Kodi na Tozo za Serikali
Hii ndiyo sababu kubwa zaidi ya magari kuwa ghali Tanzania:
Kodi ya Forodha (Import Duty) β Hii ni asilimia ya thamani ya gari (CIF value).
VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani)
Excise Duty β Kodi hii hutegemea aina ya gari, ukubwa wa injini na umri wake.
Other fees: EWURA, TBS, na road safety fees.
Mfano:
Ukileta gari lililonunuliwa kwa USD 3,000, unaweza kulipa kodi zaidi ya milioni 6 hadi 8 TZS kutegemeana na umri wa gari na engine capacity.
Gharama za Usafirishaji (Shipping Costs)
Gari linahitaji kusafirishwa kutoka Ulaya hadi bandari ya Dar es Salaam.
Gharama hizi ni kati ya USD 1,000 hadi 2,000 au zaidi kutegemeana na umbali na kampuni ya usafirishaji na ukubwa wa gari.
Pia kuna handling fees, clearing agent charges, n.k.
Utaratibu wa Bandari (Clearing & Delays)
Mchakato wa ku-clear magari bandarini unaweza kuwa mrefu na wenye gharama za ziada kama demurrage fees (gharama kwa kuchelewa kuchukua gari).
Watu wengi hutumia agents nao huongeza gharama.
Kupanda kwa Thamani ya Dola (USD)
Magari hununuliwa kwa dola lakini watu hulipa kwa TZS.
Dola ikipanda thamani dhidi ya shilingi hata gari la bei ya kawaida linaonekana ghali.
Tofauti za Kibiashara
Magari mengi Ulaya yanauzwa kwa sababu ya depreciation au kwa kuwa yameanza kuzeeka, hivyo ni nafuu.
Wauzaji nchini Tanzania huongeza faida yao (profit margin) baada ya gharama zote na hiyo pia huongeza bei ya mwisho.
Umri wa Gari (Age Restrictions)
Tanzania hairuhusu magari yenye umri zaidi ya miaka 10 kuingizwa bila adhabu ya ziada. Magari ya zamani hulipiwa kodi kubwa zaidi (penalty).
@highlight
Kwa Ufupi:> Magari ni nafuu Ulaya kwa sababu hayajatozwa kodi. Yanafika Tanzania, bei inapanda kwa sababu ya kodi za forodha, VAT, excise duty, usafirishaji, mfumuko wa bei, na ada mbalimbali za bandari.
(Kwa majirani huko kwenu vipi?)
Hizo ni moja ya sababu,kama kuna nyingine unaijua sema apa chini,elimu haina mwisho..