muda wa kwenda kula,mashost wanataka twende pamoja nyumban kwetu.
Maisha yakaenda mara pap nikaingia darasa la sita si nikavunja ungo hee na hivyo nilikua nishasoma darasani kwenye sayansi nikaona kumwambia bibi yangu sio kweli,nikakausha, nikamwambia shost angu mmoja ye alikua ashavunja ungo muda,akanielekeza pale nikaelewa maisha yakaenda. Tulipofungua shule Ile mwezi wa 7 kuna mwalimu mgeni akawa amehanishiwa pale shule.
Sasa ikawa kila mwanafunzi anamuongelea yule mwalimu na kwa kipindi hicho darasa la sita na la saba walikuaga ni wakubwa kweli na wengi wao mambo ya kikubwa walikua wanayajua vizuri sana. Sasa ikawa darasa la sita kwa darasa la saba wote wanajigonga kwa yule mwalimu,kwa muda ule kila mtu alikua anamuona ni bonge la handsome boy(sijui ni ujinga au ni nini ila kiuhalisia hana uhandsome wowoteππ)nahisi na ule ushamba wa kijijini ndio maana tulikua tunamuona handsome boy.
Sasa kama mnavyojua watanga wanavyopenda kupika,bibi yangu alikua anasifika sana kwa kujua kupika,hivyo shuleni kukiwa na mitihani walimu wakawa wananichagua mie nikasaidiane nao kupika wakiamini na mimi najua kupika ππkumbe hamna kitu na muda huo balehe ilikua inanisumbua aweee nikiambiwa kaa hapa ufundishwe kupika kwani nakubali Sasa,nikawa namjibu vibaya bibi angu(nilishatubu).
Tukawa tumepika pale tumemaliza,muda napeleka chakula saa ngapi yule mwalimu asiniibukie eti jitahidi baadae tuonane,mi nikamjibu tu sawa,nikapeleka chakula,walimu wakala walipomaliza tukaosha vyombo na muda wa kwenda nyumban ukafika mi wala 9sikwenda. Nikaenda zangu home. Kesho yake tena kulikua na mitihani ndio wanamalizia,hivyo nikawa busy na kupika sikuonana na yule mwalimu.
Siku iliyofuata tukaonana akaanza kulalamika kwanini juzi aliniita mie sikwenda,kipindi hicho nilikua na aibu sanaπβΊοΈsiwezi kumuangalia mtu usoni hata kujitetea siwezi,akawa ana force niongee,mi siwezi,akaniambia jitahidi utafute muda tuonane mi nikamjibu tu sawa Ili mjadala usiwe mrefu ila kimoyomoyo nikawa nasema wala siwezi.
Yule mwalimu alikua anafundisha math's nyiee kama mnavyojua math ilivyo ngumu vile kumbe akawa kaniwekea kisasi sijui nisemeππikawa anatoa zoezi gumu jaman karibu kila siku,Kuna wale wanaokuaga 10 bora lazima upate β΄β΅/β΅β° kwenda juu chini ya hapo ni fimbo. Mie mwenzenu nikawa kila zoezi lake napata chini ya 45, nilikua napigwa mpaka sio poaππ
fimbo za mgongo yaani ovyo ovyo tu mpaka wanafunzi wengine wakawa wanauliza shida ni nini,mi nikawa nawajibu kuwa hata mimi mwenyewe sijui sababu,niliteseka mno hicho kipindi,nilipitia wakati mgumu mpaka basi,ikafika muda nikawa nataman aje arudie kuniambia nikipata muda nimtafute tuongee,nae akawa hata hasemiππππni mwendo wa viboko tu mpaka nikome sitii wito wa mwalimu
Itaendelea .....kupangilia maneno kazi uwiii
#funzomedia
USISAHAU KU LIKE HAPO ILI IWE RAHISI KUPATA MUENDELEZO ππ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni