Menu






Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo

Simulizi : Mke Wangu Nusu Jini, Nusu Mtu   Sehemu Ya Kwanza (1)  IMEANDIKWA NA : ALLY MBETU   Niliwahi kujiuliza kama iko siku na mimi nitapata nafasi ya kusimulia popote
Gonga94 · Stories

Simulizi : Mke Wangu Nusu Jini, Nusu Mtu Sehemu Ya Kwanza (1) IMEANDIKWA NA : ALLY MBETU Niliwahi kujiuliza kama iko siku na mimi nitapata nafasi ya kusimulia popote

Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
pale mkasa uliowahi kunikumba miaka ya nyuma. Ni kuhusu mke wangu niliyefunga naye ndoa ya serikali. Nilibaini kwamba alikuwa mtu lakini pia alikuwa jini kwa sababu mbalimbali, anasema Abigaeli, mkazi wa Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Anaendelea: Siku ya kwanza kukutana na mke wangu ilikuwa kwenye kikao cha kupokea mahari ya mtoto wa kaka yangu aliyekuwa anataka kuolewa na Msambaa mmoja kutoka Lushoto, Tanga. Ilikuwa mwaka 2002.

Kuna kitu kilitokea kwenye kikao hicho na kama ningekuwa makini, nisingeingia kwenye matatizo makubwa yaliyowahi kunipata katika maisha yangu.

MSICHANA MREMBO ANAOMBA NAMBA

Kitu hicho ni kwamba, baada ya kikao, msichana mrembo ambaye alikuja kuwa mke wangu alinifuata na kuniomba namba zangu za simu, nikamtajia, akaziingiza kwenye simu yake.

Alipoondoka, baadhi ya ndugu tuliokuwa pale tuliulizana yule msichana ni nani. Hakuna aliyekuwa na jibu. Bahati nzuri ndugu mmoja wa upande wa wanaume waliyoleta mahari alikuwa hajaondoka, tukamuuliza kama walikuja na msichana yule, akakataa kutomtambua tena huku akisisitiza kwamba, walikuja kumi tu na yeye ndiye alibaki kumalizia mambo mengine.

Kaka aliniuliza aliponifuata kuniomba namba ya simu alisema anatokea upande gani katika tukio lile, nikamwambia kwa waleta mahari.

Nilianza kuingiwa na wasiwasi mkubwa, niliwaza mengi. Kaka alinilaumu akiniambia kwamba siku nyingine nisikubali mawasiliano na watu ambao hawajulikani sawasawa. Lakini nilijitetea kwa kusema mtu kusema kaja na watu wengine ambao kweli walikuwepo sidhani kama unaweza kumtilia shaka.

WIKI MOJA MBELE

Wiki moja baada ya tukio hilo la kuombwa namba, nilipigiwa simu na mtu aliyedai kuwa yeye ndiye yule msichana, akasema anaitwa Munil.

Alisema amenipigia simu ili kunijulisha kwamba, yule mchumba aliyekuja kutoa mahari kwa kaka amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea nusu saa iliyopita.

Nilishtuka sana kusikia taarifa hizo kwani zilikuwa za ghafla sana kwangu. Lakini jambo jingine sasa, niliamini yule msichana ni ndugu na wale walioleta mahari ila pengine yule mtu wa mwisho hakumjua tu.

Nilimshukuru kwa taarifa kisha akakata simu. Nikampigia kaka kumuuliza kama analijua hilo, naye alishtuka, akasema hajasikia, akaomba nimpe dakika tano tu ahakikishe kwa ndugu wengine halafu atanirudia. Lakini kaka hakuniuliza nilikozitoa habari zile.

Baada ya dakika tano kweli kaka alinipigia, akasema hakuna ndugu hata mmoja aliyesema kama ni tukio la kweli. Akasema amepiga simu ya mhusika mwenyewe anayedaiwa kupata ajali, haipo hewani.

MSICHANA AMTATIZA KAKA

Niliendelea na shughuli zangu, nusu saa mbele kaka akanipigia tena na kuniuliza zile habari aliniambia nani, maana hata huyo binti wa kaka aliyekuwa anataka kuolewa, alipopigiwa simu alisema hajui na inaweza kuwa habari za uongo ingawa na yeye alipompigia simu huyo mchumba wake hakumpata.

Nilipata wakati mgumu sana kumwambia kaka kwamba aliyenijulisha ni yule msichana kwani alishanionya kutofanya mawasiliano na watu nisiowajua. Lakini ningemtaja nani sasa.

Ilibidi nimwambie ukweli, kaka akashtuka. Akasema:

Hivi huyo msichana ni wa kivipi kwanza? Yaani taarifa apate yeye, wengine wasijue? Au kamgonga yeye?

Mimi sijui kaka, lakini yeye ndiye kanipigia simu, nilimjibu.

Mara, kaka akasema anapokea simu nyingine inaingia kwake atanipigia.

Zilipita dakika kumi nzima, kaka akapiga na kuniambia habari za mchumba wa binti yetu kufa katika ajali ya gari ni za kweli na maiti ipo katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha.

MAUZAUZA KWA MBALI

Nilishtuka sana, nikamuuliza kama anakwenda hospitalini, akasema anakwenda ukweni kwake ambako kutakuwa na kikao kifupi na mimi nikaondoka kwenda huko kwenye kikao. Nikiwa pale, nilitarajia sana kumwona yule msichana lakini kila nilipoangaza macho sikumwona, nikaamua kumpigia simu, akapokea ndani ya sekunde mbili tu baada ya kuita, akasema:

Nakuona hapo.

Niligeuka kulia, kushoto, mbele, nyuma lakini sikumwona. Nikamuuliza uko kwa wapi kwani, akasema yupo kwa ndani kisha akakata simu. Sasa nikajiuliza, kama yupo kwa ndani ananionaje? Nikampigia tena, akapokea haraka sana kama mwanzo, nikamuuliza:

Kama kweli umeniona nimevaaje? Mimi nahisi hujaniona ila unabashiri tu.

Si wewe umesimama, umevaa shati jeusi na suruali nyeupe.

Nikakata simu kwani ni kweli nilikuwa nimevaa nguo hizo. Safari hii nilipokata akanipigia yeye, nikapokea huku nikisema moyoni huyu mwanamke ni jini nini? Mbona kama simwelewielewi?

"Haloo," aliita.

"Haloo," nilisema.

"Mbona una wasiwasi na mimi. Mimi si jini bwana, ni binadamu mzuri tu," kisha akakata simu.

Kwangu ulikuwa mtihani mkubwa. Kwa nini aseme yeye si jini wakati mimi nilikuwa nawaza hivyo?

"Hapana, wala sina wasiwasi na wewe. Ila nashangaa unasema unaniona mimi sikuoni halafu unasema unaniona ukiwa kwa ndani. Sasa unanionaje?

"Nilikuwa nakuona kwenye dirisha lakini sasa nakuona sawasawa maana nimetoka nje.

Niliangalia mlangoni nikamwona kweli akiwa anawaka kwa uzuri wake, mweupe pee! Kama Mwarabu. Alionekana kuwa tofauti na wengine pale.

Wakati yote hayo yanatendeka, watu walikuwa wakilia sana. Hata mimi niliweza kuongea na simu kwa sababu nilisimama mbali kidogo na watu walikuwa wakiendelea kumiminika eneo hilo la msiba, hasa wanawake.

"Nimekuona sasa Munil. Da! Umependeza sana leo," nilimwambia.

"Kweli ee?"

"Kweli kabisa. Da! Yaani, una mvuto we mtoto wa kisasa," sasa nilikuwa katika hali ya kimahaba maana hata sauti yangu iliashiria hivyo. Na yeye alionekana kupenda kuendelea kuzungumza na mimi huku sauti yake tamu ikirindima masikioni mwangu.

Kikao kilikuwa kikiendelea, mimi nikaenda kusimama mbali zaidi huku nikiendelea kuongea na Munil ambaye sasa naye alizidisha maneno ya mahaba kwangu. Lakini ghafla nilijikuta namuuliza swali nje ya mazungumzo yetu:

"Hivi Munil, huyo kijana aliyefariki dunia kwa ajali wewe ni nani yake?"

"Mtoto wa shangazi," Munil alinijibu kwa haraka sana kuonesha kwamba hakuwa na wasiwasi na alichokisema, nikaamini lakini kichwani yakaja mawazo mawili tofauti, kama kweli ni mtoto wa shangazi yake mbona amevaa vizuri sana yeye halafu ni kwa nini siku ya kutoa mahari, ndugu mmoja alisema hamjui?

"Umenielewa Abigaeli?"

Nilishtuka sana kujua kwamba Munil analijua hadi jina langu kwani katika mazungumzo yetu sijawahi kumwambia ila la kwake alinitajia mwenyewe.

"Kumbe unalijua jina langu?"

"Si nililisikia siku ile ya kutoa mahari."

"Ooo! Sawa," nilisema kwa kujibalaguza tu lakini kila nilipofikiria moyoni sikukumbuka kama siku ile kuna mahali jina langu lilitajwa kwa namna yoyote ile.

Oke, basi baadaye," alisema Munil na kukata simu.

Wakati naongea nilikuwa naangalia upande wa barabara watu wanapotokea, kwa hiyo msiba niliupa mgongo.

Nilipogeuka kuangalia kama nitamwona Munil, sikumwona nikajua alirudi ndani.

Nilitembea kurudi msibani lakini mawazo yangu yote yalikuwa kwa Munil.

"Mtoto mzuri sana tena sana. Ameumbika kwelikweli. Sijui ana jamaa yake? Anafaa kupigwa ndoa," nilisema moyoni mwenyewe huku nikiwa nakaa.

Ile namalizia kukaa tu, meseji ikaingia kwenye simu yangu, moyoni nikasema siyo Munil huyo?

"Abigaeli nakupenda sana, naamini kuwa na wewe ni furaha ya maisha yangu."

Wakati nasoma meseji hiyo mwili ulikuwa ukinisisimka na kuhamishia mawazo yangu kutoka pale hadi kitandani. Nikamjibu haraka sana:

"Mimi ndiyo naamini nitakuwa na furaha zaidi yako kwani nimetokea kukupenda sana Munil. Tutafute muda tuongee basi, sawa mpenzi?"

"Sawa sweetheart wangu, utaniambia basi," alinijibu kwa maneno ya mahaba nikazidi kuchanganyikiwa. Nilitamani kuaga palepale ili niondoke nikakae mahali halafu nimwite Munil aje tuzungumze kwa kupanga mambo yetu, hasa kuhusu mustakabali wake na wangu, namaanisha ndoa!

NALISHANGAA HILI NALO

Nikiwa nimetulia nikaamua kuisevu namba ya Munil kwani sikuwa nimeisevu, cha ajabu nilipokwenda kwenye eneo la kusevu nikaambia tayari jina hilo lipo mwenye simu yangu, nikafuatilia na kubaini jina la Munil One!

"Mh!" niliguna kwanza. Nilikataa kichwani kwamba sijawahi kusevu namba ya Munil kwenye simu yangu, nilikuwa nimeishika namba yake kichwani. Nikawaza.

"Munil One Munil One? hapana, sijasevu namba kama hii kwenye simu yangu," niliendelea kuwaza na kujiridhisha kwamba hakuna kitu kama hicho.

"Kuna kitu kinaendelea kwa Munil," nilisema mwenyewe moyoni.

Kama ndiye aliyenitoa kwenye mawazo, akaniambia tuondoke kwa muda tutarudi baadaye. Nilitamani kumwambia atangulie nitamfuata baadaye maana nilitaka kukutana na Munil kwanza ili tumalize mambo yetu.

Hata hivyo, nilishindwa kutumia ujanja wowote, tukaondoka na kaka huku njiani akisema sisi ni wakwe pale kwa hiyo si lazima tujishirikishe sana lakini baadaye tungerudi tena.

Mbele kwa mbele nilikwenda kuachana na kaka, mimi nikakatiza mitaa na kutokea kwenye Baa ya Kontena

ambako nilikaa kwenye kona na kumtumia meseji Munil ili kama anaweza aje pale. Meseji niliiandika hivi:

"Mpenzi, kama unaweza njoo hapa kwenye Baa ya Kontena."

Nilishtuka sana meseji ilipomfikia kwangu ikaandika Munil Only!! Badala ya Munil One!

"Ha! Nooo! Kuna kitu, inawezekanaje kwanza?" nilijiuliza. Kama kuna mtu aliyeniona sura muda huo aligundua kuna jambo la kushtua limenipata.

"Nakuja mpenzi wangu," Munil alinijibu bila kuniuliza hiyo baa iko wapi! Lakini hilo halikunishangaza sana kwani kwa mji mdogo kama wa Kibaha sidhani kama ni ishu kubwa.

Ilikuwa ndani ya dakika tano tu, Munil aliingia kwenye baa hiyo akiwa amebadili nguo. Alivaa gauni nyeupe, refu hadi kufunika miguu wakati awali alivaa gauni jekundu pia refu!

Alikuja moja kwa moja nilipokaa mimi kwenye meza ya peke yangu, akanibusu kwanza kisha akavuta kiti na kukaa huku akiniangalia kwa uso uliojaa tabasamu laini. Kwa mara ya kwanza mimi na Munil tulikaa pamoja hapo kwenye baa.

Nilianza kuhisi ni mwanamke wa tofauti sana kwani walio wengi hawapendi kukaa baa, hasa kwa mwonekano wake wa kiimani. Hakuwahi kuniambia wa imani gani lakini jina lake, Munil lilitosheleza kunijulisha yeye ni nani.Kwa hiyo kuja kwake baa niliamini kulitokana na upendo wake kwangu ambao ulitimilika. Nilifurahi sana maana hata wakati anakaa hakutoa kauli ya kuashiria kwamba hapendi kukaa baa.

SWALI LA KWANZA KWA MUNIL

"Munil sikumbuki kama nimewahi kuisevu namba yako, lakini ghafla kwenye simu yangu imeonekana kuseviwa kwa jina la Munil One halafu sasa Munil Only, ni nini kimetokea mama?"

Wakati namuuliza hivyo Munil nilimkazia macho nikiamini ataogopa kama anajua mchezo lakini wala!

Aliniangalia kawaida na nilipomaliza akaachia tabasamu lakini huku akisema:

"Jamani, mimi ndiyo nikuulize wewe mwenye simu lakini wewe ndiyo unaniuliza mimi. Mimi mwenyewe mfano simu yangu, namba unaweza kuisevu kabisa lakini ukinipigia badala ya kutokea jina zinaonekana namba tu. Kuhusu kusevu inawezekana ulinisevu ila umepitiwa na kumbukumbu, mbona hilo ni suala la kawaida sana baba."

Munil alivyoniita baba, nilifurahi sana. Nilijiona mimi ndiyo mimi hakuna mwingine duniani. Munil alikuwa msichana mzuri sijapata kuona tangu nimezaliwa. Hata alipoingia pale baa alitazamwa na kila mtu.

Kuhusu alilolisema la simu, nilikumbuka tatizo lake hata kaka analo kwenye simu yake, anasevu jina lakini zinatokea namba kwa hiyo kaka kila akipigiwa simu huwa na kazi ya kumuuliza mpigaji, nani mwenzangu? Nikaamini kuwa huenda ni matatizo ya simu yangu.

Niliyafanya mambo hayo yawe yameisha, akaagiza soda kama nilivyofanya mimi. Lakini pia akataka na sambusa mbili kwa kumwambia mhudumu.Wakati tunakunywa huku yeye akisubiri sambusa zake, mimi nilihisi muda umekwenda na anaweza kumaliza soda yake bila kinywaji kuletwa kwa hiyo nikamuhimiza mhudumu aharakishe.

"Usijali baba, nitakwenda mimi mwenyewe," alisema Munil, mimi nikainama kuangalia meseji kwenye simu yangu, kuinua kichwa nikaona sambusa kwenye kisahani cha chai, nikashtuka."Nani kaleta?" niliuliza. Kisa cha kuuliza ni kwa sababu kuinamisha kwangu kichwa chini kusoma meseji na kuinua ilikuwa ndani ya sekunde kama kumi tu, halafu nilipoona hiyo sahani sikumwona mhudumu akiondoka kwenye meza yetu na wala sikumwona Munil akirudi kuja kukaa.

Kwa wakati ule haikuwa rahisi kusema yote, lakini baada ya kuyapitia yaliyotokea ndiyo maana nayasema haya kwani niligundua baadaye sana kwamba nilikuwa nimepatikana kwa mke wangu ambaye alikuwa nusu ni mtu, nusu ni jini kamili.

Nilipata wakati mgumu sana kuwaza kuhusu sambusa, Munil aliniambia amezifuata yeye lakini kusema ule ukweli hakuzileta yeye na wala hazikuletwa na mhudumu wa baa ile. Nilinyamaza tu lakini akili ikiendelea kuchangamka kuwaza.

"Baba," aliniita Munil baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.

"Niambie mama."

"Utakwenda kuzika?"

"Kwani mwili unakwenda kuzikwa wapi?"

"Lushoto."

"Itabidi niende sijui? We unasemaje?"

"Twende wote."

"We utaenda?"

"Mimi tena, yaani ndugu halafu nikose?!"

"Basi na mimi nitaongozana na wewe."

"Sawasawa."

Kitu gani kilichoendelea….

Usikose sehemu inayofuata
Jamani twende chapu , bonyeza LIKE-150 sasa hivi ili nipost nyingine chapu chapu .

Maoni

You're not logged in


Tangazo - Elton John - Sacrifice
Elton John - Sacrifice
Elton John - Sacrifice
Elton John - Sacrifice
Sikiliza Wimbo Kamili
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Simulizi : Mke Wangu Nusu Jini, Nusu Mtu Sehemu Ya Kwanza (1) IMEANDIKWA NA : ALLY MBETU Niliwahi kujiuliza kama iko siku na mimi nitapata nafasi ya kusimulia popote

pale mkasa uliowahi kunikumba miaka ya nyuma. Ni kuhusu mke wangu niliyefunga naye ndoa ya serikali. Nilibaini kwamba alikuwa mtu lakini pia alikuwa jini kwa sababu mbalimbali, anasema Abigaeli, mkazi wa Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Anaendelea: Siku ya kwanza kukutana na mke wangu ilikuwa kwenye kikao cha kupokea mahari ya mtoto wa kaka yangu aliyekuwa anataka kuolewa na Msambaa mmoja kutoka Lushoto, Tanga. Ilikuwa mwaka 2002.

Kuna kitu kilitokea kwenye kikao hicho na kama ningekuwa makini, nisingeingia kwenye matatizo makubwa yaliyowahi kunipata katika maisha yangu.

MSICHANA MREMBO ANAOMBA NAMBA

Kitu hicho ni kwamba, baada ya kikao, msichana mrembo ambaye alikuja kuwa mke wangu...

👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/simulizi-mke-wangu-nusu-jini-nusu-mtu-sehemu-ya-kwanza-1-imeandikwa-na-ally-mbetu-niliwahi-kujiuliza

#Nk #gonga94 #trending #simulizi #hadithi #viral #fictionwriter
#ShortDrama

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi simulizi-mke-wangu-nusu-jini-nusu-mtu-sehemu-ya-kwanza
Tafuta Simulizi,Hadithi,Michezo
Andika unacho taka.

Top 10 Kali za Leo

 *AAAAAASH BOSS ENZO* *SEASON TWO*   *15&16*

*AAAAAASH BOSS ENZO* *SEASON TWO* *15&16*

793
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 16 na 17

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 16 na 17

570
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 18

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 18

481
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 19.na 20

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 19.na 20

329
CEO USINIVUE MI MCHUMBA WA MTU* * *16&17*

CEO USINIVUE MI MCHUMBA WA MTU* * *16&17*

292
SHAMIRA sehemu ya 36&37

SHAMIRA sehemu ya 36&37

185
BLACK BUTTERFLY 🦋 5

BLACK BUTTERFLY 🦋 5

89
Some Bollywood families just have that star vibe, and Dimple Kapadia and her daughters are a perfect example

Some Bollywood families just have that star vibe, and Dimple Kapadia and her daughters are a perfect example

3

ZIMESOMWA ZAIDI

‎TUNDA LA  DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

‎TUNDA LA DADA ‎ ‎SEHEMU YA KWANZA

11.49K
RUNGU LA KIPOFU 22.

RUNGU LA KIPOFU 22.

7.25K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tisa.  👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tisa. 👉 Akaanza kunipamp sasa...👇

3.76K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya sita.  👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇  Shemeji inauma utanichana.

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..6..10 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya sita. 👉 Aaaaaaaaa chomoa...👇 Shemeji inauma utanichana.

3.22K
MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

MY WANGU❤️ sehemu ya 119 na 120.

2.65K
 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 20.  👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 20. 👉 Nikatanua mwenyewe miguu manuu..kazi kwake tu...👇

2.62K
MY WANGU❤️ sehemu ya 108

MY WANGU❤️ sehemu ya 108

2.57K
MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

MY WANGU❤️ sehemu ya 106 na 107

2.52K
🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20  KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥  Sehemu ya 16.  👉 nakupenda pia...👇

🔥 UTANI WA SHEMEJI KAICHOMEKA..16..20 KWELI...Aaaaaaaaa chomoa🔥 Sehemu ya 16. 👉 nakupenda pia...👇

2.46K
🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥  sehemu ya tatu.  👉 Sitaki sitaki mimi mdogo niache sitaki...👇

🙄 NILIONA MWENYEWE DADA YANGU ANAGEUZWA🔥 sehemu ya tatu. 👉 Sitaki sitaki mimi mdogo niache sitaki...👇

2.46K

RATIBA ZA MAKALA ZETU

Hakuna Ratiba kwa sasa

Machapisho Mapya
Vijipost vilivyotangazwa karibuni (yamekatwa hadi maneno 30)
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 19.na 20 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 19.na 20
@majario LIVE

Nikasema zena kweli ,na wew unafeel kama vile ambavyo mm nafeel acha masihara basi, akanambia lakini millan ,mi wewe sikujuhi vizur, ndo mana nilikuwa nataka mda kwanza wa kukufahamu ,nisije...

BLACK BUTTERFLY 🦋 5 Post Mpya
BLACK BUTTERFLY 🦋 5
@majario LIVE

By Babie Love Tsap 0742133100 ENDELEAAA “ Brayton..” Camilla alijikuta akimuita bila kutarajiaa Brayton alimsogeleaa na kumuonyeshaa zile picha vizur tu kwenye simu yakee huku akimuulizaa “ Unawezaa kuniambia hiki nini?!?” Camilla alishangaa kwa...

Some Bollywood families just have that star vibe, and Dimple Kapadia and her daughters are a perfect example Post Mpya
Some Bollywood families just have that star vibe, and Dimple Kapadia and her daughters are a perfect example
@majario LIVE

. Dimple became a sensation with Bobby, and the same year she married superstar Rajesh Khanna. She was only 16 when she got married and became a mom at 17...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 18 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 18
@majario LIVE

Yani ummy Alishangilia na kwambia aliimba nyimbo zote mpaka mama yake ndo alimnyamazisha, basi nikamwambia ummy aya mama yangu mzuri nimekuletea tv sasa uwe na amani sawa, akasema ndio...

CEO USINIVUE MI MCHUMBA WA MTU* * *16&17* Post Mpya
CEO USINIVUE MI MCHUMBA WA MTU* * *16&17*
@majario LIVE

Sikujua kam nililala pale mpaka asubuhi, tena nimelala kana kwamba pale ni nyumbani kwetu jamni nilikuja kushtuka tena baada ya kupigiwa simu, jamni si ndio naamka najikuta nipo kwenye chumba...

AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 16 na 17 Post Mpya
AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 16 na 17
@majario LIVE

Mwandiishi; LISSA Basi nilifika home nna hasira sana, nimechukia mnoo, yote sababu nilikuwa nimemmaind sana yule demu, yani nilimuona ana linga kinoma, nikasema bwana mi namkaushia kama.vp mana wanawake...

 *AAAAAASH BOSS ENZO* *SEASON TWO*   *15&16* Post Mpya
*AAAAAASH BOSS ENZO* *SEASON TWO* *15&16*
@majario LIVE

Nikatulia kwanza na kumuangalia madam groly kisha nikamuuliza. "Unamaanisha nini unavyosema hauna Furaha na hii siku 7 Sijakuelewa kwakweli nakumbuka ulikuwa ukitsubilia hi siku kwa hamu sana" Madam groly akacheka sana kisha akasogea...

SHAMIRA sehemu ya 36&37 Post Mpya
SHAMIRA sehemu ya 36&37
@majario LIVE

Wassap:0742443214 Mwandishi; lissa wa huru media Basi mwanaume akaondoka zake na mimi ndo nikashika simu sasa .nikampigia aisha kumpa mchapo.nikasema shoga nusu niachwe mwenzio.nimeomba msamaha kama chizi.aisha akasema mh tatizo hamadi...

BLACK BUTTERFLY 🦋 4 Post Mpya
BLACK BUTTERFLY 🦋 4
@majario LIVE

By Babie Love Tsap 0742133100 Endelea Brayton akiwa kwenye gari alijaribuu kupiga simu Hospitali ili maandilizi mapema kwaajili ya mgonjwa anae kuja nae muda huu. Hospitali nayo hakufanya makosa tayari waliandaa kitanda...

FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 21 Post Mpya
FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 21
@majario LIVE

Nikamuuliza "we umejuana vipi na D??" "Yule D ni mdogo wake na Boss wangu, ni binamu yake kitu kama hicho, mie sijawahi hata kuwa na mazoea nae kabisaaa ila kuna issue...

Honestly, these two are such a vibe together !  Priyanka Chopra and Nick Jonas Post Mpya
Honestly, these two are such a vibe together ! Priyanka Chopra and Nick Jonas
@majario LIVE

really make you believe in modern-day love stories. Different countries, different cultures, totally different careers — but somehow it all just fits perfectly. What started with a simple conversation...

*AAAAAASH BOSS ENZO* *SEASON TWO*    *SEHEMU YA KUMI NA NNE* Post Mpya
*AAAAAASH BOSS ENZO* *SEASON TWO* *SEHEMU YA KUMI NA NNE*
@majario LIVE

Muda huo Mwenyewe nilikua Nacheza kwa Furaha zote, lakini kitendo cha kumuona madam groly killharibu kila kitu, niliona kabisa birthday yangu inaenda kuharibika Maana huyu mama hana jema ata kidogo. "NAKUJA Alizungumza...

*AAAAAASH BOSS ENZO* *SEASON TWO* *12&13* Post Mpya
*AAAAAASH BOSS ENZO* *SEASON TWO* *12&13*
@majario LIVE

SONGA NAYO Nikageuka na kumuangalia ma Mdogo "Ishani umeolewa Mwanangu?" Nikamuangalia na kumwambia. "Mind your business bi mkubwa Kisha Mimi na Enzo tukaondoka kwani tayall tulishabolt Bajaji na ilikuwa ikitusubilla. Msijiulize Kwanini tunatuma Bajaji wakati Enzo...

FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 20 Post Mpya
FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 20
@majario LIVE

Lile joto la midomo yake ilipo gusana niliisi ulimwengu wote umenyamaza nikafumba macho Kulikuwa na joto la ajabu sijawahi kulipata Mkono wake alikuwa anaupitisha taratibu kama anahesabu kila pigo la moyo wangu,...

FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 19 Post Mpya
FROM BANGI TO BABY 💞💘 SEHEMU YA 19
@majario LIVE

Basi mpaka sa moja inaenda na Nusu Veda hajaja, Moyo juu juu itakuwa tu kaenda huko kwenye ma club, moyo lipu lipu muda wote kama nimemezaa kaa la moto hajabu...

Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest