"Hakukuwa na haja ya kumkaushia...." Chris aliongea
"Mguu wake unahitaji kukaushiwa ili apone haraka, mara nyingi huwa una utararibu wa kuwaonesha tabasamu wagonjwa unao wafanyia upasuaji lakini kwangu inakuwa tofauti huwa nawaonesha sura ngumu ili mifupa yao ipone kwa haraka" Dorin aliongea
Chris hakuwa na namna zaidi ya kuachia tabasamu.
Baada ya Jamila kufika nyumbani, hakuona sababu ya kuendelea kukaa hapa, kwani kila sehemu aliyogeuka alimuona Ali.
Alitafuta Mteja wa kununua nyumba yao, isingekuwa rahisi kwake kuuza kwa bei ghali kwa sababu Wateja wake walikuwa na maisha ya chini.
"Kwanini unaondoka, usiniambie ni kwa sababu ya yule Daktari" Rafiki yake alimuuliza akiwa ana msindikiza kwenda kupanda meli
"Nahitaji kujitegemea pia, ni kweli moyo wangu umevunjika lakini haimaanishi nitaendelea kuumia. Ni lazima nitafute maisha...." Jamila aliongea
"Endapo maisha yatakuwa magumu kwako naomba usiogope kurudi, sitaki kujua nitakuwa katika hali gani lakini nitakupokea" Rafiki yake aliongea
Jamila alipanda meli, alihitaji kwenda Zanzibar, kwani kabla ya kuishi Jijini Mbeya yeye na wazazi wake waliwahi kuishi Zanzibar.
Akiwa amekaa ndani ya meli alijiahidi kusahau kila kitu kuhusu Chris.
Siku iliyofuatia ikiwa ni asubuhi na mapema Chris alifika nyumbani kwa Jamila.
Alishtuka sana baada ya kukuta nyumba ya Jamila imebomolewa.
"Kitu gani kinaendelea hapa....." Chris aliuliza
"Hili eneo limeuzwa, nahitaji kuweka hapa shule ya chekechea" Mwanaume Mmoja mwenye kitambi kikubwa aliongea
"Mhusika wa kike anayekaa hapa kaenda wapi..." Chris alijikuta akiuliza
"Sifahamu, hii nyumba nimeuziwa na mwenyekiti wa huu mtaa itapendeza kama utaenda kumuuliza"
Ilikuwa hivi, baada ya Jamila kumuuzia nyumba mwenyekiti yeye naye alimuuzia tajiri mwenye ndoto ya kujenga shule mahali hapa
Chris aliondoka akiwa mwenye maumivu moyoni mwake, anaamua kwenda gengeni kwa Jamila.
"Ni kweli Jamila kauza nyumba yake, sijui ni wapi kaenda kwa sababu hajaniaga lakini nina uhakika atakuwa sehemu nzuri hivyo hauna haja ya kuwa na mashaka" Rafiki wa Jamila aliongea
"Nikupe kiasi gani cha pesa uniambie mahali alikoenda Jamila...."
"Wewe ni Mume wa mtu ni ajabu sana kumtafuta Mwanamke ambaye si mke wake huoni kama utamletea shida"
"Kuna kitu nahitaji kuzungumza naye, ni kitu muhimu sana huna haja ya kunificha"
Rafiki wa Jamila hakuwa na namna zaidi ya kutaja sehemu aliyoenda rafiki yake.
Chris aliondoka akiwa mwenye amani moyoni mwake, japo Zanzibar ni kubwa lakini alijiahidi kumtafuta Jamila.
Upande wa Dorin akiwa ana mkata kucha Babu yake alishangazwa na namna jasho linavyo mtiririka.
"Kuna baridi lakini uso wako una tiririka jasho, kuna usalama kweli!" Dorin aliuliza
Kabla ya Babu kuzungumza chochote alidondoka kama mzigo, harakati za kumpeleka hospitali zilifanyika.
Chris anapatiwa taarifa kuhusu kuanguka kwa Babu.
Anafika hospitali kujua ni kitu gani kinaendelea.... kitendo cha kumuangalia tu aligundua ana uvimbe katika kichwa chake
"Ana uvimbe katika kichwa chake, upo sehemu mbaya sana.... Mimi kama Daktari napendekeza tumuache" Chris aliongea
"Tumuache?...kwahiyo unataka kusema anatakiwa kufa!" Dorin aliongea
"Ndiyo, nadhani hata Madaktari wengine watakubaliana na Mimi kuwa Boss anatakiwa aachwe" Chris aliongea
"Nina uhakika hili swala limo ndani ya uwezo wako... niambie ni kitu gani hicho unataka" Dorin aliongea
"Endapo nitakosea tu kidogo Chairman atakuwa kichaa, kuliko awe kichaa acha apumzike kwa amani"
"Chris, hili swala limo ndani ya uwezo wako naomba umsaidie Babu yangu kisha Mimi nitakupa kitu chochote kile unachotaka" Dorin aliongea
"Ni kweli hili swala limo ndani ya uwezo wangu kama nitawekeza akili yangu, ni mapema sana kusema ni kitu gani nitataka lakini pindi nitakapo fanikiwa nitakueleza ni kitu gani nataka" Chris aliongea
Dorin hakuwa na shaka, uhai wa Babu yake ulikuwa na umuhimu mkubwa kuliko kitu chochote.
Chris alijiandaa kwa ajili ya kuingia chumba cha upasuaji, siku ya leo aliitafuna karanga ya Jamila aliyoitunza kwa muda mrefu.
Aliwekeza akili yake mahali hapa, Dorin akiwa nje ya chumba alizidi kumhesabia masaa. Alijikuta akipata wasiwasi baada ya masaa sita kukatika.
Siku zote operation za Chris huwa hazimalizi masaa mawili hata kama zinakuwa ngumu vipi...
Chris anafungua mlango, anaachia tabasamu kumaanisha kila kitu kimeenda sawa.
Dorin aliachia tabasamu pia, japo hakujua ni kitu gani Mwanaume huyu ataomba lakini usalama wa Babu yake ulikuwa na umuhimu mkubwa sana
"Ni mapema kuomba kitu nilichokuwa nataka....nitajipa uvumilivu wa siku tatu. Nahitaji kuona Chairman akitabasamu" Chris aliongea akataka kuondoka lakini Dorin alimsubirisha
"Nenda ukamtafute Jamila, naelewa hicho ndicho kitu ulichokuwa unataka kuhusu Babu yangu nina uhakika yuko fit sasa" Dorin aliongea kisha akaondoka
Chris alibakia kuduwaa, alishindwa kuelewa imekuaje Dorin akayatambua mawazo yake kwa wepesi.
Chris hakutaka kuchelewa, aliamini Dorin atamuombea ruhusa kwa Babu pindi atakaporejea.
Akiwa na haraka sana alipanda ndege inayoenda Zanzibar.
Hakujua anaanzia wapi kumtafuta Jamila lakini aliamini atampata.
Baada ya kufika katika Mji huu wa Watalii alichukua chumba.
Isingekuwa rahisi kwake kupumzika kwa sababu alikuwa na njaa sana.
Alishika simu akapiga moja kwa moja kwenye namba zilizokuwa zimeandikwa kwenye kipeperushi kilichokuwa mlangoni.
Dakika 20 zilikuwa nyingi, kengele iliyokuwa mlangoni kwako ilitoa sauti kumaanisha Mhudumu yupo mlangoni.
Moyo wa Chris ulishtuka sana baada ya kukutana uso kwa uso na Jamila aliyekuwa katika muonekano mwingine kabisa
JE NINI KITAENDELEAAA!
FULL 1000
SIMULIZI HI IMEKAMILIKA MPK MWISHO KABISA
BEI YA OFAAAAA WAHI INBOX NA 500 YAKO TU UMALIZE MPK MWISHO
NAMBA YA MALIPO 0755090082 JINA LA USAJILI ZAINABU SUNGITA MPESA
UKISHALIPIA WAHI...
WAHI WHATSAPP 0755090082.