*1- - - - - - - - 5* ๐๐๐ช๐ฌ๐๐ฅ ๐ก๐๐จ๐ ๐๐ ๐ ๐ช๐๐ก๐ญ๐๐ข ___________________________________ SEHEMU YA 1 "Kwahyo huyo mwanaume unamlilia wa nini sasa wakati ni kweli kashakuacha tayri, na bora
Sasa kaka yangu na yey yupo huko polisi ni kam wiki mbili sasa na kesi yake lazima ipelekwe mahakamani maana ni kwenye kampuni yao huko wanayofanyia kazi ni kampuni ya kutengeneza furniture na boss wake alisema kwamba kuna mali zimepotea na anahusika na ulinzi ni kaka hivyo kaipeleka kesi mahakamani na bado haijasikilizwa kwa sababu bado hatujapata mwanasheriaa kwenye hili jambo na tumepewa siku moja tukamilishe hili , na tunawaza hizo pesa za kumpatia huyo mwanasheria tunazitoa wapi na kaka kasema nisimwambie Mama wala mkewe kwasababu kaka ameoa na mkewe anamimba kubwa tu , hataki apate presha at least tungewaambiaa wazazi tungepata msaada hat wa kifedha kwa ajili ya kumpatia huyo mwanasheria wa kusimamia hii kesi , ila kak hakutaka na alinambia mimi kingine kinachoniwazisha ni kwamba kama kaka yangu hatopata mwanasheria maana yake ni kwamba atahukumiwa kwa upande mmoja na atafungwa tu jamni ,hapo namuwazia wifi kila siku namuongopeaa tu kwamba kaka kasafiri kaenda kupeleka furniture huko vijijini ndio maan hapatikani kabisa
"Mhh jamn wenzako wanakuwaga wanawapa pesa hao wanasheria sasa sisi tutafanyaje shoga yangu, au kaongee na Mama Rahel akukopeshe atakukata kwenye mshahara wako" nilimtizama tuu huyu Fatma maan na yeye nafanya nae kazi hapo dukani "kwa mshahara gani hio laki tatu na nusu ?, umesahau kama juzi juzi tu hapa nimetoka kumkopa laki tatu kwa ajili ya kodi kwahyo kwenye mashahara ntapata kama 50k tu shga yangu" nilikuwa namwambia Fatma
"Mimi mwemye kweny viakiba vyangu sina hata sent shgaa maan jana Mama katoka kunipigiaa nimtumie pesa aende hospitali, na wadogo zangu sare zao zimeisha , au umesahu kam mimi ndio kila kitu kwetu shga yangu unajizima data tu hapo nipo nakuona" nilimtizma kwa huruma maan huyu kwao yeye ndio baba ndio Mama ndio maana huwa anafanya kazi nyingi nyingi maana siku ambayo tunakuwa off hapa dukani yeye anakuwa sahem nyingine huwa na muonelea huruma mhh unaweza sema wewe una magumu ila mwenzio ana magumu zaidi yako , nilimtizam tu nilielewa hata angenipa angeniambia nimrudishie kwa riba yaani huyu hapaana
"Ila Bilqis teacher ujinga Mama Rahel mme wake si ashawahi kufungwa wewe tukaaamuulize kama alienda kwa mwanasheria yupi shga" nilimtimzama "ila wewe umesahau kam mimi Mama Rahel sijamzoeaa , wewe si unaongeaga na Rahel kwanini usimuulize " nilimwambia fatma maan yeye huwa anaongea na mtoto wa huyo Mama mwenye hili duka tunalofanyia kazi "hapo umeongeaa point" alichukua simu yake akapiga iliita akatoka pembeni akaongeaa na huyo Rahel hakutaka kuongea mbele yangu maan huwa wana mengi ya kuongeaa mimi hayanihusu wananiita mtoto mdogo , alivyomaliza alirudi
"Mhhh shga yangu , yaani ni hivi kuna namba amenitumiaa hapa kasema ni mwanasheria poa sana maan , bwana wake mmoja alipataga kesi akashughulikia na unamlipa baada ya kesi kufanikiwa na kama kaka yako anaweza kuwa na chochote kitu akitoka atamlipa afu anaonekana hana shida kubwa na wala hana shida ndogo ndogo " nilimtizama nikamshukuru sana Fatma "haya wee mimi siendi huko nakupa hiyo address anapopatikana huyo mwanasheriaa sawa madam utaenda mwenyew mimi nabaki nakaa hapa , tukiondoka wote nani atabaki hap" nilimtizma nikamuelewa maan alikuwa anasema ukweli "sawa nenda hukoo anaitwa mwanasheria Kabil" nikaagana nae nikaondoka
Ika sasa akilini mwangu mhh nilikuwa nawaza upuuzi mtupu tu maan nilikuwa nasema kaka yangu akishatoka kam hatuna hela tunakimbiaa kwan atatupata wapi anatujuaa, yaani mimi sijui navuta bangi ๐๐ maan nataka kumzulumu hadi mwanasheria dooh ๐ ila kam kweli sina nitafanyaje ๐ ๐
Itaendelea.......๐ฅ
SEHEMU YA 2
Nilifika mpaka nilipoelekezwa pale kwenye address inavyosema ni maeneo ya posta kwenye ghorofa moja hivi la vioo , nilivyofika tu pale nje nikasema moyoni mhh kama huyu mwanasheria kumkodi sio laki saba yaani mara mbili ya mshahara wangu sijui kam maeneo yenyewe anayopatika ndio haya mhh nimeyaona ๐ค niliwaza tu kichwani mwangu sasa nilikuwa nipo pale nje maan nilikuwa nishaingia ndaniya fensi ila nilikuwa sijazam ndani ya jengo , nikaingiaa ndani mpaka reception, yaani nikawa nashangaa the way palivyo unaweza sema ni kampuni Fulani hivi kumbe sehem wanayopatikana wanasheria , nilimtizama yule mdada aliekuwa pale mapokezi anaonekana ana nyodo hatari , ila nikajikaza kisabuni
"Samahani dada naweza kukutana na Mwanasheria Kabil?" Alinitizama kwa jicho la dharau basi na hivi alikuwa kavaa miwani kam, basi akawa ananitii,ama kashusha miwani nilichukiaa mimi jamani nilitamani kummeza tu maan halinijibu afu linanitizama kwa nyodo nilichukia kweli "mhh una appointment nae" alisema yule mdada " hapana mimi nimeeleekezwa tu kuja hapa sikuambiwa habari za appointment Madam, ila naomba unisaidie nina shida kweli , mama yangu" nilikuwa naongea kwa unyenyekevu kweli kam kweli vile mimi ni mnyenyekevu kiasi hikoo , alinitizama akameza mate afu akanigeukia "Sorry mam nikwambie tu kitu mimi , sio boss hapa na huyo mwanasheria unaemsemea sio rahisi kukutana nae maan leo hana appointment na mtu hivyoo hatokuja officine , hivyoo acha appointment hapa kama ni kesho kutwa ukuje hapa kuonana nae nje ya hapo sina msaada na wewe tumeelewana?" Nilimtizama jicho la huruma kwel maan nguvu za kuongea zilikata hyo kesho ndio siku ya mwisho nisipo enda na mwanasheria mahakamani it means kwamba kaka yangu atahukumiwa na upande mmoja na atafungwa , niliwaza mengi vipi kuhusu wifi yangu "dada tafadhal kuna watu wengi wanahitaji huduma nishakusikiliza kam unaacha appointment sema tu mengine nishakuelezeaa na ninahisi umeelewa si ndio?" Nilimshangaa sana huyu mdada
"Lakini dada yangu mimi kesi yangu inasomwa kesho mahakani sister nisikilize kwenye hili plz ๐ " alinitizma tu " mimi sina msaada na wewe tafadhali unaweza kwenda nakuomba sana okay , mimi sitaki kuotesha kibarua changu nyasi am so sorry madam" alisema akaendeleaa kuchezea computer yake iliyokuwa pale mbele yake , nilimtizama nikasonya bonge la Sony nikaondokaa ila bila matumaini kam ambayo nilikuja nayo kwakweli , nilikuwa hadi nguvu za kutembea zimeniishia kabisa yaani , nilitoka nikaenda kukaa kwenye mabench ya pale reception kwenye wale watu walipojipanga , nikiwa na wawazo kweli hadi machozi yananilenga kwa mbali mwisho yakanisaliti yakaanza kushuka taratibu , alikuja mtu akanipa leso , nilipokeaa tu bila kumtizam machozi nikasema asante, akanipa na maji nikafungua nikanywa bila kumtizama piaa ,nilikuwa mbali kimawazo kwakweli
"Inaonekana unapitia shida sana unaweza kunielezea shida yako?" Ndio nikashtuka nimtizame usoni huyo aliosema hayo maneno , nikakuta ni mwanaume anaonekana ni mtanshati afu anaonekana ni mwanaume sio mvulana kwenye range ukimtizama ni kama miaka 38 au 39 , nikamtizama moyoni mwangu ikaja taswira huyu ananitaka maan mimi ni mzuri ๐คญ sio poa kabisa usikubali kuhadithiwa nakwambia mwenyew mimi ni mrembo sio kidogo kwahyo nikajuaa kaanza maswali ya kujisogeza karibu na mimi, afu na mimi sipatikani kizembe
"Wee matatizo yangu yanakuhusu nini labda kwa mfano , hebu niache mimi afu nyie wakak mnakuwaga na matatizo gani labda kwa mfano?, haya nikishakwambiaa utanisaidia nini hebu achana na mimi wewe vipi?" Niliongea kwa ukali ili kam ana hisi mimi labda sijui maji mara moja ashindwe kabisa "sawa lakini mpaka unakuja hapa na jinsi unaliaa inaonekana una tatizo na mwenye tatizo yoyote anahitaji kusaidiwa binti" nilimtimza jicho baya kweli " haya sina tatizo kwaher na hii leso yako shika na haya maji yako chukua sina shida navyoo mhh yani jamani wakaka wengine hapana mhh , kwahy unahisi unaweza kunipata sahau hiloo mimi sio wa hivoo" alinitizma hakujibu akatabasamu akainuka akaondoka zake , nilibaki nimezidi kuwa na hsasira mana mazoea ya kijinga na wakaka mimi sitaki kabisa upuuzi mimi , baada ya mud kam dakika 15 hivi namuona yule mdada wa pale mapokezi anakuja upande wangu nikajua sasa nimekuja kufukuzwa hapa nitoke " samahani shika hii kadi panda lift kwenye chumba namba 23 ingiaa , ukaongee na huyo mwanasheria Kabil" nilitabasam nikasema asante , mmh nikaanza kuwaza kumbe alikuwa ananipima imani asante Mungu sijamjibu hovyoo maana mimi sichelewi
Nikafika kwa maelezo yake nikapiga hodi nikaruhusiwa hee jamani si ndio nafika namkuta ni yule niliomchamba pale reception ๐๐ nimeyatimba naelezaje shida yangu mimi nishajikuta mbabe jamani mimi nimekomaa
Itaendelea....๐ฅ
SEHEMU YA 3
"Karibu ukae nikisikilize shida yako binti nakusikiliza, pia Samahani kwa alivyokujibu yule Leyla mwanzo , nilimtizama tu kwa aibu "njoo ukae hapo kwnye kiti binti " nilibaki namshangaa nikasogea nikavuta kiti nikakaa zangu "sawa binti nakusikiliza , unaitwa nani na shida yako ni ipi tafahdali naomba unielezee " alisema Mwanasheria Kabil, alikuwa anaongea kwa ustaarabu wa hali ya juu kweli nililuwa namtizama tu , maan nilizani ni mwanaume wa hovyoo siwezi kusema ni kijana huyu sio kijana na wala sio mbaba ni mwanaume "sa...sa..samahani kwa vile nilikujibu vibaya naomba unisamehe sana tafadhali mkuu" sasa hivi niliongea kwa utaratibu sana kuliko mwanzo alitabasamu "sawa endeleaa nakusikiliza "
"Sawa mimi naitwa Bilqis , nina shida kubwa kaka yangu yupo polisi na kesi yake ipo mahakani kwa kosa la upotevu wa vitu katika kampuni yao na kaka ndio anahusika na hyo sector ya kutunza hizo mali hivyoo nilikuwa naomba msaada wako mkuu, sitaki kushirikisha wazazi wangu kaka kasema nisiiwambiee na mkewe ni ana mimba kubwa sana mimi naogopa kumpa presha pia hivyoo tumeshatafuta sana wanasheria ila kwasababu hatuna pesa ya kuwapa imekuwa shida kesi ya kaka yangu kusiikilizwa na kama nisipo pata mwanasheria leo maana yake kesi ya kaka yangu itahukumiwa kwa upande mmoja tafadhali mkuu ninakuombaa sana kwenye hili kaka yangu atafungwa kam nisipokuwa na mwanasheria , na yeye ni ana majukumu na familiaa nakuomba sana " nilimaliza kuongea yeye akawa ananitizama tu kwa makini akatabasamu
"Okay kesi inasikilizwa lini?" Nilimtizma kwa bashasha nikiamini kesi yangu tayari ishaisha jamni nilimshukuru Mungu moyoni kabala hata ya kumjibu "kesho mkuu asubuhi saa tano mahakama ya kati" nilijibu kwa utiifu mhh ila behind the seen hamna lolote " sawa tukutane mahakani kesho asubuhi, na kuhusu malipo ni baada ya kesi cha msingu uamnifu na kuwa mkweli" nilifurahi nilitamani kuruka ruka jamani mhh , nikawa nimeinuka bila hata kuaga wala nini nikatoka na baibui langu , nilitoka hata bila namba ya simu utafikiri yeye ataota yaani nililisahau hilo kabisa ila niliondoka kwa furaha sana , nikapanda daladal mpaka pale dukani maan ni kariakoo sio mbali na posta
"Yaani Fatma kama nishawahi kuwa na furaha basi ni leo jamani mhhh ni nina furaha mnoo jamni , maan najiona kama vile nishashinda kesi tayari maan yule mwanasheria kakubali moja kwa moja shga asante kwa hilo" alinitizam kwa macho ya furaha " mh vipi kuhusu malipo yatakuwaje mpenzi?" Nilimtizama "kwani wewe si ndio ulinielekeza lakini auu sio wewe ulienielekeza au kuna mengine , afu yule anaonekana ni anajitegemea sio wa serekali " tukaanza kumteta mimi na Fatma maan kwa kuteta tupo vizuri mnoo " ila mimi nitamzulumu , yaani nikifanikiwa namtapeli kwani ananijua anikomege huko kwanza hata bei hajanitajia, akinitajia chini ya 50 unadhani ntakubali labda nisiwe mimi shga " alinitizama akanza kujichekesha hovyo hovyoo kama kawaida yake huyu mpuuzi " Mhh sasa wewe shgaa yangu , mhh uliona wapi kesi ya 50k mhh labda hyo kesi ni ya baba yako mzazi sio ninayoijuaa mimi jamni hapana usinichekeshe hapa utataka kuniua kabisa , mana nakuona huo utapeli wako unataka ukatapeli hadi mwanasheria ushazoea kuwaatapeli wateja wako wa simu sio huyu pole shga angu wee jipange au kam vipi utamgawia tu hakuna mwanaume anaekataa hiko kidude hata kam angekuwa mwema wa dunia" nilimtizama nilielewa ana manisha nini nikataka kumjibu mteja akaja ikabidi sasa tumuhudumiee huyu mteja kwanza mengine baadaee , tulimaliza kazi na kila mtu aliondoka zake maan hatukai pamoja sisi
Nililala nikiwa na mawazo sana kuhusu hiyoo kesi ya huyoo kaka na jinsi ntakavyomlipa huyoo mwansheriaa akisema ni million 1 je mhh maan hapa Fatma alikuw aashaanza kunitisha nilikuwa nalala ila usingizi sipati kabisa hata akisema laki 2 na nusu sina kabisa yaani mhh mbona mazito na kaka nae siju kama atakuwa nayo ila najipa imani kaka atakuwa nayo maana kaka kazi yake ilikuwa inamlipa sana kuliko yangu hadi alikuwa ashafunguaa duka la vyakula ambalo anakaa mkewe , ila mawazo nilikuwa nayo maan naweza kusema hivyoo kumbe kweli pesa hana kabisa yaani , nilibaki nawaza usiku na usingizi sikuupata kabisa maan nilikuwa nawaza sana mhhh
Itaendelea...... ๐ฅ
SEHEMU YA 4
Kulikucha asubuhi nilijiandaa nikavaa baibui langu jeusi na mtandio wangu mweusi nikaendaa zangu Mahakamani maan niliomba ruhusa kabisa kwa Mama rahel na aliniruhusu nilifika mapema mnoo pale ilikuwa ni saa nne ,nilikaaa nikasubiri sana mpaka muda wa mahakama ukafika lakini mwanasheria Kabil alikuwa hajafika hili nalo liliniwazisha sana jamni
Maan tuliingia mahakani , jaji akatupa dakika 30 za kumsubiri huyo mwanasheria wetu tulikaaa sana maan kaka nae alikuwa ashafika kizimbani jamani alikuwa anatoa huruma kweli , mimi nae mpaka nikawa nahisi jasho ila huyo Mwanasheria hakutokeaa jamani nilijuaa kuwaza mimi , tulikaa sana pale hadi kwenye zile dakika 30 zikabaki dakika tatu hapo pia hakufika , matumaini yangu yote yaliondoka kabisa nikakata matumaini kabisa nikawa nimekaa tu sina tena matumaini nae tena, na muda ulikwisha na "haya kesi imeanza muda wa kumsubiri mwanasheria wa upande wa pili umekwisha" alisema Jaji huku akigonga lile dude lililokaa mfano wa nyundo , nilikosa matumaini yote
Mwanasheria wa upande wa muhukumu wa kaka alianza malalmiko bila hata haya "Muheshimiwa Jaji nashukuru kwa muda wako ulionipatia , malalmiko upande huu wa mteja wangu ni kwamba anashutumiwa kupoteza mali au kuiba mali za mmliki wake hivyoo mteja wangu alikuwa anahitaji haki yake" alisema yule mwanasheria wa boss wake kaka "mtuhumiwa una ushahidi kuhusu hili jambo, kuwa ni ukweli au ni uongo?" Aliuliza Jaji, nilimtizama tu huyoo kaka alikuwa hana cha kujibu nilimuona kabisa kam alikuwa hana cha kujibu kwa sababu kama kujitetea hakuna ambae angemuelewa toka mwanzo hili lilinipa mawazo mengi sana , "sawa malalamiko yaendelee , ila bado muda wa kujibu upo kwa mtuhumiwa" alisema Jaji ,
"Nina pingamizi na madam ya mwanasheria kuhusu mteja wangu" nilisikia sauti inasema naangalia mbele alikuwa ni mwanasheria Kabil "samahani muheshimiwa Jaji kwa kuchelewa kwangu ila asante pia" alisema Mwanasheria Kabil "sawa muda wa kumtetea mteja wako bado unao unaweza ukaendeleaa kuzungumza" alisema muheshimiwa Jaji , basi kesi iliendelea vikali mnoo na ilikuwa kali kweli maan wanasheria wote walikuwa wamebobeaa kesi ilikuwa imesharindima mnoo na imekuwa kali mpaka msikilizaji mwenyewe unafurahi kusikiliza nilipenda kwakweli ila kesi haikufikia Hatma na ikabidi Jaji aseme turud mahakamani baada ya siku tatu kwa maana ushahidi upande wetu haukukamilika na tulikubali tukatoka njee
"Samahani madam kwa kuchelewa kuna mambo yalitokea ulisema unaitwa nan?" Aliniuliza mwanasheria Kabil nilimtizama "naitwa Bilqis" nilimjibu akanitazama kwa makini "sawa unaweza kuchukuaa namba yangu in case kwamba ikitokea dharura kam hii utanitafuta au ntakutafuta maan lazima hyo kesho kutwa tutakuwa na ushahidi wa kutosha kutekeleza hii kesi mahakamani nadhani umenielewa" nilimuelewa na tukabadilishana namba kila mtu akaondoka na namba ya mwenzie , na kuondoka
Nikiwa njiani nashangaa gari linasimama akashusha vioo alikuwa ni mwanasheriaa maan nilikuwa naelekea stand kutafuta boda "Sorry mam unaweza kunambia unaenda wapi?" Nilimtizama "naenda dukani kariako ," nilimwambiaa "okay unaweza kukaa tukaondoka si ndio au kuna shida?" Moyoni nilishukuru nilishusha pumzi kwa nguvu "sawa haina shida" tulipanda gari tukaondoka kuelekeaa dukani" tukiwa ndani ya gari saa ngapi nisione simu yake imevunjika kioo , nikaona yes dili hili hapa na ganji nakula
"Mhh yaani mheshimiwa mwanasheria, mbona simu yako imevunjika kioo mimi nauza simu kali na kwa bei poa kabisa karibu nikungishe na wewe uniungishe , wafanya biashara huwa tunasaidiana" alinitizama tu akainamisha kichwa chini akatabasam huku akiendesha kwa mkono mmoja "mhh ila kuna sehemu huwa nanunua vitu vyangu vyote samahani" nilimtizama kwa muda sana nikaanza kujichekesha hovyo hovyoo kama mwenye kuchanganyikiwa "mhh sasa uliona wapi kila siku sehemu moja kam ngozi badili wewe acha ugaigai mimi nauza vitu quality havina mambo mengi kila kitu ni safi na warranty ya mwaka mzima jaman njoo uniungishe wewe mwanasheriaa mhh haya sawa hyo pesa ya kukulipa sijui ntaitoa wapi mimi sawa " nilisema akabidi acheke tu akaniangalia kwa muda " mhh sawa hakuna shida tutaenda wote dukani kununua hyo simu" hapo moyoni nikasema kashajaa kwenye mfumooo huyuu anajifanya anakaza kaza hovyoo๐ , "enhee hyoo pesa yako ndio bei gani?" Alinitizama akaniangaliaa tu akatabasamu๐"tutaongeaa baada ya kesi kuisha" nilikaa kimyaa maaan sikuwa na sababu ya kuuliza swali lingine nilituliaa tu mpaka tukafika dukani nikamuuziaa hyoo simu alioichagua alinunua iPhone 13 pro max ila alinunua mbili nilihakikisha nampiga beii balaa yaani cha juu lazima mimi ndio Bilqis mtoti wa kichaga
Itaendelea....... ๐ฅ
SEHEMU YA 5
Baada ya hili siku zilipita za kutosha hasa nilikuwa nishamzoeaa sana huyuu mwansheriaa jamani , maan kesi iliendaa sana kutokana na utata wa ushahidi na mambo mengine ikaendaa kam wiki mbili zingine na ilikuwa ni kama kila baada ya siku moja nakutana na mwanasheria Kabil mahakani nikajikuta nimeshamzoeaa sana huyu mtu kwakweli nilijikuta tu namzoea kuachana na mambo ya kibiashara na kesi akawa ashakuwa kam rafiki yangu yani hizi wiki mbili alikuwa hadi ananiletea wateja dukani afu na mimi si mchangamfuu yani sijapoaa hata robo yaani๐ na hii siku ilikuwa ndio siku yangu ya mwisho kukutana na yeye nilihisi hivyoo maan ndio ilikuwa siku ya mwisho mahakani na kesi tulishinda
"Asante sana Bilqis, nakushukuru maan bila jitihada zako sidhani kam ningetoka mdogo wangu" nilitabasam tu "usijali kaka, kwenye ukweli hakuna kitu kinaharibika kaka yangu hata kama itachukua muda vipi " alinitizama sana kaka yangu kwa jicho la shukurani
"Sawa enhe vipi mke wangu anaendeleaje?" Aliuliza kak " hhhh nilimuongopeaa kwamba umesafiri si unajua ni mam kija tena vurugu isije kuamka tena si unaelewa ? Aanze vilio mwisho azae kabichi" nilijikuta naongea na kaka yangu kam vile shoga yangu maan haijawahi kutokea mimi na yeye kuongea hivi maana huwa ni mkali sana kwangu ni mtu wa amri , alinitizama nikajua tu hapa nishakosea uchangamfu umezidi sasa , nikaaa kimya nikainamisha macho chini "enhe kiongozi vipi kuhusu malipo?" Alisema kaka akimuuliza mwanasheria Kabil , alitabasamu tu
"Tutaongea nenda kwanza kwa mkeo, ni mtu ambae anaonekana hata licha ya kuwa mdogo wako alimuongopeaa ila hana uhakika na jibu la dada yako kamtoe hofu tafadhali " aliongeaa kwa hatua kama nilivyomzoeaa nishamzoeaa, huwa anaongea point tu na sio mambo ya kipuuzi hili linaonesha thamani ya elimu yake sio kama mimi maneno mengi nishazoeaa uwinga wa kariakoo , alimshukuru " ila kam mnaona hakuna tatizo naweza kuwapeleka maan mimi nipo free baada ya hili " Kaka alikataa yani yeye wa kiume apewe lift mimi hapo sichangii nalia moyoni naomba dua zote kaka akubali niepushe pesa yangu ya nauli , maan alikua hana pesa hapo kwahy lazma ningetumia ya kwangu ila mwanasheria alifanikiwa kumshawishi mwisho akakubali nilifurahi ,tukapanda gari kuelekeaa nyumbani kwa kaka, tulifika na wifi alitukaribisha vizuri tu alikuwa kavaa msomali wake , kaka kapanga ila nyumba nzima ya geti , hatukuishiaa hapo maan mwanasheria alitaka kugeuza kak akamuomba aingie ndani aliingiaa
"Haya wewe na wifi yako nendeni jikoni mkandae chochote kitu kwa ajili ya mgeni " nilikasirika mimi hawajui tu nikaanza kurusha rusha miguu tu maan nimetokaa huko nilitaka ninyooke dukani naanza kuambiwa habari za jikoni nilichukia ๐คจ uwii mimi nilijihisi kufa "wewe husikii au Bilqis" aliongea kaka niliinuka kwa makasiriko kweli nikaenda jikoni kukaa na wifi tukaanza kupika ,
"Yaani kaka mgeni hamjui eti ashaanza kusema tumuandalie mgeni jamani huyu kaka hapana mimi ananikera" nilikuwa najisema peke yangu , wifi ananitizama tu "haya nambie ukweli wifi maan hapa naona dalili zote za kuwa mume wangu hakuwa safarini, na yule mwanasheria ni wa nini" alijua kama ni mwanasheria baada ya kuona sare zake mimi nikaona wasinichanganye zangu kukaa na siri zio shida zangu nikabwaga yote yanayoendeleaa mimi ila nilimuambia kwanini hatukumuambiaa alilalamika ila akaelewa , wakati tunaendeelea kupika simu yangu iliita alikuwa ni mama Rahel , alinipa ujumbe mzitoo hapo wa kufukuzwa kazi maan alinipa siku mbili za kufuatiliaa kesi ya kaka nimemaliza sasa wiki mbili kazini nakuja kwa kusua sua na leoo ndio sijakanyaga kabisa , mhh nilikata simu kwa hasira ila sikutaka kaka wala wifi wajuee maan wataniambiaa niamie hapa na mimi kukaa kwa kaka sitaki ni dictator sana , nilivumiliaa maumivu yangu , tukapika nikatenga muda huoo mwanasheria Kabil bado yupo hapo akili zangu zikantuma labda kaka kamwambia asubuli chakula , tulikula tukamaliza na mwanasheria akaagana vizuri na kaka , na kaka akatoka nae nje kumsindikiza mimi ndio nilivyoelewa pale , akarudi ndani akaniita
"Bilqis njoo hapa au unaenda huko kazini kwako?, maan nina maongezi na wewe hivyo kama unaenda hakikisha ukitoka hapo unakuja huku" nilimtizama maan alikuwa serious sana najua ni kawaida yake ila hii siku ilizidi "ndio leo sina pa kwenda nina ruhusa kazini , hivyoo ntaenda kesho" alinitizama akameza mate " mhh omba ruhusa ya au omba kuacha kazi kabisa maan kesho kuna wageni wako , wanakuja kutoa barua unaolewa" nilitoaa macho mimi "jamani kaka mimi sina mchumba wa kuja kunioaa ujue hebu acha matani kaka nani ahe kunioa mimi " kaka alinitizam tu " huyu mwanasheria alietoka hapa ameomba ruhusa ya kukuoa na nimemkubalia kwa sababu ni lazima uolewe ushakuwa mkubwa sasa na hakuna kitu cha maan unachofanya ambacho unaweza sema kikuzuie kuolewa, husomi wala nini hivyoo jiandaee kwa ndoa ukubali ukatae utaolewa nimemaliza na hii ndio kauli yangu ya mwisho na ninawapigia wazazi wako waje huku, maan kuhusu ndoa hakuna atakae pinga "
Itaendelea........๐ฅ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi








Maoni